π£ππ‘ππ ππ πππππ‘π πͺπ πππππ‘ππ SEHEMU YA 8 Nilikimbia ndani kwa Zuri na kujifungia. Aliyekuja
"Zuri hivi Ney anashida gani mbona amenikimbia?"
"aaahmm aliondoka kunywa maji tu subiri nimwite"
Zuri aliingia ndani na kunitoa nyuma ya ndoo.
"wee Ney ndio nini sasa unamkimbia mgeni"
"bana Zuri fanya mchongo huyo kiumbe aondoke hapo"
"eeeh kwanza mwenzio nimezama nahisi kubaki namtazama tu"
Zuri alinitoa nje nikakaa huku nikifinya vidole nusu nivivunje.
"haya Ney umeanza drama au sio? nimepita kwa mama akanielekeza hapa nikakufuata"
"oh kumbe karibu. Nilikuwa nimelala kwa mama nikaona bora nije kusalimia hapa ndio nipitilize kazini"
"ndio na mimi nimekupitia hapa unisindikize nikachague zawadi ya kumpa girlfriend wa kaka Mohan"
Ndugu msomaji nilishtuka sana. Ila nikajizuia asiwepo mtu wa kujua chochote. Nikajichekesha pale kisha nikamuaga Zuri na kuondoka. Tulifika sehemu aliyokuwa anaenda Raj kununua hiy zawadi. Akaendelea kuchagua na mimi nikiwa natazama nguo za bei sana. Raj akapita upande wa 2 mi nikaingia ndani kwenye duka sasa. Nikiwa natembea huku nikiangalia juu ghafla nikapamiana na mdada mmoja asili ya kihindi.
alisimama na kunitazama.
"okey aunty i will call you back "kaliweka sim yake kwenye mkoba kisha akanisogelea vizuri vizuri.
"hivi nyinyi masikini mnashida gani hata hamueleweki unanipamia ili useme nimekuumiza upate pesa au unajua tuna mti tunachuma pesa are you crazy?"
Yaani msomaji nilikuwa nimemuacha atukane aondoke kitendo cha yeye kuniongezea kizungu chake kilimponza.
"kwani nyinyi matajiri mnatak tuwaone nyinyi tu kwamba mnapita au hii njia ni v.I.P haturuhusiwi kupita?mashauzi kibao kumbe libaya .na ushukuru rangi"alipoona watu wanaanza kujaa aliondoka.Raj nae akaniuliza nikamwambia hakuna. Tulivyofika nyumbani tulisikia kuna sauti zinapiga makelele kwa kilio sana.
"amenidhalilisha sana ningemjua hangepona nakwambiaπ"
Sisi tukazidi kuingia ndani. Binti aliyekuwa kakumbatiwa na bibi si akageuka π³ ni yule binti wa dukani. Na yeye baada ya kuniona alishtuka sana. Ila akavunga tukaendelea kuongea na wengine. Mi nilikuwa sitak kuonana na Mohan, nikaondoka jikoni baada ya kusikia ameitwa sebuleni. Sebuleni huko nilimkuta Mwaju akiwa analia kwa uchungu sana.
"hei na wewe unashida gani?"
"Ney mpenzi wangu kaniacha na kasema mwaka ujao anaoaπ"
Nilishangaa mana siku zote najua kama Mwaju anampenda Mohan. Na yeye anaoa mwezi ujao. Sasa huyo anaeoa mwaka kesho ni nani. Nilitoka nikaangaza hakun mtu .Nikamtoa Mwaju hadi chumbani. Simu yangu ilianza kuita na mpigaji alikuwa Mohan, mi sikupokea hata. Nikiwa mule akaingia Amla na yule binti wa dukani.
"wifi huyu ndie Naima mwizi wa wanaume za watu"
"najua sana maana sio mwizi wa wanaume tu bali hata vingine anaiba huu ndiye mwizi aliyenidhalilisha dukani"
"wifi Antara huyu dawa yake ni kumfukuza humu ndani"
Walivomaliza kutukana wakaondoka. Zuri nae alipiga sim nikapokea akanipa habar kwamba Swaumu anaujauzito ila haunulikan ni wa nani. Mi nilikausha maana najua ni wa Simon. Raj alikuja kuniita kwamba naitwa na mama yake.
Nilipofika nilikuta Antara analia huku akibembelezwa na Amla. Bibi alikuwa kakaa bila kuongea chochote.Mama sasa nae alikuwa kafura kwa hasira.
"hivi wewe umekuja kufanyakazi au kuwatega wanangu?nishasema wanangu wataowa kabila letu na sio watu weusi"
"dawa ya huyo ni kumfukuza atazidi kumuumiza wifi"
Nilipotaka kuongea mama alinirushia pic. Ile kutama tobaaa! kibarua kinashamba sio nyasi.
Itaendelea......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi