REALLY LOVE* *SEHEMU YA 37*
basi ikabidi mzee fahad awaeleze wote juu ya taarifa za msiba huo, kwakuwa harusi ilikuwa Imeisha haraka watu walijiandaa kwenda hospitari, familia ya cathe ilikuwa na majonzi sana haikuamini kama imempoteza cathe,
mama cathe alilia sana alijiona yeye ndio sababu ya kila kitu, sababu ya kumpoteza mwanae kipenzi alilia sana, basi ikabidi kesho yake waandae mazishi hakuna aliyekuwa na furaha siku hiyo,
hata fahim hakupata furaha ndio alikosewa sana na cathe lakini sio kufa aliumia sana sana mno, nafahima nae pia aliumia kwasababu bado cathe atabaki kuwa mdogo wake tu japokuwa hakuwa na mema
basi mazishi yalifanyika watu wote walimuaga cathe familia ilitawala na majonzi makubwa sana, baada ya mazishi kila kitu watu walisambaratika, ilipita wiki moja kidogo ikawa anafuu watu wakaanza kuchangamka kama zamani huku maisha yakisonga mbele
mzee fahad aliamua kuoa mke mwingine yote. sababu hakupata amani kabisa akiwa na mama. fatuma, basi furaha ilizidi kutawala sana katika familia hizo
fatuma nae alikuwa na majanga tu alibebeshwa mimba na mwanaume ambaye hakuwa anamuhudumia chochote wakawa wanahangaika. tu kuhudumia wenyewe, kutokana na vitimbi vya mama fatuma mzee fahad akaamua kumuacha kabisa mama fatuma huku akabaki na mkewe wakati huo aliweza kujimudu kutokana na kazi zake
fahim alizidisha mapenzi sana kwa mkewe fahima, alikuwa anampenda sana kupitiliza, selina nae aliwafanyia sapraiz kuwatambulisha mpenzi wake ambaye ni john aisee wengi hawakuamini
""dah ila john wewe ni msiri sana unaweza kupindua nchi alsee" alisema fahim baada ya john kumvisha pete selina
***hahaahaha mapenzi usiri ndugu yangu:*** alisema john basi siku hiyo furaha ilizidi kutawala sana, baada ya miezi mitano selina akafunga ndoa na john kwa uhalali kabisa rasmi akawa mke wa john,
hatimae miezi ikasonga mbele fahima. akajifungua mtoto wa kiume yaaani copy na fahim furaha ikazidi sana hususani kwa mama fahim kwa kupata mjukuu jembe, mtoto akapewa jina la fahari, jamani yani mama fahima baba fahim na mtoto fahari aiseeee walijua sana kumetisha,
miezi ikazidi kusonga mbele huku kwa mama fatuma hali yao ya kimaisha ilikuwa ngumu sana wakaamua tu kurudi kijijini kwao tanga ili wakalime angalau iwe nafuu maana hata kula yao ilikuwa shida sana, basi wakaamua kisafiri wakaondoka mjini hapo,
baada ya miezi mitatu siku moja fahima na mumewe wakaamua kwenda nyumbani kwa mama fahim kusalimia, siku hiyo walipanga familia zote ziwe hapo hata selina na mumewe wakaja na mzee fahad na mkewe pia basi wakapika chakula kizuri san mazagazaga kama yote,
mara katika story walishangaa mtu akija akiwa amechakaa sana alifika na kusimama mlangoni hapo, watu wote walishangaa ninani maan hawakumjua kabisa kwajinsi alivyo chakaa mwili pia alikuwa ananuka sana mara akaja mlinzi kutaka kumtoa akidai kwamba alilazimisha kuingia ndani lakini fahim akamwambia amuache ili aeleze shida yake
seven mimi ni devi aiseeeeeeeeee watu. wote walishangaa hawakuamini kama ni devi kwajinsi alivyochakaa hadi wakamsahau kabisa
""fahima najutia sana makosa yangu nimekuja hapa ili kukuomba msamaha maana sikuwahi kabisa kukiri kosa langu, nikweli nilitembea na cathe nisamehe sana maana dunia imenifunza nilipata bahati nikaichezea leo najuta najuta mara elfu najuta mimi, napia naomba mnielekeze kwakina cathe maana nimeenda nimeambiwa wamehama mda sasa sijui anakaa wapi maana niliikataa mimba nikaikataa damu yangu kwakweri mimi sina akili nimekili naomba mnisamehe sana wote aiseee devi aliongea kwa huruma sana kwakweli alijutia sana
""sawa tushakusamehe lakini huyo cathe unayemzungumzia hapa tayari alishatangulia mbele za haki ulimuacha akapitia magumu akateseka sana mwishowe akaenda zake muombee dua huko alipo aiseeeee maneno ya fahim yalimchoma sana devi alijikuta akidondoka chini hakuamini kabisa alichoambiwa,
devi akaanza kulia sana kwa uchungu akajikuta akiwahadithia maisha yake baada ya kuikataa mimba mpaka kuingiliwa kinyume mpaka. kutupwa akajikuta hospitari kutoka na kusaidiwa na watu wema hapo ndo akaanzisha maisha mapya ya kuokota makopo hakuw na pesa hata ya nauli kwenda kwao aliliaa sana
cathe najua nimekukosea sana mama nisamehe mama najuwa nimekosa mimi. ndosababu ya yote mama nimekuua wewe na mwanangu mama sirudii tena** aiseee devi alijuwa kulia nyieeee mpaka huruma
ikabidi fahim ampe pesa ya nauli arudi kwao maana hakutaka tena ukaribu na devi hata kidogo basi devi alishukuru tu kisha akaondoka na kurudi kwao kijijini
maisha yaliendelea familia hizo zilipendana, urafiki wa fahima na agness ulikuwa zaidi ya ndugu wakati huo agness nae aliolewa na kuzaa mtoto mmoja basi furaha iilizidi kutawala katika maisha yao
asiyefunzwa na mamae hufunzwa na ulimwengu, ukiendekeza tamaa Inaweza kusababisha kuharibu maisha yako na kuja kujutia sana wakati huo tayari ushachelewa, chunga tamaa mbaya, ukipendwa pendeka...
MWISHOOO
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni