*AAAAAASH BOSS ENZO* *season two* *SEHEMU YA KWANZA*
SONGA NAYO
Kwanza nilishtuka sana, nilimuangalia Enzo kwa makini sana lakini enzo hakuwa na uwezo ata wa kuniangalia, muda wote alipepesa macho akiangalia pembeni tu wakati akizungumza. Maneno makali sana juu yangu.
"Enzo huyu sio wewe, Enzo wangu me nakujua umepatwa na nini jamani"
Niliendelea kulia nikimshikilia kwa nguvu ili asiweze kupanda gari na kuondoka bure
"Enzo, usinifanyle hivyo Mwenzio, nakupenda sana mume wangu mtalajiwa, nakupenda mno, please usinitese moyo wangu"
Nilikuwa nikizungumza uku nikilia kwa uchungu sana Tena mbele za watu, kwenye kupambania penzi langu sikuona albu ata kidogo zaidi nilitamani Enzo anielewe.
"Ishani Ebu niachie unanichafua Mimi"
Alizungumza Enzo na alipoona Kuwa naendelea kumng'ang'ania, haraka akanichapa kibao kimoja matata na kwa SAUTI ya hasira akafoka.
"Nimesema sikupendi, Sikultaji Mbona uelewe wewe"
Nilibaki nikiwa nimepigwa na bumbuwazi uku akili yangu ikikataa kabisa juu ya Maneno makali ambayo Enzo ananipatia.
Muda huo huo mlango wa gari ya Enzo ulifunguliwa na Pully akashuka kwa mwendo wa Madaha akiwa na tabasamu pana sana.
Polepole pully akamsogelea Enzo na mbele za watu akamkiss mdomoni na kuzungumza.
"Nakupenda mume wangu kipenzi
Enzo akatabasamu na kumkumbatia Pully vizuri kabisa, Yaani walikuwa ni Kama wananitambia hivi Binti wa watu mwaya.
Nilibaki nikiwaangalia uku machozi yakinitililika kutokana na maumivu makali ambayo nilikuwa nayo
"Huyu ndiye mwanamke wa maisha yangu, Ishani sahau kuhusu Mimi"
Alizungumza enzo kisha akanishika mkono Pully na moja kwa moja wakapanda gari Yao ya na kuondoka.
Siku hiyo Bwana nilikuwa kituko cha mtaa. mzima, Yaani Sijui niwaambie nini lakini ndugu. yenu nimejua kuzalilika, shoga yenu nimejua
kuaibika Tena mbele ya kila mtu Mpaka
wajumbe wa Nyumba kumi.
"Twende Ndani kipenzi
Alizungumza shoga yangu Pili na kuangaika kuninyanyua pale chini ambapo nilikuwa nimekaa.
"Pili Niache tu, nimeumbuka mimi
Nilijibu na kuendelea kulia tu.
Mashoga zangu wengine nao wakasogea na kunisaidia kunyanyuka kisha moja kwa moja wakanipeleka Ndani kwangu.
Siku ilikuwa nguvu sana na nzito kwangu, nilikuwa ni mtu Mwenye huzuni kuliko maelezo, nilikuwa ni mtu wa kulia tu Kama nimepatwa na
msiba
Nimepoteza vitu na watu muhimu kwenye maisha yangu lakini Mbona Kama Enzo
ameniuma zaidi au kwakuwa Ndio mwanaume wangu wa kwanza ? Au kwa Kuwa nimempenda sana kuliko nilivyojipenda Mimi Mwenyewe
Week nzima ilipita uku nikiwa ni mtu wa kujitenga tu peke yangu na kulia, chumbani kwangu kulikuwa Kama dampo Yaani, nguo
chafu kuzikuta kitandani ni kawaida, kukuta vyombo kwenye kabati la nguo ni kitu cha kawaida sana aiseeeh
"Hivi Ndio nimejisusa ikiwa Enzo anaendelea na maisha yake ?"
Nilijiuliza kimoyomoyo nikiwa nimesimama mbele ya kioo nikijitazama jinsi ambayo nimebadilika na Kuwa hovyo Ndani ya week
moja tu.
"Lakini Kwanini Enzo ? Kwanini ulinionesha kunijali sana? Kwanini ulinifanya niamini Kuwa unanipenda sana, nakuchukia Enzo, nakuchukia mno, sikupendi
Nilizungumza kwa SAUTI uku nikilia tu.
Baada ya muda nikaangalia chumba changu na kila kitu, Walahi sikupendezwa na kila kitu kilivyokuwa kimekaa.
Nikachukua mtandao wangu nikafunga tumboni kwa nguvu kabisa kisha nikaanza kufanya usafi uku na uku
Kuna Namna niliona Kama sifaidi hivi,
nikawasha sabufa langu na kuweka SAUTI ya juu kabisa, nikaweka taarabu zangu pambe tu Maana kipindi iko pia uswahili nilikuwa nauweza kuliko maelezo ni vile tu, Enzo alikuwa sio mtu
wa uswahili
Hapo nikafanya usafi wangu kwa raha mustarehe na nilipomaliza tu nikaenda nje nikaoga na kurudi Ndani kwajili ya kuvaa,
"Khaaaaaah week moja tu tayali mshape wangu. wote umepululuka aaaaah, mapenzi kubabako
Nilizungumza uku nikijiangalia kwenye kioo.
"Lazima nijikaze na life iendelee, Enzo hakuwa wangu"
Niliendelea kujipa moyo tu Maana sikuwa na chagua ikiwa mwanaume Mwenyewe Ndio ameshachagua njia yake.
Nikavaa mavazi yangu mazuri na kutoka nje
amsha ya hatari
"Wewe iko kigoma wapi Maana kimenipa amsha.
Nilimuuliza mpangaji mwenzangu ambaye yeye. ni mlokole
"Ni birthday ya Pili, Ndio wameenda kukipokea kigoma hapo stendi
Alijibu msichana huyo wa kilokole kisha akaingia zake Ndani Maana haya mambo ya kidunia na yeye ni vitu Sita tofauti.
Haikuchukua muda mrefu kigoma kikafika,
kwanza Ishani Mimi nikakipokea na sarakasi moja ya nguvu, hapo kwiza kila mtu akaganda. akinishanga maana hawakutalajia kabisa. kwamba Ishani Mimi naweza kufanya kitu Kama
iko kwa wakati huo
Siku hiyo Bwana nilikuwa Kama nimevulugwa vile, imagine sikulewa ata Pombe sikunywa lakini nilikuwa na vibe la hatari, Yaani Nilicheza
mpaka nikawa najiambia iki nini jamani
Hatimaye Giza likaingia na kigoma kikaondoka,
Walahi nilikuwa nimechoka, mwili uliniuma sana kutokana na misalakasi ambayo nilikuwa
naipiga kwenye kigoma.
Ila nyie maumivu ya mapenzi Yaacheni tu, imagine, nje nilikuwa nimechangamka sana,
lakini nilivyoingia tu chumbani kwangu, nikajikuta nikipata huzuni Tena na nikajikuta nikianza kulia upya.
Hatimaye week nyingine Tena ikapita uku nikiwa single, singula, singwengwella nyieeeh upweke unatesa Sana.
Kwa upande wa Enzo Sijui ata alikuwa na hali gani, lakini hakuwai kunitafuta ata siku moja na online namuona kila siku.
"Kwahiyo ni kweli Enzo unitaki Tena?"
Nilijiuliza nikiwa nimekaa kitandani na muda huo Ilikuwa ni Saa 4 asubuhi.
"Ishani, Ishani kuna mgeni wako"
Ilikuwa ni SAUTI ya shoga yangu pambe Yaani pili
"Nakuja"
Nilijibu, kisha nikajiuliza.
"Moeni? Mgeni gani Tena? Au shemeji nick? Itakuwa katumwa na Enzo mwaya
Nilijikuta nikifurahi sana uku imani yangu kubwa.
ikiamini Kuwa ni nick Ndio amekuja. kunitembelea.
Kwa shauku na Furaha Kama yote, nikashuka kitandani na kusogelea mlango, ile nafungua tu, mtumeeeeeeh uso kwa uso na mama mzazi wa
Enzo, Yaani madam groly.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni