VYOTE NDANI GONGA94
FORGIVE ME, MOM ππ NISAMEHE MAMA SEHEMU YA: 12
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
SONGA NAYO.....
Muda huo huo aliingia mama mdogo wa kiume wa Benny bila kupiga Hodi nilichukia Sana nilitamani nimpige hata konzi yaani ashike adabu yake
"Kaka unaitwa "
"Waambie nakuja "
Benny akaniaga na kutoka nje nilibaki nikiangalia uku na uku, kwakuwa Benny aliitwa nikaona nitumie muda huo kuweka vitu sawa nikapanga, nikabadili kila kitu muda wote huo benny alikuwa nje na familia yake, njaa iliniuma nikamtumia sms kwakuwa tulikuwa tumeshasajili laini mpya
" Njaa inauma Sana hata sielewi "
Ndipo nilipogundua kuwa simu ameweka kwenye begi, nilipata hasira Sana nikaona ngoja nimfuate uko uko, nikatoka nje na kukuta wakiwa na ugomvi
" Unakujaje na mwanamke nyumbani bila taarifa ?? Kwanza mwanamke mwenyewe anaonekana kabisa kuwa Hana adabu atujamkaribisha ameingia tu ndani "
"Mama tutaongelea hili baba akirudi kutoka shamba, me sipendi kelele kabisa ndio kwanza nimefika mnajua nimepitia mangapi uko?? Mama mbona ubadiliki, huyu binti wa watu ndio kwanza amefika aujakaa nae ukamjua umeanza kumuongelea hivyo "
Nikaona huu msala polepole nikarudisha komwe langu ndani, nikabaki kujilaumu mwenyewe tuu
" Haya yote kwasababu mama hayupo mama asingeruhusu niyapitie haya"
Mwisho nilipitiwa na usingizi nilikuja kustuka kagiza kameanza kuingia nilipiga kelele baada ya kumuona mtu akiwa pembeni yangu
"Usiogope naitwa Veronica Ni Dada wa Benny wa pili kuzaliwa kaka Benny amesema nikuangalie yeye ameenda mjini "
"Oooh sawa"
" Ila wifi yangu we mzuri "
Alisema hivyo nikatabasamu tu, tukaanza kupiga story za hapa na pale nikimpa story za dar kulivyo na maisha mengine niliingia mtandaoni na kumuonesha vitu tofauti tofauti mwisho uvumilivu ulinishinda nikalopoka
"Njwa inaniuma sana "
"Kaka atakuja na chakula chako ndo amekufatia uko "
Nikashika simu na kumpigia lakini hakupokea na muda huo huo akaingia
"Njaa itakuuwa wewe sio kwa kunitumia sms na kunipigia "
Nikacheka na kumpokea mfuko ambao alikuwa amebeba, ulikuwa unanukia chips kuku tu. Kwa kipindi iko kiukweli tulikuwa na hela aswa Benny maana mijimama yake ilikuwa ikimpa Sana hela hata Mimi pia nilikuwa na pesa lakini sifikii za Benny.
"Vero ajakusumbua huyu...??"
" Amna ajasumbua, mbona Yuko vizuri sijui kwanini mama amtak......"
Kabla ajamaliza benny akamziba mdomo hakutaka Mimi nijue ingawa Mimi nilishajua kitambo, na Mimi nikapotezea Kama sijaelewa kitu, nikafungua chakula na kukiweka juu ya godoro, kikiwa kweye foil
" Kwani we umekula...??"
" Yaani Mimi Nile na wewe ujala unafanya matani matoto wangu wewe "
Alijibu Benny akiwa na furaha ingawa nilijua anajifosi kufurahi Basi nikatoa na vinywaji tukaanza kula sikugusia chochote kuhusu familia, tulikula na kupiga story nyingi sana.
Siku iliyofuata niliamka mapema Sana nakumbuka ilikuwa saa Tisa ile nikaanza kufanya usafi wa nyumba niliifanya usafi kila Kona ambayo niliweza kuifikia, Katina kibanda ambacho walifanya Kama jiko nilikuta Kuna miogo nikachukua na kuimenya na kuandaa kifungua kinywa kwa kuikaanga kwani kila kitu kilikuwepo mdani umo, nikakata kachumbali nzuri ya mjini mjini, limao kwa sana yaani niliandaa kila kitu nikapika na chai nikaweka mchai chai kwani walikuwa wamepanda nje ya nyumba yao.
Nikiwa nimemaliza nikabandika maji nikastuka nikiongeleshwa
"That's too much, unawezaje kuamka mapema yote hi unatakiwa upumzike mtoto wangu anaitaji mapumziko kuliko maangaiko "
Alikuwa Ni Benny nilibaki kumtazama tu
" Haya kulala"
Tukaingia ndani na kulala
Majila ya saa 12 kila mtu ndo alianza kuamka wa kwenda shamba walikuwa kuwa wakijiandaa wanafunzi pia nikamsikia mama Benny akilalamika
" Na Mimi nasema Nina mkwe mpaka mda huu amelala ajali kuwa Kuna watu wanaenda shamba ata kuwasaidia kazi, Benny akatoka nje kwa hasira Sana
"Mama kunakoelekea utasema Mimi Nina mdomo mchafu au nimebadilika hi nyumba unavyoiona Ni chafu? Chai IPO au amna...? Umeangalia chochote au ndio mdomo mali yako...??"
Nikaona Mambo yanazidi kuwa mengi nikamua kutoka nje
" Shikamoo mama "
Mama benny aliniangalia na kuondoka kwenda kibanda Cha jikoni, gafla akapiga kelele na kutoka nje.
" Nani ametumia mafuta yangu kupikia hile miogo na itakuwa wewe binti unayejifanya wa mjini"
Muda huo huo, baba Benny alitoka nje..
" Kelele asubuhi subuhi ma Vero una nini wewe, kwa ooh Benny my boy "
Kisha benny na baba yake wakakumbatiana baba Benny alifurahi Sana kumuona Benny
" Naona umetuletea mgeni "
Aliongea baba Benny uku akiniangalia akamuachia Benny na kunipa mkono
" Shikamoo baba "
"Marahaba binti jisikie uko nyumbani "
"Asante "
" Nina haraka Sana hivyo Basi jioni tutakuwa na kikao nitajitaidi kuwai kurudi Kuna Mambo yangu nafatilia uko, wa shamba waende wa shule waende, wa vibaruani waende sitaki kelele hapa, Benny akikisha unamuonesha mazingira mgeni wetu "
Sawa baba.
Baba benny akaondoka yaani alikuwa Hana Mambo mengi nilimuelewa kwa ucheshi wake nikajisemea
" Kwahiyo tatizo hapa Ni huyu mama anisumbui ntamuonesha me Ni Nani "
Kila mtu akaondoka nikabaki na Benny wangu kiufupi familia nzima ilikuwa haishindi nyumbani kila mtu alikuwa bize na Mambo yake
"Benny baba ako ni mtu simple Sana "
" Yaaah ni msomi wa miaka hiyo Sasa hivi anakula pensheni tuu"
Tukajiandaa na kwenda mjini kwa kuwa tulikuwa tunalala kwenye godoro chakavu, tulinunua kitanda, godoro, dressing table SI unajua Tena Mambo ya mjini mjini, na kabati la nguo, nikanunua na Madera kidogo yatakayonistili siku mbili tatu maana mavaz yangu nilikuwa nayajua mwenyewe ukizingatia gubu la mama Benny naweza nikachapwa vibao kweupe.
Majila ya jioni tulirud nyumbani na almost familia nzima ilikuwa umesharudi isipokuwa baba, tuliposhuka kwenye gari Kuna msichana alimkimbilia Benny na kumkumbatia Benny alionekana kufurahi Sana huyo msichana walinyanyuana na kuzungushana nilibaki nikiangalia tu, nikamuomba dereva anisaidie kushusha mizigo.
"Waoooh Amina daaaah kitambo saa unaendeleaje...??"
Huyo Amina alikuwa mtoto mashallah kaumbika nyuma kafungasha hatari, ila sura ndo ya baba rangi na ngozi vilimtupa mkono na yote kwaajili yamaisha ya kijijini, yaani eneo lile kina Benny ndio walionekana kuwa na maisha mazuri
" Nipo nimefurahi nilipokutana na mama shamba na kuniambia umerudi "
"Yeah nimefika Jana "
", Naona tunamteni "
Alizungumza msichana huyo na kunigeukia Mimi ambaye niliamua kusimama pembeni yao, wanasemaga abilia chunga mzigo wako π, nikatabasamu kinafki
"Oooh yaah ni mke wangu anaitwa saada, saada huyu Ni Amina nilisoma nae shule ya msingi na secondary"
" Nashukuru kumfahamu,"
Kisha nikamgeukia dereva
"Nashukuru kwa msaada wako, ulisema Ni kiasi gani....??"
Akataka kiasi nikafungua wallet na kutoa pesa lakini Benny aliwai kutoa kabla yangu tukabaki tukichekeana tu, hapo niliona amina alivyochukia.
" Kakae kivulini utulie nitaingiza vitu ndani na kupanga sawa...??"
"Sawa "
Niliambiwa nikatulie chiini nikanza kutoa vitu ndani kisamha nikachukua kapeti jipya ambalo tulinunua na na kuja kutandika, kiukweli siku hiyo tulinunua vitu vingi mno, vyakula vya ndani fliji kwani kulikuwa na umeme lakini fliji alikuwepo pia, ingawa kulikuwa na tv ya chog.
Baada ya muda tukiwa tunaendelea kupanga panga baba Benny pia alirudi na vyakula hivyo tukawa na vyakula vya kutosha ndani, muda wote huo Amina alikuwa akitusaida kazi uku wakikumbushiana Mambo ya shule.
Muda wa saa mbili chakula kilikuwa tayali, wote tukaja sebleni na kukaa kwenye mkeka isipokuwa baba na Benny , tulipakua na kuanza kula.
" Uku tunakula bahisi kikao chetu kianzie hapa hapa hivyo wote mnisikilize kwa makini, Zima hiyo tv kwanza "
Alizungumza baba benny.
"Kwanza nimshukuru Mungu kwa kumrudisha kidume wetu salama, maana kwa mimi binafsi nilikata tamaa juu yake baada ya kukosa mawasiliano kwa muda mrefu na kwenda jijini kumtafuta bila mafanikio "
" Baba ulikuja dar?"
Aliuliza Benny kwa shauku
"Ndio maana nilikosa amani kabisa nilikaa lakini chakula akipiti, nilivyokukosa ndo kabisa nimaruri nikiamini utakuwa umekufa "
Alinyamaza kidogo na kufuta machozi aisee niliumia Sana nikikumbuka baba angu Mimi ndio ajali kabisa na alishaitelekeza familia muda mrefu niliumia sana.
" Nashukuru umerudi na umekuja na mgeni nafikili tunaitaji utambulisho"
Baba Benny alikuwa akiongea kisomi Zaidi yaani nilibaki kucheka tu, lakini mama Benny alivimba kwa hasira yaani ingekuwa Ni puto Basi lingepasuka.
" Niwape pole wazazi wangu ndugu zangu na kila mtu ambaye alikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu mimi lakini nimshukuru Mungu kwa hapa nilikofikia naomba kwanza nianze na utambulisho, huyu mbele yenu mgeni wetu anatwa saada Ni binti ambaye nimetoka nae dar es salaam, saada huyu Ni baba yangu na huyu Ni mama angu, sisi tumezaliwa nane, wa kwanza Ni Dada yetu ameolewa mwanza uko , wa pili Ni mimi, wa tatu vero, wanne huyu kelvin, wa tano Julius"
Alivyotaja Julius moyo wangu ulifanyw paaaah na kuanza kwenda Kasi Sana
"Wa sita Ni susan, wa zaba neema wa nane Mike huyu kama unavyomuona , na huyu ni mtoto wa Dada Vero anaitwa side awa wengine Ni wadogo mno nafikili utapewa utambulisho na wenyeji hata siwafahamu "
"Aaaaah........"
Baba Benny alitaka kuzungumza lakini Benny alimkatisha
" Nimepita mengi uko lakini nimshukuru saada amenisaidia sana yeye ndio alinifanya nione Niko hata duniani, tumekuja kuishi uku, Mungu akijaalia tutafunga ndoa, nampenda Sana na hapo alipo Ni mjamzito "
"Ilo lime........"
Baba Benny alitaa kuongea Tena lakini alikatishwa na mke wake
" Etiii unasema Nini wewe yaani unataka kututia aibu watu watatuonaje sisi hapa, tulishamuandaa Amina kuwa mkwe wetu na sio huyu sijui umemuokota wapi "
"Mama neema ebu tulia kwanza mbona unakurupuka Sana Amina yupi kwanza huyu au ??"
", Huyo huyo "
"SI Ni mke wa mtu huyu ??"
" Mke wa Mtu wapi wakati amesharudishwa kwao "
" Amina mwanangu umepewa taraka ??"
Aliuliza baba Benny , Amina akatikisa kichwa kusema bado, Benny akainuka na kumshika mkono Amina na kutoka nae nje, nilibaki nikiangalia tu madrama yanayoendelea umo ndani yaani chuki ya mama Benny juu yangu ilikuwa waziwazi kabisa alikuwa akiniangalia Sana nami nikajifanya mpole Zaidi kuliko wote....
"Amina kwani wewe unataka kuolewa na Mimi ?"
", Ndio nimekusubili kwa muda mrefu Sana niliolewa kwa kulazimishwa tu, lakini bado nakupenda"
"Unanifurahisha hivi unakumbuka ulishawai kuniambia Mimi sio level zako, nikuombe kitu Amina nakujua wewe mkolofi Sana Sana please muache mke wangu usije ukamfanyia vurugu yoyote "
Aliongea Benny ana kutaka kurudi ndani na Amina akawa anafata akamgeukia
"Unaenda wapi muda huu baada ya kwenda kwenu "
Amina aliogopa Sana maana Benny alifoka kw hasira aliingia ndani na Moja kwa Moja akaingia chumbani, nilimaliza kusafisha tulipokuwa tunakula kisha kwenda chumbani kwangu, nilimkuta Benny akiwa amelala nikakaa na kumshika kichwa
" Ebu niache na wewe na ulale "
Eeeh nikaona makubwa haya jamani, nilijisikia vibaya sana nikatoka nje kabisa ya nyumba na kukaa nje peke yangu
"Maumivu ninayoyapata Sasa hivi sijui Kama yanaelezeka, kwani Mimi Nina mikosi gani au ndio kumkosea mama , kokote ninakoenda lazima atokee wakunichukia na chuki ya waziwazi nimechoka jamani Mungu nichukue Mimi "
Nililia na kukufuru Sana moyo wangu ulishachoka kuyavumilia maumivu, nilikaa nje na sikutaka kabisa kurudi ndani niliona Bora kuwa peke yangu, Kuna muda niliwaza mpaka kutoloka usiku huo lakini niliwaza nitaenda wapi je na huyu mtoto ndo kitamtenganisha na baba yake kama baba alivyomtenganisha mama na Julius, kichwa changu kiliwaza mengi sana, mwisho Benny alikuja na kunishika nyuma yangu
"Am sorry"
Nilibaki nikimuangalia tu, tukaingia ndani na kulala lakini usingizi haukuja kabisa siku hiyo nilikuwa nawaza tu.
Asubuhi Kama kawaida niliamka lakini Nika..........
ITAENDELEA.....
Umesoma kwa utulivu Β· dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi forgive-me-mom-nisamehe-mama-sehemu-ya