VYOTE NDANI GONGA94
NILIZANI AMEFIA GETO....01
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Nyie nyie, acheni tu yaliyonikuta…
Jina langu ni Ismail, ingawa wengi wanapenda kuniita Suma. Mimi ni fundi magari, nafanya kazi kwenye gereji moja kubwa kule Mikocheni.
Siku hiyo nilikuwa natoka nyumbani, maeneo hayohayo ya Mikocheni, ingawa nyumbani kwangu kuna umbali kidogo kutoka gereji ninayofanyia kazi.
Nilikuwa natembea taratibu, nimevaa earpods nikisikiliza muziki huku nachezea simu yangu.
Njiani nikapishana na gari fulani, nikaendelea na safari yangu.
Haikuchukua muda mrefu kabla rafiki yangu, ambaye pia tunafanya kazi pamoja, akanipigia simu.
Akanambia kuna gari lina shida karibu na maeneo ninayoishi, na kwakua sijafika kazini basi nitakua bado sijatoka nyumbani hivyo atanipa namba ya mwenye gari ili nisaidie kuangalia tatizo.
Nikamsikiliza vizuri, nikasimama pembeni nikisubiri anitumia namba. Ghafla simu yangu ikaanza kuita.
Nikapokea, nikasema “Hello…”, sauti ya kike. lakini kabla sijaongea sana nikageuka nyuma yangu na kumuona mwanamke amesimama karibu na lile gari nililolipita muda mfupi uliopita.
Nikamuomba anipe maelezo mafupi kwanza ili nijiridhishe, nikasogea karibu naye tusikilizane vizuri.
Nilipothibitisha kuwa ndiye aliyekuwa ananitafuta, nikakata simu. Tulisalimiana kisha nikamuuliza shida ya gari. Akanambia limezima ghafla tu bila dalili yoyote.
Nikaanza kulikagua, na baada ya kama dakika tano hivi nikagundua tatizo la awali. Nikamwambia:
“Hii gari inaonekana imekaa muda mrefu bila matumizi. Itakuwa vizuri zaidi kama utaniruhusu niipeleke ofisini nikaiangalie kwa ukaribu.”
Akatizama saa yake, kisha akauliza, “Unaweza kuitumia muda gani kuichunguza? Na je, naweza kuipata baada ya muda gani?”
Nikamuambia ukweli mtupu: “Siwezi kukupa ahadi yoyote mpaka nikiichunguza vizuri.
Nikikuahidi sasa nitakuwa nakudanganya.”
Akatabasamu kidogo kisha akasema, “Sawa basi, twende ofisini kwako niifahamu, halafu nitafanya maamuzi.” nilihisi kama ananilaghai kwa kutokujua ofisni kwangu lakini sikutaka. Kujua namba ya rafiki yangu aliipataje..
Nikachukua ile gari nikaendesha hadi ofisini. Nikaanza kuifungua baadhi ya sehemu na hapo nikagundua kuna vifaa kadhaa vilikuwa na tatizo, na vilihitaji kubadilishwa kwa vipya. Nikamueleza kila kitu kwa uwazi, nikamwambia kama atanunua vifaa haraka basi ndani ya siku moja na nusu gari litakuwa tayari.
Alinishukuru sana, kisha akanipa pesa ya usumbufu pamoja na fedha ya kununua vile vifaa nilivyoviorodhesha.
Kwa kweli, sikuamini. Msichana mdogo kama yule, anatembea na pesa nyingi hivyo ndani ya gari! Cha kushangaza zaidi, akanipa pesa yote ile siku ya kwanza kabisa ya kufahamiana, bila hata kuonyesha wasiwasi kama naweza kutoweka nazo. Sijui kama aliniona mtu mwaminifu au ni roho yake tu ilikuwa safi.
Aliniomba namba yangu ya simu, nikampa, kisha akaondoka akiniachia ahadi ya kurejea kesho yake mapema.
Baada ya kuondoka kwake, nilikaa chini kidogo nikishusha pumzi, nikijaribu kuielewa hali.
Nikajikuta nikimfikiria yule msichana kwa namna alivyoumbika…
Kwanza alikuwa mrefu, karibu kama twiga, rangi yake kama chotara fulani hivi. Umbo lake namba nane, kati kwa kati—sio mnene wala mwembamba. Wataalamu mnajua ninachomaanisha.
Alikuwa mrembo sana, sura ya kitoto iliyopambwa na macho yaliyolegea taratibu, kipua kidogo cha kupendeza, na midomo laini yenye mvuto wa ajabu.
Kwa kweli, muda wote ule nilikuwa bize na kazi, lakini macho yangu yalikuwa yanamfuata kwa kuibia. Nilijikuta nikijiuliza kimoyomoyo… je, kweli nimekutana na binadamu wa kawaida, au malaika aliyeshuka duniani?
Usikose Itaendelea. ..
Umesoma kwa utulivu · dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi nilizani-amefia-geto