FROM BANGI TO BABY ๐๐ SEHEMU YA 14
Nikasogea hadi karibu na Geti yeye alikuwa kwa nje akanifanya na mie nivuke geti kidogo yaani mguu mmoja ukawa nje ya Geti mwingine ndani
"Enhee" yaani nilikuwa makini nae mno
"Aunt, Unaitwa na huyu" akaonesha kidole pembeni ile nageuka hata sijaona mtu nilishtuka nimevutwa
Aliponivuta akanibana ukutani, pumzi yangu ikakatika ghafla. Harufu yake tu niliitambua kabla hata sijainua macho, ile harufu ileile iliyokuwa inanifanya nisahau hasira zangu zote. Mkono wake mmoja ulikuwa umenishika kiunoni halafu kanibana kwa ukuta
"V...Veda" Nikajikuta nimeita kwa sauti ya kutetemeka ya chini kabisa, moyo unapiga mbio kana kwamba unataka kunitoka kifuani.
Nikainua Macho yakakutana na yake, yalikuwa mazito, yananitazama kama mtu ana ya hisia hivii
Nilipo muita jina akashusha pumzi ndefu halafu nzito mpaka niliisikia ikipiga shingoni kwangu, mwili ukasisimkaa nilikuwa nameza mate kama jinga hiviii ...
โKwanini hutaki kuongea na mie" akanongโona karibu na sikio langu aloo Sauti yake ilichoma roho, ikanichanganya hasira na hamu humo humoo, maumivu na wivu vikajichanganya kwa pamoja, Nikameza mate, nikageuza uso pembeni nikajaribu kujifanya kama simjali hivii, lakini mapigo ya moyo aah wee nahisi alikuwa anayasikia
โHatuna cha kuongea mie naweweโ nilisema sina hata uhakika na ninachokiongea sauti enyewe ilinisaliti maana ilitoka dhaifu mpaka basi
"Kipo Vero..."
"Kama kuhusu mama yako, Sikujua kama ni mama yako kwahiyo nilifanya kama namfanyia mgongwa tu ambae alikuwa na uhihitaji kwa wakati huo"
"Kuhusu mimi na wewe, tuna vingi kwa kuongea"
"Sina cha kuongea nawewe Veda niache" nikamsukuma ili nijinasue lakini hata halinatikisika nili mwamba kweli kweli
Akanibana vizuri nikahisi joto lake nikaanza kuhema juu juu
"Tutaacha kile kipite kama hakuna kilichotokea, Sijawahi kusahau hata nukta ya ule usiku Vero, Kwanini unakuwa kama hakuna kilichotokea..."
"Ooh ....Sikia Veda mie sikumbuki chochote kwahiyo niache"
"Hapana Veda ona hii inaninyima usingizi..." wacha atoe shanga zangu nililitoa jichoooo heheh hizi shanga hata sikuwa nakumbuka zilipo baada ya purukushani zotee kile kipindi dah , ile siku nilizivaa zilikuwa mpyaa ili kumpagawisha D, hahaha kumbe zikampagawisha Veda mpaka akaondoka nazo mie habari sinaa hahah
Nilizikwapua aibuuu kama zote "Umezitoa wapiii???"
"Uliziacha kwenye gari ya D, sikutaka azione ndio maana nikazichukua, Vero embu jipe muda basi nipe nafasi hata kidogo tu mie nitakuwa tayar kubanana na Huyo D mpaka siku utakapo fanya maamuzi"
"Mh kwahiyo unaniona mie malaya sanaaa eeh, Vile mnavyo changia wanawake na huyo mpuuzi mwenzio, basi unajua namie unaweza kunitumia muda wowote ukitaka ....Sikia Veda mie sio muhuni kiasi hicho naweza kuwa malaya kama unavyofikiria lakini sijafikia bado viwango hivyo....." yaani nilikuwa naongea kwa hasira natetemeka ghafla tu aliniaharibia mood yangu yoote , nikamsukuma kule nikawa naondoka kurudi ndani mpaka machozi yananitoka natetemekaa huyu kaka nampenda sana ila nahisi ni malaya tu bwanaa aaah nitaumia kama nitakuwa nae huyuu aaah ...
Ile navuka geti nataka kuufunga akalizuia halafu akaingia "Toka D yupo ndani??"
"No!!! Umenielewa Vibaya nipe muda unisikilize, Vero labda mie sipo vizuri kwenye kutongoza kila ninapo jaribu ndio naharibu lakini nakupenda"
"Mungu wangu we kaka embu toka nje, D atakuku...." Kabla hata sijamaliza kusema
Alinivuta ghafla.
Sikupata hata nafasi ya kupumua.
Midomo yake ikafunika yangu kwa busu zito la ghafla, Busu lenye hisia za hasira na maumivu kwa pamoja.
Busu ambalo hata hakuomba ruhusa, yangu ooh jamaniiii
Nilishtuka, macho yakanitanuka, mwili ukakakamaaโฆ moyo wangu ulivyo msaliti ukaanza kudunda kwa nguvu.
Mikono yake akanibana mabegani, kama vile anaogopa nikimponyoka nitapotea kabisa.
Lile Busu lilikuwa kama adhabu ya maneno yote niliyomrushia, nikajaribu kumsukuma kwa nguvu ndogo ile ya sitaki nataka yaani kama nina ogopa asije kuache hiviii, baada ya denda kama la Dakika moja akatoa mdomo wake akabaki ananitazama machoni huku anavuta na kutoa pumzi, Paji lake la uso limegusana na langu
Halafu akarudi tena taratibu kuja kuvamia midomo yangu safari hii mwenzangu moyo ukanisaliti nikajikuta tu nampokea ile naanza tu kujilimbwasa miutamuuu, D huyooo
"Verooo....!!!!?" Hakuamini anacho kionaa mwenyewe nilishtuka nikajirusha nyuma chap
"Vedaaa, yaani vee...Eeh Au nimechanganya mambo"
ITAENDELEA....
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni