VYOTE NDANI GONGA94
FROM BANGI TO BABY ππ SEHEMU YA 1
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Leo ni Weekend bwana sasa kuna rafiki yangu Tulikuwa tunasoma wote secondary yaani ni rafiki yangu kweli kweliii haswaaa, Ana kama wiki amehamia sehemu ingine yaani kuna changamoto alipata kwahiyo akahama pale alipo kuwa anaishi mwanzo akahamia sehemu ingine mitaa ingine kabisaaa ni mbali na alipo kuwa anaishi ..
Sikuwahi kupata nafasi ya kumtembelea ila nilimuahidi mwisho wa wiki hii nitakwenda kumtembelea, Sa ndo leo hapaa nimefunga safari kwenda ..
Yaani alipo hamia aisee ni mbali na bara bara kubwa et kisa tu amepata nyumba ya bei rahisi halafu nzuriiii yaani nzurii kweli, nikasema embu nikaone hiyo nyumba maana shost sio kwa kupapamba huko jamani ...
Njia mbayaaa jamani na hivi gari yangu ya bei rahisi inangonga chini hatari nilikuwa natamani hadi kulia yaani nilijuta aisee ..
Sasa nikafika sehemu palikuwa ni mtaani tu mbele kuna kilima kirefu halafu njia inamashimo kama yotee, mmh nikaionea huruma gari yangu jamani si naiua hapo kabisa ..
Ikabidi nimpigie simu nikampa lawama kama zote nikamwambia yeye aje tu tusalimiane hapo mie nirudi kwangu hapana huko hata siwezi kupandisha halafu ni mtaani yaani mtaani sijui unaelewa au niseme uswahilini mpaka basiiiii mtaa umejaa vibanda vibanda vichafuuuu mmh yaani huyu Tinner jamani sa ndo nini kuja kupanga huku hata kama ndo vya rahisi aah mie hapana mwenzangu hapana ...
Nikamwambia "shogaa mie sitoboi huko kwako mwenzangu "
"Kwani umefika wapi"
"Hata sipajui ila mbele yangu kuna kilima hapa kurefuuu hicho mmh halafu njia mbayaa sana nitauwa gari yangu bwana"
"Vero ...embu acha utoto hapo ukipandisha hiko kilima tu unaona geti langu yaani umefika embu njoo bwana!!"
"Sasa si ushuke tu hapa chini"
"Utakuwa haujaja kwangu... kwahiyo na hiki chakula nikibebee nikuletee huko chini tushinde ndani ya gari yako?? Embu acha mambo yako bwana njoo " jamanii nilikiangalia hiko kilimaa nikashusha pumzi ndefuuu halafu nikaitazama gari yangu mwenyewe navyoitunzaa jamani hiki ni kilima kikubwa halafu mashimo mawe kama yoote daah halafu ki gari chenyewe nilichukua tu mkopo kazini jamani daah ...
Kabla sijajibu Tinner akanambia "sikia chukua boda hapo akupandishe nakuja kulipa hela "
"Heee na gari yanguuu???" Yaani nilishtukaa huyu anataka niache gari yangu jamani mweeeh
"Iache hapo bwana we funga" mmmh nilitazama pembeni mwenzangu kulikuwa na wakaka wamekaa chini ya mti nyiee yaani wahuni mpaka wahuni tenaaa kwanza nilivyowaangalia tu nikajua hawana kazi kabisa ni wizii mmh afu niache gariiiii??
"We Tinner utakuwa haupo serious wewe, yaani niache gari yangu hapa!!" Niliongea huku nashusha sauti sasa nikasogea pembeni kidogo, hapo muda wote naongea na Tinner ananielekeza nilikuwa nje ya gari naupima huo mlima .
Nikajivuta pembeni kidogo ili kuzuia wale wakaka wasisikie mana walikuwa pembeni tu ya ile njia kuna mti ...
"Sasa....Vero mbishi wewe embu chukua Boda hapo "
"Mmh sio kweli.... kuna wakaka hapa wavuta bangi wamechokaa yaani ukiwaona tu wamekaa ki wizi wizi unataka nikute wameiba hadi siti za gari Jamani mmh "
"Hahah .... hamna kitu kama hicho bwana embu njoo, basi pandisha nayo!" Kupandisha nayo siwezi, na kuacha siwezi
"We umehamia hapa una wiki tu huna unaemjua sehemu enyewe uswahilini mpaka basi... kwanza hujawaona hata hawa wahuni hapa wamepinda wanavuta tu bangi mmh .....Tinner haya ni majizi mwenzangu tena majambazi kabisaaa wasuje niondolea mataili ya Gari mie nitafanyaje ...."
"Hahahah .....Yaani Veroo , Dalali alinambia huku wahuni wengi ila sio wizi bwana we njoo"
"Hap......" nilikuwa naongea huku nageuka kutazama nyuma mana nilihisi kama kuna mtu hivi, Hamadiii mbona nilihisi kutetemekaaa nyieee
Kuna mkaka alikuwa nyuma yangu ameegamia mti, Tukakutanishana nae macho jamani Aibuuu, Moyo ulipiga paaa!! Hivii amesikia nilio kuwa naongeaa auu?? Mungu wangu weee weee mbona nilibabaikaaa nikaanza kujichekesha chekesha kwa Tinner maneno yotee yamekimbiaa...
Itaendelea.....
Umesoma kwa utulivu Β· dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi from-bangi-to-baby-sehemu-ya