FATE TO LOVE YOU π 16 MTUNZI UHURU MEDIA Siku hiyo ilikuwa siku ya Jerry na Lina kuelezana juu ya hisia zao.
Walienda kukaa bustani na kuongea mambo mengi sana. Hali ya hewa ilianza kuwa ya kiubaridi lakini hakuna alietamani kwenda ndani. Jerry alivua kiti lake na kuliweka vizuri kwenye mabega ya lina ili kuzuia baridi.
Mwili wa Lina ulikuwa ukisisibmka kwa jinsi Jerry alivyokuwa akimuonyesha upendo na kumjali. Hakuwa na hiyana aliamua kumuachia na kumpa Jerry mapenzi yake yote .
Mapenzi yao yalianza kwa kasi kubwa sana. Jerry alitimiza kila alicho kuahidi ikiwepo na mapenzi moto moto na kumjali kwa kila jambo.
Siku moja walikuwa wametoka walikaa sehemu huku wakipata vinywaji.
" J unajua kuna swali moja huwa nataka kukuuliza lakini huwa nasahau ila leo nimekumbuka naomba nikuulize.
" Uliza tu mpenzi wangu.
" Natamani kujua ilikuwaje taarifa zangu na mara ya kwanza kuniona ilikuwa wapi?
Jerry alitoa tabasamu dogo kisha akachukua grass ya kinywaji akanywa kidogo , aliishika grass mkononi na kuiangalia kisha akaanza kusema.
" Siku ya kwanza kukuona ilikuwa nyumbani kwa Maxwell, nilikuja kuonana nae kwa mambo ya biashara . Tukiwa kwenye ofisi yake pale nyumbani ulikuja kutuletea kahawa. Kwa kiasi fulani nikitokea kuvutiwa na wewe kutokana na usikivu wako, upole na heshima ulioonyesha pale.
Mara ya pili nilikutana na wewe ukiwa na Stephen mlikuwa Villa super market mlikuwa mkifanya manunuzi na wewe ulikuwa ukila ice cream.
Nikitokea kuvutiwa sana na wewe , siku hiyo kuna kitu niliona ndani yako ambacho siku ya kwanza sikuwa makini sana kumuangalia. Lina nilijiuliza nakupenda nikapata tamaa na kuwa na wewe lakini sikuweza sababu ulikuwa kwenye penzi zito na Stephen.
Ila muda uleule mkiwa mnafanya manunuzi Stephen alipokea simu akasogea pembeni kuongea na simu. Akiwa bado anaongea na simu aliwaona mabinti wawili wakiwa wanachagua vitu, Stephen aliwaangalia sana , baada ya kumaliza kuongea na simu aliwafuata nikaona wanabadilisha na namba za simu na kuongea maongezi ambayo sikujua wanaongea nini.
Baada ya muda Stephen alikufuata mkaongea kitu kisha akaondoka na wale mabinti walimfuata nje, wakapanda kwenye gari yake na kuondoka .
Wewe ulifanya manunuzi kisha ukachukua usafiri na kuondoka.
Niliendekea kufuatilia nikaja kugundua Stephen hana msichana mmoja na wewe alikuwa akikitumia tu. Nilijiuliza naumia sana nilijaribu kutafuta historia yako na jinsi anavyoishi kwenye ile nyumba kiukweli sikupenda nilikuwa nauliza sababu tayari nilikuweka kwenye moyo wangu.
Siku ya tatu kukuona ni siku ya sherehe ya kuzaliwa ya Osca.
Tangia unaingia pale ndani nilikuwa nikiangalia sana mpaka stespan alipomuacha na kuondoka na mwanamke mwingine wakaenda hotelini.
Alipoenda chooni nilikufusta nyuma nilitamani sana siku ile niongee na wewe ila sikujua naanza je. Wakati unatoka nilishindwa kabisa kujizuia nilikuvuta na kupiga busu la mdomo.
Jerryson alicheka kidogo huku akitingisha kichwa.
" Mapenzi yanaweza kumfanya mtu akawa chizi yani sijui nilianza je kufanya lile tukio la busu.
" Kumbe ulikuwa unajua kila kitu nilichokuwa na pitia?
" Kila kitu hata siku ulipoondoka nilipewa taarifa na mtu niliempa kazi ya kukuangalia.
" Ni nani huyo?
" Tuachane na hayo mpenzi, kwa sasa hayana umuhimu . Sasa tuongelee mambo yetu yani mimi na wewe basi.
Lina alikaa kimnya akimuangalia Jerry huku akivuta kumbukumbu ya matukio aliyomuelezea .
Jerry alimshika na kumuuliza
" Vipi mpenzi upo sawa?
" Nipo sawa. Unajua sikuwahi kufikiria kama kuna mtu ambae anafuatilia maisha yangu kwa undani kiasi hicho. Kila jambo unalonifanyia linanifanya kuwa mimi ni mtu muhimu.
" Lina wewe kwangu ni zaidi ya mtu muhimu, ni zawadi kubwa ambayo kila nikiiona moyo wangu unafurahi na kuwa na utulivu. Unajua kuna wakati napitia mambo mazito pindi ninapokuwa kazini lakini nikiwa na wewe hasira, uchovu na mashaka yote huwa yanayeyuka kama barafu.
Unaniweza mama hakuna mwingine anayeweza kunifanya nijisikie hivi.
Lina alijikuta alimsogelea Jerry na kumpa busu laini kwenye shavu lake. Jerry akimkumbatia Lina kwa nguvu huku akiwal na hisia kali za mapenzi.
" Lina.... Jerry aliita jina la Lina kwa sauti ndogo lakini ilipenya vizuri kwenye sikio la Lina na kuleta msisimko fulani.
" Mmmmmh.. lina aliishia kuguna tu.
" Wewe ni wangu na mimi ni wako, Nakuahidi kula siku nitakupenda, kujilinda na kukutunza.
Kila mmoja alikuwa kwenye msisimko mkubwa hawakuweza tena kuendelea kuwepo pale . Walinyanyuka na kuondoka kwenye lile eneo na kurudi nyumbani kwao huku wakitamba kwa macho ya mahaba . Walifika nyumbani na siku hiyo haikupita hivihivi ilikuwa ni jioni moja ya kukumbukwa kwa mahaba mazito wakiyopeana yani yalikuwa ni mapenzi yasio na mipaka mpaka Jerry akasema.
" Kwa sasa siwezi kukaa kimnya kipa mtu anatakiwa kujua kuwa lina miwa Jerry na Jerry niwa lina mpaka milele.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi