Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya β Gonga94 Semajambo
Gonga94 Β· Stories
06 Nov 2025
527 views
VYOTE NDANI GONGA94
π£ππ‘ππ ππ πππππ‘π πͺπ πππππ‘ππ SEHEMU YA 12 Hapo sikusubiri masimango na kudhalilika kwa zaidi, maana jibu alilotoa
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Mohan ni udhalilishaji tosha. Bibi na yeye alinifuata hadi chumbani kwangu."Naima usijali kila kitu kitakuwa sawa"bibi alinisogeza miguuni mwake kisha akanipapasa kichwani .Nikayafumba macho yangu. Mohan aliingia lakini bibi akampa ishara ya kwamba aniache nipumzike tutaongea baada. Ila sio kwamba nililala hapana !sikutaka tu kuongea na Mohan. Mida ya jioni watu wote walikuwa na furaha sana. Mi nilikuwa chumbani kwangu nikiwa napanga nguo niondoke zangu asubuhi. Ghafla Antara aliingia huku akila chocolate.
"oh masikini !unajua nini Ney nasikitikia hicho kiumbe ambacho kinaenda kuishi bila baba solution ni moja tu. Toa mimba au utoweke katika maisha haya ya Mohan"
"Antara ,sina mood yakujibizana vibaya ya wewe nataka kupumzika niache"
"kweli kabisa yani upumzike sio ulale moja kwa moja"
Baada ya hapo aliondoka kwa majivuno sana. Mohan alikuwa kajibanza kwenye nguzo ili asionekan na Antara ,kisha akaingia.
"Naima tunahitaji kuweka hili sawa wala usijali. Naima nakuhitaji wewe na...."
"Mohan,mwanangu hana baba kuanzia leo. Nachagua kuwa single mother nipambanie maisha ya mwanangu. Mohan kumbe nyie hamna utu eeh nilikupa bikra yangu nabado tuliendelea kukutana nikiamini utanioa .Kumbe najidanganya mapenzi yenu ni ya kwenye movie tu. Mohan maisha mema yawe juu yako na baraka zangu nakupa kama zote mlango ule toka nje nilale"
"lakini Naima tuna...."
"Mo nimesema toka njeeeee!"
Baada ya kuona nimefoka,akatoka nje kisha nikafunga mlango. Nililia sana tena sana.
Asubuhi mapema niliamka kabla ya yeyote nikatoka nje na kujiambia niende zangu tu kwenye nyumba ya mama huko nitaishi vizuri. Kisha nikipata kibiashara nihame nikapange ambapo sitasumbuliwa na kina Mohan.
Sasa nikiwa njiani Simon alipita na gari lake akatishia kunigonga mi nikaanguka akashuka.
"we vipi unatembea huoni barabara ya kwenu hii!kama unamawazo kaa pale vile πvile vijiwe sio vya kulipia. Uwaze ukimaliza nyanyuka ondoka"
"samahani sikuwa muangalifu"
"saa hizi tungekuwa tunaisikia hiyo samahani yako au mpumbavu kabisa"
Nilimtazama sana Simon ile kutazama vizuri kwenye gari nagundua alikuwa na Mwaju. Nilizidi kupata hasira sana.
Basi hapo mbele nikakutana na zuri akiwa mbio na kapu la samaki. Akaniona tukashirikiana njiani. Akanipokea bag akaliweka ndani kisha nikampa mkasa wote. Zuri alinisikitikia sana pia akasema hapa Mohan na Raj wanapajua ,hivo nirahisi kunipata. Nikamshawishi tuhame akakubali. Tulihama mji kabisa tukaenda kuishi pengine tukapanga nyumba kumbwa na nzuri. Mohan na Raj walizidi kunitafuta kwenye sim. Nilivyoona wanaweza kunipata kupitia GPS nikatoa line nikabadili kabisa. Na Zuri akafanya hivo.
Tulikaa na kuanza kutafuta biashara ya kufanya. Hapo matumbo yakiwa kama yote. Tukaona bora tufanye mgahawa. Tuliuza uji na vitumbua mchele asubuhi,mchana tulipika ugali usiku tuliuza chips na nyama choma. Biashara haikuwa rahisi kutoka lakini kwa uwezo wa Mungu tulianza kufanikisha.Tulikuwa pia na jirani yetu ambaye anauza maembe anaitwa bi Ngere. Alitupenda sana na sisi tukampenda.
Asubuhi moja bana, Zuri alijisikia vibaya sana. Kumbuka yeye ndiye alinitangulia miezi 2 kwenye ujauzito, hivo siku zilikuwa zimetimia. Mimi nilikuwa nimetoka nimeenda kutafuta mishkaki maana tuliishiwa. Na hapo ni baada ya kumaliza biashara yetu ya asubuhi uji na vitumbua mchele. Bi Ngere alimsaidia hadi hospitali. Akanipigia sim nikawakuta.
"bi Ngere vip hali ya Zuri anaendeleaje?"
"usijali punguza pressure yupo salama anashughulikiwa huko"
Tuliwa pale daktari aliniita na kuniagiza baadhi ya vifaa. Nikatoka na kwenda kwenye pharmacy nikanunue. Nikiwa pale nikasikia sauti ikiniita kwa nguvu sana.
"Ney!Ney!Ney!"
Itaendelea....
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
MY WANGUβ€οΈ sehemu ya 69 na 70
Basi nilipata kafuraha mno. Nikachukua pesa yangu .nikarudi darasani kuendelea na ratiba zangu. Uwiiiiii nilifurahi sana...
7 MPAKA 9 π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘π‘ Basi bwana tukivyotoka kula sasa. Mi nikaludi ndani i...
π£ππ‘ππ ππ πππππ‘π πͺπ πππππ‘ππ SEHEMU YA 12 Hapo sikusubiri masimango na kudhalilika kwa zaidi, maana jibu alilotoa
Mohan ni udhalilishaji tosha. Bibi na yeye alinifuata hadi chumbani kwangu."Naima usijali kila kitu kitakuwa sawa"bibi alinisogeza miguuni mwake kisha akanipapasa kichwani .Nikayafumba macho yangu. Mohan aliingia lakini bibi akampa ishara ya kwamba aniache nipumzike tutaongea baada. Ila sio kwamba nililala hapana !sikutaka tu kuongea na Mohan. Mida ya jioni watu wote walikuwa na furaha sana. Mi nilikuwa chumbani kwangu nikiwa napanga nguo niondoke zangu asubuhi. Ghafla Antara aliingia huku akila chocolate.
"oh masikini !unajua nini Ney nasikitikia hicho kiumbe ambacho kinaenda kuishi bila baba solution ni moja tu. Toa mimba au utoweke katika maisha haya ya Mohan"
"Antara ,sina mood...
π Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/penzi-la-kijana-wa-kihindi-sehemu-ya-12-hapo-sikusubiri-masimango-na-kudhalilika-kwa-zaidi-maana-jib
Umesoma kwa utulivu Β· dakika chache tu Asante Endelea kusoma chagua hapo chini
Umependezwa ?? Asante Soma Zaidi penzi-la-kijana-wa-kihindi-sehemu-ya
π£ππ‘ππ ππ πππππ‘π πͺπ πππππ‘ππ SEHEMU YA 15 Alinisogelea kabisa na kunishika mikono huku akiliita jina langu na machozi ya furaha yakamtoka
π£ππ‘ππ ππ πππππ‘π πͺπ πππππ‘ππ SEHEMU YA 10 Kwa kweli hali niliyo kuwa nayo sikutaka hata kumjibu,alimaliza akaondoka.
π£ππ‘ππ ππ πππππ‘π πͺπ πππππ‘ππ SEHEMU YA 17 - 18 Mohan alitoka nje ili mkuu wa shule asijue chochote
π£ππ‘ππ ππ πππππ‘π πͺπ πππππ‘ππ SEHEMU YA 16 Niliwabembeleza watoto wakakubali kula japo kwa mbinde sana
π£ππ‘ππ ππ πππππ‘π πͺπ πππππ‘ππ SEHEMU YA 11 Kwanza nilijitoa mikononi mwa Mohan. Kisha familia ikatusogelea. Mama Mohan aliuliza kwa mshangao sana. "nini hiki Mohan?" "mama mimi siwezi
π£ππ‘ππ ππ πππππ‘π πͺπ πππππ‘ππ SEHEMU YA 19 - 20 Baada ya cake kuletwa watoto wangu wote walisogea, birthday boy
π£ππ‘ππ ππ πππππ‘π πͺπ πππππ‘ππ SEHEMU YA 13 Niligeuka kwa uoga pole pole nilishangaa kumuona Swaumu
π£ππ‘ππ ππ πππππ‘π πͺπ πππππ‘ππ SEHEMU YA 8 Nilikimbia ndani kwa Zuri na kujifungia. Aliyekuja
π£ππ‘ππ ππ πππππ‘π πͺπ πππππ‘ππ SEHEMU YA 7 Niligandaa baada ya kumuona Zuri akiwa mbele na Simon akiwa nyuma yake
π£ππ‘ππ ππ πππππ‘π πͺπ πππππ‘ππ SEHEMU YA 9 Mwenzenu picha zilikuwa zile ambazo tulipigwa na Mohan