π§ππ§πππ’ ππ¨ππͺπ ππ‘ππ‘ππ’ππ’π£ππ¦ππ SEHEMU YA 10 Mchungaji alimnyamazisha mwanamke huyo asiendelee kulia kwani kulia isingeweza
"Mchungaji nakushukuru kwa hii nafasi uliyonipa nafasi hii iwe sadaka mbele za Mungu aweze kuikumbuka hii siku mpaka siku ya hukumu, kwani utakua umefanya jambo la msaada sana kwenye maisha yangu. Naitwa Consolata, mkiniita Conso tu itapendeza, miaka mitano iliyopita nilikua nafanya kazi kama dada wa kazi nyumbani kwa kina John. Kazi hiyo nilifanya kwa muda wa miaka mitatu mpaka pale nilipofukuzwa kwao na sababu kubwa ya kufukuzwa ni ujauzito ambao nilikua nimeubeba, na baba wa huu ujauzito ni yule bwana John ambae anafunga ndoa leo, huyu bwana ameyaharibu maisha yangu kwa kiasi kikubwa kwani alinihadaa kwa ahadi nyingi kama asali ya mwituni na ahadi hizo zikageuka shubiri na kuyaharibu maisha yangu kabisa, aliniahidi kwamba atanioa ila nilipopata mimba yeye na familia yake walinitimua nyumbani kwao kama mbwa aaaaah aaaaaaaaaaah" Conso alishindwa kuendelea alijikuta anazidi kulia tu ilibidi kazi ya kumnyamazisha ianze upya, wahudhuriaji wa ndoa hiyo walimwonea huruma sana kwani ongea yake ilibeba hisia za maumivu makali aliyokua nayo moyoni mwake.
Aliponyamaza aliendelea kuongea.
"Nililea mimba hii kwa shida na taabu nyingi bila hata kipande cha sabuni kutoka kwa baba wa mtoto, nilijifungua kwa oparesheni ambayo ilichukua akiba yangu yote ya pesa hata nilivyomtafuta John aweze kunisaidia mimi na mtoto bado alinifungia vioo, kama mama wa mtoto iliniumiza niliuza mboga barabarani nikiwa na mshono wa upasuaji yote niweze kumlisha mwanangu jamanj binadamu ni makatili na wabaya sana" Conso aliweka kituo hapo na kuendelea kulia tena, alinyamazishwa upya na kuendelea kuongea.
"Nawaomba wachungaji na kila mtu aliepo hapa aweze kunisaidia hii ndoa isifungwe naomba mfanye hivyo kwaajili yangu kwani nampenda sana John pia natamani niweze kuishi nae, tulee mtoto wetu pamoja hii itaniondolea sonona ambayo niko nayo itaniondolea mawazo mabaya kutaka kuchukua uhai wangu kwani sioni kuendelea kuishi endapo sitoishi na John naomba mnisaidie sana jamani niko chini ya miguu yenu, nisaidieni mimi na mwanangu nawaomba sana sana" Conso alipiga magoti kabisa ikiwa ni ishara ya kulisindikiza ombi lake, wapo wamama waliolia, wapo waliojikaza ila hawakuweza kuacha kuumia ndani kwa ndani Conso alijua kutubebesha huzuni iliyo kuu kabisa.
Mdogo ake na John aitwae Selemani ila jina ambalo wengi tulizoea kumwita ni Sele, ni bhange bhange hivi hakuweza kuvumilia alimfikia Conso na kumchapa vibao vya moto sana, watu walimshika ili asimwumize Conso, kanisa lilikua katika hali ya ukimya, John aliwaza cha kuongea ila alikua anashindwa aliinamisha macho chini. Diana kumwona John katika hali hiyo alishindwa kujizuia alijikuta anaanguka chini na kuzimia mambo yalikua makubwa na mazito ambayo alishindwa kuyahimili. Waumini wa kanisa waliokua wauguzi walimbeba Diana kumpeleka Zahanati ya kanisa, mchungaji alimwomba John asitoke ili aweze kusema kile anachokifahamu. John ulimi ulikua mzito sana kuzungumza ni kama hakujua atetee vipi ili aweze kueleweka, sauti ya mwanaume mwingine ilisikika huyu ni mdogo mwingine wa John aliitwa Peter alikua mtaratibu kuliko Sele ambae akili yake huichetua kwa pombe na bhange.
Peter aliomba nafasi ya kufafanua ni kipi alichokua nacho cha kuweza kuleta mwanga na kubalance mizani katika jambo hilo.
"Mchungaji ahsante mimi ni daktari wa binadamu hiyo ndo kazi ninayoifanya kwa muda mrefu kidogo, hapa nipo kuthibitisha kidaktari pia kiteknolojia kwamba huyu mtoto si damu ya John, naomba muwe makini kunisikiliza na kama ikiwezekana nishikishwe biblia hapa na niweze kuapa kama nitakachosema ni uongo bhasi nianguke hapa hapa na nife" Peter aliongea kwa kujiamini sana, ni kama kanisa liligeuka mahakama kwa muda mfupi, mchungaji alizuia swala la kuapa ila alimpa nafasi Peter aweze kuthibitisha juu ya maneno yake kwanini anasema mtoto wa Conso si wa John, patamu hapo.
Itaendelea.........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi