MY CRAZY BOSS 06
Majira ya saa saba yalifika ambapo mimi na boss tuliongozana wote hadi kwenye kikao
Kama ilivyodesturi boss wangu yupo smart kweli kweli, watu wote wanamwogopa na kumuheshimu hana masihars kabisa kwenye kazi yake.
Kikao kiliisha kisha tuliongozana na boss hadi nyumbani kwake kwaajili ya mapumziko
"Nahitaji kwenda na wewe kwenye sherehe nyumbani kwetu naomba uruhusu hilo". Boss alizungumza.
Mimi tena ile kusikia sherehe🤣🤣na vile napenda kula sikuona sababu ya kukataa nilikubali moja kwa moja.
Ni sawa boss nitaenda nawe. Nilijibu.
Sawa nifuate , boss alizungumza hayo na mimi nilimfuata na kuingia ndani ya gari
Safari yetu iliishia kwenye duka kubwa la nguo kwa ushamba wangu na mandhari ya mahali pale aikutambua ni wapi kabisa
Tuliingia wote kisha akanipa amri ya kumfuata yule dada, huku na yeye akielekea kwenye chumba ambacho kiliandikwa "MALE" kwa nnje.
Ilichukua lisaa limoja tu ambapo nilichaguliwa gauni zuri pamoja na kupambwa vizuri si haba nilipendeza sana🥰flat skini mimi nilinoga haswaa, mdomo wangu mweusi ulibadilika na kuwa mwekundu chezea wewe. Nikatoka nnje ya chumba kwa manjonjo yote kama sio mie
Nnje sasa🙌🙌😳😳nilishangazwa sana baada ya kumkuta boss akiwa kavalia suti yenye rangi nyekundu sawa na gauni langu, 🥰🥰🌹ukituangalia vema waweza sema ni romeo na julieth, japo julieth wa bei ya jioni😁🤣
Boss aliponiona aliniangalia kwa mwangalui wa oooooh waooo🥰ila ni vile tu alishindwa kusema
Tuliongozana hadi kwenye gari lake na safari ya shereheni ilianza
Ilichukuwa muda mfupi sawa kisha tukawasili mahali hapo, mwa mara ya kwanza boss alishuka na kuja kunifungulia mlango😳😳nilibaki nikiduwaa tu
Akanishika mkono tukaongozana hadi kwenye sherehe hio
Ndani sasa🙌🙌🙌so beatiful jamani khaaa hili si kasri jamani ni ikulu,tuliingia wote mimi na boss wangu huku tukiwa tumeshikana mikono,mwa pamoja tulikaa kwenye kiti ambapo tulizungukwa na watu wachache si zaidi ya saba kwa mahesabu yangu ya haraka haraka
Hello dad hello mom👋
Yes hello son.
Mmmh hawa na hii english yao ntaweza kweli,na hapa sijui ndo kwao sio akwa ushua huu nikipiga hesabu ya fasta hapa hili kochi ni zaidi ya milioni tano,hii taa ni milioni moja ,kichwa cha mama.wigi laki tano,hereni zake laki tatu😳😳🙌🙌🙌mmmh yesuuu ni ajabu hii mtu anavaa kiwanja sikioni 🙌🙌
Joyce joyce greet my parents,boss aliniongelesha
Ooooh hello everybody,nkatia udhungu kidogo😁
Yes hellowakanijibu mambo yakaendelea
Basi buana baada ya hapo tukaelekea mezani kwaajili ya kula ,tukiwa tumekaa tukisubiri msosi keki ililetwa mezani
Baada ya muda nilishangaa wazazi na watu wengine wakiimba Happy Birthday to you,happy biday to you,nikamgeukia boss kumwangalia ajabu alikuwa akishangaa kama mimi
"Happy birthday my son live long,".Mama erick alizungumza
What !!ni birthday yangu leo ina maana?boss aliuliza
Ndio ina maana hukumbuki??
Hapana mama kazi nyingi sana ,anyway asanteni sana wazazi na ndugu zangu lets celebrate
Basi keki ikakatwa hapo wakalishana kizungu na vistiki mie natamani wamalize niikombe icing niile maana mie ninyime keki sio icing jamani🙌🙌🙌
Mara naona Erick ananisogelea huku kaweka keki mdomoni😳😳khee huyu boss kichaa etii,kwanza nikarudi nyuma kwa kushangaa japo bahati haikuwa upande wangu,nikajikuta nimejikwaa ile nataka kudondoka boss akanidaka halafu akaniwekea keki mdomini kiulazima,mie tena amuu🥰🥰nyie kama kuchi kuchi hotahe😁😁
Papapapapa papapapa!!! Sauti za makofi zikasikika kutoka kwa ndugu na wazazi wa Erick ,mie tena aibuu ilinijaa hatari,japo nilipoona vyakula nilijikuta nachangamka gafla
Nilipakua mikuku minyama na kuanza kuifakamia,sijali kabisaa nilikuwa natafuna hadi mifupa
Boss ananiangalia tu huku anashushia wine sijui ni pombe ile ila hata sikujali kabisa😁nyie hata ungekuwa wewe ungeacha mfupa na kuku nyama adimu kwa mtu kama mie😁👌
Baada ya zoezi la chakula kukamilika ,tukatoka nnje kidogo hapo tukaanza kushushia kinywaji ,mie tena nikaidaka savanna na vile ni afu tano kwetu😁nilizifakamia haswaa🙌nafasi kuja mara mbili uongo aiii
Erick we Erick nipeleke chooni,hapo nishalewa tena sielewi kituu
😳Kwanza boss alishangaa na watu wote walibaki wakinitazama,haraka sana akaniziba mkono kisha akaniongoza hadi chumbani huku akiyumba yumba ishara ya kulewa
Niliingia hadi chooni nikakijia kisha nikawa narudi chumbani huku nayumba
Gafla nikaanguka chini puuh kama mzigoo,baada ya muda Erick akaja kunibeba
Akanikokota hadi kitandani ambapo akanilaza kisha akaniinamia kwa juu akawa ananiangalia
Kwa jicho la mahaba🥰🥰nyie🙌 sijui ni upwiru au ni pombe tukajikuta ndani ya sita kwa sita
Itaendelea
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni