*MMMM DADDY NIKIKUPA UTANIOWA KWELI?!* *SEASON TWO* *SEHEMU YA 29* Nilishangaa kumuona Dada na lile rundo la pesa nikamuuliza mbona umeomba pesa nyingi hivo???..
Dada akaanza kujiuma uma mara oh mi nimeomba buku kaka akaanza kunidadisi nikajikuta nimemwambia hali halisi ndo akanipatia hizi pesa zote😟😟😟..
Toba toba toba Rehema umenivua nguo😖😖😖lete hizo hapa tuone☹️☹️akanipa nikazihesabu ni laki mbili na nusu🙏🙏
Kwanini umefanya hivyo Rey😖😖sema tu pesa haikataliwi wacha tutumie tu😩😩😩vipi umemwambia asante??.
Ndiyo dada na amesema tukiwa na shida yoyote tumwambie🙂🙂heee haya sawa☹️☹️..
Niligawa ile pesa nikamlipa Dada yakwake ya mshahara naye atatue shida zake ingine tukanunulia chakula na umeme nikaeka na vocha pesa ikaisha🤣
Yani ukiwa huna pesa ukija kuipata ukaitia tu mkononi inaisha kama imepeperushwa na upepo🤣🤣
Tulipika bufee pale tukala baada ya hapo sasa nikaamua kuwapigia wazazi wa Kingston😖😖😖nishachafukwa naona kabisa nisipokuwa makini nitatelekezwa pale..
Nilimpigia mama akapokea tukasalimiana akanijulia hali baada ya hapo nikamwambia mama nina mazungumzo na wewe naomba nije tuzungumze..
Kitu gani mwanangu???. Au ni kuhusu kazi???.
Kazi yenyewe ukiwa tayari njoo nilikuwa nasubilia tu simu yako wala sikutaka kukuharakisha🥰🥰nilikuacha upate muda wa kusalimia ukiwa tayari mwenyewe utaniambia nikutumie nauli..
Nilimwambia mama siyo kuhusu kazi kuna kitu kingine😭😭mie lie lie nikashindwa kuzuia hisia🤣 kwanini unalia hebu niambie kuna tatizo gani zarina???..
Mama hatuwezi kuongea kwenye simu😭😭😭nina shida nataka nikuelezee wewe..
Uko wapi??? Nikamwambia niko Arusha😳😳😳mama akashangaa uko arusha??? Ulikuja lini??.
Nikamwambia nina miezi mitatu 😰😰 ina maana hauko nyumbani kwenu zarina??.
Hapana mama siko nyumbani🥹🥹🥹Mama Kingston aliguna kwa mshangao😳😳😳akajisemea mabinti wa siku hizi sijui mna shida gani??
Baada ya hapo akaniambia walisafiri kwenda Dar es salaam hivo wakirudi atanitaarifu niende nikamuone..
Nikamwambia sawa🙂🙂sikujua atarudi lini na kilichonitisha zaidi ni ile kauli aliyoisema mama...kwamba mabinti wa siku hizi jamani sijui wana shida gani😰
Sizani kama ataniamini tena😰😰niliwaza mnoo nitaenda wapi na hili tumbo??.
Sikuwa na majibu...siku hiyo jioni Tristan alikuja kututembelea akaniuliza kwanini mnakuwa na shida alafu hamniambii??
Nikamwambia tu wala sikujua kama tutafikia huku ni vile tu mchumba wangu hapatikani wala sijui amepatwa na nini😰
Hahahaa mchumba wa nyoko nilijimwambafai tu lakini hata nyie mnajua jamaa kanitia kibendi na hajawahi kunitongoza wala kunitamkia kama ananipenda😂😂😂
Mimi ndo niko bize kuwaambia watu ni mchumba wangu ye wala hana habari🤣🤣🤣
Tristan alinipa pole kisha akaniambia kwa hali nilonayo ya ujauzito kibaya zaidi mwenye ujauzito kaingia mitini....
inabidi mimi ndo nijipambanie kwa ajili yangu mimi na mtoto ajaye...alinishauri nifanye kazi kabla tumbo halijafika ile miezi ya kujifungua..
Nitafanya kazi gani😰😰 akaniambia usijali hiyo niachie mimi..
Wow nilihisi kufarijika😞😞 aliniuliza elimu yangu lol nikaona aibu hata kumwambia😂😂jamani nyie ambao mko shule someni muepuke aibu ndogo ndogo kama hizi🙌🙌
Kuna muda unakutana na kidume cha maana kinakuuliza level yako ya elimu unaona aibu kujibu🤣🤣
Nilimwambia Tristan mi nimeishia secondary wala hata sikuweza kumaliza 4m4 maana sikuwa na mtu wa kunisomesha🙈🙈
Aliniambia usijali nitafix🥰🥰 wapi kelele ya Mr fix wewe🥳🥳🥳🥳🥳...
Kazi gani atatafutiwa Shost yetu zarina???.. Kingston yuko wapi??... huyu Tristan kama nimeanza kumwelewa fulani hivi😂basi tukutane sehemu inayofuata...
Full 1000
WhatsApp 0742133100
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi