π£ππ‘ππ ππ πππππ‘π πͺπ πππππ‘ππ SEHEMU YA 9 Mwenzenu picha zilikuwa zile ambazo tulipigwa na Mohan
"Mama anaumwa pesa ya matibabu inatoka hapa sina msaada wacha nijishushe huenda wakabadili mawazo"Raj alibisha hodi nikamkaribisha. Alinipa maji na sambusa nikaanza kula huku nikilia sanaπ. Raj alinipa leso nikawa napangusa machozi yangu.
"Matatizo ni moja ya mitihani hivo vumilia utakuwa sawa tu.Na ukihitaji chochote pls nijuze nitakusaidia" Raj baada ya kuongea hivo nilimuomba aniache nipumzike kidogo. Siku zilikatika na kweli bana sikufukuzwa ndani mule baada ya kuwa kama kikaragosi kwao. Mohan alikuwa anachukizwa na hali ile maana hakupenda kabisa.
Asubuhi moja kulikuwa kumechangamka hapo ndani. Nikamuuliza mfanya kazi mmoja kuna nini. Ndipo nikaambiwa Mohan anamvisha Antara pete leo jioni. Aiseee nguvu zilikatika nikarudi chumbani. Nililia sana nikaondoka hadi nyumbani.
"eeh haya mbona mapema yote hii?"
"Mama sijisikii vizuri ndio maana nikasema nikuje tu nitaondoka kesho"
Nikapitiliza hadi chumbani kulala. Simu ilikuwa ikiita muda wote na mpigaj ni Mohan na Raj. Zuri nae akajaribu kupiga lakini sikupokea badala yake nikazima kbs sikutaka usumbufu. Hapo mama Ney alizidi kuona siku zinakatika na mimi siendi kazini.
"Ney, wiki moja sasa inakatika mwenzetu kazini huendi au umelikoroga huko?"
"hapana mama nasikia vibaya tu"
"sasa si twende hospitalini"
"Mama bana ni uchofu we siunaona lile jumba lilivokubwa "
Mama alicheka na ghafla Raj akawasili. Mama alimkaribisha kisha akatuacha na kwenda ndani.
"Ney ndio nini sasa? unajua ni siku special kwa ajili ya broo halafu unao ndoka?"
"Raj hapa nilikuwa najiandaa niende hospital maana sijisikii vizuri kabisa"
Raj aliniomba anisindikize nami nikakubali tukaondoka. Ila mama nikamuaga kuwa naenda sokoni namsindikiza Raj. Nilifanyiwa vipimo majibu yakatoka nina mimbaπ³!.kwanza msomaji nilizimia. Nakuja kuamka nipo wodini Raj na Simon wakiwa hapo.
"oh Ney umeamka!doctor! "Raj alimuita daktari nae akasema niko salama mimi na mtoto. Basi Raj alijua mimba niya Simon ndio maana akamwita. Raj akatupisha maana aliona tunatazamana bila kuongea chochote.
"Ney unaweza kuniambia huo ujauzito niwa nani?"
"Simon si wewe ulisema tusijuane? haya huu ujauzito si upo kwenye tumbo langu? unakuwasha wapi?"
Simon hakupendezwa na majibu yangu alitaka kunizaba kibao lakini mlango ulifunguliwa akaingia Zuri akiwa na kapu la chakula ndipo Simon nae akatoka nje kwa hasira sana.
"Ney kwanini ulificha kuwa unamimba ya Simon?"
Hapo sasa ilibidi nimpe Zuri ukweli wote. Alishangaa na kuniambia nikae kimya. Raj aliingia na kusema ameshalipia na atakuja kutuchukuwa jioni. Mi nikamwambia asimwambie chochote mama Ney.
Tukiwa pale niliamua kumwambia Zuri tuondoke na Raj asijue wapi tulipo. Tulipofika nje mwamba huyu hapa Mohan mwenyewe kafika ametusubiri tu. Akafungua mlango wagari nakututaka tuingie. Mi niligoma nikaanza kumvuta Zuri. Mohan akaona wee usinitanie alinipiga tax bega hadi kwenye gari kisha Zuri akafuata. Alituondoa hapo haraka sana.
Tulifika kwenye nyumba ambayo siijui hata.
"Mohan unashida gani lakini? naomba utuachie tuondoke!"
"Naima, sipo tayari kumpoteza mtoto wangu wa 1 kwaajili ya ujinga wako"
"kwa hiyo unajali mtoto haya mama Ney ulimfikiria au?"
Mohan hakutaka kutusikiliza alitoa sim nakupiga sehemu.
"hello!niandalie tikcket 3 za ndege ya saa kumi na moja alfajiri"
"Mohan siwezi enda popote mi sio mtumwa wako"
Mohan alinisogelea akanitazama sana kisha akatufungia na kuondoka.Sim nazo alikuwa kazitunza yeye. Tulishindwa tufanye nini. Baada ya muda alirudi akiwa na chakula kisha akatupatia simu zetu nilipowasha tu nilikutana na ujumbe ufuatao:"Naima ukitaka usalama wa wewe na mwanao pamoja na mama yako, ondoka nchini hama. Nipo tayari kulipia gharama zote"
Nilipotezea bana nikamtafuta mama na kumwambia niko kwa kina Raj. Nilimfuata Mohan chumbani.
"Mohan,kwanini umenileta hapa?"
"Naima, mtoto anahitaji uangalizi wa hali ya juu huko uswailini kwenu sipaamini sana"
Kumbe anajali mtoto wala sio mimi haya sawa. Mohan hakulala pale aliondoka usiku huo huo. Jumba lilikuwa kubwa hadi raha. Nikalala na Zuri chumba kimoja. Asubuhi nilikuja shtuliwa na makelele ya Zuri akiliita jina langu kwa hofu sana nikashuka hadi sebuleni. Akawa ananionyeshea simu kwamba ona hii. Kabla sijaona Mohan alikuja akapokonya sim kisha akanishika mkono na kunitoka nje hadi kwenye gari.
Mohan tunaenda wapi sasa jamani huyu kijana vipiπ. Aliwasha gari tukaondoka. Tulipofika nyumbani kwetu,nilikuta watu wengi sana na baada ya kuniona walianza kulia sana . Yaani majibu niliyapata baada ya kuliona jeneza la mama Ney linatoka ndani nilipiga fujo tu moja Mamaaaaaaπ.Nilikuja kupata fahamu nikiwa nyumbani kwa kina Mohan. Watu wote walinipa pole.
Baada ya Muda, Mwaju aliingia akafunga mlango.
"vip Ney, ujumbe umeuona au?"
"ujumbe !ujumbe gani?"
"Ney najua unamimba ya Simon bas kwa usalama wako utoe au umwambie sio wake la sivyo utamkosa huyo mtoto"
Itaendelea......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi