AAAAAAAH IMETOSHA BOSSππ N0 34ππ
Usiku ule nilipanga nguo zangu kwa ajiri ya safari hapo kesho mapema baada ya kuandaa kila kitu nilipanda kitandani nikalala..... kesho yake mida ya saa 12na nusu asubuhi nilidamka mapema nikasafisha chumbani kwangu nikatandika baada ya hapo nilitoka kwenda kufanya usafi jikoni ndani mara nyingi alikuwa anadeki idris.... nimefika jikoni nikaanza kupata kizunguzunguπ΄π΄ nilirudi nyuma ili nijiegeshe ukutani nisije nikadondoka lakini ghafla nilienda kutua katika mikono ya Hemed..... recho unaumwa?! Aliniuliza Hemed huku akiwa amenishikilia mikononi mwake.... hapana Hemed siumwi ila nasikia tu kizunguzungu.... pole sana itabidi tuelekee hospital haraka ili ukapimwe tujue tatizo ni nini..... Hemed alinibeba hadi sebleni alinilaza kwenye sofa alimuomba idris aandae gari upesi kisha alinimbia pole mama ngoja nivae nguo kisha nije nikupeleke hospita ucjali utakaa sawa nilimuitikia alielekea chumbani kwake alivua zile nguo anazovaaga akiwa anaenda kuimwagilizia bustani akawa amevaa za kawaida.... pole unajisikiaje?!.... aliniuliza Hemed nilimwabia bado nasikia kizunguzungu oh usijali mamaaa tunaenda hospital utapatiwa matibabu utakaa sawa.....
Hemed alinibeba hadi kwenye gari tuliondoka kuelekea hospital kule hospitali nilifanyiwa vipimo nikagundulika kuwa ni mjamzitoππ Hemed aliniangalia kwa maskitiko hakuniuliza chochote kwa muda huo lakini alionekana kushtushwa sana na swala la ujauzito wangu.... tukiwa kwenye gari tunarudi nyumbani hemed aliniuliza recho kwa hiyo tayari ulishampata mwanaume unayempenda hadi umeua kumzalia?!!
Nilinyamaza tu sikuwa na cha kumjibu ..... tulirudi nyumbani nikashuka kwenye gari nikaanza kujongea kuelekea ndani...... recho.....aliniita Hemed nilimuitikia alinifuata pale nilipokuwa alinishika mkono hadi ndani tulikaa pale sitting room aliniuliza ni nani mhusika?! Niliendelea kunyamaza Hemed aliniomba niongee chochote nilimwambia ipo siku nitamwambia kila kitu kuhusu maisha yangu aliniomba nimwambie nilimuomba awe na subra..... nilinyanyuka pale sebleni nikawa naelekea chumbani kwangu mara nikashikwa mkono niligeuka nyuma mmmhhh alinishika Hemed nilishindwa kumwelewa huyu kawaje leo nilibakia kumtizama tu aliniambia recho basi nakuomba mimi ndo niwe baba wa huyo mtoto aliyeko tumboni kwako...... kheeeeeπππ jomon kwa hiyo na yeye tayari kaishanipenda au niaje niaje...... sikumjibu kitu nilijitoa mkono wangu nikakimbilia chumbani kwangu nilijitupia kitandani nikajilaza pale nilikuwa najihisi vibaya sana haikupita muda niligongewa mlango sikuweza hata kujibu wala kuamka kwenda kufungua aliyegonga ni Hemed aliingia ndani chumban kwangu alikuwa kaniletea chakula aliniomba niamke nipate kula chakula nilimwambia asante alinisaidia kuamka pale kitandani nikakaa alikaa pembeni yangu akawa ananibembeleza nile nilikula et baada ya hapo nilimuaga Hemed nilimwambia mimi leo nitaondoka kurudi dar es salaaam..... hapana recho tafadhari nakuomba usiondoke..... nakuahidi nitarudi et...... basi nakuomba twende wote kama hautojali nikusindikize et..... duh hapana Hemed siwezi kuondoka nawewe niache tu niende peke yangu nakuahidi baada ya siku mbili nitarudi tena zanzibar Alinielewa alinisindikiza airpot aliniomba kwa hali niliyonayo ni bora niondoke na usafiri wa angani ili kuepuka kukaa sana alinilipia nauli alinipatia na pesa za kutumia nikawa nimeondoka kurudi dar nilifikia lodge ambayo iko mafichoni sana kule zanzibar nilinunua zile nguo za kuficha sura yangu kwa ajiri ya kuzitumia pale nitakapofika dar......
nilifika lodge nikachukua chumba nikapumzika nililalaa kama masaa tano hivi then nikaamka nikaoga nikavaa zile nguo za kuficha sura baada ya hapo nilitokapale lodge nikaenda kutafuta vitu vichachu vya kula baada ya hapo nilichukua usafiri ilikuwa ishafika usiku kwenye saa saa moja moja hivi nilielekea pale ofisini kwa boss paschal niliona ofisi yake ikiwa iko wazi mlango ulikuwa umerudishiwa tu ni kama vile bado kulikuwepo na watu ndani...... nilienda dukani nikanunua pen na daftari niliandika barua kwa boss paschal baada ya kuiandika ile barua nilisogea pale ofisini kwake nilimpatia mlinzi nilikuwa nimeifunika sura yangu na mlinzi aliyekuwepo pale alikuwa mgeni machoni kwangu nilimfuata nikamsalimia baada ya hapo nilimuuliza kama kuna watu pale ofisini aliniambia wafanyakazi wote wameshaondoka ila huko ndani yumo boss pekee...... nilimpatia kile kikaratasi nikamuomba anifikishie kwa boss wake baada ya hapo mimi nilianza kuondoka kule kwenye ile sehemu...... nilifika mbele nikaitisha tax nikapanda kule mlinzi alikuwa hawezi kuniona tena baada ya kupanda ile tax nilimuomba dereva arudishe gari karibia na pale ofisini tusimame kwa muda pale nilitamani angalau niweze kumtia hata machoni tu nilimkumbuka sana boo wanguπ₯²π₯² sister utaniongezea pesa..... ucjali nitakulipa zaidi nilifunga vioo then dreva aliondoa gari akasogea kule karibu na ofisini kwa boss paschal aliegesha gari pale isingekuwa rahisi mtu kuhisi kitu kwa kuwa pale ofisini huwa kuna kakituo kadogo ka boda na tax....
Tulisimama pale kwa muda kama wa nusu saa hivi ndipo nilipomuona paschal akiwa anafunga ule mlango wa ofisini kwake nilipatwa na hisia za kulia nilitamani nisogee pale niende nikaonane naye...... alimaliza kufunga pale then akaanza kutembea taratibu kuifuata gari yake sehemu ilipokuwa kabla hajafika pale kwenye gari yule mlinzi alimsimamisha akawa amempatia ule ujumbe......
Boo aliupokea ule ujumbe then alisogea pale kwenye gari yake alipanda kwenye gari baada ya muda mfupi alitelemka alimfuata yule mlinzi akaanza kumhoji cjy alikuwa anamuuliza juu ya nini make mimi nilikuwa niko mbali.... boo alianza kuangaza huku na kule nahisi alikuwa ananitafuta mimi.... alianza kutembea maeneo ya pale jirani huku akiwa anaulizia kama kuna mtu aliyefanikiwa kuniona niliumia vile alivyokuwa anahangaika kunitafuta na ilihali mimi nipo na ninamwangalia nilimuomba dreva tax tuondoke pale nampenda sana boo wangu kila nikimuona huwa natamani tu niende nikajilaze kwenye kifua chake kizuriππkwenye ile barua nilimwandikia kila kitu kilichonitokea nilimwambia pia juu ya ujauzito wake nilionao mwishoni nilimwambia kuwa yeye ndo mwanaume wa pekee aliyeuteka moyo wangu nampendaππ....... nilirudi kule lodge nilikuwa mpweke sana nilijikuta tu naanza kukumbuka vitu vya kuumiza vilivyonifanya nitoe machozi...... kulia siyo suruhu pendo amka ukafanye kilichokuleta dar cha kwanza ni kumpa taarifa baba wa mtoto wako aliyeko tumboni juu ya ujauzito wake hicho tayari umeshakifanikisha cha pili ni kwenda nyumbani kwenu kuchukua vyeti vyako na vitu vyako vingine bila wazazi wako kukuona..... nilijishauri na nafsi yangu tu..... niliamka tena nikaificha sura yangu ilikuwa ni usiku mida ya saa 3 nilipanda boda kuelekea kule nyumbani kwetu kwa ajiri ya kwenda kuchukua vitu vyangu.......
Itaendeleaaaaaaa
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi