kisha aliniachanisha na kugeuka ndipo aliponiona mimi akasema:
"Laura?
"Ndio mimi Laura "
"Mbona upo hapa mpaka sasahivi si mmeruhusiwa kuondoka wewe imekuwaje umebaki hapa?
"Nilikuwa nakungoja wewe General"
"Mimi, kwanini?
"Nilikuwa nataka kuongea na wewe General"
"Haya niambie unataka kuongea kitu gani Laura?
"Nikweli nakupenda sana General, japo nilikuwa nazikataa hisia zangu zakweli, lakini tangu umeondoka kambini hisia zangu juu yako zimezidi kuongezeka, nimeteseka sana sili silali nakumis sana mwenzio, kunamuda nilikuwa nalia tuu nikitamani kukuona ata kukusikia tuu japo sauti yako, moyo wangu umeondoka nao General nisamehe mimi nakuhitaji mno"
Niliongea huku nikilia kwa hisia zandani ya moyo, General alinitizama kwa romantic sana kisha alinivuta na kunikumbatia, kisha akaniambia:
"Haya ingia kwenye gari tuondoke sasa, au unamsubili mjomba wako"
Alinifungulia mlango wa gari, kisha nikamjibu:
"Hapana nilimuambia atangulie, kwani nakusubili wewe kunajambo nataka kuliweka sawa"
"Wow! Mbona hujamuambia ukweli unaenda kulipambania penzi lako eeh! Hahahaaa"
Aliongea kwa utani tukacheka wote kwa pamoja, tuliingia kwenye gari na kuanza safari ya kurudi mjini Dar-es-Salaam, akaniambia:
"Laura kiukweli nilijua nimekupoteza, nilihisi kuwa nilikuwa najidanganya mwenyewe kwamba unanipenda, na kumbe haukuwa unanipenda kweli, hakuna siku nilijisikia vibaya kama ile siku uliyiniambia hunipendi nawala hutokuja kunipenda, niliumia sana sikufichi na machozi yalinitoka nilijikuta nalia kwa mara yakwanza, sijawahi kumlilia mwanamke ila ulinifanya nilie wewe, na hata nilipo ondoka nilikuwa najitahidi sana kukufuta kwenye kumbu kumbu zangu, hata nilipokuja hapa sikutaka kukuona kabisa, ndio maana nilipo maliza kilichonileta hapa nikaingia haraka kwenye kikao, ili nilitegemea nikitoka nitakukuta umesha ondoka kabisa maeneo haya, asante mungu kwa marahii naona umenipa kile nilichokuwa nakitaka nilichokuwa nakiota sikuzote, Laura nakupenda sana hujui tuu"
Aliongea na kunitizama usoni kwa macho yake mazuri, kisha alinyanyua mkono na kunishika usoni kwangu, huku akiwa ananitizama kwa macho yamahaba, nilijikuta machozi yananitoka kwa raha niliyokuwa nayo, nikamuambia:
"Ethane siamini upo namimi hapa leo hii hapa, Ethane hujui tuu nilifikia hatua kila alieniona kambini aliniona kama nimechanganyikiwa, nilikuwa kichaa kwaajili yako, namshukuru sana Nancy kwani alikuwa nami bega kwa bega kuhakikisha namalizia mafunzo yangu, sizani kama ningefika leo hii hapa nahisi hata ningefukuzwa kambini au ningekufa, kwani nilidhoofika kabisa sikuwa nakula wala kulala mimi mwenzio, sikujua kama mapenzi ndio yananguvu namna hii, nilichukia huu ulimwengu ulioniingiza alafa sikuoni kabisa nilikuwa gizani pekeangu"
"Ssshii"
Alinishika mdomo na huku akinizuia nisiendelee kuongea huku machozi yalikuwa yakimtililika, akaniambia:
"Nipo hapa sasa sitaki kuona huli wala hulali, nataka kuona tabasam lako tuu, mimi ndio taa yako kwenye huu ulimwengu mpya haupo mwenyewe tena, sawa kipenzi changu"
Niliinuka nanilivyo mwembama sasa, nikaenda kumkalia miguuni huku akiendesha gari , nilimkumbatia kama mtoto mdogo huku nikimbusu kila mahali, nampenda sana General Ethane, aliniambia:
"Tulia hapa siku zote, kwani hapa kifuani kwangu ndio sehemu sahihi kwako tulizo lamoyo wako, namimi pia"
"Asante sana Ethane, upo sahihi kabisa"
Aliendesha gari kwa kasi sana niliwa nimetulia tulifika sehemu moja njiani nimaharufu kwa chakula General aliingiza gari hapo na kupaki, kisha alifungua mlango na kunifungulia nishuke, akaniambia:
"Nataka nikakulishe mtoto mzuri, maana sitaki kuona unapitia kipindi kigumu tena, wakati upo namimi sawa?
Nilitabasam kisha alinishika mkono baada ya kufunga mlango wa gari, na tuliingia moja kwa moja restaurant, hapo tuliandaliwa meza nzuri na muhudumu kisha walitusikiliza nini tunataka, General aliniambia:
"Kipenzi changu agiza chochote unachotaka kula sasahivi, nitakulisha"
Kiukweli General alikuwa ni mkaka mwenye mahaba sana, kwa kumtizama tuu yaani utajua, na ndio maana wadada wengi wamekuwa wakivutiwa kuwa nae, lakini bahati mbaya hakuwa anapenda kujiingiza tuu hovyo kwenye mahusiano, mpaka alipokuja kukutana namimi, japo kuwa nilikuwa namkataa ila kiukweli moyoni nilimpokea kwa mikono miwili kabisa, na kumkaribisha ndani ya uvungu wa moyo wangu, nampenda mpaka mimi mwenyewe najishangaa, basi bwana chakula kililetwa hapo, nikataka kuanza kula lakini General akanianbia:
"Nilisema leo nakulisha mimi, hivyo tulia hivyo hivyoo sawa"
Nilitabasam nakuitikia kwakichwa, kisha alinawa mkono General na kuanza kunilisha, tena huku akikipuliza kwa mdomo wake kwanza ndio ananilisha kama mtoto, na kunifuta mdomo vizuri yaani achatuu, nilikuwa naona aibu lakini General ndio kaamua, wakati tunakula hapo muda ulikuwa umeenda, General akaniuliza:
"Unakaa dar sehemu gani mpenzi?
"Mimi nakaa maeneo ya kunduchi, wewe je?
"Mimi naishi dodoma ila hapo dar huwa nafikia kambini, nitakupeleka hadi kwenu usihofu, alafu nyumbani unaishi na nani?
"Mimi nilichukuliwa namjomba tangu nikiwa mdogo, mjomba na mkewe wamenilea kama mtotowao wakuzaa"
"Ok vizuri"
Tuliongea huku akiendelea kunilisha chakula hapo muda huo wakati General ananilisha kumbe mjomba nae alishuka hapo kula alishukudia General akipuliza chakula nakisha akanilisha mjomba aliganda akinituzama nilishtuka nilipomuona nilishindwa hata kujitetea
Je unavyo dhani mjomba wake Laura atafanyaje na kushuhudia kabisa Laura analishwa kimahaba na General nini kitatokea endelea kuifuatilia.............
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni