πππ’ π‘π π π₯ππ ππ’ πͺπ π§πππ§π’π SEHEMU YA 6 ENDELEA..... "Nini kinaendelea " Bryant Kobe alizungumza huku akiinyanyua picha yake
"Kinaendelea nini sasa Mwanaume unataka kusemaje hapo." Tasha alijichekesha huku akitafuta namna ya kujitetea, ingekuwa ni aibu kubwa sana kama angekosa jibu la kusema.
"Siyo ucheke, naomba uzungumze picha yangu imefikaje mikononi mwako "
"Mama yako alinipatia ni kaikuze anataka kuiweka nyumbani kwake ' Tasha aliongopa.
Bahati nzuri au mbaya Zara alifika, basi Bryant Kobe alimgeukia kutaka uhakika.
Zara ni kutoa tu mijicho, hakuelewa ni kitu gani kijana wake anataka kuthibitishiwa.
"Hii picha ulinipatia ni kaikuze, Kijana wako wa kambo kaiona imekuwa shida tupu nisaidie kumuaminisha" Tasha aliwahi kuweka mambo sawa.
"Picha nimekupatia Mimi kwani kuna shida gani imejitokeza " Zara aliongea.
Bryant Kobe hakuongea chochote aliondoka, aliwafananisha Wanawake hawa wawili na matapeli ingawa hakusema.
"Imekuaje upo na picha ya Bryant Kobe na huku nilikupatia za Philips Kobe "
"Sielewi hata, lengolangu lilikuwa ni kuiba picha moja ya Kijana wako si unajua tena ni mzuri cha ajabu nimejikuta na picha ya huyo kichaa"
"Mna uhusiano gani nimestaajabu kuona mkibadilishana mate"
"Ndio maana namuita kichaa, sielewi ni kitu gani kilimpata akanivaa au huwa ana hali ya kupoteza kumbukumbu"
"Tuachane na hilo kwahiyo ulikuwa unataka kukaa na picha ya Philips Kobe vipi umemuelewa si ndio?.....kaa hapa unisubirie na kuletea" Zara aliongea kisha akaondoka kwa kukimbia.
"Mbona halikuwa lengo langu ....sipo tayari katika hili" Tasha alijisemea kisha akaondoka.
Baada ya kutoka nje ya geti alisimamisha bajaji akaishia zake.
"Imekuaje tena nimekuja na picha ya Bryant Kobe nilipaswa kuiacha pale bustanini" Tasha alijisemea huku akiiangalia picha, moyo wake ulizidi kushtuka kana kwamba ana muona Mwanaume huyu live.
Upande wa Zara anarudi bustanini akiwa na haraka huyo anashangaa baada ya kumkosa Tasha.
"Huenda kapata dharula lakini ndio aondoke na picha ya Bryant Kobe .....yawezekana alikuwa ametingwa sana" Zara alijitia moyo.
Upande wa Bryant Kobe akiwa anajiandaa kwenda bafuni alitumiwa ujumbe na Mdogo wake (Philips Kobe) kuwa yupo uwanja wa ndege.
Kwa jinsi alivyo mkumbuka ndugu yake hakuona sababu ya kuoga.
Alielekea chapu uwanja wa ndege.
Ilikuwa ni furaha kubwa kwa wawili hawa, walitembezeana makonde kwanza eti wanapimana nguvu.
"Hatugombani ...." Philips Kobe aliongea baada ya kuona watu wamewajalia.
Basi kwa pamoja waliingia kwenye gari.
Bryant Kobe ndio alishika usukani
"Ni harakishe haraka nimebanwa mkojo, yaani ukizembea tu kidogo tu nalimwaga " Philips Kobe alilalamika.
Bryant Kobe kusikia hivi aliongeza kasi, hakutaka mdogo wake alimwage kwenye gari.
Bahati mbaya sasa Bryant Kobe alishindwa kumuona Tasha, ilisikika tu paaaaaaaaaa.
Kojo lilimpita Philips Kobe , Bryan Kobe hakuwa na hofu hata kidogo kwa sababu majeruhi ndio alikuwa na makosa.
Alifungua mlango wa gari akiwa mwenye kujiamini, alishtuka baada ya kumuona Tasha Mrembo wa Tiktok....
ITAENDELEA.....
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi