π§ππ§πππ’ ππ¨ππͺπ ππ‘ππ‘ππ’ππ’π£ππ¦ππ SEHEMU YA 7 "Niko zanzibar Cuzo, nakula maisha kidogo" "Mmmh weee Diana
"Heee usiniambukize uoga, najua mama atakaa wiki moja huko kwa mumewe, wacha na mimi nifurahia maisha ndo muda wangu wa kufurahi hivyo, emu badqr kidogo tunataka twende forodhani hapa" Diana aliniaga na kukata simu niliishia kuguna tu mwenzangu hakuonesha kuwa na woga hata kidogo juu alichokua anakifanya cha kusafiri bila kuaga, alichowaza yeye ni kufurahia maisha kwa madai kwamba ndo umri wa kuiponda raha kwa uwezo wote, wauza madini hawa John na Meckson walionesha kuwa na pesa, kwao pesa halikua jambo gumu kuitoa.
Niliend jikoni kwaajili ya kuandaa chakula cha mchana, kidogo Meckson alinifuata jikoni, aliniuliza kama nimewasiliana na Diana nikamjibu ndio nimewasiliana nae.
"Ooh sawa vipi hufikirii twende Zenji kama Diana na John au hata Africa ya kusini tukale maisha siku mbili tatu dear?" Meckson aliniuliza.
"Mmmh hapana kwakweli, kwani unajua kama wamesafiri?"
"Ndio najua wamesafiri tangu jana ni vile sikutaka kukwambia maana ningekwambia ungelianzisha turudi nyumbani usiku wa jana ungegoma kabisa kulala pale hotelini"
"Hahaha wewe bhana" tulijikuta tunacheka pamoja kwenye mapishi yangu kuna viungo havikuwepo kwenye friji, hakukua na kitunguu wala hoho, nilitaka kwenda kununua ila Meckson alinizua na kunambia ataenda mwenyewe kuninunulia, jamani nilimzuia ila alibisha kwamba atakwenda yeye hataki niteseke akaenda mbali zaidi na kudai ananifanyia mapenzi ya tanga ili moyoni mwangu pasibaki na chumba hata kimoja, nilibaki nacheka tu, nilijihisi moyo wangu unafunguka zaidi mbele yake, sikua na sababu kubwa ya kumpenda ila furaha aliyokua ananipa kwangu ilikua inatoshea kabisa.
Alikwenda gengeni na kurudi haraka eti ananiomba msamaha kwa kuchelewa kurudi wakati hakua amechelewa hata kidogo, nilibaki naguna na kucheka ila penzi jipya lina ushatq shata wake, tulipika pamoja bila kutegeana, akaniahidi mpaka kufua tutakua tunafua pamoja kama yeye anafua bhasi mimi nasuuza au mimi nqfua yeye anasuuza, nikamwambia huo utapeli tu wa kutaka kunifungia ndani na akishanioa ndio nitajua majukumu hayo ni yangu peke angu tulicheka, ugali nyama alikua tayari, tulimwita mlinzi kuja kula nae kwani Meckson alikataa tusimpe chakula peke ake kwani nae ni mwanafamilia mwenzetu.
Mlinzi alifurahi sana kula pamoja na sisi mezani kwani tangu aanze kulinda hapo ndo mara ya kwanza kukaa mezani kula chakula na watu wa familia, mlinzi alikua anachekesha sana ongea yake na stori za uongo na kweli alizokua anatupatia.
"Kaka huyu mwanamke nitamuoa, sioni kama kuna mwanamke mwingine anaeweza kunifaa mimi kwenye haya maisha isipokua yeye, nikuombe jambo moja ikitokea kijana yeyote kaja kumuulizia huko getini, usiwakutanishe maana ataniibia bure na mimi sitaki kuibiwa jamani nitaua mtu, nimemuwahi huyu hahahaha" maombi ya Meckson kwenda kwa mlinzi yalikua yanachekesha sana hivyo tulijikuta tunacheka kwa pamoja baada ya kumaliza kula, tulishushia kwa juice ya mchanganyiko wa matunda.
Meckson aliniomba tujiandae tutoke tena, nilimuuliza wapi tunaelekea, alinijibu ni kumbi ya cinema pamoja na eneo lingine la kula Ice cream ambapo tutatazama na mpira wa kikapu(basketball) ni mchezo aliokua anaupenda sana.
Mimi nilimwomba tusiende huko kwani sikua na amani ya hizo safari za mfululizo, sikua nimezoea bata, mimi wa ajabu kwelikweli.
Nilitoa pendekezo lingine kwamba twende kituo chochote cha kulelea watoto yatima ili tukawaone watoto hao, niliamini safari hiyo itanipa furaha. Meckson hakukataa bali alinipongeza kwa wazo zuri sana hivyo tulijiandaa, tukaingia kwa gari, tulipitia madukani ambapo tulinunua vitu mbalimbali vya kupikia, nilikua mwingi wa furaha kwani mambo hayo ya kuwatendea wema watoto yalikua kwenye ndoto yangu ila sikujua nitaitimiza vipi ndoto hiyo.
Baada ya kumaliza tulikwenda mpaka kituo kimoja cha watoto kinaitwa Mtima Orphanage Centre, tulipokelewa vizuri sana na watoto, walituimbia kwa furaha kubwa sana.
Wakati naangaza angaza macho huku na kule nilimwona mwanaume fulani, huyo mwanaume alinipa hisia mchanganyiko, hisia hizo zilinifanya nikumbuke siku za nyuma, sikua sawa tena.
Itaendelea.......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi