πππ’ π‘π π π₯ππ ππ’ πͺπ π§πππ§π’π SEHEMU YA 13 ENDELEA.... "Na....na....nawahi kuandika ripoti tutaonana baadae" Tasha akiwa mwenye hofu kubwa aliaga.
Philips Kobe alimdaka mkono kisha akamfungia zipu ya suruali, hakuishia hapo alimvalisha koti lake na si kwenda nje na kitop.
"Ahsante...." Tasha aliongea kwa wakati huu alikuwa na macho makavu, kwa kifupi aibu ilikata, alichukua pochi yake kisha akasepa
"Ni kitu gani hiki ulikuwa unafanya naona unazeeka vibaya " Philips Kobe aliongea huku akimvalisha Kaka yake boksa pamoja na suruali.
"Nahisi nampenda Tasha....nasikia aibu kupita kiasi kumpenda mpiga vita wa wanaume mtandaoni " Bryant Kobe alijibu tofauti na alivyo ulizwa.
"Wewe ni mvulana mkubwa wa familia, naomba uache hii michezo kwa sababu itakuchafuliwa nafasi yako ....nilikuja kukuambia kesho ni birthday ya Mama tunatakiwa kufanya jambo" Philips Kobe aliongea kisha akakaa kwenye kiti.
"Tofauti na keki kubwa sidhani kama kuna kitu kingine anapenda β....hii keki nitaitengeneza mwenyewe" Bryant Kobe aliongea.
Philips Kobe hakuongea chochote, badala yake aliishia kumtazama Kaka yake.
"Kwanini unanitazama namna hiyo "
"Upo serious sana kupita kiasi sikutarajia kama unaweza kufanya vile na Tasha"
"Hisia ni kitu cha ajabu, lakini sitarudia tena. Naomba ufanye kuwa siri "
Basi kwa pamoja waligonga tano lakini moyo wa Philips Kobe ulikuwa unaumia....
Siku iliyofuatia bonge la sherehe kwa ajili ya birthday ya Zara liliandaliwa.
Ilikuwa ni siku yake muhimu lakini hakuonesha furaha hata kidogo.
"Kitu gani kina kusumbua " Bryant Kobe alimuuliza.
"Naonekana kusumbuka ?"
"Ndiyo, ni kama kuna jambo linakutesa... naomba uniambie sifurahi kukuona hivyo "
"Kuna jambo natamani unifanyie, sina uhakika kama utatenda pengine ndio sababu sina raha "
"Leo ni siku yako muhimu, hivyo chochote utakachoomba nitafanya..."
"Kweli?....kweli una maanisha utatimiza nitakacho kuambia "
"Nitatimiza endapo utaonesha tabasamu usoni mwako na si kukaa umenuna namna hiyo "
Basi Zara alichangamka kupita kiasi, wageni waalikwa walianza kuja mmoja baada ya mwingine.
Familia ya Tasha walifika pia, macho ya Bryant Kobe na Tasha yaligongana walitazamana kwa sekunde kadhaa kisha kila mtu akageukia pembeni, basi ndio ilikuwa kazi yao kutazamana kwa kuibia kila walipopata muda.
Philips Kobe alikuwa ana wafuatilia kwa ukaribu sana. Aligundua wawili hawa wanapendana ni vile tu hawaja zungumza hisia zao. Alijikuta akifakamia wine yote iliyokuwa kwenye glass.
Basi kila mualikwa alizungumza mazuri kwa Zara.
Zawadi zilianza kutolewa, wakati Tasha anasogea kutoa zawadi Secretary Annie alisimama pia.
Lengo lake lilikuwa ni baya, alitegesha mguu wake kwenye hatua za Tasha.
Ile Tasha anataka kwenda chini Bryant Kobe aliwahi kumdaka.
Basi watu waliwashangilia kwa namna walivyo dakana. Baadhi yao walirukwa akili na hata wakapaza sauti kuwa wawili hawa wanaendana.
"Badala ya kubomoa nimejenga " Secretary Annie alijisemea huku akiweka zawadi kwenye kapu.
Zamu ya Bryant Kobe kuweka zawadi kwenye kapu ilifika.
Aliweka kibahasha kidogo tu....ile anataka kukaa kwenye kiti Zara alisimama akamkumbatia kwa mahaba yote.
"Uliniambia utatimiza jambo langu endapo nitakaa kwa uso wa tabasamu "
"Nakumbuka, niambie ni jambo gani hilo unataka Mimi hapa nitimize "
"Natamani nimuone Philips Kobe akikalia kiti cha CEO....natamani aitwe Boss pia. Tafadhali sana naomba umuachie eeeh...yeye pia ni Mtoto wa Kobe ana haki zote hivyo taf....." Kabla Zara hajamaliza sentensi yake Bryant Kobe alimkatisha
"Nilikuwa na mpango huo pia, na ndio sababu nilitamani sana arudi nyumbani "
"Una maanisha "
"Ndiyo ..."
"Kuna kitu kingine pia nataka umuachie, ujue wewe umefaidi vitu vingi sana kuliko yeye. Nitafurahi kama utamuachia pia "
"Kitu gani hicho ongea "
"Natamani Tasha awe na Philips Kobe "
"Sawa nitatimiza hilo pia ...." Bryant Kobe aliongea kwa kumaanisha.
"Natamani Philips Kobe angekuwa ananisikiliza Mimi kama ufanyavyo wewe "
"Kama sitakusiliza marehemu Baba yangu atakwazika kupita kiasi " Bryant Kobe aliongea kisha akarudi kukaa.
Kwa kuwa kaweka ahadi ya kumuacha Tasha hakujishughulisha tena kumuangalia mrembo wa Tiktok, kila Tasha alipomgeukia Bryant Kobe hawaku gonganisha macho kama mwanzo.
Hii ilimpa tabu sana, ingawa ni mtu makini sana lakini huwa ana kasoro ya kutawalia na hisia.
Wingi wa watu haukumtisha alisimama mpaka sehemu alipo Bryant Kobe, bila hofu yoyote alimshika mkono akampeleka mpaka sehemu isiyokuwa na watu π€
"Kwanini hatugonganishi macho kama mwanzo " Tasha aliachia swali na kumfanya Bryant Kobe ashangae
ITAENDELEA......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi