AAAAAAAH IMETOSHA BOSSππ SEASON 02 (21_25)
Pendo kwanini unafanya hivyo Kwa mgeni!? Aliniuliza da Prisca! Mtoe huku mpeleke chumbani kwake! Daddy aliamuru nipelekwe chumbani kwangu! Da Prisca alinishikilia mkono akanipeleka chumbani kwangu!
""Pendo Kuna Nini kati Yako wewe na huyo handsome!?""
""Siyo handsome dada muite Mika ""
""He is your boyfriend ππ"
""No"
"" So why ukamfanyia hivyo!? Ni ex wako""
""Hapana Dada ππ,""
""Niambie kitu mdogo wangu huyo ndo aliyehusika na utekwaji wa wazazi wetu!?""
""Hapana siyo yeye""
""Sasa kwanini ufanye vile mbele ya daddy and Mom!?""
""Dada Niache peke Yangu ""
""Umeshakua ehππ""
""Dada nimesema ondoka chumbani kwangu Niache peke yanguπ°π°""
Da Prisca aliondoka kule chumbani Kwangu nikafunga mlango nikawa nimelala zangu nilikuwa na hasira Hadi kichwa kilikuwa kinawaka Moto! Pendo fungua mlango Binti Yangu alikuja niita Mom nilikataa kufungua mlango Niliwaomba waniache peke yangu ππ Mom alinibembeleza Hadi nikafungua mlango alinikumbatia π« Kuna Nini pendo kwanini umefanya vile sijakulea hivyo mwananguπ₯Ίπ₯Ί I'm sorry Mom haitojirudia tena π§π§ Kuna ugomvi Gani kati Yako wewe na Mika!? Mama nilikuwa tu na hasira Yani najikuta namchukia Kila mtu kutokana na hiki kilichowakuta nyie wazazi wangu ππ namhisi Kila mtu aliyeko Karibu yanguππ hapana Binti yangu hautakiwi kufanya hivyo hiyo kazi waaachie police kipenzi changu wao watawakamata watuhumiwa wote waliohusika kututeka sisi usirudie Tena kugombana na marafiki zako Kwa sababu hiyo! sitopenda kuona ushenzi kama huo Tena ukijirudia! I'm sorry Mom sitorudia Tena kufanya hivyoπ’π’
Haya tuombe kwanza ili tuweze kukemea hiyo roho ya chuki inayojinyanyua rohoni kwako Alf baada ya Hapo utakwenda kuomba msamaha Kwa Mika kabla hajaondoka! Msamaha π₯Ίπ₯Ί mama utanisamehe lakini siwezi kumuomba Mika msamahaπ pendo Mimi ni mama Yako Alf tambua ya kwamba wewe ni Binti hautakiwi kuwa na tabia za hovyo ukiwa hivyo utaolewa na nani!? Yani hata kijana ambaye tulishaanza kumtarajia huenda yeye ndo akawa mchumba wako Leo hii unakuja kumfanyia vile mbele yetu ni tabia Gani hiyo hujui kama unanidharilisha hata Mimi mama Yako!? Unataka nichekwe kuwa cjy kulea!?
Mama yangu aliongea sana nilimkubalia nikamwambia sawa mama nitakwenda kuomba radhi Kwa Mika nilichukia kinyama Yani sema wazazi wangu walikuwa hawajui kile kinachoendelea tuliomba pamoja na Mom baada ya Hapo nilitoka Hadi pale sitting nilianza kuomba radhi Kwa Mika ππ I'm sorry Mika Yani nivile tu nimechanganyikiwa kutokana na kile kilichowakuta wazazi wangu ninamuhisi Kila mtu kuwa ndo mhusika nisamehe Kwa kukuumiza Mika ππ
Ucjali Pendo naelewa et haukutakiwa hata kuomba msamaha Kwa sababu Mimi ninaelewa vile unavyojisikia! Mika aliendelea tu kuleta maigizo kule ndani kwetu alizidi kuuchota uaminifu mkubwa kutoka Kwa wazazi wangu na kweli alifanikiwa Kwa Hilo Kwa sababu wazazi wangu walimwamini sana Mika walimuona kama kijana wa kisasa Mwenye heshima na adabu mpole aliyefunzwa vyema lakini hawakujua ya kwamba Mika ni tofauti na vile walivyomdhania! Pale nilipomchana Mika tayari Mom alikuwa kaishamsafisha kampaka dawa kamfungia na bandage! My mom Huwa ni nurse! Na pale nyumbani Huwa vipo vifaa vingi pamoja na dawa za kumsaidia mtu Kwa huduma ya kwanza!
Baada ya kumuomba Mika msamaha nilifanya vile tu Ili kuwaridhisha wazazi wangu lakini sikufanya Kwa moyo wangu! Baada ya kumuomba msamaha yule shetani niliwaomba radhi wazazi wangu make hawakupenda kabisa kile nilichokifanya but najua tu ni vile hawakujua nilifanya kwanini lait wangelijua Nina Imani wangejiunga nami kumuangamiza yule ibilisi Mika! Mida ilizidi kwenda Hadi saa sita ndo Mika aliaga kuwa anaondoka pale nyumbani kwetu Yani sikutaka kulala bila Mika kuondoka kwetuπ€£π€£ hachelewi kutuchomea ndani yule mshenzi! Mika aliaga akawa ameondoka tulifunga milango tukaingia kulala! Kesho yake asubuhi Mimi ndo nilikuwa wa kwanza kuamka na kwenda kufungua mlango nilitaka niwahi kujiandaa Ili niweze kuwahi kazini kama mnavyojua kamoyo kangu kote Kako Kwa boss Paschal ππ na vile na yeye kaishaanza kunielewa basi sikutaka Kabisa kumkera Kwa kuchelewa kazini Yani nilitamani tu niwahi kazini Ili niende nikaonane naye anipe kissππ nampenda ππ vile akiwa ananipa denda mwili wote Huwa unanilegeaππbaada tu ya kufungua mlango nilikutana na kitu Cha ajabu sana pale mlangoni kwetu nilipiga yoweππ Mom & Daddy waliamka haraka kuja kuangalia ni kipi kilichonisibu Hadi nipige mayowe walifika pale na wenyewe wakabakia vinywa wazi......
Kuna Nini Jamani mbona mayowe na asubuhi yote hii!? Aliuliza da Prisca! Alifika pale tukampisha na yeye asogee ajione ilikuwa ni cake ndefu kubwa tu Ile cake ilikuwa imetapakaa damu nyingi Kila kona pale kwenye cake kulikuwepo na kisu kilichokuwa kimejaa damu na kilikuwa kimechomwa katikati ya Ile cake!....... Cake ilikuwa imewekwa mlangoni Iko juu ya box! Nini hiki Mungu wangu!
Kila mmoja katika familia yetu tulibaki kuulizana tuliogopa hata kuigusa Kila mmoja wetu aliogopa kukatiza pale katika ule mlango Yani hakuna hata Mmoja aliyeweza kutoka nje wote tulirudi ndani tukaufunga na ule mlango hakuna aliyerudi chumbani kwake kulala wote tulibakia kule sebleni tuliungana tukawa tumeanza kufanya maombi uoga ulimtawala Kila mmoja kati yetu! Simu yangu iliita ikiwa chumbani wote tukashtuka pale sebleni ππ Yani Kila mmoja aliogopa kule ndani! niliogopa hata kwenda kuichukua simu yangu chumbani kwangu ππ
Pendo ni simu Yako inaita.... Aliniambia Mom.... Acha tu iite mom Mimi naogopa kwenda chumbaniπͺπͺ pigeni simu police waje kukitoa hicho kitu hapo mlangoni Mimi naogopa Kwa kweli sijui hata ni mambo Gani haya yanayoikumba familia Yangu Mungu wangu π₯π’ aliongea Mom! Twende nikupeleke uchukue simu Yako! Aliniambia Da Prisca
tulikwenda chumbani kwangu nikachukua simu Yangu alikuwa anapiga "my Boo" Nilipokea Ile simu Paschal aliniambia ya kwamba nitapita hapo Nyumbani kwenu kuwajulia Hali wazazi wako naomba ujiandae Ili twende wote ofisini my love! Hapana boo siwezi kwenda ofisini Yani mlangoni kwetu Kuna kitu Cha ajabu sana boss naogopa etπ° Kuna Nini Pendo;? Niambie kipi kimetokea!? Ni cake iliyojaa damu na kisu chenye damu kimechomwa kwenye hiyo cake tumeikuta Iko mlangoni kwetu boss naogopa et π° usiogope kipenzi changu basi subilia nipitie police nitakuja nao hapo Nyumbani waje kuiondoa hiyo cake nitawafungia na cameras hapo Nyumbani Kwa ajiri ya ulinzi zaidi nitaweka na mlinzi pia! Sawa boo Asante π΄ Paschal alikata simu! Nani huyo Pendo!? Aliniuliza da Prisca! Ni boss wangu Dadaππ boss ndo unamdekea hivyo!? Au mnadate!? Hapana dada ni boss wangu ni rafiki Yangu pia! Lakini pendo yule Mika ni nani Yako!? Mimi mbona nimeshaanza kuwa na mashaka juu ya Mika nini kilikufanya wewe kumchana Mika na kile kipisi Cha kioo kichwani kwake!? Hebu niambie ukweli mdogo wangu Kuna vitu havihitaji Siri pendo tutakuja kuwapoteza wazazi wetu angalia haya yanayoendelea yatawafanya kuugua pressure! Hebu niambie ukweli ni kwanini ulimjeruhi Mika!? Je Mika ndo mhusika wa hizi shida zote zinazotokea hapa nyumbani!? Hapana Dada π! Kama siyo ni kwanini Jana ulimletea fujo pale mbele ya wazazi wetu na nilikusikia ukiwa unamwambia aache unafiki na aondoke nyumbani kwetu na Kwa Yale maongezi ya Jana ya Mika yalikuwa ni ya kuwajulia wazazi wetu Hali ni kwanini wewe ulimuita mnafiki!? Pendo nakuuliza Tena ni Mika ndiye anayewatesa wazazi wetu waliohangaika na sisi Hadi tumekua wakubwa hebu niambie ukweliπ₯Ίπ₯Ί da Prisca aliivaa sura ya hasira hakutaka kunibembeleza Tena.... Pendo ukishindwa kuniambia ni kipi kinachoendelea basi Mimi na wewe Leo tunaenda kuuvunja undugu wetu hapa!π₯Ίπ₯Ί sitokutambua kama ndugu yangu Kwa sababu nahisi wewe ndo sababu ya haya yote! Nakuuliza Kwa mara ya mwisho je ni Mika ndiye mhusika wa haya matukio yote!? Ndiyo Dada ni Mika ππ°π yeye ndiye aliyewateka wazazi wetuπ₯.
Itaendeleaaaa.........
NO 22...23ππ
Ndiyo da prisca ni Mika Yeye ndo mhusika wa Kila kitu na Yeye ndiye aliyewateka wazazi wangu Ndiyo maana nilichukia Sana kiasi Cha kumjeruhi baada ya kumsikia Yeye akiwa anaendelea kuwainjoi wazazi wanguππ da prisca alinikumbatia tulijikuta wote tunatokwa na machoziπ°π° nisamehe mdogo wangu Kwa kukutishia kuvunja undugu na Wewe nimefanya tu hivyo Ili kukutisha uweze kuniambia ukweli! Tulikumbatiana Tena Dada aliniambia nakupenda Sana nitakulinda pia kutoka mikononi mwa Mika! Mika alikutongoza!? Ndiyo Dada alinitongoza lakini nilimkatalia siku ileile aliyonitongozaπ wow Vizuri Sana vipi msg za vitisho anazokutumia si unazo kwenye Simu Yako?! Ndiyo Dada ninazo lakini now naogopa kuendelea kuziona msg zake Kwa kuwa zinanifanya nikose uwezo wa kujiamini Ilinibidi niziondoe line zangu kwenye simu Ili nisiendelee kuziona msg zake! Ni Sawa nakuelewa mdogo wangu nipatie hizo line Mimi nitaziweka kwenye simu yangu nitazuia mtu yeyote kupiga nitabakiza mawasiliano ya njia ya msg tu nataka tuendelee kutafuta ushahidi zaidi wa kumtia mikononi mwa police huyu shetani mjaa laana! Nilizichukua zile line zangu nikampatia da prisca! Je huyu Paschal unamwamini!? Aliniuliza da prisca! Ndiyo Dada ninamwaminiππ ni nani Yako!? Niambie ukweli pendo Mimi ni dada Yako usinifiche kitu! Unampenda boss wako!? Ndiyo Dada nampenda boss Paschal ππ au Huyo ndo Sababu ya Mika kuleta maluweluwe kwenye familia yetu!? Hapana Dada sizani kama hiyo ndo Sababu Mimi nahisi nimeingizwa tu kwenye hii vita baada ya Mika kugundua ya kwamba Mimi ninampenda Paschal na siyo yeye! Lakini inaonekana Mika ana kisasi kikubwa na boss Paschal cjy hata ni kisasi Cha Nini lakini Mika alithubutu kunitamkia et alishawahi kumuua mwanamke wa Boss Paschal ambaye alikuwa ni mjamzito alikufa yeye na mtoto wake Mika ni katili Sana Dada naogopa asijeniua na Mimi π°π°!
Usiogope mdogo wangu Niko hapa na nitakulinda hatuwezi kukubali mtu mmoja kuvuruga amani yetu ya siku zote! Paschal alifika pale nyumbani akiwa na maaskari walikuja wakatuchukua maelezo wakaichukua Ile cake na kile kisu pamoja na box lake wakawa wameondoka! Boss Paschal alibakia akiwa anazungumza na da Prisca walifika wale watu wa CCTV camera wakaanza kutufungia camera pale nyumbani kwetu! Boss Paschal aliniomba nijiandae Ili tuondoke wote kwenda ofisini nilijiandaa nikawa nimetoka naye!
"" Pendo kwanini ukanifichaπ€¨π"'
""Nikakuficha Nini Boss!?""
""Kwanini hukuniambia mapema ya kwamba Mika ndiye mtesi wako kumbe Mika ndiye aliyeniulia Raya pamoja na Mtoto wanguπ₯Ήπ₯Ή""
""Duh kimeumana da Prisca kaishafanya yakeππniliwaza kimya kimyaπ""
""Huyu mshenzi atajutaπ¬π¬ aliongea Boss Paschal Kwa hasira huku akiwa anaongeza mwendo wa Gari niliogopaπ₯Ί boss tafadhari drive taratibu tutapata ajari etππ Paschal alilia alikuwa na hasira kiasi kwamba alitamani kushuka atembee Kwa miguu make aliona ni kama gari haliendi Kwa Kasi anayoitakaπ«£π«£ nilitetemeka gari ilikuwa inakimbia Ile Yani ni shwaaa shwaaaaa kiroho changu nilikiweka mkononi Kwa muda lolπππ gari ilienda kuweka kituo ofisini Kwa Mika ππ boss tafadhari niahidi ya kwamba utaweza kuzizuia hasira zako nakuomba please Niko chini ya miguu Yako π§π§ hapana pendo siwezi kukuahidi kitu kama hicho tafadhari nakuomba ubakie kwenye gari!
Boss Paschal alitelemka pale kwenye gari akatembea kuelekea kule ofisini Kwa Mika nyie nyieeeeeeee mwanaume alikuwa na hasira Hadi mikono Ikawa inamtetemekaπ€¨π€¨ Paschal aliita wewe mwana haramu Toka nje upambane na Mimi! Wafanyakazi wote wa kule kazini Kwa Mika walitoka nje kuja kumshangaa huyo anayefoka hapo ofisini ni Nani!? Nilichukua cm yangu haraka nikamtafuta mama Paschal nilimwambia aje haraka katika Ile campuni anayofanya kazi Mika nilimtajia jina nikamuomba afike pale aliniuliza Kuna Nini nikamwambia Boss Paschal anaonekana kuwa na hasira sana nahisi Kuna kitu hakiko sawa kati yake yeye na Mika tafadhari Mom nakuomba ufike haraka! Nilimaliza kuongea na mama yake Paschal nikakata simu nikawa nimetoka kwenye gari Mika alivyoniona alicheka sana akamwambia Paschal Kwa hiyo umekuja kunikolomea ofisini kwangu Kwa sababu ya huyo Malaya!? Aliongea Kwa dharau sana Hilo jambo lilimkera sana Paschal alimtwanga Mika ngumi ya pua damu zikasambaa mahari pale alimuongezea ngumi ya kichwani Alf alimtusua palepale nilipomjeruhi na kile kipisi Cha kioo πππ damu zikaanza kumwagika kama Bomba la maji lililoachwa wazi kama mnavyojua siku hizi mnaweza kuuana na watu wasiwasaidie wafanyakazi pale ofisini ndo kwanza walikuwa busy kurecord lile pambanoπ nilisogea pale Karibu Yao nikamwambia Boss Paschal please stop itππ Mika alinishona teke la kiunoni nikaenda kudondokea kuleeeee alikuja Boss Paschal kuniokota pale chini na hapo ndipo Mika akawa amepata upenyo wa kumshughulikia Boss Paschal Mika alikuja akaivuta Ile tai ya Mr paschal Kwa nyuma akaanza kumnyonga my Boo Mika ni mkubwa Kwa Paschal japo wote miili Yao imejazia lakini kiumri Mika ni mkubwa nilianza kupiga kelele nikiwa pale chini nilimuomba Mika amuachie Boss Paschal lakini hakumuacha nililia huku nikiwa namuomba Boss Paschal apambane Ili Mika asije akamuuaπ°π’ Kwa bahati nzuri wazazi wa Paschal walifika pale eneo la tukio baba Paschal alichefukwa sana baada ya kumkuta mtu waliyemzania kuwa ni Rafiki wa Mtoto wao akiwa anamnyonga kijana wake bila hata uogaπ³π³ yule Mzee wa kizungu aliichomoa bastola akaikoki then akainyoosha kuelekea pale alipokuwepo Mika! Kila mtu pale alilala chiniπ₯²π₯²
Baba paschal alimuamuru Mika amuachie Mtoto wake vile Mika anashangaa shangaa Boss Paschal sangapi asimzime na ngumi ya jichoπ₯²π₯² jicho lote likawa jeusi duh usiombe ukawashuhudia wanaume wakiwa wanapiganaππ baada ya Boss paschal kumshona Mika ngumi ya jicho Mika alidondoka chini Paschal alianza kumnyonga Mika huku akiwa anasema muuaji mkubwa wewe Leo nakuua mama Paschal alikimbia kwenda kumzuia paschal asijeua Mika alivyomuona yule mama alimwambia muache aniue usimuzuie au umesahau kama wewe ulishaniua hapo kablaπ₯Ίπ₯Ίnakuchukia sana wewe mwanamke najuta kuzaliwa na shetani kama wewe niueni make katika maisha yenu mlishaniua tayari nawachukia natamani hata mteketee muondoke katika uso wa hii Dunia!
Eh unaongea kuhusu Nini Mika π±π± Kila mmoja pale alibakia kinywa wazi hata Paschal alibakia na mshangao! Mom Anaongea kuhusu Nini huyu muuaji hawezi kuwa ndugu yangu huyu aliniulia Mtoto wangu momππ huyu ndiye aliyemuua Raya tafadhari mama Naomba ukanushe huu uzushi wake anajaribu kutafuta huruma tu Kwa kudai et wewe ndo uliyemzaa mama huyu ni shetani usije ukamsikiliza anafaa kwenda jera alimuumiza Hadi pendo aliwateka hata wazazi wake na Bado hakuacha kupeleka vitu vya kutisha katika familia ya akina pendo mama huyu mtu ni muuaji hafai kuishi katika Jamii Yani boss aliongea Kwa hasira Hadi baba yake akadondokwa na machozi baba yake alimkumbatia Paschal akamwambia be strong my sonπ’π’ mama Paschal alichanganyikiwa baada ya Mika kumtamkia et anajuta kuzaliwa na shetani kama Yeye Mika aliendelea kutukana na kuongea bila kituo Boss Paschal aliinama pale akamuokota Mika na kuanza kumsokota ngumi za tumbo mama Paschal uvumilivu ulimshinda alimwambia Paschal huku akiwa analia mwanangu tafadhari acha kumpiga usimuumize mwenzako mama paschal alimshika Paschal Ili asiendelee kumuumiza Mika! Alimsogelea Mika pale akamuuliza ni Wewe ππ hapana sizani kama atakuwa hai alikufa hayupo Tena siyo wewe yule mama alipoteza fahamu maaskari walifika pale walipigiwa simu na wafanyakazi wa kule kazini Kwa Mika! Mimi na Boss Paschal tulimuwahisha mama paschal hospital Alf Mika na baba yake Paschal bila kuwasahau maboss wa pale kazini Kwa Mika walichukuliwa wote kuelekea kituo Cha Police Mimi na Boss baada ya kumfikisha Mama yake hospital Boss Paschal aliondoka kuelekea kituo Cha Police Mimi nikawa nimebakia kule hospitalini kumuangalia mama paschal nilitamani sana aamke Ili anielezee ilikuwaje kuwaje Hadi Mika akatamka vile!? Kwani mom Paschal alishawahi kuzaa Mtoto mwingine??
Itaendeleaaaa......
NO 24...25ππ
Ilikuwa ni mida ya saa Moja jioni ndiyo mida ambayo mama yake Paschal alirudiwa na fahamu zake..... Mamaaa nilimuita huku nikiwa naugusa mkono Wake...... Uko sawa mama!? Vipi Hali Yako unajisikiaje Kwa Sasa tafadhari nakuomba utulie Mimi nakwenda kukuitia doctor nilitoka haraka na kwenda kumuangaza doctor huko katika wodi zingine samahani doctor yule mgonjwa katika wodi namba Saba amerudiwa na fahamu zake muda si mrefu! Sawa Binti basi nenda ukamuangalie Mimi nachukua vifaa vyangu ofisini mara Moja nitakuja huko muda si mrefu! Sawa doctor nilimuitikia doctor na baada ya Hapo nilirudi kule aliko mama yake Paschal! Nilimchukulia na maji ya kunywa nikawa nimempelekea tafadhari mama nakuomba unywe hata maji huku ukiwa unaendelea kumsubilia dactari! Asante sana pendo alikunywa maji na baada ya Hapo nilimuuliza swali samahani mama paschal hivi Mika ni Mtoto wako Kweli!? Na kama ni mtoto wako ni kwanini haukuwatambulisha wakafahamiana!? Ulipaswa kuwakutanisha Ili wafahamiane Yani kiukweli cjy hata nawaza Nini mama yangu hivi uliwezaje kuwatenganisha watoto wako wa kuwazaa Mwenyewe hivi ilikuwaje kwanza Hadi Mika akawa mtoto wako??! Pendo ni kweli Mimi nilishawahi kuwa na mtoto enzi za ubinti wangu lakini ukweli yule mtoto nilimtupa baada tu ya kuwa nimemzaa Yani sikutaka Kabisa kuwa mama Kwa kipindi kile ilikuwa ni mambo ya ubinti tu kufanya mapenzi kama starehe lakini Kwa bahati mbaya nilinasa mimba na baada ya kuipata Ile mimba niliogopa hata kuwashirikisha watu wa nyumbani kwetu nilifanya hivyo Kwa sababu baba yangu alikuwa ni mkali sana na pia alikuwa ni mchungaji nilificha Ile aibu katika familia Kwa sababu familia yangu walikuwa wakiniamini sana sikutaka kupoteza uaminifu wao kwangu!
Hata baada ya Ile mimba kufikia miezi Tisa nilienda katika geto la rafiki yangu ambaye nilikuwa nasoma naye chuo kipindi hicho Mimi nilikuwa nakaa hostel lakini yeye alikuwa amepanga chumba nje ya chuo! Nilienda kwake nikawa nimejifungulia huko Kwa kuwa yeye alikuwa anachukua course ya udactari basi aliweza kunizalisha bila shida yoyote! Baada tu ya Mimi kujifungua nilimdanganya Rafiki yangu ya kwamba baba wa Mtoto anataka Mimi nimpeleke Mtoto wake Ili akamuone ampatie na Jina! Rafiki yangu alitaka kunisindikiza lakini nilimzuia! nilikwenda peke yangu Hadi Katika kichaka ambacho ndicho nilichomtelekezeapo Mtoto wangu! nilimtupa mwanangu bila kujali lolote baada ya Hapo nilirudi kule getoni Kwa rafiki yangu alivyoniuliza Mtoto nimempeleka wapi nilimdanganya kuwa Mtoto amechukuliwa na baba yake hakufuatilia sana ila alichoniambia ni kwamba lakini ungekaa Nako hata mwezi mmoja tu ukanyonyeshe maziwa ya Mama! Niliendelea kumdanganya nikamwambia kuwa baba yake amemng'ang'ania ikabidi nimpatie tu! Nililala hiyo siku kesho yake nilirudi kwenda kuchungulia kule nilikomtupia mwanangu lakini sikumkuta pale katika Ile sehemu nilijua huenda tayari ameshakufa Kwa kuliwa na wanyama ! nilirudi kule Kwa Rafiki Yangu aliendelea kuniuguza Hadi nikamaliza wiki tatu nikawa nimerudi chuoni niliendelea na masomo japo sikuwahi kuwa na Amani ya moyo kutokana na hicho kitendo nilichokifanya !
Mara Kwa mara nimekuwa nikirudi kule katika Ile sehemu nilikomtupia mwanangu Ili kwenda kuangalia kama naweza hata nikamkutapo kimiujiza lakini haikuwa hivyo niliendelea kuamini kuwa mwanangu ameshakufaπ’π’ pendo sijawahi kumwambia mtu yoyote hiki kitendo Cha kikatili nilichokifanya Kwa Mtoto wangu wa kumzaa kimekuwa kikiishi ndani ya moyo wangu na kusema kweli ckuwahi kuona Raha ya kuishi japo nilishatubu sana hiyo dhambi naona aibu Mimi ni mama wa aina gani nitawezaje kumtizama Paschal machoni nitawezaje kujitetea Kwa Mika Mimi wanangu hawatonielewa nakuomba wewe pendo ndiye ukawe kiungo katika familia yangu waunganishe watoto wangu Paschal na Mika wapate kuelewana Naomba uniombee radhi Kwa watoto wangu wote waambie ninawapenda sana eh yesu wangu uliyejitoa msarabani Kwa ajiri ya kutufia sisi wa dhambi nakuja mbele zako Mimi mkosefu Naomba unisafishe dhambi zangu nifutie makosa yangu yote Kisha jina langu uniandike katika kile kitabu Cha uzima wa milele baada ya mama paschal kuongea hivyo alianza kurusha rusha miguu na mikono yake nilikimbia haraka kwenda kumuita doctor nilikutana na doctor akiwa na vifaa vya vipimo alikuwa anakuja huku katika wodi aliko mama paschal doctor nilimuita huku nikiwa naogopa machozi yalianza kunitoka nilibanwa na kigugumizi nilijikuta nimeshindwa kabisa kuongea doctor alinipita huku akiwa anakimbia kuelekea wodini Kwa mama paschal nami nilimfuata nyuma tuliingia kule wodini lakini ilikuwa tayari mama Paschal ameshaaga Dunia!
Mamaaaπππ nilimuita huku nikiwa namgusa kichwani kwake lakini hakufungua hata macho yake maaaaaaaaaaaam mam please Mimi peke yangu sitoweza kuwaunganisha Paschal na Mika mom kumbuka paschal ana hasira sana Juu ya Mika mamaa kwanini umeniachia kazi ngumu kiasi hichoπππ yule doctor alinikumbatia akaniambia mtangulize Mungu huyu mama hajakuachia hayo Kwa matakwa yake ni Mungu ndiye amependa wewe ndo uifanye hiyo kazi! Nilitolewa nje ya Ile wodi Jamani Jamani kumbe mtu anakata roho vile duhπππ nilikuwa nawaza tu namna ya kumwelezea boss Paschal ya kwamba mama yake hayupo Tena Katika Dunia hii! Mom Paschal alipelekwa katika chumba Cha kuhifadhia maiti Bado niliendelea kujipa matumaini ya kwamba ataamka huenda atakuwa tu kazimia niliendelea kujipa muda nikijua mama yake Paschal ni lazima tu ataamka muda ulizidi kwenda! Ilikuwa ni saa Moja za jioni pale hospital ilikuja gari nyeusi aina ya range ilikuwa ni gari ya boss Paschal alipeleka gari parking akaiegesha vizuri na baada ya Hapo alitelemka kwenye gari akawa anatembea kuja pale nilipokuwa nimekaa alikuwa Wala hajabadiri zile nguo zenye damu zilizoloana damu kipindi wanapigana na Mika! Nilisimama nikamkumbatia huku nikiwa nalia!
""Usilie et tayari yule mshenzi ameshawekwa nyuma ya nondo hatokusumbua Tena Wala kukutisha! Aliniambia Paschal bila kujua kinachoniliza ni kitu Gani!? kama kawaida ya my Boo alihitaji nimpoze na deeply kiss Kila alipozisogeza lip's zake mdomoni kwangu Mimi nilizikwepesha za kwangu Bado nilikuwa naendelea tu kulia "mine" aliniita boss Paschal Kwa sauti ya chini sana! Kwanini unaliaπ’π’ aliniuliza my Boo nilishindwa kumwambia et nilishindwa π mida hiyo hiyo alikuja baba yake na paschal hospitalini pale nilimkimbilia baba paschal nikawa nimemkumbatia alinifuta machozi akaniambia pole sana Binti yangu tayari Mika ameshakamatwa na police ni mshenzi sana kumbe! Yani ni kijana mpumbavu sana na ni katili kupita kiasi! lakini atalipia Kwa hayo yote aliyoyafanya!
Daddy samahani najua wewe ni mtu mzima na utaelewa hiki ninachoenda kukwambia nimeshindwa kabisa kumwelezea Paschal Kwa sababu sijui vile atakavolipokea swala hili kitu Gani Pendo Daddy achana kwanza na habari za Mika daddy ni Mom amefa...... Ameeeeee....... Amefarikiππππππππ whatπ’π’π’π’ Nancy nooooo nooooooo hapana Nancy hawezi kuniacha Mimi na Mtoto wetu tuliahidiana ya kwamba tutabakia wote hawezi kutuacha yule Mzee alichanganyikiwa Paschal ni kama vile tayari alisikia kitu alichuchumaaa pale pale alipokuwa amesimama akawa anadondosha machozi yake ardhini nilisogea pale Karibu yake nikamuita bossππ alitikisa tu kichwa chake akasema nooooo niambie ukweli mamangu hajafa pendo si et πππ Pole sana boss Paschal lakini tayari Mom ameendaπππ nilimkumbatia Paschal nilimwambia tafadhari boss Naomba ujikaza maskini aliumia sana boo wanguπ’π’ kweli hata Mom ameniacha Mimi πππ why Mom kwanini hata hukuniaga Mom why! Baba Paschal alikuja akamnyamazisha kijana wake anampenda sana! Tuliondoka pale hospital tukaenda kuweka msiba nyumbani Kwa wazazi wa Paschal! Muda wote nilikuwa nawaza tu namna ya kumuelewesha Paschal ya kwamba Mika ni ndugu yake! Nilimuomba baba paschal pamoja na Paschal Ili tukae kikao kidogo nilitaka kuwashirikisha juu ya kile ambacho mama Paschal maarufu kama Nancy aliniambia niiambie familia yake kabla hata ya mazishi yake!
Baba na mwana walikubali kukaa kikao namimi nikawa nimewaelezea Kila kituππ Kila mmoja alisikitika Paschal alikataa katakata ya kwamba Mika hawezi kuwa ndugu yake na Wala hawezi kumsamehe Kwa makosa yote aliyomfanyia! Nilijaribu kumsihi na kumuelewesha lakini alikataa Kabisa!
Baada ya mazishi ya Nancy ambaye ni mama yake na paschal............................
--------------------------------------------------
Ilikuwa ni mida Fulani hivi ya jioni nilitoka kazini na kurudi nyumbani kwetu lakini pale nyumbani nilikutana na ugeni wa ghafla sana! Nilipoingia pale nyumbani kwetu mama yangu alianza kupiga vigeregere na kuja kunipokea mkoba wangu alinikumbatia na kuniambia hongera sana mwanangu unaenda kutuheshimisha aririririiiiiiiiiiiiii shangazi yangu alikuja akanikumbatia na kuniambia hongera sana mwanangu hongera aririririiiiiiiiiiiiii nilibaki mdomo wazi huku nikiwa najiuliza ni Nini kinaendelea mahali hapa! Kulikuwepo na shamra shamra kama vile Kuna kishereheπ Shangazi yangu alinishikilia mkono akanipeleka ndani kule ndani nilikutana na wazee wanne pamoja na vijana mahandsome wazuri sana wawili pamoja na baba yangu, mjomba wangu na baba mdogo wangu! Niliwasalimia wale watu wote pale sitting room baada ya Hapo baba yangu aliniambia mwanangu pendo umekua Sasa mwanangu na sisi tunatamani kukuona ukiwa na mji wako kama dada Yako Prisca! Huu ugeni hapa ni Kwa ajiri Yako Binti Yangu! hii ni familia ya Mzee kasim kasimir kutokea nchini South Africa wamefika hapa nyumbani Kwa ajiri ya kuja kukuposa Wewe Binti yetu kiukweli tunajivunia sana Kwa tabia Yako njema uliyonayo Kwa kuwa hiyo ndiyo iliyoivutia familia hii kuja kuomba kijana wao aoe katika familia yetu! Wale wazee walijitambulisha kwangu Yani ni wazee wa heshima siyo watu wa mchezo mchezo walijitambulisha wote aliyekuwa wa mwisho kujitambulisha alikuwa ni huyo kijana muoaji ambaye anaitwa Hakim alisimama akanisogelea alinipatia mkono π€ I'm Hakim! I'm Pendo wow Pendo Nice nameππ Hakim alinikumbatia na baada ya Hapo alirudi pale katika siti yake ni mkaka kama wa kiarabu hivi na hata hao wazee waliokuja nao ni weupe kama waarabu! Nilijiuliza maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu Kwa muda ule...
Itaendeleaaaa......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi