VYOTE NDANI GONGA94
MY WANGU❤️ sehemu ya 9
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Eeeeh . Mama aksema jamni baba nikushuruje ww. Umezaliwa na mama mzuri sana.mungu abariki sana tumbo lake nashukuru baba. Sir mlige akasema usijali mama . Sasa kwa hili suala niliona siwezi kumueleza baba. Hapana ila wala usijali nataka faridah awe katika mazingira mazuri tu. Kisha sir mlige akavuta droo ya meza.kisha akatoa pesa .nakumbuka alihesabu laki 2. Akampa mama. Nyie mama hakumini. Sir mlige Akasema mama mimi nataka apate fomu nzuri na vitu vyake vyengine vyote vya shule. Apate begi na viatu. Ili akiferi nimdunde vizuri.asiwe na kisingizio chochote . Looooh apo akanikata mjicho uooo.mi nikainama chini.
Mama akasema baba akiferi mvunje kabisa .we mwalimu una moyo sana na una roho nzuri mungu akupe sana na mungu akupe zaidi. Mlige akasema asante mama.ndo nilikuitia ayo tu. Mama akasema asante sana. Basi mama alimshukuru jamani. Yani alimshukuru mni kama kapewa milion. Baada ya apo . Mama akaaga sasa. Akanmbia we faridah baki muache mama aende. Basi kweli mama akenda. Sir mlige akaningalia sana. Mpka nikajistukia jamani. Akanmbia nimekusamehe ile adhabu ila ukichelewa tena nitakuvunja. Alafu kuanzia leo pesa ya kutumia mda wa saa 4 unakuja kuchuua kwangu. Kila asubuh mapema tu sawa. Nikasema sawa mwalimu asante sana nashukuru kwa wema wako. Akanmbia sawa nenda darasani
Basi mie taratibu nikaingia darasani. Mh nikamuona ni mwema kumbe uyu baba. Huenda ni mkari lakini ana roho nzuri sana jamani.basi kama mnavyonijua siwezj kuvumilia kitu nikamsimulia yusta kuwa mwalimu kanisaidia kipata fomu za shule begi na viatu. Na pesa ya matumizi kila siku. Mh yusta akanambia sio ww tu. Kuna wengine nimesikia kawanunulia viatu .na wengine kawanunulia mashati. Na yule jmal mlemavu wa form 2 nadikia kamnunjlia kile kiti anachotembea nacho sasa hivi. Ila mm kanipiga jana kanitibua tu. Naliona kama libwege tu. Nikacheka sana .nikasema basi akipita muite bwege. Akasema weee unataka aniue akaa nikome mie. Ninacheka kwa sauti sana .
Na mchana nilivyorudi home mchana jamani.nilifikia kwa fundi. Mama ana kihere here. Nikaenda kupima fomu. Mana mama alishanininjlia vitambaa na kila kitu. Nikaona kaninunulia begi zuri jamani . Viatu .mpaka chupi mama kaninunulia .na niliishiwa jamani. Yani mpkaa nilikuwa navaa chupi kisha naifunga kwa pembeni nyie maisha ayaaa acheni.basi nilifurahi mno mwenzenuu. Yani nilifurahi sanaaaa
Basi ata baba. Alifurahi sana .akasema akipata mda atakuja kumshukuru mwalimu mlige. Mie nikasema swa na jioni sana nikaenda kuchukua fomu zangu kwa fundi.basi kesho yake niliingia shule nna kila kitu kipya na nilipendeza jamani. Mm ni mzuri mno matunzo tu. Ila. Hii siku niliwaka na fomu zangu.mpaka yusta alioniona alinambia dada unawaka mno .kama umevaa shera kumbe nguo za shule yani umependeza nikawa nacheka tu. Yusta akanmbia we ushaenda kwa mwalimu kuchukua pesa ya matumizi si alikwambia. Nikasema hapana ila mama kanipa pesa leo ilibaki jana. Mh yusta akanmbia we fala nn nenda kachukue ela uko. Tunakuwa nazo nyengi tunakula tunachotaka nikacheka .shoga yenu nikaenda kwa mkuu
Basi nikagonga mlango .na akanikalibisha nikamsalimia vizuri. Akaitikia kisha akanmbia. Umependeza sana naomba uzidi kusoma na uzidi kuwa smart sawa. Sio unachukua hela zangu ala alafu uzingue .ntakuvunja.nikabaki kimya .akavuta pochi kisha akanipa elfu 5. Mh sikuelewa ni ya siku moja au ya week nzima .ila nilishindwa kumuuliza kwa kweli.nikamshukuru sana pale.akanmbia ebu nenda darasani bwana . Kushukuru gani kila saa.nikajikuta nimetabasamu na nilipomungalia na yeye nikakuta anatabasamu woow. Nyieeee ndo ilikuwa namuona kwa mala ya kwanza anatabasamu uyu baba. Acheni kabisaaaaaa
🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi my-wangu-sehemu-ya
