*MMMM DADDY NIKIKUPA UTANIOWA KWELI?!* *SEASON TWO* *SEHEMU YA 30* Zilipita kama week moja hivi Tristan akanifuata akaniambia kazi imepataikana na kwa kipindi chote hicho yeye ndo alikuwa anatuhudumia kwa kila kitu🥹🥹
Aliniambia ameniombea kazi ofisini kwao... lakini mimi sijasoma nitawezaje kufanya kazi ofisini😰😰akasema usijali nitakuelekeza..
Week iliyofuata siku ya jumatatu Tristan alinichukua tukaenda kazini pamoja🙂🙂
imagine yeye ndo Boss aliyetakiwa kunifanyia interview🥹 kwa vile mimi na yeye tunajuana aliniambia hakuna haja ya interview..
Alinipa maelekezo namna ya kufanya kazi yangu na kwa vile sehemu niliyowekwa ilikuwa tayari na mtu basi niliambiwa vingi nitajifunza kutoka kwa mwenzangu..
Nilifanya kazi pale huku kila siku asubuhi na jioni nikiwa nategemea lift kutoka kwa Boss wangu Tristan..
Siku moja jioni tukiwa tunarudi nyumbani Tristan aliniuliza kama ninajua kudrive...yani kuendesha gari...
Hapana sijui🤭🤭aliniambia ningekuwa najua kuendesha gari angeniachia gari yake maana yeye anataka kusafiri safari ya muda mrefu kidogo🥹🥹..
Nilivosikia habari za safari moyo ukafanya paah😰😰nilishamzoea jamaa yeye ndo kama msaada wangu kwa sasa😢😢nitaishije ye akiondoka??.
Tristan aliniambia usijali zarina nitakutafutia Dereva atakuwa anakuleta kazini asubuhi na jioni atakuwa anakuja kukuchukua🥰..
Oh afadhali nashukuru sana Tristan...na je unasafiri kwenda mbali sana??.. akasema hapana siyo mbali ni hapahapa Tanzania vijijini huko kwenye migodi..
Aliniambia kuna mgodi umenunuliwa na baba yake na yeye ndo kateuliwa kwenda kuusimamia...
Vipi kuhusu kazi ya pale ofisini???.. akasema kwa vile ile ni kampuni ya familia kuna mtu mwingine atasimamia na mambo yataenda vizuri...
Kiukweli nilijihisi mpweke sana lakini sikuwa na budi kukubaliana na kila kitu..
Baada ya siku mbili Tristan alisafiri kuelekea kahama huko migodini...aliniambia muda na wakati wowote nikiwa na changamoto yoyote nisisite kumwambia..
Tuliagana as a friends niliachiwa gari kwa ajili ya kuwa nalitumia na funguo za nyumba ili mara moja moja tuwe tunamsaidia usafi kule ndani kwake kusifubae..
Tristan pia alinitambulisha kwa kijana wake ambaye ndo alimwachia kama mlinzi wa pale kwake akaniambia huyo ndo atakuwa ananipeleka kazini na jioni atakuwa anakuja kunichukua nikitoka..
Nilimshukuru sana yule mkaka🥹🥹🥹nilikuwa naona kama miujiza maana kwenye Dunia hii kupata mtu wa kukusaidia vile ni ngumu mno..
Maisha yaliendelea ujauzito wangu ulipofikisha miezi nane tulikuja kudaiwa kodi ya nyumba ya pale tulipokuwa tunakaa🙁
Na kipindi hiko pesa ninayolipwa kazini nilikuwa najiwekea kwa ajili ya uzazi wala isingetosha kulipia kodi ya lile jumba🙂↔
My wenu nikawaza nimtafute Tristan tena??. Hapana nitakuwa nampa majukumu yasiyomhusu..
Nilichokifanya nilimuomba Dada yule msaidizi wangu wa kazi aende kwanza nyumbani alafu mimi nikatoka kwenda kumtafuta Kingston mtaa kwa mtaa☹️☹️..
Kwanza nilienda kwao Kingston bila kuwataarifu niliwafanyia surprise☹️☹️kumbuka mama niliongea naye miezi michache iliyopita akaniambia atanitafuta nikamuone but hakunitafuta😴
Huu mzigo ni wao na wao ndo watahangaika nao..
Je nini kitafuata??..kivumbi leoooo😂😂😂mi naogopa mwenzenu nyie hamuogopi🤣..tukutane sehemu inayofuata
Full 1000
WhatsApp 0742133100
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi