LOVE BETWEEN US (Upendo kati yetu) Xxxxxx++++++xxxxxx++++++xxxxxx 1 - - - - - - - - 5 SEHEMU YA 1
Katika mtaa mmoja wa Uswahilini uliochangamka sana, kilionekana kikundi cha wanawake watano waliovalia vijora wakiwa wamemzunguka msichana mmoja.
Ilikuwa wazi walitaka vita.
“Nyooo, emu jiangalieni kwanza juu mpaka chini au angalianeni kwa zamu mjithaminisheni wenyewe msiseme nawasingizia bureee,” aliongea yule dada huku ameshika kiuno na kuwaangalia kwa dharau.
“Hua mnajiangalii kwenye vioo kweli nyie mkiamka asubuhi au mkienda uko kwenye vigodoro vyenu?
Maana kwa mabwana wa maana hamnao tuseme tu ule ukweli.
Ningesema mnajiangalia kwenye vioo mkipaka wanja kwenda kwa hao mabwana zenu halafu niangalieni na mimi juu hadi chini tena msiniangalie kwa jicho la woga niangalieni vizuriii.
Ngoja nigeuke na nyuma maana hamjaniona vizuri bado,” aligeuka huku anatingisha wowowo lake.
“Mmmh, hilo tako la Mchina ndo unatulingishia sisi tunayo ya kwetu tangu tunatoka matumboni mwa mama zetu tumebarikiwa sio kama nyie mnaolazimisha uzuri ovyooo,” aliongea dada mmoja mweusi, si haba nae alikuwa mzuri.
“Weeee jishikilieee binti wewe cheusi mangara, acha kuniangalia kwa woga kitu natural hichi ukiniangalia mie ni wa kufoji mambo mimi sifosi vitu kama nyie… mpooo,” aliongea yule dada waliyemzunguka kwa kujiamini.
“Umeendekeza umalaya tu hapa mtaani nani asiyejua umemchukua bwana wa Chausiku na Mwantumu na hizo pesa unazokula zitakuja kukutokea puani shenzi wewe,” aliongea dada mwingine huku anamsukuma kichwa.
“Taratibu na kichwa changu.
Nywele tu nimesuka kwa elfu 50 na kwanza hao mabwana zenu wananifata wenyewe sikumuita mtu eee mpooo.
Na kwa taarifa yenu hao mabwana zenu wananuka shombo si shombo hawana mbele wala nyuma na sijawahi kula senti tano yao.
Mtoto mzuri napendeza kwa pesa zanguuu.
Mmmh habari ndo hiyo mtavuta midomo mpaka ifike miguuni mwaka huu.”
“Acha kujitetea mbweha wewe kila mara kujipitisha kwenye vijiwe vya kahawa ili tu usimamishwe nani asiyekujua.”
“Akaaah mimi ni wa kunufananisha na nyie vikaragosi tena nawatuma mfikishe ujumbe tena msipunguze neno labda muongeze yenu.
Siku ile mliona mmeniwezaa wenyewe kwa taarifa yenu niliwastahi tu.
Nendeni kamwambieni huyo malkia wenu karaba huyo Chausiku kwamba namsubiri kwa hamu.
Hii ndo timu ya mtu tanoo japo mmenikuta leo pekeangu wala siogopi kitu.”
Yule dada aliwapiga kikumbo akaondoka.
Ruby ndo jina nililopewa na wazazi wangu ila kwa mtaani wamenizoea kwa jina la Ru na wengine huwa wananiita Baby Ru.
Wengine wananiita Baby Face na hili ni maarufu sana kwa vijana wa kiume hapa mtaani.
Ukiulizia Ru Mcharuko au Ru Baby Face hata mtoto wa miaka miwili anakuleta nyumbani kwangu bila hata kukupoteza.
Nyumbani kwetu sisi tumezaliwa wawili tu mimi na pacha wangu Rose.
Rose yeye ni mzuri mashallah nisiache kumsifia na mie huwa nikisifia kitu ujue uhakika kiko vizuri.
Ni mzuri wa sura na tabia pia alafu ni mpole kinyume kabisa na mimi.
Mdomo wangu huwa siwezi kabisaaa haipiti siku sijacharuana na mtu.
Siku ikiisha hivi hivi wala sioni kama siku yangu imekamilika.
Basi bhana sisi kwetu tumelelewa kigeti kali zaidi kusema ule ukweli.
Baba yetu Mr Alphonse ni mfanyabiashara mkubwa sana na mama yetu ni mama wa nyumbani tu ila ana saloon za kike za hadhi ya juu pamoja na maduka ya nguo za kike.
Baba anampenda sana Rose kuliko mimi na upendo wake ni wa wazi wazi kabisa kwa sababu Rose alionyesha jitihada katika masomo mapema na kwa sasa yupo nchini Marekani kumalizia shahada yake ya biashara.
Ila mimi sikua najiweza kiivyo ila niligoma kwenda chuo cha biashara nilitaka kwenda chuo cha mitindo Marekani pia lakini baba alikataa kunisomesha kama msimamo wangu utabaki pale pale.
Ila ninachoshukuru ni kwamba muda wote mama alikuwa upande wangu.
Alinisaidia kupata walimu nilijifunza mambo mbalimbali kama make up kupamba ukumbi wa sherehe na kutengeneza keki namshukuru sana sanaaa.
Alinipa mtaji bhana ndo maana saizi naringa mjini kwa msaada wa mama yangu.
Kwa sasa nina miliki duka la nguo za maharusi za kike na za kiume nina saloon na pia nina bakery natengeneza keki.
Pia nina ka restaurant changu nimekifungua hapa juzi na ninafanya delivery ya vyakula pia.
Pesa ndogo ndogo hazinipigi chenga.
Baba huwa hakai sana Tanzania muda mwingine yupo nje kwenye biashara zake na mimi muda huo ndo nautumia kukaa chumba changu nilichopanga huku Uswazi.
Mama yeye ni mtu poa sana wala hanifatilii sana kwenye mambo yangu ilimradi nipo salama na nina furaha yeye ananipa ruksa tu niishi nipatakapo.
Ila siku nitakayosikia daddy karudi Tanzania napiga mbio nyingi sana kurudi nyumbani.
Huwa hatabiriki ana hasira za karibu na kufoka hovyo hasa kwangu mimi.
“Ruu nimepata habari zako,” alisema Bi Tija jirani yangu.
“Mtaa huu kwa umbea tayari mmepata mkanda mzima na ndo kwanza muhusika sijafika bado.”
“Chezea wewe mtaa huu ila umenifurahisha sana umejua kuwakomesha maana wanajiona huu mtaa wameushika wao kwa uzuri wakati hawana lolote.”
“Hehehe aiiii bora na wewe umeliona hilo nikisema mimi naonekana mbaya ila haya yote yana mwisho nitawakomesha tu.”
“Hicho ndo ninachokisubiri kwa hamu mtaa huu kila siku kelele mara oh bwana angu mara vile kelele haziishi na ukiangalia mabwana wenyewe wapi hao wanaovaa suruali chini ya makalio.”
“Hahaha Bi Tija leo umejua kunifurahisha acha mimi nijiandae nikaendelee na shughuli zangu.”
Nilijiandaa nikaelekea kwenye moja ya duka langu la nguo.
Siku moja mchana kijua cha saa saba kimechanganya kuwaka nilipokea simu kutoka kwa mama.
Akanipa taarifa za baba kurudi nyumbani tena safari hii alirudi pamoja na Rose.
Rose alikuwa amemaliza masomo yake.
“Mama kuwa serious basiiii… ni kweli Rose anarudi leo pamoja na daddy?” niliuliza huku nimeweka mkono wangu kifuani.
SEHEMU YA 2
“Mama kuwa serious basiiii.. ni kweli Rose anarudi Leo pamoja na Dady?” niliuliza huku nimeweka mkono wangu kifuani.
“Ndiyo kipenzi chako Rose anarudi Leo na ufanye haraka urudi nyumbani si unamjua baba yenu alivyo mkali,” mama aliongea kwa sauti ya upole kama kawaida yake.
“Yesssss… hata usijali mama sasa hivi nitakuwa hapo,” nilikata simu haraka sikutaka kumsikiliza tena mama.
Nilifurahi sana kusikia Rose anarudi ni mwaka sasa umepita tangu tuonane.
“Monica nakuachia ofisi unajua nini cha kufanya sito kuwepo kwa muda kidogo usiniangushe,” niliongea kwa msisitizo.
“Sawa dada hata usijali kila kitu kitakuwa sawa siwezi kukuangusha dada angu,” Monica ni msichana mmoja mpole sana na mchapakazi nilimuamini na biashara yangu.
“Okay kama nilivyokwambia,” nilichukua pochi yangu nilienda kupanda bodaboda.
Dakika kumi zilitosha kufika kwenye geto langu, chap nikaoga nikabadilisha nguo nikafunga chumba changu nikampa funguo shoga angu Mboni aniwekee nikasepa zangu.
In short mashoga zangu wanajua kila kitu kuhusu maisha yangu, yani mtu tano Mboni, Sophia, Anita, Grace na mimi mwenyewe ndo tunatimiza kikundi cha mtu tano kusema ule ukweli.
Tulikuwa ni pisi kali za mtaa sio warembo kivile ila tunavishape flani hivi vya kichokozi na tunajua kuvaa na usmart unachangia.
Basi nikachukua boda mpaka nyumbani muda huo nafika mama ndo anatoka kwenda airport kuwapokea.
“Mbona umechelewa sana mimi ndo natoka hivyo.”
“Mama mimi wala sikusindikizi wewe nenda tu mtanikutaga ngoja nibadili nguo nisaidiane kazi na mama Ester kupika mapochopocho.”
“Okay ngoja mimi niwahi,” mama akakubali kwenda mwenyewe wala sio mbishi nampendea hapo tu.
Tukaandaa chakula tukatenga mezani muda si muda waliingia baba mama na Rose.
Nilienda kumkumbatia Rose tulifurahi sana nilimsalimia na baba.
Walienda kuoga tukaja kupata chakula cha mchana tulipiga story nyingi sana.
“Ruby nina zawadi zako chimumy tukimaliza kula tu nitaenda kukupa, mama nimeshampa zawadi zake, mama Ester, Faraja na Yaya Flora nimeshampa pia bado wewe tu aaa na nani vile yule Alex pia nimeshampa zawadi yake,” aliongea Rose huku anatabasamu.
“Awww that’s my sister nakupenda sana sanaaa… mmwaaa,” nilitamani nimalize kula haraka nikapewe hizo zinazoitwa zawadi.
“Mmmh kwa hiyo mimi sipendwi si ndio,” aliongea baba kwa utani.
“Usijali dady wewe mara zote nakupenda sanaaaa.”
“Na mimi je?” akadakia mama tulibaki tunacheka.
“Jaman mimi nawapenda wote na upendo wangu kwenu haupimiki kwa mizani na wote mnazawadi zenu.”
“Apo sawa,” mama aliendelea kula huku anatabasamu.
Nilibaki nakuangalia sana Rose nilitamani sana kuwa kama yeye mpole, mtaratibu na anapendwa na kila mtu.
Baada ya chakula baba alinipa zawadi ya tablet PC na iPhone 14 Pro Max nilifurahi sana.
Nilienda chumbani kwa Rose.
“Muone unapenda zawadi utakuja kuibiwa haya njoo lete lile begi,” Rose aliongea huku anatabasamu kama kawaida yake.
Mimi huyo mbele ya zawadi hata unitumie wapi naenda yani Rose anajua vile vitu napendaga aliniletea viwalo vya nguvu na viatu kama vyote.
“Asante sana twinnie ndomana nakupendaga,” nilimkumbatia Rose kwa nguvu.
“Hata mimi nakupenda pia wakati mwingine tutaenda pamoja Marekani kufanya shopping.”
“Wee nilishangilia kama mwehu hii ilikuwa ni ndoto yangu siku moja kwenda Marekani hata kutembea tu sema dady alikuwa ananibania sana.”
Basi tulipiga story nyingi baada ya chakula cha usiku kila mmoja alienda kulala chumbani kwake.
Asubuhi mapema nilishtuka kumuona Rose yupo chumbani kwangu ananiamsha.
“Wee Ruby… amka basi kipenzi kuna kitu nataka nikuombe bhana acha uvivu,” Rose alinivuta mkono niliamka kwa kujivuta sana nikakaa kitandani.
“Sema basi Rose nataka kuendelea kulala nina usingizi debe,” niliongea huku nimefumba macho.
“Sikiliza sasa Ruby mimi nataka kutoka lakini si unajua baba haruhusu mtu atoke mmoja mmoja sasa tutoke wote nataka kwenda madukani,” sauti ya Rose ya upole na maneno yake yalinifanya nifumbue macho yangu.
“Mmmm hebu kwanza nicheke huna cha madukani wala nini unataka kwenda kuonana na kibwana chako… hicho ki Raphael au nakusingizia?” nilimuuliza Rose huku namkazia macho.
SEHEMU YA 3
Asubuhi mapema nilishtuka kumuona Rose yupo chumbani kwangu ananiamsha.
“Wee Ruby… amka basi kipenzi kuna kitu nataka nikuombe bhana acha uvivu,” Rose alinivuta mkono.
Niliamka kwa kujivuta sana nikakaa kitandani.
“Sema basi Rose nataka kuendelea kulala nina usingizi debe,” niliongea huku nimefumba macho.
“Sikiliza sasa Ruby mimi nataka kutoka lakini si unajua baba haruhusu mtu atoke mmoja mmoja sasa tutoke wote nataka kwenda madukani,” sauti ya Rose ya upole na maneno yake yalinifanya nifumbue macho yangu.
“Mmmm hebu kwanza nicheke huna cha madukani wala nini unataka kwenda kuonana na kibwana chako… hicho ki Raphael au nakusingizia?” nilimuuliza Rose huku namkazia macho.
“Amna hata sio hivyo nataka tu kwenda madukani bhana sitanii nitakununulia na zawadi,” Rose alimbembeleza.
“Uongo tu na hujui kudanganya macho yako mwenyewe yanakusaliti mimi siendi hadi uniambie ukweli,” nilijifanya nataka kulala.
“Basi basi nakwambia usilale mimi nataka kwenda kwa Raphael kweli nipeleke basii hata nusu saa tu litatosha mimi kuwa nae please,” Rose aliniangalia kwa macho yake yanayotia huruma.
“Nyooo nilijua tu sawa unataka twende saa ngapi?” nilimuuliza Rose huku nashuka kitandani.
“Jioni mida ya saa kumi hivi atakuwa tayari ametoka kazini.”
“Okay usijali mie na weye tena,” nilivua night dress nikafunga taulo kwa ajili ya kwenda kuoga.
Rose aliniangalia sana.
“Mbona unaniangalia sana unanitisha ujue,” niliongea kwa utani.
“Ruby una tabia mbaya mimi unamjua shemeji yako lakini mimi huyo shemeji yangu hata simjui hujawahi kunitambulisha tabia mbaya hiyooo.”
“Usijali Rose utakuja tu kumjua mimi pia sijui hata anaonekanaje sasa tunaishia kuchat kwenye messenger basi lakini kitu kimoja cha uhakika shemeji yako ni handsome wakwendaa,” niliongea kwa kuringa kabisa.
“Ni yule yule si ndio?” aliuliza Rose huku amenikazia jicho.
Niliitikia kwa kichwa.
“Wewe kweli kichwa maji mapenzi yenu ya utotoni hadi leo mmeyaendeleza unauhakika hana mwanamke huko wewe jifanye mama maria unamtunzia mtu hujui huko anaishije imepita miaka 12 sasa jiongeze binti,” Rose alisimama kwa hasira.
Sikujua kwa nini alitaka kutoka chumbani kwangu nikamzuia.
“Mbona umekasirika hivyo kama kuna kitu unajua kumuhusu Benjamin si uniambie,” nilimuuliza swali la mtego.
“Nakuonea tu huruma unapoteza tu muda bure kwa mtu kama yule ni wazi atakuwa ameshapata mwanamke wa kizungu huko,” aliongea Rose huku amebinua mdomo.
Nilimuangalia bila kummaliza sikuelewa ni kwanini aliongea maneno kama yale.
“Afu Rose tutagombana sasa hivi nitakuwa sikupeleki tena hizo safari zako.”
“Heee basi na wewe ngoja niondoke nisije nikayabananga bureee usisahau tunamtoko jioni,” Rose aliondoka faster ila aliniachia maswali mengi kichwani.
Yani mimi kweli nina mapenzi ya kitoto tangu nna miaka 13 nilianza kumtumia barua Benjamin.
Tumekuwa wapenzi kwa barua tangu utotoni na sasa bado tunaendelea ila hata hatujui kila mmoja mwenzie amekuwa na kuwa na muonekano gani.
Tulipanga tutakuja kulijua hilo tukionana ana kwa ana.
Basi jioni ilipofika tukajikwatua watoto wa kike tukatoka na gari yetu.
Tulikataa kutoka na dereva mimi ndo nilikuwa na drive.
Tulifika mpaka kijihoteli flani kipo maeneo ya beach tulimuona Raphael kashafika.
Mimi sikutaka kufika alipo kiufupi mimi na huyu kaka damu zetu hazijaendana kabisa.
Tukiongea lazima tuchambane afu sipendi anajiweka rafu sana hata ndevu hanyoi hizo nguo ndo usiseme hajui kupangilia nguo.
Kuepusha shari nilimpungia tu mkono nae alinipungia kama salamu.
“Ruby ndo kweli kabisa unaishia hapa?” Rose aliuliza kwa kulalamika.
“Unajua vizuri kabisa nikiwa karibu na huyo Raphael ni lazima tugombane kuepusha shari ngoja tu mimi nikusubiri hapa.”
“Tabia mbaya tu mfyuuuu,” Rose aliondoka huku amenuna.
Mimi hata sikumjali nilikaa meza nyingine nikawaacha wapendanao wajinafasi nikaagiza kinywaji.
Niliingia messenger nikamtumia message Benjamin alijibu muda huo huo.
Nilifurahi sana sikuwa bored nilikuwa busy kuchat.
Mida ya saa 12 waliagana tukaanza safari ya kwenda madukani kutafuta hizo nguo za kumpoteza maboya.
Mama na baba hatukukaa sana madukani tukarudi nyumbani.
Ile tunafika tu tunaskia baba anaongea na mtu kwenye simu ila anaonyesha dhahiri anafuraha sana.
Tulimsalimia mama tukapanda juu chumbani.
Baada ya kuoga tulishuka kupata chakula cha usiku.
“Mabinti zangu na mke wangu nina habari njema kwenu Mr Wilson ametualika kusherehekea sherehe ya kumkaribisha nyumbani mwanae Benjamin kwa hy…”
Kabla baba hajamaliza kuongea nilijikuta nashangilia kwa sauti kila mtu alibaki ananiangalia mimi.
“Mmmh dady samahani,” nilijishtukia mwenyewe nikaanza kujieleza baba.
“Unajua nimefurahi sana kwa sababu najua tunaenda ile nyumba yao ya shamba kuna ranch kule nimemiss kupanda farasi,” niliongea huku najichekesha.
Ila Rose alikuwa ananiangalia usoni alijua fika kwanini nimefurahi vile.
Hahaha baba alicheka sana akasema sawa usijali binti yangu utaenda kuwapanda farasi hadi uchoke mwenyewe maana tunaenda kukaa kama week 3 hivi.
“Awww dady for real!!!” niliuliza kwa furaha.
“Ndiyo hivyo baba yenu kashasema hivyo,” alijibu mama huku anatabasamu.
Tuliendelea kula huku nikiwa na furaha sana.
Baada ya chakula nilipanda chumbani kwangu nikakuta missed call za mashoga zangu.
Nikampigia Mboni chap nimpe mchapo kwanza wa kukutana na vikaragosi wa Chausiku maana sikupata nafasi ya kuwapa ubuyu na pili kuhusu safari yangu.
Nilipompigia wala hakukaa sana akapokea.
“Shogaa shogaaaa…..” Mboni aliipokea kwa makelele hatar.
“Kwema huko shoga?” ikabidi niulize.
“Shoga huku kwema sanaaaa yanakupita mengi shoga angu tupo timu nzima kasoro wewe kiongozi ila hakijaboa kitu.”
“Mmmh nipeni michapo shoga angu nimeshakaa mkao wa kula,” hapo nahisi kuwashwa kwa umbea natamani nipae nikashuhudie hicho wanachotaka kuniambia.
“Shoga angu Chausiku mchana kweupeee kafumaniwa na mume wa mtu tena lijibaba jituzima haswaa.”
“Akaaah msiniambie kumbe nakosa mengi Ru mimi,” niliongea kwa kulalamika.
“Ndiyooo unakosa mengii,” nilisikia sauti ya Sofia.
Nilicheka sana.
“Na huyo kin’gora nae haya mpiti looh usiende kwenu kulala.”
Tumezoea kumuita kin’gora kwa sababu anakasaiti kembamba hatari lakini kwenye kuchamba nambari moja tena hakubakishi anakumba vichambo vya hela yote.
“Ndiyo yupo yani hapa tumechoka kwa kuchamba mtu ilibidi tumsaidie Bi Mtumwa kumfunzia mtu adabu.”
“Hahaha kama namuona uso ulivyomshuka pyeeeeee vipi kikundi chake wakina Cheusi Mangara walikuja kumsaidia?” niliuliza huku nakaa vizuri.
“Weee waje kumsaidia wagundue nini hawajaleta hata pua zao.”
“Haya bhana mashoga zangu mmenikosha hatari enheee kidogo nisahau harafu juzi si ndo nikutane na Cheusi Mangara na Joana wakajitia kunibinulia midomo nilisema niwaache lakini nikasema hataa watanizoea niliwachamba afu nikawapa na ujumbe wa huyu malkia wao Chausiku.”
“Weeee usitwambieee shooo kwa hiyo kumbe uliwatembezea dozi pekeako.”
“Hehehe mimi tenaaa si mnanijua nilivyo kama pele lililoiva ukinigusa tu tayari habari yake utaipata,” niliongea kwa kuringa kabisa.
“Hongera kiongozi ngoja sisi turudi nyumbani tukaoge kwanza maana tangu mchana tupo huko tunachamba mtu chezea wewe kilikodiwa hadi Kigoma.”
“Hahaha basi mimi nisiwachoshe mashoga zangu mie nataka kuwaaga mwenzenu sitokuwepo kama week 3 hivi kwa hiyo chumba changu nawaachia chukueni mnachotaka ila halahala dressing table yangu msiisogelee foundation zangu na marembo yangu niyakute kama yalivyo ila chakula nguo pochi na viatu vitumieni tu kama mnavihitaji.”
Nikaskia Mboni anawaambia “mmeskia boss lady alichosema kasema kila kitu ruksa kutumia.”
Nikaskia “woyoooooo umeua madam Ruu.”
Nilibaki kucheka nikawatakia usiku mwema nikaikata simu.
Siku hiyo nilikuwa na furaha sana nilimuwaza sana Benja wangu nahisi yeye pia nilikuwa kichwani kwake.
Mara nasikia message inaingia messenger niliidaka simu kama mbwa kaona mfupa.
Nilitabasamu kuona message inatoka kwake.
Tulichati sana hadi nikapitiwa na usingizi.
SEHEMU YA 4
“Hahaha basi mimi nisiwachoshe shoga zangu, mie nataka kuwaaga mwenzenu sitokuwepo kama week 3 hivi kwa hiyo chumba changu nawaachia chukueni mnachotaka ila halahala dressing table yangu msiisogelee foundation zangu na marembo yangu niyakute kama yalivyo, ila chakula, nguo, pochi na viatu vitumieni tu kama mnavihitaji.”
Nikaskia Mboni anawaambia, “Mmesikia boss lady alichosema, kasema kila kitu ruksa kutumia.”
Nikaskia, “Woyoooooo umeua Madam Ruu.”
Nilibaki kucheka nikawatakia usiku mwema nikaikata simu.
Siku hiyo nilikuwa na furaha sana nilimuwaza sana Benja wangu nahisi yeye pia nilikuwa kichwani kwake.
Mara nasikia message inaingia messenger niliidaka simu kama mbwa kaona mfupa.
Nilitabasamu kuona message inatoka kwake.
Tulichati sana hadi nikapitiwa na usingizi.
Niliamshwa asubuhi sana mida ya saa 11 na mama.
“Ruby kipenzi amka ukaoge ujiandae Rose ameshajiandaa mwenzio tunaanza safari mida ya saa 12 ili tuwahi kufika,” mama aliniamsha taratibu hakutaka kunishtua unaweza sema ananibembeleza.
“Sawa mama ila mimi sijapanga hata nguo itakuwaje sasa,” niliongea huku napikicha macho.
“Hilo tu hata usijali Rose ameshakupangia nguo unazozipenda kwenye begi wewe jiandae unywe chai tuanze safari.”
“Okay mom naenda,” nilikurupuka.
Dakika 2 nilikuwa nimeshamaliza kuoga siku hiyo sikuoga kirembo nilijimwagia tu maji nikavaa chap nikatoka.
Nilimkuta baba na Rose na mom wanapata kifungua kinywa na mimi nikajiunga nao.
Baada ya kifungua kinywa tuliwaaga Mama Ester na Yaya Flora pamoja na mlinzi.
Baada ya hapo tulianza safari.
Muda wote kwenye gari nilikuwa nachat na Benjamin muda wote na tabasamu tu kama mwehu.
Na muda huo mama yuko busy kupiga story na dereva safari isiboe dereva asije akasinzia bureee.
Na Rose alikuwa anachat na mpenzi wake Raphael.
Safari ilichukua masaa matano mpaka kufika nyumbani kwa bwana Wilson baba ake Benjamin.
“Wow hata hapajabadilika pazuri sana,” nilijiongelea mwenyewe huku natabasamu.
Tulishuka kwenye gari kwa kujivuta tulikuwa tumechoka hatari.
Tulikaribishwa na sura za watu wenye furaha sana.
Alikuwa Mr Wilson na mkewe Bi Naomi.
Japo imepita takribani miaka 12 lakini wanaonekana vijana kabisa.
“Oh Mr Ellison karibuni sana,” alikuja Mr Wilson akamkumbatia baba alimpa mkono mom kama salamu.
“Karibu sana shemeji.”
“Asante sana shemeji,” mama aliitikia huku anatabasamu.
Alikuja Bi Naomi alimkumbatia mama kwa nguvu ni marafiki wa muda mrefu.
“Si amini kama Angelica wangu yupo hapa tena kaja na mabinti zake warembo sana,” alitusifia na kutukumbatia pia.
“Karibuni sana vyumba vipo tayari itakuwa mmechoka sana mkaoge mpate chakula ili mpumzike,” alisema Mr Wilson.
Tulipewa kila mtu chumba chake palikuwa pazuri sana sanaaa.
Baada ya kuoga tulishuka chini kupata chakula.
Kulikuwa kunafanyika kama kasherehe kadogo ka kutukaribisha kabla ya sherehe ya kumkaribisha Benjamin.
Baada ya chakula tulienda kupumzika mimi na Rose tuliwaacha wazee wakikumbushana mambo yao ya enzi hizo za ujana wao.
Usiku huo sikuchat sana na Benjamin kama ilivyo kawaida yetu.
Ila nilijikuta namuuliza swali.
“Ola kipenzi ivi ukiniona utanijua kweli maana tumeonana tangu wadogo sana?”
Tulikuwa tunatumia nickname yeye alitumia Ola Wilson na mimi alinijua kwa jina la Ry Ellison.
“Mmmm swali gani tena hilo mpenzi wangu?” Benjamin aliuliza.
“Honey au nikwambie tu mimi jina langu halisi ni nani eti,” sikuwa na amani kabisa nilitamani kumwambia tu ukweli.
“Jaman babe huniamini au? Mimi hata bila kuniambia utambulisho wako ni nani kati ya wale mapacha wawili nakujua siku nyingi ndiyo maana nilianzisha haya mahusiano na wewe kwa miaka 12. Usiwe na shaka moyo wangu unadunda ukilitaja jina lako kila siku. Siku tukionana hata kama hatutazungumza ila macho yetu yakitizamana tutaelewana kwa sababu mioyo yetu inaongea lugha moja ya mapenzi.”
Message ya Benjamin niliisoma kwa mapozi nilijikuta natabasamu kwa maneno yake matamu.
“Honey natamani kukuche mapema nikuone mbele ya macho yangu,” nilituma message huku machozi yanatishia kutoka.
“Usijali mpenzi utaniona na nitakuwa wako wa milele,” alijibu Benjamin.
Nilijikuta nacheka kama chizi.
“Okay honey usiku mwema.”
“Na kwako pia malkia wangu,” alijibu Benjamin.
Niliweka simu nikalala nikiwa na amani moyoni.
Kesho yake asubuhi niliamka mapemaaa nikaenda jikoni kusaidia kufanya maandalizi ya sherehe.
Bi Naomi mama wa Benjamin aliniona jikoni akanisifia sana.
Alisema anatamani apate mkamwana kama mimi mcheshi nina heshima na pia najua kupika.
Basi hapo kichwa naliona linazidi kuwa kubwa kwa sifa.
Nilijihisi nimeshapita kwa mama mkwe tayari sasa presha ya nini.
Tulimaliza maandalizi kama mida ya saa nne hivi.
Mida hiyo ndiyo Rose anatoka kuamka.
Alishuka chini kupata kifungua kinywa na mimi nilienda kuoga ili nijiunge nao.
Tulipata kifungua kinywa na story za hapa na pale.
Mama Naomi alikuwa ananisifia sana.
“Binti yako Ruby yuko vizuri sana ni hodari kwakweli ameamka mapema sana amesaidia kuandaa vitafunwa na maandalizi yote ya sherehe kanishinda hata Mama Mjengo,” alisema Bi Naomi huku ananiangalia.
“Vipi Angelica hautatupa binti yako kama mkamwana wetu?” Mr Wilson alimuuliza mama.
Wote walibaki kucheka.
Ila kwa upande wa Rose alionekana tofauti kidogo hakufurahia kama zamani.
“Inategemea kama watoto wakilidhia sisi wazazi hatuna kipingamizi,” mama alijibu huku anatabasamu.
Nilianza kuona aibu.
“Nitafurahi sana na watapendezana sana kweli,” Bi Naomi aliongea anatabasamu.
Rose alibinua mdomo ndiyo mara ya kwanza namuona akaifanya hivyo.
Hakuchukua muda sana tuliskia surprise.
Watu wote tuliokuwepo mezani tulishtuka na kusimama kwa pamoja.
Mbele yetu alisimama kaka mrefu rangi ya maji ya kunde tunaita brown ana mwili wa mazoezi kiasi handsome balaa.
Hilo tabasamu sasa nilijihisi kupagawa.
Akili yangu ilitoa majibu huyu ni Benjamin wako.
Nilimuangalia huku uso wangu umepambwa na tabasamu pana.
Alisalimiana na baba yake na mama yake na baba na mama pia bila kusahau wafanyakazi wa pale nyumbani.
Alikuwa akimtania sana Yaya Jane mfanyakazi aliyemlea tangu akiwa mdogo.
“Yaya Jane nimerudi sasa mume wako ujiandae sasa kuvaa shela,” alisema Benjamin huku ameshika mikono ya Yaya Jane.
Watu wote walikuwa wakicheka kwa matani ya Benjamin.
“Mambo zenu warembo,” Benjamin aliangalia upande wetu.
“Poa,” niliitikia huku anatabasamu.
Alinipa mkono tukasalimiana nikasema mambo.
Nilijisemea sindiyo hayo ameshanijua mali yake.
Lakini nilibaki mdomo wazi alipofika kwa Rose.
Alimpa mkono kumsalimia kisha akampa kiss.
Weee nilihisi moyo wangu unataka kutoka.
Na kwa jinsi alivyokuwa anamuangalia nikasema kwisha habari yangu.
Alimuangalia kwa macho yaliyojaa upendo.
Nilitamani kumwambia Benja sio huyo ni mimi baba angu umekwamia wapi kunijua.
Ila nikasema ngoja nisubiri labda nahisi tu vibaya.
Lakini kila muda ulivyozidi kwenda ndivyo nilivyozidi kumuona Benja alivyojenga ukaribu sana na Rose.
Niliumia kusema kweli.
Ikafika mpaka jioni ambapo Rose na Benja walikuwa hadi chumbani.
Mimi nilikuwa kimya tu.
Sherehe zikaanza pale keki ikakatwa.
Kulikuwa na watu wengi sana waliohudhuria.
Kulipofika upenyo nilimvuta Rose pembeni.
“Wewe Rose Benjamin kakwambia nini anahisi wewe ni R sio? Namaanisha anahisi wewe ndiyo mimi?”
Nilikuwa namuuliza mara mbili mbili.
“Ndiyo anahisi hivyo yani inachekesha,” Rose alinijibu huku anacheka kama kinachotokea ni kizuri.
“Sasa itakuwaje Rose mimi namfuata Benjamin namwambia kakosea R ni mimi sio wewe,” nilisema.
Nilitaka kuondoka Rose alinivuta mkono kwa nguvu.
“Hapana usifanye hivyo usiwe na haraka kipenzi acha tumpe muda tumtest tuone atachukua muda gani kujua ukweli. Usijali kila kitu kitakuwa sawa acha wivu wivu hadi kwa pacha wako,” Rose aliongea huku ananikumbatia.
Nilifikiria mwisho nikafanya uamuzi.
“Sawa mimi nitakaa kimya kama sioni chochote lakini niahidi utamwambia ukweli.”
Nikakubali.
Nilikuwa namuamini sana Rose kuliko hata ninavyojiamini mwenyewe.
SEHEMU YA 5
Ndiyo anahisi hivyo yani inachekesha
"Rose alinijibu huku anacheka kama yanayotokea ni mazuri"
"sasa itakuwaje rose mimi namfuata Benjamin namwambia kuwa kakosea R ni Mimi na sio wewe"
nilitaka kuondoka rose alinivuta mikono kwa nguvu
"Hapana usifanye hivyo usiwe na haraka kipenzi acha tumpe muda tumtest tuone atachukua muda gani kujua ukweli , usijali kila kitu kitakuwa sawa acha wivu ,wivu hadi kwa pacha wako"
rose aliongea huku ananikumbatia niliwaza mwisho nikafanya uamuzi
"sawa mimi nitakaa kimya kama sioni chochote lakini niahidi utamwambia ukweli"
nikakubali nilikua namuamini sana rose kuliko hata ni avyojiamini mwenyewe
"Kwa Hilo tu hata usijali ruby wangu"
rose aliniacha akarudi kwa Benjamin alimshika mkono rose walienda kacheza mziki mimi nipo tu nawaangalia roho inaniuma lakini haya tu , usiku wa sherehe uliisha huwezi amini hadi tunaenda kulala Benjamin hajaniongelesha Zaid ya salamu nilienda kulala baada ya sherehe nilikua nimenuna hatari
"Ruby kuwa na subira kila kitu kitakuwa sawa kama ni wa kwako ni wakwako tu afu si ndonikakumbuka kuwa rose pia anampenzi wake wanapendana sana Raphael nilicheka sana nikasema sasa wasiwasi wa nini kwanza benja yupo na ndugu yangu na sio mwanamke mwingine afu cha muhimu zaidi ni kuwa rose anampenda sana Raphael hawezi msaliti hata kwa bahati mbaya ,apo angalau nilijipa MOYO nikapitiwa na kausingizi"
Asubuhi kama kawaida niliamka mapema nikasaidia kazi na kuandaa kifungua kinywa , wakati natenga mezani na wafanyakazi wengine alipita benja akasalimia za asubuhi nilijibu nikiwana tabasamu Pana usoni ila benja wala hakunichangamkia alinipita kama hanijui akapandisha chumbani kwake alikua anatoka mazoezini basi nilijiskia vibaya
Yaya Jeni alijua hilo
"Ruby kapumzike tu ndo kwamba huyu Benjamin hajasahau mambo ya utotoni hadi leo"
aliongea Yaya jane huku anaendelea na kazi nilimuuliza Yaya Jeni
"mambo yapi hayo ?"
alinipiga kichwa
"tuseme ndo umesahau au unafanya makusudi tu wewe si ndo ulimpoteza mbwa wa benja wewe na ulikua kabishi kweli saizi umebadilika sana umekua mrembo na unajituma vyema"
nilibaki kucheka ni kweli tangu utotoni benja alikua hanipendi kabisa alisema naongea sana kama chiriku mara aseme maskio yake yanakaribia kutoka damu kwa kelele zangu hatukuwahi kupatana siku hiyo nilimchukua mbwa wake na kwenda matembezi ndipo alipopotea naona hicho kilichochea benja kuzidi kunichukia alikua akija na zawadi anampa rose tu mimi hanipi kuna siku rose alikua anacheza akatoboa bomba la maji ila cha ajabu benja alisema ni Mimi ndo nimetoboa nilichezea kichapo kwanzia hapo nilimchukia pia, ila nilianza kumpenda ghafla siku alipo nisaidia nilienda mtoni na kwa bahati mbaya nilitereza nilihangaika sana mpaka nikakata tamaa nikahisi labda huu ndo mwisho wangu alikuja benja alijitosa kwenye maji akanisaidia kwanzia hapo nilimpenda kama aliniroga vile ,nilibaki kucheka tu nilivyo kumbuka matukio yetu ya zamani
Watu walishuka kupata kifungua kinywa kama kawaida muda wa mezani story kwa sana baada ya kifungua kinywa Benjamin alimuomba baba na mama ruksa kutoka na sisi
"Mr Ellison na bi Anjelica samahani ninaweza kutoka na mabinti zenu tukashangae mji kidogo"
alisema Benjamin huku anatabasamu
"Sawa wewe nenda nao wala usijali kafurahieni hatutakua na wasiwasi tunajua wapo Mikono salama"
alisema mama na baba aliunga mkono ,benja alifurahi sana
"warembo tunaweza kwenda au mpaka mkajiandae ?"
aliuliza Benjamin mimi nilijibu ndiyo sikuwa nimevaa nguo ya maana
"Mimi nipo tayari"
alijibu rose huku anatabasamu ,kwa upande wa rose alikua kapendeza sana kama alijua vile kunamtoko basi walisema watanisubiri wakatoka nje na kwenda kwenye bustani mimi nilipanda chumbani mbio nilitafuta nguo nikavaa ilikua ni kigauni kifupi na raba nilipendeza hatari nilikua najiangalia tu kwenye kioo nilitoka mbio hadi bustanini ila sikuwakuta nilipiga simu ya rose ilikua haipokelewi nikataka kumtumia message benja ila nikakumbuka rose aliniambia nisimtumie benja message tena kwa muda ili tumpime kama atanijua nilienda kwa mlinzi nikamuuliza
"Benjamin na rose wametoka ?"
"wameondoka muda sana kama dakika kumi zilizopita"
alijibu mlinzi, niliishiwa nguvu nikajisemea kwahiyo nilipoingia tu ndani waliondoka hawakutaka hata kunisubiri nilitoka kurudi ndani huku nikiwa na huzuni sana ghafra nilipata wazo la kwenda kwenye mabanda ya farasi, nilicheza sana na farasi siku hiyo hadi mood yangu ikarudi kama kawaida
Zilipita week mbili ukaribu wa rose na Benjamin wangu ulizidi sana kila mara nilikua namsumbua rose
"Rose tumwambie ukwel benja naona siku zinazidi kwenda"
niliongea kwa kulalamika
"Usiwe na papara kama ulimsubiri kwa miaka 12 sasa papara ya nini mrembo"
rose alijibu kirahisi tu hakujua ni jinsi gana naumia moyoni siku hiyo sitokuja kuisahau baada ya chakula cha usiku Mr Wilson alituomba tubaki kidogo anamazungumzo na sisi wote kama familia aliwaita hadi wafanyakazi nilikaa vizuri kuskiliza atasema nini
"jamani leo nina furaha sana sana"
mr Wilson alisema huku anamuangalia baba walitizamana wakatabasamu kisha akaendelea
"kijana wangu Benjamin amekua sasa anataka kujenga familia tumeona sio mbaya tukiunganisha undugu si ndio mzee mwenzangu ?"
Mr Wilson alimuuliza baba
"Ni kweli"
aliitikia baba huku anatabasamu kwa furaha
"kijana wangu Benjamin anaenda kumchumbia binti wa rafiki yangu mr Ellison , rose ...."
Mr Wilson aliweka kituo
"whaaat ...?"
nilikua nakunywa maji nilishangaa glass inaenda chini nilimuangalia rose usoni rose nae alinikazia macho huku anatabasamu kama hakuna kinachoendelea vile
"Ruby una nini ?"
aliuliza mama
"Amna.. Amna kitu mama ni glas... glass imeniponyoka tu samahanini naenda kubadilisha nguo"
machozi yalianza kutishia kutoka kwenye macho yangu nilipandisha chumbani kwa speed zote nilifika nikajitupa kitandani Ivo ivo Wala sikubadili nguo nikaanza kulia hata siamini kinachotokea nilikaa kitandani nikiwa sielewi au naota nikaanza kujifinya mara naskia kuna mtu anagonga mlangoni nikafuta machozi nikajiweka sawa aliingia rose
nilipandwa na hasira sana nilipomuona nilimfuata na kumshushia kibao cha nguvu alipojiloga akanirudishia
"Ruby kumbuka mara zote Mimi ni pacha wako haijalishi wewe unasura nzuri na umbo zuri kunizidi ila Mimi.. Mimi mara zote ni wa kwanza tu na itabaki kuwa hivyo"
rose alikua anacheka kwa kejeri sio kama nilikosa cha kumjibu nilipatwa na mshangao
"Huyu ni rose wangu kweli au ni mtu mwingine tofauti?"
Nilijiuliza mwenyewe
"Ruby .. usijali utapata mwanaume wa hadhi yako kwanza huna elimu ya kutosha huoni kama utamtia aibu Benjamin kwenye kazi zake anatakiwa apate msomi kama Mimi na kingine uache umalaya mtoto wa kike benja ni shemeji yako usitoke na night dress chako sitting room umalaya wako kaufanyie huko uswazi unapokaa"
rose alikisukuma kichwa Cha ruby kwa kidole kimoja
Sikutaka kukaa kinyonge nilimrukia nikaanza kumdunda siku hiyo mdomo ulikataa kusema lakini ndo nimuache awee nilimchezeshea kipigo wakati huo watu wapo sitting room hawasikii heka heka za huko chumbani rose alivyoona namdunda sana alianza kujitetea
"Ruby nina mimba usinifanye hivyo dada ako itatoka"
ilibidi niwe mpole nimuache rose alianza kulia
"hiyo ndo sababu naolewa na Benjamin sikukusudia kukusaliti ila tulilewa tukalala pamoja"
rose aliniomba sana msamaha huku kapiga magoti nilimnyanyua pale chini niliona bora niyaache yapite undugu uendelee kuliko kujenga uadui alimuomba pia nisije kumwambia mtu kuhusu mpenzi wake wa zamani Raphael nilikubali rose alifurahi sana akatoka chumbani kwangu muda SI mrefu alikuja Yaya jene alineuliza upo
"sawa ruby ?"
nilisema ndiyo
"hapana haupo sawa kama unataka kulia Lia mpaka urizike, hasira zako zote ziishe najua unaumia"
sikujua ni kwanini amesema hivyo ni kwamba alisikia kila kitu au vipi alivyoniambia hivyo nililia kama nimefiliwa alinikumbatia muda wote nilipitiwa na usingizi kuja kuamka ni saa nane za usiku ila nilijihisi MOYO mwepesi nikasema huenda benja hakuwa fungu langu, wangu yupo mahali flani ananisubiri tena kwa hamu kubwa nilitabasamu nikaendelea kulala
Maandalizi ya sherehe ya kuvishwa Pete ya uchumba wa Benjamin na rose yalianza na sherehe ilikua pambeee picha nyingi zilipigwa, mitandaoni zilisambaa picha zao wakiwa kama couple mpya inayo trend mitandaoni.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni