SIJAKASIRIKA KWA SABABU NIMESHUHUDIA TIMU BORA NA MPYA IKICHEZA KWA MTINDO ILEULE WA MWAKA JANA; IKIADHIBIWA KWA MAAMUZI YALEYALE YA KIMAKOSA KAMA MSIMU ULIOPITA NA IKIONGEZA REKODI YA HASIMU WETU AMBAYO ITATUCHUKUA MIAKA MINGI KUWEZA KUIFIKIA KWA KUFUNGWA MARA SITA MFULULIZO.
NAAMINI WANASIMBA WENGI WANAOIPENDA TIMU YETU NA WASEMA KWELI WAMEKUBWA NA UBARIDI HUU ULIONIKUMBA MIMI. NAJIULIZA HAWA YANGA NI KWELI WAMETUZIDI KIMCHEZO KIASI CHA KUJIAMINI HATA WAKIAMSHWA KUTOKA USINGIZINI LAZIMA WATATUFUNGA !! HAPANA NAKATAA.
NIKIANZA NA HILI LA KUFUNGWA MARA SITA MFULULIZO; HATA INGEKUWA TUNAFUNGWA NA AL AHILY, NAMUNGO AMA APR LAZIMA KWA WATU WENYE MAPENZI NA TIMU WAJIULIZE KULIKONI; SEMBUSE KUFUNGWA NA YANGA JAMAA ZETU WA PALE JANGWANI !
SINA SHAKA KABISA NA USAJILI. TUMEPATA KIKOSI BORA NA KIPANA SAFARI HII. LAKINI KUNA KENGERE IMEANZA KULIA MAPEMA KUHUSIANA NA BENCHI LA UFUNDI. NASUBIRI KUONA MECHI MBILI ZIJAZO; JIBU SAHIHI LITAPATIKANA.
HAPO HAPO KWENYE KUFUNGWA MFULULIZO; VIONGOZI WETU WANALIPOKEAJE. AMA WANASUBIRI TUFUNGWE IFIKE MARA KUMI MFULULIZO ? HAPO NAPO MAJIBU TUTAYAPATA BAADA YA DABI IJAYO.
JUU YA HILI LA WAAMUZI IMEKUWA BAHATI KALIFANYA MWAMUZI WA KIMATAIFA. KWA HESHIMA YAKE CAF TUNAMSAMEHE BURE. ILA IWE NI ONYO KWA WAAMUZI WA MICHEZO IJAYO. EBU WATENDE HAKI BILA KUANGALIA INAWAHUSU SIMBA, MBEYA CITY, YANGA AMA COASTAL UNION. LEO SIMBA KAIKOSA NGAO YA JAMII KWA KOSA MOJA LA KIBINAADAMU; HATUJUI NANI ATAKOSA POINTI NGAPI KWA MAKOSA YA AINA HII. TUJIPE MUDA.
NIMALIZE KWA KUWAPA POLE WANASIMBA WENZANGU. NAJUA HII NI NGUMU KUMEZA LAKINI TUJIPE MOYO NA MUDA. TUNA TIMU NZURI SANA MSIMU HUU. TUONGEZE MAOMBI NA TUZIDISHE UMOJA.
MUNGU IBARIKI SIMBA.
UBAYA UBWELA; SEASON TWO..
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments