MY CRAZY BOSS 07
SONGA NAYO
Asubuhi wa kwanza kuamka nilikuwa mimi,nilijikuta na uchovu wa ajabu sana,nikaona niamke nielekeee chooni kukojoa
Ile natoka tu kwenye shuka 😳😳nikagundua nipo uchi wa mnyama🥲hapo ndo akili ikanirudi nikagundua yaliyojiri jana
Mamaaa!!!!!!!!!!!!Erick erick umenibaka ,umenibaka etick ,nikaanza kupiga kelele hapo kama sio mie niloutaka🤣🙌
Sikuridhika nikamfata boss pale kitandani acha nimtingishe,umenibaka Erick umenibaka kweli??
"Nikubake kwa kipi na uliutaka mwenyewe,em nitolee kelele zako sehemu za siri zangu zinahitaji mapumziko"
😳😳khee manake kwanza nilishangaa sana sikuamini nilichokisikia eti ken* zake zinahitaji mapumziko sio??sawa.
Kwa hasira nikatoka nikavaa haraka haraka nikatoka hadi nnje ,sebleni nimewapita wazazi wake kama sijawaona bila salamu bila nini yaani kama nna utahira hivi
Nikiwa njiani sasa nikawa nawaza kile kitendo cha jana" mmmmh sema niliinjoy mmmh🥰🥰anajua hadi anajua tena".Nikiwa nawaz hivyo kuna kauli inanambia amka Joy kuwa na msimamo kama mtoto wa kike🤣🙌akili inakinzana na moyo
Basi buana nikatoka mkuku mkuu hadi mchikichini nipo hoi kama mbuzi wa kimasai,moja kwa moja nikaelekea bafuni kuogaa,nilipomaliza nikabana mlango nikalala
Kwa muda huo sikuwa na wazo la kwenda kazini wala wapi yaani nilivurugwa haswaa🙌🙌
Nikiwa nimelala nasikia kuna mtu anagonga mlangoni na vile mlango wenyewe wa mchongo nikaitikia karibuuu upo wazi
Khee kumbe mama ashrafu nkajua sijui nani ,aya nambie nakuskiliza
'khoo mie sio mtu wa maana sio,ulimtegemea samia au majaliwa mbwa wewe?." Mama ashrafu alizungumza
Mama na wewe ushaanza em nambie shida nini lakini,nilizungumza.
Enhee hayo ndo maneno sasa so unabwabwaja tu.Joy yule bwana mapesa alokuwa akikukimbiza siku ile amekuja kukuulizia na kanipa elfu kumi ya soda pindi tu nikimpa taarifa zako,sasa tuongee biashara,unipe cha juu au nikakuchome?🤣
Khe mama ashrafu,we wa kuniuza mimi kweli mi si mwanao?niliuliza.
Sina uzazi mie mayai nshakaangia chipsi ,nipe jibu unanchelewesha.
"Nakuja sina hela za mchezo mimi,nilijibu."
Mfyuuu nyoo mnuka njaa tu kazi kulala si bora uje unioshee vyombo nkupe afu mbili,msichana mzima hovyo kabisa🤣🤣🙌🙌ila mama ashrafu🙌🙌kiboko kwa kweli
Sikuchukua muda nilifika mahali lilipopaki gari la boss kama nilivyopeea taarifa
"Ajabu sikumkuta Erick zaidi ya wafanyakazi wake tu".Boss wenu yupo wapi?Niliuliza
Hayupo,katuagiza tukupeleke kazini hivyo usilete usumbufu tuongozane mara moja.
Ni sawa,nilinibu na kujifanya kama nataka kuingia ile wanafunga mlango tu mie huyo nikajirusha kama jonsina,nikala chocho za kwendra nikajua kabisa hawa hawanipati
Nikiwa nimejibanza huku nikichungulia kujua yanayojiri ,nilishtushwa na simu ikiita tilitili tilitili,kuangalia ilikuwa namba ngeni,huwa sina kawaida ya kupokea namba hizo hivyo nilipuuzia
Tilitili tilitilitili simu hio haikuacha kuita hivyo niliamua kupokea
"Haloo Joy?." Mbona unanisumbua hivyo lakini?
Sauti hio haikuwa ngeni na nilivyogundua ni Erick nilikata mara moja na kuzima simu kisha nikarudi kwenye chumba changu cha giza.
Itaendelea
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni