*CEO USINIVUE MI MCHUMBA WA MTU* *1-3* *______________________________________* *SEHEMU YA KWANZA* Hivii we huoni aibu mchumba mwaka wa pili huu ni mchumba tu yaani barua tu basi
Dada jamani mhh hata kama ni mambo tu yatakaa sawa hakuna shida wala usijali , yule ananipenda na atanioa haina shidaa kabisa katika hili kuwa na amani sawa dada yangu?, "hivi wewe Salma unaa akili sawa sawa kweli mapenzi yanakuchanganya sana mpaka unashindwa kumjua mwenye upendo wa kweli ni yupi? Hivi mwanaume anaekupenda kweli anaweza kukuacha hakupi huduma hapo ulipo kila kitu unanitegemeaa mimi halafu unasema anakupenda yaani mwanaume hata basi vihela vya pedi mara moja moja hakuna" alikuwa ananisema sana dada Mariam kuhusu huyo Hussein lakini mimi hata simsikii nipo namtizama tu namuona kama juha flan maana yanaingilia sikio la kushoto yanatokea la kulia basi ni shida tupu na hakuna analoweza kubadilisha etty niache kumpenda Hussein wangu , yaani nilikuwa namuona Hussein wangu ndio kila kitu hakuna mwingine
Haya endelea kumuona huyo mjinga wako ni wa maana sana utakuja kukumbuka maneno yangu siku moja wee mjinga yaani huyo hakupendi hata kidogoo , alisema dada Mariam lakini niliona ananichanganya tu nikainuka nikatoka zangu nikaenda kwa akina Zakia ambae ndio shga angu pale mtaani muda huo nna kijora changu
Zakia mambo , "washakutibuwa nafsi kuwa udugu wangu maana nakujua , ukija hivyoo bila wanna hata wa chini ya macho shga angu unakuwa ushavurugwa wamemsema tena huyoo bwana wako Hussein?" Alisema Zakia akinamabia mimi muda huo hat chini sijakaa , yaani alikuwa ananijua sana kama vile ni mama yangu maana mimi siwezi kutoka bila wanna wa chini ya macho hata niwe naenda gengeni akuu mwenzangu siwezi miee mh kwanza shga yangu nimekumbuka kuna kampuni hivii naweza kukuonganisha wewe si umesoma mwenzangu ,huwezi lingana na mimi niloishia chekechea hhhh, bwana wangu anafanya kazi pale hivyoo taongea naee ntakufanyiaa mpango wa kazi pale wangu hata usijali mimi na wewe ten damu yang, maana naona kukaa pale kwenu dada yako kila siku anakusema na wewe unakereka bora ukafanye kazi" wee nilijikuta nimemkumbatia Zakia kwa furaha kubwa sana maana kwangu ule ulikuwa ukombozi mkubwa sana maan nilikuwa nishatafuta kazi muda mwingi nimekosa hivyoo nikaona hili litakuwa jambo zuri sana kwangu kwanza ntakuwa nipo bust hata wakinisema sijali na kuhusu mahari nitampa hata Hussein wangu aje anioee wakae kimya, muda huo nilikuwa na mawazo ya kijinga tu hamna kitu ntafanya ndani asiwepo Hussein maana mimi na huyo Hussein mhh toka tupo chuo japo hajawahi kunila , na kwa nilivyokuwa namuona ananielewa nikimwambia kuhusu hilo kwamba siwezi mpa kabla hajanioa kwasababu nampenda sana hivyo tulikuwa tunaishiaga kwenye kisses tu basi tunaishia hapo, asaante Zakia utakuwa umenisaidia pakubwa sina chakukulipa udugu wangu
Tuliongea mengi mwisho nikaondoka zangu kurudi nyumbani , ilikuwa mchan dada alikuwa kashatoka tayari kaenda kwenye mahangaiko yake hukoo ya maisha maana dada angu anafanya kazi saloon kwa mtu na ndio tunaishi kupitia hyo hyo kazi yake wazazi wetu ni wa kulima kwahyo hata kusoma kwangu ni waliuza mashamba ili nisome,
Dada alikuwa kaacha funguo pale kwa Mama Amina ni jirani yetu , nikaingia ndani nikakuta kaacha elfu 2 pale mezani , na unga upo ndani kwahyo kaacha hela ya mboga pale na mimi ni mdada wa diet nikasema hapa sipiki mpaka usiku ili tuje kula na dada, na dada yangu alikuwa ananiaminia haswa kwenye maswala ya bajeti bajeti, nipo bomba elf 2 hapo lazima chenji aikutee na mambo mengine yaendelee
Usiku ulifika na dada yangu akarudi sasa kutoka kazini , nilikuwa nimesonga ugali na vidaagaa Mchele nimenunua vya buku vya kukaanga na hivi unga ulikuwa ndani basi hapo buku likabaki "yaani hapa nakuaminia kwenye bajeti , hushindwi kutulisha ugali na kachumbari ili tu ubaki na pesa ya bando, ila pote hunikeli unaanza kunikera kwa huyo mpenzi wako ambae hajui mchumba wake anaishiije jamani mhhh , afu mbona haonekani kam ana shida kabisa lakini kukuhudumia inakuwa jau kwanini etty?" Aliulzia daa , yaani dad alikuwa ananikera akimzungumzia mchumba wangu naona kama anazibia rizki yaan kuna muda mpaka nilikuwa nawaza ujinga etty dada pengine anampenda Hussein ila hizi akili, kwakweli nilikuwa nampenda sana yule mwanaume jamni khaa! Niliinuka hata bila kumaliza kula nikaingia ndani , kwenda kulala jamani nililala hata bila kuoga hiyo siku, dada alimaliza mambo yake na yey akaja kulala ndani ,
Asubuhi ilifika na dada aliondoka maana alikuwa kila akijaribu kunisemesha simjibu nikaamua kumkalia kimya simjibu , akajua fika kabis animekasirikia , hakujisumbua kunibembeleza maana udhaifu wangu anaujua akaondoka akaacha pesa pale mezani , na kuondokaa zake , mimi nikabaki nimevuta domo tu sina lolote , la kufanya mara muda huo simu ikaita alikuwa ni Hussein nikapokea nikaanza kumwambia kuhusu, dada angu anavyonisema kuhusu yeye na mimi sipendi akaniambia tu nivumilie kila kitu kitakaa sawa na kama nisihofu kuna ishu haijakaa poa bado ikikaa poa kila kitu kitaenda sawa kabisa kuusu hili halina shida kabisa atanioa tu kisha akakata simu nilifurahi kweli jamani yaani nilikuwaga nikiambiwa hivyo tu yaani napagawa nakua chizi kabisa maana nakuwa naona mimi napendwa sana na muda huo mtu hata aje anishauri vipi kuhusu Hussein, namuona mchawi tu maan nishaambiwa ntaolewa basi naona kam vile dunia nimeikamata miee hhhhh, nikaaamua kulala kabisa na usingizi nisikilizie raha usingizini, nililala sana nakuja kushtuka hivi ni saa 10 jioni , kuangalia hivi Zakia alikuwa kashapiga sana jamn mhh nikaamua nimpigiee , akanambia kwmba niende kwake maana Zakia amepanga sio kam mimi ninae kaa kwa dada yangu , ikabidi tu niende kwake
Nakuta pale kwa Zakia pamepack gari, nikaingia ndani namkuta Zakia na mkaka mmoja akanitambulisha akaniambia" huyu ndio shemeji yako usiwe na wasi wasi sana" alisema Zakia huku akimsogelea karibu sana yule mwanaume na kumlalia mabegani
Sawa Zakia kanielezea kila kitu kuhusu wewe hivyo nilimwambia kwamba akwambie kesho uje na vyeti vyako kazini ili ufanyiwe interview na pia uanze kazi rasmi sawa? Maan nilimwambia akwambie akasma hawezi jielezea ila huyu mwanamke naee " alisema yule mwanaume huku akimtizama usoni Zakia naitwa James alisema yule mwanaume na kunipa mkono nilitoa mkono wangu pia na kumwambia kwamba naitwa Salma Juma , alisema kafurahi kuniona kisha me nikaomba niwapishe ili waendelee na mambo yao , waniniruhusu niliondoka na furaha sana ila nilikuwa na mawazo Zakia kwanini kaweza kuishi na mwanaume wa dini tofauti jamni mhh hapana mbona nakuwa sielewi ila baadae nikasema. Ni mambo yao hayanihusu mee , ila me nae nilizidisha umbea
Nilikuwa namsubiri dada kwa hamu, kweli nimuelezee kuhusu furaha yangu, ya moyoni nikasahau kabisa kam asubuhi nilikuwa nimemnunia ila mee naee nikiwa tu na furaha nasahau kuhusu makasiriko yangu na dada ashanizoeaa , alirudi nikampokea kwa uchangamfu kweli yan akauliza Hasira zimeisha au umeona nimekuja na Kidali umeeanza shobo mdundiko? Aliuliza Dada Mariam nilicheka tu nikamwambia hamna ikabidi nimuelezee kwanini nina furaha ila da Mariam sasa akanza nichamba huku aninipa hongera " haya hongera mdogo wangu ila sas .nenda kwanza kaangalie hyo kesho ila sasa , usijaribuu kufanya ujinga kam uliokuwa unafanya sikuzote maana ntakung'oa maskio yaaan unafanya kazi hela unampa mwanaume wako sasa wee endeleaa tu utankuta nimejaa tele kam pishi la ubwabwa wee haya , uliona wapi mwanaume anapewa hela jiongezeee wee mjingaa" yaani dad hajawahi kuniacha hata mara moja niwe na amani kila siku ananisema nilikuwa sijui kwanini yan, nilibidi tu nivumilie maana kususa kuku siwezi , ili nimalize nikaoge , nikalale ili mambo mengine yaendelee niamke na nguvu mpya keshoo maanna nilikuwa naisubiri kw ahamu sio powa yaani .....kupata mwendelezo bonyeza link hii hapo juu au chini ukasome yote hadi mwisho kwa buku tu…
*SEHEMU YA PILI*
Siku mpya ilifika, ila cha ajabu kitandani aliniamsha dada angu "hivi wewe mjinga yaani hadi nimekuandalia kila kitu na wala ushtuki kabisa yaani , sijawahi kuona mvivu kam wewe dah!" Ebu amka ukaoge uwahi kwenda , yaani ndio kwanza siku ya interview unachelewa Je hiyo siku siku ya kuanza kazi hivi wewe binti jamani unanini wewe?" Alisema dada angu Mariam akiniamsha kwa makelele kweli mpaka nikashindwa kujizuiaa , maana alikuwa ananikaraisha , yaani kitu kingine mimi napenda kulala sana , yaani ningekuwa nimekutana na mwanaume wangeshasema nina mimba tayarii, niliamka nikaenda kujiandaa
Nilielekea kazini sikuwa nimevaa nguo nzuri sana , nilikuwa nimevaa zangu abaya langu la 32k , tena kanipa dada me nilionaa nimevaa nguo nzuri kweli maan lilikuwa limenikaa na hivi nina kishepu cha uchokozi weee asikwambiee mtu yaani, mpaka mwenyew nilikuwa najitamani nijitazame mara kumi , kumi na kasura kangu nikivaa ushungi mbona utapenda, nikaingiaa officine nilielekezwa moja moja chumba cha kufanyia interview kwasababu ilikuwa kila kitu kishapangwa na shga angu Zakia hivyo taarifa zote watu walikuwa nazo kuhusu ujio wangu
Chumba cha mahojiano yaliendaa sawa kabisa bila wasi wasi , na niliambiwa nisubirie majibu yangu nikiwa nimekaa nje , nilikaa nikiwa , ghafla mtu akinikanyaga tu bahati mbaya ila kwa jinsi ninavyoupenda ugomvi kuliko kula nikaamua nianzishe topic, enhee wewe huoni au , mbona una kiherehere hivyoo unatembea utafikiri hii office ni yako vile , ujuee unaboaa kwanini unikanyage sasa kwamba huoni au unajikuta na hiyo suti yako ya mkopo? Yaan wew, muda wote nipo naropoka mtu ananitizama tu yaani ni ananishangaa
Hivii wewe ndivyoo ulivyofunzwa hukoo kuomba samahani huwezi, afu bado unanitizama tu kama vile mimi ni mdori wako nimebandikwa si ndio? Hivi wewe kijana mhh yaani watu wengine, kwahyo kufanya kazi hapa unaona kam vile umemaliza duniaa si ndio? Nilikuwa naongea wala hata simezi mate cha ajabu mtu mwenyew nilokuwa naongea nae hata hashuhuliki na me kabisa, yaani alikuwa ananiona mimi sijui kama mdorii yaani naa muda huoo , nilikuwa sijui ni nani huyoo mkaka , naropoka tu kam ni boss sijui kam ni muajiriwa tu kama mimi sijui yaani nilikuwa namuona anadharau mnoo, na jinsi nina kamdomo basi ni kumchamba tu , bila hata wasi wasi..
Chaa ajabu yule mkaka hakunijibu alinitizama tu kwa jicho moja kali kweli, akaondoka zake asee nilibaki nalalamika haataree nilikuwa naona kam vile ananichanganya tu maan nilikuwa simuelewi kabisa yaani , maana sijui ntajibiwaje kabisa ,ila niliona yule mkaka ameingia chumba kile nilichotoka mimi hapa, nikajua tu atakuwa na yeye labda alikuwa kaja kwenye interview, ila baada ya dakika chache nikashaangaa akatoka akaenda kupanda lift, nakuelekeaa juuu , mara baada ya dakika 30 nikamuona yule alokuwa ananifanyia interview katoka na kaniita na mimi bila hiyana nikainuka na kumfuataa kule kule officine kwake tulipokiwa tunafanya mahojiano...
"Samahani miss. Salma nakuomba nikuelekeze ujueee wewe ni mgeni na tayari umekurupukia mtu usiemfahamu unajua ni nani yulee?" aliuliza yule alikuwa ananifanyia interview mimi nikamjibu tu sijuii lakini alinikanyaga sasa kwanini asiambiwe yeye ni nani hasa mkuu? nilimuuliza pia kama unavyojua wabongo tukiulizwa na sisi tunauliza yaani bampa tu bampa hatujibugu swali, bali tunauliza swali na sisi , yulee kijana aliendelea kuongea" ujue wewe kilichokuokoa hapa ni vyeti vyako tu na hakuna kingine bali ni vyeti vyako tu ndio vimekusaidia katika hili maana viko vizurii , ila kwa hili kosa ulikuwa tayari ushakosa kazi " weee nilishtuka ila nikajakaza tu kuuliza tena kaa upole mno kwani ni nani yule niliompamia? " Yule ndio CEO hapa" wee nilishangaa na nikajiona chizi kweli yaani nimekurupukia mtu nisie mjua Yaani mimi jaman , ila si ninaweza kwenda kusema samahani? , " Hata hivi ni namna moja tu ya kwamba kakusamehe , maana isingekuwa rahisi kwako kupata kazi, huwaga hachekeshi kabisa katika haya mambo ya mtu kumjibu hovyoo, ila kwako naweza sema una bahati sana binti, haya shika mavazi yako haya hapa na kesho saa moja na nusu uwe hapa uwahi , maana boss hapendi uchelewaji wa kazini kabisa" nilichukua nguo zangu zilikuwa ni suti za kike , na nikapewa pia pesa ya nauli shilingi 25 elfu , hee nilishaangaa ila yule mkaka akaniambia ukiachana na pesa ya mshahara pia huwa wanawapa wafanyakazi wote pesa za nauli ili wawahi kufika nyumbani na pia wawahi kufika kazini, nilishukuru pia nikaoandoka
Ila nikapitia sehemu, kabla sjafika nyumbani nikampigia mchumba wangu Hussein nikamueleza hapo hapo hat bila hongera wala pole nusu nifukuzwe kazi akaniambia nimsaidie 15k kuna sehem kakwama hapa na mimi nikamtumiaa na kwa vile nilikuwa nampenda sana kama kachizi sikuona wapi alipokosea kabisaa wala sikuona kosa lake nikamtumia bila wasi, yaani kwa sababu ya upendo naweza nikajinyima nikampa mwanaume ila me 🤭 nachekesha sana
Nilifika nyumbani nilitumia kam 2k tu kwa nauli ya dalala nyingine nilibaki nayo kabisa, kwa ajili ya kesho na nilipaanga simwambii dada chochote maana atanichamba buree, kuhusu mchumba wangu na nilikiwa sitaki asemwe, dada alirudi, usiku ila nikampa tu umbea wa kwamba nimemchamba CEO na nusu nikose kazi kabisa , akanichamba sana kama kawaida yake , na nikasusa kam kawaida yangu mimi tena😅😅 , nikaenda kulala ila niliweka alarm ⏰️ ili iniamshe mapema niwahi kazini , dada nae akanisindikiza na neno " haya nenda ulale mapema cha maneno wangu, usije ukasema etty ulichelewa kulala ndio maana umechelewa kazini, na kwanzia leo ntakuwa na kukera ili uwahi kulala , maaan nikikuacha humalizi kuongeaa" sikumjibu kitu nikaingia zangu ndani kimya nikalala , hapo naiwaza kesho na nishapasi kijisuti changu cha rangi ya dark blue .... Kupata mwendelezo bonyeza link hii hapo juu au chini ukasome yote hadi mwisho kwa buku tu….
Itaendelea .....🔥
*SEHEMU YA TATU*
Siku yangu muhimu ya kwanza kazini ilifika dada angu aliaamka mapema sana , maana alarm niliweka ya saa 11 ila ililia na sikuamkaa nakwambia mimi ninavyopenda kulala niamke mapema mhhh sijui itokee nini , yaani ila dada angu aliniamsha mapema na kichambo juu kama kawaida yake dada yangu " We Salma hivi humo kichwani zimo kweli? Yaani hadi alarm imelia lakini wewe mwanamke mvivu hujaamka kabisa , yaani sijui upoje wewe mtoto, uvivu umekuchongea na huna lolote, hebu amka wewe binti yaani wewe mhhh kam vile una mimba chnga kwa jinsi unapenda kulala" alisema dada akiniamsha kwa fujo kweli
Niliamka nikaamua tu nimsikilize sikuwa na jinsi , japo nilichukia ilikuwa tayar saa 12 asubuhi , nilijaiandaa nikavàa kale kasuti kangu na high hills zangu, nikabeba kapo hi changu, jaman mimi nilijua kupendeza mhhh, mpaka dada akawa ananishangaa maaana nilionekana mrembo sana hii siku kuliko siku zote ambazo nishawahi kuonekana kupendezaa , hii siku kwangu ilikuwa ni motoo maana nilipendeza sana , na hivi nina kisura cha upole na ni mzuri Mungu alipatia kuniumba ukiniangalia unasema hakuna kitu ambacho sina , kumbe nina kasoro zangu kibaoo hhhh🤭 , dada yangu alinipatia 2k kwa ajili ya nauli , nikapokea kwahyo na ile 5k nikapata 10k , nikaamua zangu kupanda dala dala me habari za kubolt nisibaki hata na 1k ya bando ya kuchungulia status za watu sio kweli kabisa siweza fanya huo ujinga.
Nilifika kazini japo kwa kucheleaa ila nilifika niliambisa saa 1 na nusu niwe nishafika , mimi nikafika saa 2 na dk 5 , sikujali kwakuwa niliona nimewahi kufika hata hivi, sasa hivi ningekuwa nimelala bado kitandani kwa dada , yaani kitu kingine nilikuwa sijali kabisa kuhusu mu beenda yaani nilikuwa naona kawaida zangu tu , kila kitu nachukulia poa maan ikitokea mtu ana meeting na me saa 7 basi ategemee kuniona saa 10 maana huo muda mwingine me ntakuwa nazunguka tu na nina kuwa sijali ..
Ile nafika tu shemej James akanidaka " shem hivi ni kweli kabisa umefika kazini , muda ambao hadi boss kashafika?, mbona unataka kuwasha moto sasa hivi na kibarua chako kiite nyasi siku ya kwanza tu jaman , na rafiki yako aaanze kunilaumu mimi kweli ila jamani wee msichana hapana kwa hili hapa sio sawa kuchelewa kabisa sijui itakuajee, kwanza ushaenda kusain?, alikuwa anaongea hapumziki baasi mimi kunichosha , niliskia tu neno la mwisho bado kwani wanasaini wapi? Niliuliza huku nipo serious ila sikuwa na wasi wasi juu ya maneno aliyoyasema shem, alinielekeza nikaenda kusaini
Mara alikuja mdada anaitwa Careen nilimtambuaa tu nilipoona jina lake kwenye kakibao kadogo upande wa kushoto wa suti yake ta kazini" Miss Salma , "tafadhari unahitajika na CEO, tafadhari wahi" niliitikia tu sawa na yule Careen akaondoka zake na kuniacha mimi namalizia mambo yangu , nilimpuuza tu wala sikutilia maanani hilo mpaka nilipofatwa na mtu mwingine tena shemej James akaniambia " Salma kwani si umeitwa na CEO, hivi unatka kufukuzwa kazi siku ya kwanza kazini si ndio?" Sikujibu nilikuwa namtizama tu maàna alikuwa ananichanganya tu maana nilikuwa sipendi kuambiwa kitu kimoja mara kumi kumi , mwisho akasem tuongozane, tulipanda ngazi mpaka flour ya 9 ya juu kabisa akanipeleka mpaka officine kwa CEO wa ile kampuni, akabisha hodi tukaruhusiwa
"Unaweza ukatoka James nina maongezi na huyu new comer naona sheria hazijui kabisa" aliongea kwa msisitizo mkubwa sana hadi nilijihisi kutetemeka mwili maana ilikuwa ni kama vile amri na sio ombi na usoni alionekana kuwa amefura hasira , hapo nilianza kupata wasi wasi na kuanza kukumbuka kwanzia maneno ya dada yangu, hadi nilivyoitwa na Careen mpaka nilipofika nimeitwa na James shemej yangu na nilikuwa namuona mzinguaj tu hama lolote ,nikaona yess hapa nafukuzwa kazi mapema
"Uliambiwa kazini uliport saa ngapi? " aliuliza boss kwa msisitizo mhh niliambiwa saa moja na nusu , " na sasa hivi ni saa ngapi?" Ni saa tatu sasa " uliingia kazini saa ngapi?" Saa mbili na dakika tano "woe kumbe nyumbani kwenu ni mbali si ndioo au kuna sababu zinakufanya uchelewe kazini ?" Ndio nyumbani kwetu mbali mkuuu , mbali sana yaani we hujui tu sir , yaaani hapa napanda dalala tatu kufika hapa kazini , nilikuwa naongea kwa ustaaarabu na kwa unyenyekevu wa hali ya juu maan nilijua nikileta kamdomo kangu hadi kwa boss ni siku ya kwanza kazini na. Ndio inakuwa ya mwisho pia nilikuwa najibu kwa utulivu sana , tena wa hali juuu
"Umeolewa?" Aliuliza sir hapana nilidakia sijaolewa ila....." hiyo hiyo inatosha usijielzee san mwisho maneno yakakuishia sawa madam?, sasa hujaolewa na bado unachelewa kazini ukiolewa si ndioo itakuwa kizaaa zaaa jaman weee mdada , ukiona umeolewa acha kazi sehem utakayokuwa unafanya" yale maneno ya mwisho yalinichanganya etty sehem nitakayo kuwa nafanya kazi nilidakia juu kwa juu aseee boss samahani kabis , sasa nikiacha hapa kazi naenda wapi jamani , dada angu ataniuaa mee kwakweli jaman hii sio sawa mkuu jua hivyoo , mimi Salma Juma sitaki historia ya kuacha kazi siku ya kwanza kazini, mkuu nakuahidi kabisa hili halitajirudia tena vile tena mkuu kuwa tu na imanii na mimi hili halitajirudia tena nakuahidi usinifukuze kazi , niliongea kwa kulalamika kwa kuumanisha nilichokuwa nasema…
Kupata mwendelezo bonyeza link hii hapo juu au chini ukasome yotehadi mwisho kwa buku tu…
Itaendelea ......🔥
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni