*DAKTARI WA JESHI SI UNGENIOMBA TUU* Chapter 19&20
Nikatoa macho, maana kwa kumbukumbua zangu ni ile mara moja tu ndio alikutana na mimi kiumwili, sasa anaposema kuwa amekuwa akilala na mimi kwa muda mrefu sikuwa nimemuelewa amemaanisha nini..
nilijenga ghorofa na kuelekeza dirisha la chumba changu sehemu ambayo ningeweza kukuona vyema ukiwa kwenu, na kwe.i nilifanya hivyo, nisamehe mke wangu maana nimejichukulia sheria mkononi mara nyingi kwa kukuchungulia dirishan bila wewe kujua, nilikuwa natakan nilale na kuamka na taswira yako kila siku, akasema....
ila wewe mwanaume sikuwezi, nilishangaa kweli kuona ukikaa pale chumban kwako unaona kila kitu kwenye chumba changu, nikasema nisijipe mawazo yasiyo ya msingi, kumbe hata hilo ulilifanya kimkakati, shikamoo zako. comrade, nikasema nikiwa nacheka, nikagundua kuwa mume wangu alikuwa ananipenda sana, na hata mambo yote ambayo ameyafanya ameyafanya kwa upendo mkubwa sana kwangu, hivyo nitakuwa nakosea sana nikisema nimuhukumu, basi nikamsamehe na maisha. yakawa yanaendelea...
Baadae nikaja kugundua kuwa nidaktar wa jeshi, maana sikuwa namuelewa maana kuna muda nilikuwa namuona kama muuguzi na muda mwingine ninamuona na magwanda yake ya kijeshi, siku moja kwenye story zile za kuchangamshana, nikamuuliza " ile siku ambayo ulinikula, kwa mfano ungekuja na kunambia, alice naomba shoo, unafikiri ningekataa na ulivyo mtanashati hivyo..
weeee nilikuwa nakuogopa kinyama, yaan sikuwa najua kama ukimpenda mtu sana kuna namna unakuwa unamuogopa, mimi ndio nilikuwa hivyo kwako, akajibu..
"yaan nilikuwa nakupenda ulikuwa hujui tu, ila kwa sababu ulikuwa unanipuuza nikaamini kuwa una mwanamke wako, sikutaka kuyaharibu mapenzi yako, ila niwe mkweli tu daktari wa jeshi kwa namna nilivyokuwa nakupenda ungeniomba tu mchezo uone kama ningekunyima, tena ningekupa nikiwa na kumbukumbua za nimelala na nani, nikasema..
unaongea sasa hivi kwa sababu mambpo yameshapita, na kwa namna nilivyokuwea nakuona una mdomo mrefu, nina uhakika. ungenichamba mpaka nizimie, akajibu tukajikuta tunacheka tu, nikawa namsisitizia kuwa angeniomba tu, ili mchezo uwe wa maridhiano, ila alikataa kabisa kukubaliana na mimi, kuwa angeniomba ningekubali....
Basi maisha yetu yakawa yanaendelea kama kawaida, na familia ya mume wangu mara baada ya kujua kuwa Solomon ndio aliniingilia kwa nguvu na kunibbesha mimba ambayo niliamin kuwa sikuwa namfahamu baba ni nani, basi waliacha maneno, na wakaja kuniomba msamaha, nikawasamehe ila kiukweli sijui kama nilifanya jambo sahihi au laa, maana sikuwah kutaka mazoea nao hata kwa bahati mbaya, maana niliwaona kama wanafki tu...
Wifi yangu alibeba mimba akiwa kidato cha nne mwanzoni, akafukuzwa shule, yale maneno yote ya mama yangu mkwe kwangu, kuwa nilikuwa Malaya na nikabebeshwa mimba, atimae yakamrudia mwanae, na hapo ndio nikaamin kuwa, usithubutu kumnenea mtoto wa mtu mabaya yamkute, ikiwa na wewe una kizazi, kwa sababu ni swala la muda tu yatarudi kwenye kizazi chako...
Mama mkwe akawa mpole sana, na wakataka kumtoa mimba, nusu imuuwe, ndio mume wangu akaingilia kati akasema atalea mimba ila wasithubutu kuuwa kiumbe kisicho na hatia...
Basi wakawa wanajifanya wananisifia kwa watu, na kujifanya wananipenda sana, baada ya mambo yote waliyowah kunifanyia, nikawa na mimi nawachekea ila niliamua kukaa nao kwa akili, maana sikuwah kuwaamin hata mara moja....
Siku zote penzi la kweli, na bahati yako haiwezi kuondoka karibu yako hata iweje, na ukiona jambo limekuepuka ujue sio rizki yako...
MWISHO
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi