MY WANGU❤️ sehemu ya 101 na 102
Nikasema ni kweli yusta nimemfanyia mengi mabaya. Najutia na naumia . Ukipata mda mwambie anisamehe sana. Yusta akasema wee wala sitaki kumtibua mume wangu kipenzi. Yani mume wangu akisikia jina lako anapagawa . Anataamani kutapika. Na kama alikuwa anakula anasusa chakura. Na mm wala sitaki kumvuruga tu. Na apa mie nimekuja kukuomba sana ukae mbali na mume wangu. Mh nikasema yusta mm wala siwez kutembea na mlige tena . We kua na amani kabisa ya moyo. Mi nipo nyumbni najiangalizia tu. Nikikaaa powa naludi zangu dar wala sijaachikaaa. Mh akacheka akanmbia mh ila umefabaaa . Mrs tajeer mh na uhuu mwili ulikuwa unapigwa ama. Mie kimyaaa. Nikajua shoga kaja kunikashifu walaah. Akatoa simu yake kali nakwmabia kubwa kwenye screen kamuweka mlige . Akajifanya kuichezea nikajua ananirusha rohoo miee
Nikamuuliza nasikia una waroto 2 akanmbia yaa nnao wawili shoga wa kwanza aa mika 3 anayefata ana 2 mlige kanizalisha haraka haraka wala hataki masihara. Wamefanana sana na mlige. Yani ukiwaona wala huulizi na mlge navyowapenda wanae sikwambii. Acha tu. Nikamuuliza mh kwann ujawabeba sasa. Akanmbia wala siwabebi wapo na dada . Mi nna miangaiko sana. Mlige kanifungulia biashara kama zote ndo nipo napambana sna yani. Mh nikasema sawa umependeza shoga angu. Niachia ata elfu 50 basi shogaaa . Basi yusta akacheka. Akasema heeeee we si umesema hujaachikaa. Looh umeisha aya bwana apa mi sina pesa nyingi nna elfu 10 hii itakusaidia. Apo katoa pochi yake. Imejaa elfu 10 . Kama zote ..akanmbia usione nyingo zina mahesabu shoga .nikasema sawa asante wala usijali ata hii itanitoosha. Mh akaaga uyoo akondoka zake. Mh mdada mchoyo uyuu. Mie nilikuwa nmpa pesa zangu kama mwehu . Ye ndo hivi. Nikajishukulia tu miee.
Basi bwna zikapita week 3. Nipo ndani najifungia tu . Siku iyo mama akanmbia kwani ww kinachokufanya ujifungie ndani ni nn eeeh kwani we umeua au umeiba. Toka njee na fanya mambo yako. Ujaua mtuu. Asa utakaa ndani kila siku mpaka lini. Mie nikasema sawa mama. Ila wapi wala siendi mbali .bala balani siendi kabisaaa. Yani siendi naona aibu .na apo ndo week 3 nipo home kamwili kanaludi . Acheni kabisaaa. Basi siku iyo mama akanmbia twemde tukatembee bala balani tukaemeee . Mie nikagoma mama akanmbia ebu twende ukooo we una shida gani mjinga ww. Basi bibi mie ndo nikakubali nikavaa. Dela langu ma mtandio nikajifunika. Mama akambeba mwanangu. Tukaenda road . Na tukaemea. Tukaludi . Asa mam ndo akwa ananifanyia hivyo kila siku usiku tunaenda road najichangamshaaa kidogooo.
Basi apo road mlige alipashika. Alijenga maduka kama 3 . Na kaweka wanafunzi wake tulomaliza nao. Namjua mlige ana rohoo safi . Naona alifanya kama kuwapa ajira. Hivyoo. Nilikuwa namjutia sana .ila sikuwa natamani kukutana na mlige ata kidogooo. Yani sikuwa natamani kumuona . Naogopa sana na naona aibu mnoo ntamuangaliajee mimi. Basi ndo ikawa hivyoo mpaka ikakata miezi 3. Mk sijaonana kabisa na mlige. Ila yusta namuona na mbwe mbwe jamnk mhh. Nikimuomba pesa ananipa elfu 5 au elfu 10. Nabaki kuguna tu mana mengine niliyataka mwenyew ningetulia na mlige wala yasingenikuta mieeee
Basi bwanaaa . Siku iyoo sasa . Mama akanipigia simu kwamba nikachukue mchele dukani nipike kabisa mana yey yuko shamab. Basi mie nikasem sawa. Bibi mke nkachukua pesaa mpaka dukani . Nikanunua mchele na mafuta. Basi nikiwa pale napimiwa . Ikapaki gari pale. Tena kali mnoooo. Mh nageuka hivi. Na mligee ndo anashuka . Aseeee moyo wangu ulifanyaaa paaah. Mlige wal hakustuka kuniona. Aseee mi nikageuza sula yangu chapu pembeni . Alikuwa kavaa pensi nyeusi na t shrt ya kijani flani hivi kawakaa sana yani kama alitokea nyumbani vile . Hakuwa kavaa official .nyie uyu baba wala hazeeki.. ni amezidi kuwa handsome. Sikutamani kumuangalia tena naona aibu na nilivyojiishia mimi.
Yule kijana alokuwa nanaihudumia .aksema boss karibu. Mlige akasema thankss. Endelea kumuhudumia mteja. Mh kumbe na hili duka ni lake wala sikuwa nimejua mm. Yule mkaka akaniwekea . Nikataka kuondoka . Mlige akaniita faridaah. Nikasimama uku natetemeka ile ya wazi kabisa. Mlige akanisogelea akanmbia ndo hutaki ata kunisalimia sio. Nikasema hapana akanmbia nilikuwa mwalimu wako pia . Haitoshi ww kunipa salamu. Nikasema shikamooo. Aakaningalia kisha akatabasamu tu wala hakuniitikia salamu yangu. Akanmbia nenda. Mh mimi ata kugeuka sikutaka ni mbioo. Mungu wangu kwa nn kaniona sas. Na nilivyoishaa mimi doooh nimejitia aibu sana mbele yake. Basi nimeludi nyumbani na nikaandaa chakura ila mawzo .mlige kapendeza nyiee kwanza ata siendani ane tena nilivyojisshia . Mh
Basi usiku ndo mama kaludi na mambo mengine yakaendelea . Mwenzenu nilikuwa ni mtu wa nyumbani sana . Au siku niende shamba kumsaidia mama kulima baso nakuja kupumzika . Road sitokei aibu watu walikuwa wananisema sana jamani. Mh siku iyo bwna ilikuwa mida kama ya usiku sa 2. Nipo nyumbani na mama tunaongea. Ongea . Mana rahul alilala mda mrefu sana. Basi tukawa tunaongea ongea . Mala mlango ukagongwa .mie ndo nikaenda kufungua . Alikuwa ni mkaka flani nimesoma nae shule ya sekondari pamoja. Na ni kuna duk moja la mlige uyu kaka anaiuza anaitwa juma. Nikamshangaa kuja kwetu ule mda nikamsalimia nikamuukiza umekuja kumuona mama nikuitie. Akanmbia hapana nimekufata ww nataka tuongee kidogo jambo la siri. Mhh mie nikaludi ndani nikamwmabia mama nakuja kuna mtu anongea nae apoo. Mama akniukiza nanai. Nikasema juma yule alikuwa mwanafunzi mwenzangu. Mama aknmbia sawa
Basi mi nikatoka kwa pembeni kumsikiliza juma . Mh nashangaa ananmbia mlige anakuta yupo. Uku . Kanambia nikupelek. Nikapgopa sana mm. Nikasema hpana smi sitaki kwnda. Akanmbia unaogopa nn sasa anataka kuongea na ww tu na wal sio si lengine. Ebu plsss umsikilize. Mh nikamuuliza yupo wapi. Akanmbia kwangu kule bondeni chapu tu. Mh mume wa mtu sasa .mlige nikawa naogopa jamani. Juma akanambia twende bwana . Anahitaji sana kuongea na ww. Mh mie nikawa naogopa je akinipiga may be bado ana hasira na mimi kwa niliyomkosea . Mh nikawa naogopa ila juma akanibembeleza sana . Mie nikakubali tukaenda mpaka kwa juma . Ni kajumba cha udongo chumba kimoja tu.juma akanmbia ingia ndani yupo umoo nakungojaa mh nikawa naogopa ila nikajikaza nikaingia na kweli nikamkuta mlige ameekaa juu ya kitanda cha kamba.
🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴🔴
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni