Kwa karne nyingi, dunia iliitazama Milki ya OTTOMAN EMPIRE kama ngome kuu ya Uislamu. Kutoka milima ya Anatolia
Watu waliamini kuwa dola hii ingedumu milele iliitwa “ngome ya Waislamu,” kwa sababu ililinda ardhi takatifu, iliongoza kwa sheria za Kiislamu, na iliwapa hifadhi mataifa mengi yaliyokuwa chini ya bendera yake.
Katika karne ya 16, dola hii ilifika kilele chake chini ya utawala wa Suleiman mkuu. Huyu alikuwa mtawala aliyekuwa kama kivuli cha haki na nguvu kwa wakati mmoja.
Aliiongoza dola kwa mkono wa sheria na upanga, akapanua mipaka yake hadi Hungary, Balkan, Mashariki ya Kati, na Mediterania. Istanbul ikawa kitovu cha dunia...mahali pa elimu, biashara, na siasa. Lakini baada ya kifo chake, kila kitu kilianza kubadilika. Sio kwa mara moja, bali taratibu mambo yalianza kuharibika......
Masultani waliokuja baada yake hawakuwa na ule moto wa uongozi. Wengi wao walianza kujifungia ndani ya ikulu ya Topkapi, wakiacha mambo ya dola mikononi mwa washauri, mawaziri, na makundi ya kijeshi. Utawala ukawa wa mbali na wananchi, rushwa ikaanza kuota mizizi ndani ya dola, na maamuzi yakaanza kufanywa kwa maslahi ya wachache. Hivyo ikawa kama nyumba kubwa ambayo baba mwenye nyumba ameacha kuisimamia....
Wakati huo huo, kulikuwa na jeshi maalum lililokuwa uti wa mgongo wa dola: Janissaries. Mwanzoni walikuwa ni jeshi lenye utii na nidhamu.
Walichukuliwa wakiwa watoto, wakafundishwa kwa bidii, wakawa askari wa kipekee waliomtii sultani moja kwa moja.
Lakini kadri miaka ilivyosonga, nao wakaanza kubadilika.
Wakaanza kujiona kama wamiliki wa dola badala ya watumishi wa dola.
Wakadai mishahara ya kudumu, wakaruhusiwa kurithisha vyeo vyao, na wakaanza kupinga mageuzi yoyote ambayo yangewafanya wapoteze nguvu.
Ulaya, kwa wakati huo, ilikuwa inabadilika kwa kasi. Walianzisha viwanda, silaha zikaboreshwa, meli za kivita zikatawala baharini, na jeshi la kisasa likaundwa kwa sayansi na nidhamu mpya.
Ottoman, kwa upande wake, ilibaki katika mifumo ya zamani.
Kila jaribio la mageuzi lilipingwa hasa na Janissaries.
Hata masultani waliothubutu kubadilisha mfumo waliondolewa au kuuawa.
Ilipofika mwaka 1826, Sultani Mahmud II aliamua kukata mzizi wa tatizo.
Aliwaangamiza Janissaries kwa nguvu kubwa katika tukio lililojulikana kama (Auspicious Incident.)
Lakini ukweli mchungu ulikuwa huu: tiba ilikuja wakati ugonjwa ulikuwa umeenea mwilini kote.
Uchumi nao ulikuwa umeanza kulegea. Njia mpya za biashara za Ulaya kupitia bahari za mbali zilipunguza umuhimu wa Ottoman katika biashara ya dunia. Fedha zikapungua, deni la nje likazidi, na dola ikaanza kutegemea mikopo kutoka kwa mataifa yale yale yaliyokuwa yanaitamani ardhi yake.
Ulaya wakaanza kuiita Ottoman:
“mgonjwa wa Ulaya”
jina lililobeba kejeli, lakini pia ukweli mchungu.
Ndani ya dola, upepo mpya wa mawazo ulivuma. Watu wa makabila na dini tofauti walianza kujiuliza: “Kwa nini tusitawale wenyewe?” Wazo la utaifa (nationalism) likachochewa na Mapinduzi ya Ufaransa. Wagiriki waliinuka kwanza, wakafuatiwa na Waserbia, Wabulgaria, na mataifa mengine ya Balkan. Ardhi ikaendelea kupotea, uasi ukazidi, na dola ikaanza kusinyaa.....
Kisha likaja pigo la mwisho..Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Ottoman ikaungana na Ujerumani, ikipigana vita nyingi kwa wakati mmoja dhidi ya maadui wenye nguvu zaidi. Ingawa kulikuwa na ushindi wa kihistoria kama Gallipoli, uchumi na jeshi vilichoka kabisa. Vita vilipoisha, washindi waligawana mabaki ya dola kupitia Mkataba wa Sèvres... .
Lakini kutoka katika majivu hayo, alisimama mtu mmoja mwenye maono mapya mtu huyo si mwingine bali ni Mustafa Kemal Atatürk. Aliongoza mapambano ya mwisho, akaondoa kabisa mfumo wa usultani mwaka 1922, na ikazaliwa Jamhuri ya Uturuki. Hapo ndipo pazia lilipofungwa rasmi kwa Dola ya Ottoman baada ya zaidi ya miaka 600 ya historia.
Naam hii hadithi ya kuanguka kwa Ottoman empire si hadithi ya kushindwa kwa siku moja tu. Ni wazi inatufunza kwamba nguvu bila mageuzi hudhoofika, mamlaka bila haki huanguka, na dola yoyote haijalishi ni kubwa kiasi gani ikikosa busara, umoja, na uwezo wa kubadilika, mwisho wake hufika polepole… hadi siku historia inaandika mstari wa mwisho.
Kwa history, story, reallife events na visa na mikasa ya dunia nifollow Maher bey.
✍️Maher bey
#like
#shere
#comment
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni