JAMANI NIPE CHANCE KIDOGO ___________________________________* *SEHEMU YA KUMI NA MOJA* Walikaa akimsubiri Abisai baada ya dakika 15 alifika na kuwachukua moja kwa fundi
Waliingia pamoja na kuangalia mishono walichagua mishono waliyokuwa wanataka na Abisal aliafikiana nayo.
Baada ya hapo fundi alichukua tepu kwajili ya kuwapima.
Leyla alikuwa wakwanza kupima huku Abisal na Leyna wakiendelea kuangalia picha za mishono mingine.
"Huyu fundi kwa nguo za sherehe na harusi ni hodari sana alafu bei zake wala sio kubwa sana "Mmmm...
Abisai alikuwa anaitumia huku alitupia jicho kuangalia jinsi Leyla alivyokuwa alipimwa.
Alipoona wanaelekezana huku fundi akishika kipimo jaribu na kifua mara kiunoni akawa anagundua ndani kwa ndani.
Sasa upimaji gani ule, na huyu kichaa wangu atapimwa kama vile? Alijiuliza.
Baada ya Leyla kumalizwa kupimwa Leyna nae akaenda kupimwa. Wakati fundi anampinga kifua huku akisema.
Sasa kwa huu mashono inatakiwa nguo ikushike kifuani.
Sawa fanya kazi yako fundi mimi sina ninachojua.
Abisal alivyoona jinsi ya ule upimaji sijui kaka kiuno nala hipsi akaona huu ni ujinga isije ikatokea Kalala na bibi harusi siku moja kabla ya harusi. Alisogea mpaka pale wanapopimana.
"Samahani fundi kwani huwezi kunipa hiyo tepu nikampima mwenyewe huyu mwanamke wangu?
Fundi hakutaka maneno alitoa tepu akampatia.
Leyna alimuangalia Abisai kwa mshangao.
"Abisai ulikuwa fundi lini na leo ikajirudia. Abisal hakujibu alimuangalia fundi na
kumwambia.
"Uwe unaniambia nipone nini na wapi.
"Sawa boss. "
Una wivu mbaya sana wewe. Akiongea Leyna. Aisee tulia ipimwe maneno mengi ya nini?
"Sasa wewe unajua nini? Hii ni nguo Abisai sio msingi wa nyumba.
"Fundi nipime wapi?
"Kiuno.
Abisal hakuwa anajua chochote ila wivu wake ndio ulikuwa unanipeleka vibaya.
Wakielekeza na mpaka vipimo vikaoatikana wakati huo Leyla alikuwa amekaa pembeni hana mbavu kwa kucheka yani ilikuwa zaidi ya stand up comedy.
Leyla aliamini kweli Leyna amepata mwanaume yani hakutaka kumpa nafasi hata kidogo.
Kweli Mungu ni mtaalamu wa kumechishia wanaendana kabisa. Na ukisikia dawa ya moto ni moto ndio hii sasa. Leyna kupatikana.
Baada ya vipimo kukamilika, fundi akawa anapanga tarehe ya kwenda kuchukua nguo zao.
"Boss, wiki mbili tu nguo zitakuwa tayari. "Sawa, nitazofuata mimi.
"Sawalla nyie wanandoa mtanirudia tena kwa final fitting."
Leyla akapiga makofi huku akisema,
"Yaaah! Ndio maana nakupenda fundi, kazi zako ni za maana sana. Ni bora kama hawa wanaume wenye wivu?"
Alipomaliza kusema hivyo, macho ya Abisai yakamgeukia.
"Leyla, unamaanisha nini sasa? Wivu wangu unahusiana vipi na kazi za fundi? "Utani tu shemeji yangu.
"Usiwe unanitania mbele ya watu.
Leyna alijikuta akicheka huku akitingisha kichwa.
"Abisai wewe bwana, unajipa mashaka kwa
mambo madogo. Wivu wako utakuuwa bure. "Achana na mimi, haya tuondokeni.
Wote wakatoka pale fundi akiwa amebaki ameshika mbavu kwa kucheka.
Jamani sijawahi kuona mwanaume mwenye wivu kama huyu jamaa.
Unajua mimi mwenyewe nimeshangaa, amejipa mpaka kazi ya ufundi ili mke wake asipapaswa hipsi.
Ilibaki kuwa story na vicheko
Walipokuwa njiani kurudi nyumbani, Abisai hakujaa kimnya.
"Leyna, kumbuka hili sitaki mwanaume yeyote kukushika shika hovyo. Kuanzia sasa mambo
yote yanayokuhusu nguo, viatu, hata vipodozi nitashughulika mimi mwenyewe.
Sasa wewe unajua nini kuhusu vitu vya mwanamke vinavyounda na wakati. "
Nitajua tu, kwaajili yako nitajifunza. Leyla alikuwa amekaa siti ya nyuma ya gari,
"Yani utaingia hadi saloon kumtengeneza nywele? Abisai fundi nywele sasa... hahahah.... Leyna naye alicheka.
"Naombeni hii mada ifungwe ninachofahamu kwaajili ya mwanamke wangu ni kwa faida yangu.
"Mpaka hizi hela heka za harusi ziishe nitakuwa nimejionea mengi. Alisema Leyla.
Sio kuona tu pia unatakiwa kujifunza kwenye mapenzi ya kweli kuna wivu.
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni