Simulizi: *KIJIJINI KWA BIBI* Na Mwaisa Story Sehemu Ya 3 ______________ ILIPOISHIA ______________ Walipofika nyerere square, wakamuona kwa mbali stellah
rafiki yake aitwae Tausi,
"Leo kazi ipo" sauti nzito ilipita
kwenye masikio ya Kayoza na
kushindwa kuelewa inatokea wapi,
na cha ajabu sio Denis wala Omary aliyeweza kuisikia sauti hiyo....
_________________
MUENDELEZO
_________________
"Jamani hamsikii sauti yoyote ya kutisha?" kayoza aliwauliza wenzake baada ya kuwaona kama hawasikii anachokisikia yeye,
"Sauti gani?" Denis aliuliza,
"Sauti nzito inakwaruza masikioni" Kayoza alijibu na wenzake wakaishia kucheka,
"Acha mawenge wewe, au unapata uoga kukutana na Stellah?" Omary aliongea huku akimcheka kayoza,
"Acha ujinga, mimi sijamuongelea Stellah hapa, naongelea ishu nyingine" Kayoza aliongea baada ya kutofurahishwa na maneno ya Omary,
"Yaishe basi, kifupi sisi tunasikia sauti za magari tú na hatusikii sauti nyingine. Au sio Ommy?" Denis aliuliza huku akimgeukia Omary,
"Ndio maana ake" Omary alijibu huku akicheka.
Wakiwa wanaendelea na mwendo, kwa mbali waliweza kuwaona Stellah na Tausi , ila walikua nje ya sehemu husika.
"Sasa mbona wapo nje?" Omary aliuliza kwa mshangao,
"Labda wamekaa nje ili tuwaone kiurahisi" Denis alijibu.
wakina kayoza walipowafikia
wakapeana salamu,
"jaman twendeni sehemu
nyingine, hapa hata hapaeleweki" Stellah aliongea baada ya salamu,
"kwani hapa kuna nini?, kayoza akauliza?" Kayoza aliuliza kiubabe ubabe,
" Jamani shem hapa
wamesema mda umeisha" Tausi
ndivyo alijibu namna hyo,
"We mpuuzi nini, nani Shemeji yako?" kayoza aliuliza kwa hasira,
"Nini wewe, Acha fujo Kayoza, huwezi jua labda Shemeji yako kwangu" Omary aliongea huku akimcheka Kayoza,
"Huyu mwenzenu vipi, mbona ana hasira za karibu hivyo?" Stellah aliuliza huku akimtazama Dennis,
"Mzoeeni tu huyu mshkaji wetu" Denis alijibu huku akitabasamu,
" sasa tunaelekea wapi?" Kayoza akauliza,
"Mhm...mi hata cjui ni sehemu gani nzuri kwa hapa mjini usiku huu" Stellah akajibu,
"Mi naona twendeni hapo
Saturnight bar" Denis akatoa mwelekeo,
"Bar tena?" Kayoza aliuliza kwa mshangao kwa maana yeye hatumiagi kilevi,
"Bar hata soda zipo" Omary alijibu huku akionekana kumpuuza Kayoza,
" hiyo Saturnight ni mbali kwani ili tuchukue taxi?" Stellah aliuliza,
"Ahaa wapi ni hapo tu nyuma ya TRA" Denis akajibu na mwisho wote
wakakubaliana waende hapo Suturnight Bar.
Walipofika wakakuta
watu wengi sana na hii ni kutokana na mpira wa ligi kuu ya uingereza
ilikua inaonyeshwa pale nyakati za usiku,
"Kwa hiyo tufanyaje? Maana naona kote kumejaa na hakuna nafasi" Tausi aliuliza,
"Ebu subirini kidogo" Denis aliongea
kisha akaingia ndani akatumia mda
kama wa dakika kumi hivi hivi, kisha akatoka,
"jamani eee, nimeongea na wahusika
wakasema kama tunahitaji sehemu
tulivu, tunaweza kuchukua chumba
kimoja tukawa tunakitumia ila lazima
tukilipie, wenzangu mnasemaje?" Denis aliongea baada ya kutoka ndani,
"haina shida tena ndo vizuri" Stellah
akajibu,
"Mhm, kwani jaman
tutatumia mda gani kula na hayo maongezi kiasi kwamba mpaka tuchukue chumba?" Kayoza akauliza,
"Boy acha maswali ingia utengeneze shavu, leo tuifanye siku kuu" Omary akasema.
Baada ya mvutano
wa hapa na pale, wakakubaliana
kuingia mule ndani, wakaagza
chakula cha kutosha na vinywaji pia,
so ikawa kula na kunywa, paka
wakawa wako hoi kwa ulevi. Ila wakati wote huo Kayoza alikuwa anakunywa soda. Ila mwisho wenzake walimrubuni na kujikuta akionja bia moja, katika hali ya ajabu kabisa, alijikuta anazima kwa bia moja tu mpaka wenzake wakamshangaa.
Baada ya wote vilevi kuwakolea, vibweka vikaanza mara Stellah amkumbatie
kayoza, mara omari amtukane denis
kisa tausi.
Ilipofika saa 7 usiku, mhudumu
akawaambia anataka kufunga kwa
hiyo waondoke, ila wao wakadai
watalala pale pale na waongezewe
chumba kingine, Mhudumu akawapa
ufunguo wa chumba kingine ambacho kwa makubaliano yao hicho chumba wangeenda kulala Denis, Omary na Tausi.
Stellah akawaomba wote watoke abaki yeye
na kayoza, kipindi hicho kayoza hajielewi amepoteza kujitambua kutokana na bia moja aliyokunywa, tena ukizangatia ndio ilikua mara yake ya
kwanza kunywa pombe.
Walipotoka tu wakina Denis, stellah akafunga
mlango haraka, akajitahidi kumbeba
kayoza paka kitandani, alafu Stellah
chap chap akavua nguo kisha akawa
anamvua kayoza, huku akiamini hiyo siku ni moja kati ya siku bora kabisa ya kutimiza moja ya ndoto zake, kulala na mwanaume anayempenda.
Alitumia dakika
tano kukamilisha zoezi zima, kisha akapanda kikatandani na kuanza kumchezea Kayoza kimahaba, ila kuna hali aliiona, kila baada ya dakika moja mwili wa Kayoza uliongezeka ubaridi kiasi kwamba akawa kama chupa ya soda iliyotoka ndani ya friji.
Stellah aliliiona hilo ila alitaka kupuuzia kutokana na hamu zake za kimwili. wakati akiwa bado anaangaika, ghafla bin vuu kayoza aliamka mithili ya mshale huku macho yake yakiwa meupe na kiasi kwamba mboni hazikuonekana, macho yakawa
yanang'aa tena kama tochi, Stellah ndipo akapata mshtuko,
"Vipi tena Kayoza?" Stellah aliuliza huku hofu ikianza kumtawala, lakini kayoza hakujibu kitu na badala alitoa tabasamu moja la ajabu na kufanya meno yake yaonekane na kwa kasi ya ajabu yale meno yakaanza kurefuka na kuwa makubwa kama ya mnyama anayefahamika kwa jina la ngiri.
Stellah akiwa kama amepatwa na
mshango au bumbuwazi, alijikuta ameganda Pale pale kwa kihoro huku akiwa hana nguvu kutokana na tukio analoliona.
Mwishowe akajikaza na kuanza kujiondoa ndani ya shuka kwa lengo la kukimbia,
"Unaenda wapi usiku huu, huogopi kutoka nje na giza hili?" Kayoza alimuuliza huku akiwa katika hali yake ile ile,
"Naenda chooni mara moja" Stellah alijikuta anajibu bila kutegemea huku mwili ukiwa unamtetemeka,
"Nisubiri nikusindikize" Kayoza akaongea huku nae akiwa anashuka kitandani, Stellah akahisi ni bora kukimbia kuliko kumuamini huyo kiumbe wa ajabu. Akiwa anaanza kukimbia, Kayoza aliruka na kutua mbele yake, Stellah akataka kupiga kelele, ila alichelewa, tayari mkono wa Kayoza ulikuwa mdomoni kwa Stellah kumziba asipige kelele na huku mdomo wa kayoza ukiwa shingoni mwa Stellah na yale meno makubwa yalitumika kuung'ata mshipa mkubwa wa damu na Kayoza akaanza kuinyonya hiyo damu huku akitoa muungurumo wa ajabu uliosikika kwa sauti ya chini. Alipomaliza kazi ya kufyonza damu ya mwili wa Stellah, aliuachia ule mwili na kudondoka chini ukiwa hauna tena uhai, ndio ukawa mwisho wa Stellah, mwanaume aliyedhani wa ndoto za maisha yake ndiye mwanaume aliyempotezea ndoto za Maisha yake.
Kayoza aliuangalia ule mwili kwa dakika chache na yeye nguvu zikamuishia akapoteza fahamu na kuanguka chini pembeni ya mwili wa Stellah.
Asubuhi Kulipokucha, Kayoza aliamka huku akiwa na uchovu usio wa kawaida, ila alijishangaa akijikuta amelala chini huku akiwa mtupu hana nguo na pia alihisi mdomoni ana harufu ya damu ila alipuuza huku akiamini labda alijing'ata usiku, kitandani hakukuwa na mtu. Akapeleka mikono chini ili ainuke, hapo ndipo alipohisi amegusa mwili wa mtu, akapeleka macho yake Pale alipohisi amegusa mtu, ndipo alipoweza kumuona Stellah akiwa amelala tena akiwa mtupu na shingoni alikuwa na damu, hapo akashtuka, akajivika ujasiri na kumgeuza, akakuta alama ya meno kwenye shingo ya Stellah, Kayoza akajikuta anatema mate kutokana na zile alama za meno zilizotengeneza kidonda kikubwa shingoni kwa Stellah. Kayoza alipotema mate alishangaa kuona mate yake yametapakaa damu, akaona sasa hiyo kesi ni yake.
"mama yangu, kumeshaharibika hapa" kayoza aliongea baada ya kuhisi kuwa inawezekana Stellah amekufa na hakuna mwingine atayekamatwa zaidi yake.
Akaona njia sahihi ni kukimbia hakutaka kujua hata wenzake wapo wapi.
Akaamua kuvaa fasta ili
akimbie mule ndani kabla mtu yoyote hajajua tukio alilolifanya, mara akasikia
sauti ya mtu akigonga mlango,
*****ITAENDELEA******
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi