Menu






Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track
Tangazo - CHUKUA BONASI YAKO
CHUKUA BONASI YAKO

MTOTO WA BOSS Sehem ya pili Wangesi alimsalimia tena lakini dereva alimjibu kwa nyodo!

20th Dec, 2025 Views 41



Habari kaka alisalimia wangesi
Fresh kwan vipi alijibu dereva
Hapana kaka nimeona unahangaika hapa muda mrefu Mimi nilikuwa naanda shamba pale hivyo nimekuja kujua tatizo ni nini tusaidiane hat kwa mawazo
Hata kama ukijua huwez kuwa na msaada wowote hapa kama nimeshindwa Mimi mtoto wa mjini utaweza wewe mtoto wa shamba we endelea kuandaa shamba
Hapana kaka mawazo tu ni msaada tosha alisema wangesi
Hebu toka kwanza huend wew unataka kuniibia alisema dereva

Gafl sauti ya msichana ilitoka ndani ya gari lile ikilalamika majibu ya dereva wake alianza kumtetea Wangesi alisema ahaaaaaaaaaa kaka muache atusaidie bwana mbona hivo huyu ni mwenyeji wa sehemu hii huenda akawa anapafahamu vizuri embu mpe nafasi atusaidie!

Dereva alisema na wew Monica endelea kukaa huko huku hayakuhusu Mimi niko na huyu jamaa

Monica alisema kaka tunachelewa embu mruhusu atusaidia maana muda unaenda sana!

Hapo dereva alimuita wangesi aliyekuwa ameshaanza kuzipiga hatua kadhaa kuelekea shambani kwake ailiita we jombaaaaaa brother nakuomba kidogo .

Wangesi aligeuka na kusimama muda huo alirudi kwa ajili ya kumsikiliza dereva yule wangesi alifika na kuitika wito

Dereva alianza kuomba radhi na kusema samahani kaka naomba utusaidie nisamehe kaka!
Wangesi hakuweza kuongea kitu alijisemea ufundi wangu utakujibu pumbavu wew.

Muda huo wangesi alifunua gari mbele ya bodi na alianza kutengengeneza na alikuta hitirafu kwenye betry ya gari kuna waya ulikatika hivyo aliunga kufunika tena derveva wa gari lile hakuwa na ujuzi wowote zaidi ya kuendesha tu!

Wangesi alimaliza na aliingia ndani ili kuendesha gari lile duuuuu alipoingia alikutana na msichana nzuri sana kiasi kwamba alihisi mwili kusisimuka alijikaza na kuanza kulitoa gari mahali pale na kulipeleka sehemu nzuri

Alifanikiwa kuliwasha na kulitoa sehemu ile muda huo Monica aliyekuwa amekaa nyuma alianza kuvutiwa na kazi nzuri ya kijana Wangesi baada ya Wangesi kuhakikisha kuwa gari liko sehemu salama alimgeukia Monica alitabasam na kusema mnaweza kuendelea na safari gari iko salama

Monica alishukuru na dereva wake aliingia na kuanza kuendesha gari lile!
Monica alianza kufikilia tabasam la kijana Wangesi

Wangesi alizipiga hatua kuelekea shambani kwake!

Muda huo Monica alizidi kufikilia tabasamu la Wangesi na alianza kuwaza atampata wapi ...ikiwezekana aweze kuongea nae lakini asingeweza kumpata maana alikuwa anapelekwa shule na huko atakaa muda mrefu sana !

Huku wangesi aliendelea na kazi yake akiwaza kwenda mjini kutafuta kazi muda huo maana ufundi wake anaiamini na udereva wake pia siku hio ilipita alimaliza kazi zake na kurudi nyumbani kama kawaida yake hakuweza kumsimulia mtu yeyeto yaliyotokea shambani alibakia kuwaza tu uzuri wa Monica muda huo japo asingeweza kumpata

Maana hakupatiwa namba wala yeye kuwapatia namba za simu ilifika muda akasema haitowezekana kuonana nae tena hivyo ngoja nifanye mambo yangu!

Asubuhi mvua ilinyesha sana na muda huo mtaa wa pili kutoka kwa nyumbani kwa mzee Kamau kuna msiba ulitoke kuna binti aitwae Salome alibakwa na kufa hivyo watu walikusanyika kushuhudia tukio lile kitu ambacho kiliwasikitisha wengi na ndugu wa salome walitoa taarifa kwa ndugu na jamaa ambapo police walikuja kufanya uchunguzi na baadhi ya vijana walichukuliwa huku wengi walikimbia mazingira yale

Muda huo Wangesi alikuwa hajui lolote kuwa police walikuja alishangaa tu anakamatwa muda huo wananchi wengi walisema huenda ni yeye maana hana mwanamke na hawajawahi kusikia kuwa mchumba wake ni yupi muda huo akichukuliwa na kupelekwa kituoni kwa ajiri ya kuchukuliwa maelezo alifikishwa na kuwekwa sehemu ya mahojiano aisee wangesi alipigwa pamoja na wenzake

Kulingan na ukaidi alikuwa nao wangesi police walimuonea sana maana alipigwa huku alikuwa haongea chochote alijua kabisa kuwa sio yeye na hawafahamu waliofanya vile!

Walisoteshwa kwa muda Kule police na waliweza kuhukumiwa miezi sita jera muda huo wangesi shuguli zake zilisimama na kama ujuavyo jela wangesi alionewa sana na wenzake kwa muda akiwaza kutoroka lakini akiwaza ataelekea wapi wakati alipelekwa kwa gari na hakuweza kuiona njia ya kupitia wangesi alikonda na mwili wake ulipungua sana

Kwa muda huo aliamua kuvumilia tu maana miezi sita sio mingi japo ataharibikiwa na mambo mengi baada ya kuvumilia na hali iliyopo alianza kufanya kazi za jera akiwa na wenzake na hali ile ya ufungwa akaizoea na mwili wake ulianza kurudi

Muda ulienda na miezi sita ilikatika watu wale waliachiwa huru baada ya kumaliza kifungo chao wangesi na wenzake waliachiwa baada ya kuonekana hawana kosa lolote

Wangesi hakutaka kurudi nyumbani tena maana alipachukia tangu siku hio baada ya kupewa vitu vyake aliwatoroka wenzake na hawakujua ameelekea wapi waliamua kurudi zao nyumbani huku wakimuacha Wangesi mjini na dhamira ya Wangesi ulilikuwa ni kutafuta kazi ya kufanya yoyote atakayoona lazima angefanya tu!
Baada ya kuwatoroka wenzake Wangesi hakuwa na sehemu ya kuishi aliamua kujificha kichakani usiku huo na uaingizi ulimpitia alisinzia sana kichakani pale kulingana na maisha ya mbanano huko jera sehemu ya kulala ilikuwa mbaya sana hivyo sehemu ile alipaona ni pazuri mno

.
Tangazo - MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA

MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
MTAKATIFU GEMMA UTUOMBEE SHIRIKA LA MASISTA WA MT GEMMA WA DODOMA
Tunao Wapenda ndio wanao tuua baba
Sikiliza Wimbo Kamili
   
X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MTOTO WA BOSS Sehem ya pili Wangesi alimsalimia tena lakini dereva alimjibu kwa nyodo!  >>> https://www.gonga94.com/semajambo/mtoto-wa-boss-sehem-ya-pili-wangesi-alimsalimia-tena-lakini-dereva-alimjibu-kwa-nyodo



#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #war

#love #photooftheday #fashion #beautiful #happy #tbt #followme #picoftheday #art #nature #travel #fitness #motivation #life #fun #instagram #friends #smile #food


 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 
MWENDELEZO SOMA HAPA

Maoni

You're not logged in


gonga94 official track
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi mtoto-wa-boss-sehem-ya-pili-wangesi-alimsalimia-tena-lakini-dereva-alimjibu-kwa-nyodo
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
You're not logged in


Tangazo - Hongera sana
Hongera sana

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Privacy Policy Contact us
Terms & Conditions About us Latest