FROM BANGI TO BABY ππ SEHEMU YA 13
Nikasikia kuna nini hapoo???" Halafu muda huo Veda alikuwa ananitazama machoni na mie nimtazama yaani tunatazamana nina uhakima mioyo yetu ilikuwa inaongea maana kwa yale macho ya veda daah achaaaa
Nikageuka kutazama haraka eeh si naliona li D, yaani sijui limetokea wapi, Nikamsukuma haraka Veda nyuma, D alikuwa anatutazama kwa zamu yale macho ya nini kinaendelea hapa.??
"Tunatakiwa kuongea....?" Veda hata hakujishughulisha na D akanambia afu akaachana na mie akaenda kupanda Honda yake akaondoka mwendo wa kasii hadi nikamuonea huruma yule mtoto jamani maana ule mwendo ni hatari
Uuh kwanza nikameza mate sijui niite fumaniz au nini
"Una issue gani na Veda, mmeanza lini mazoeaaa??" Nikashusha pumzi kwanza sikujua hata nijibu ninii kwa muda kidogo nikatafakari maana nisije kunyimwa hata ka gari kangu ka mkopo ...
"Aa...siii yaani huyo Veda alikuwa anaumwa mama yake yaani walikuja kumleta mama yao..." nilikuwa naogea huku najikuna kichwa
"Yaani Vero aisee nikija kugundua kama yule ms*nge anakugonga aisee nakuapia nitakuuwa kweupeeee ....Unaishi wapi siku hizi"
"Kwa rafiki yangu!!"
"Yupiiii, Mwanaume ??"
"Sioo...yule Tinner "
"Yaani unaishi kwenye majumba ya watu kama huna kwako bwana haya hapa tunaondoka unarudi kwako acha ujinga" yaani anavyoongea kama mie ndio ninamakosa jamani sioni hata kama anajutia alicho kifanya ile siku na sio ajabu alishasahau kabisaa
"Kule kuna nguo zangu nitaenda kuchukua afu kesho nitarudi nyumbani"
"Tunaenda wote unachukua nguo tunarudi wote " nilimtazama jicho la limwanaume jinga hiliiii
Nikakubali twende wote huko kwa Tinner nikamtumia sms Tinner shoga nakuja na D mie linanikeraa akachekaa akanambia Penzi pajaaa naona mapenzi yamerudi nikasema wapiii namzonga zonga tu hapa nipate vitu vyangu sina hata shida nae nikipata hata gari yangu tu mie mbele, Tinner akacheka akasema yaani wewe na hiyo Gari jamani Duuuh hahah hicho ndo kitu changu cha thamani jamani eeeh embu niacheni mieee ...
Nikapanda kwenye Gari ya D ananiambia story kibaoo mara atanichukua twende wote china nikashangae et mmh mie nasonya tu kimoyo moyo yaani alivyonitoka huyu kakaaaa sina hata hamu nae ila ingekuuwa kipindi kile yupo moyoni mmh hizi taarifa za kwenda chini jamani hata sijui ningeruka vipi kushangilia ...
Tukafika mpaka kwa Tinner , Akamchangamkia hatari et akampa laki mbili kwa kile kipindi alichonipokea, Tinner akawa hataki kupokea analinga linga wee nilimkata bonge wa jichoo mbona alipokea unaleta ushem wa kijinga hapaa ...
Tinner alikuwa ameshaivisha maana nilimwambia nina njaa sanaa, tukala kwanza ndio nikasema naenda kupanga nguo zangu, na hapo sikuwa na nguo wala nini, nilitaka tu kuongea na Tinner peke yetu, Tukaliacha sebleni limejaaa puuh, Tukaenda chumbani
"Enhee naww imekuwaje umekuwa nae tena "
"We acha tu embu kwanza tuachane na huyu mwehu, Kuhusu Veda.."
"Waooh Hizo ndio tam tamuuu enhee" Tinner akajiweka vizuri kitandani huku anacheka
"We mwenzangu kumbe yule mama niliekuwa nahangaika nae weeeeh kumbe ni mama ake Veda, Hehehe hakiamungu sina hamu"
"Nambie Koma"
"Koma dadaa na adabu ikushikee"
"Mmmh heheh yaani hata sijui nikuulize swali gani mwenzangu Eeh kwahiyo ulikuwa una muhudumia ma mkwe hahaha"
"Hahah we mwehu kweli weweee...... Eeh yaani nilipo muona mwenyewe yaani nilihisi kuzimia ...." nikamuhadithia ilivyokuwa kule hospital Muda wote alikuwa anatabasam mpaka Kile kipengele Cha D kutukuna aah akasonya huyooo
"Hivi Vero, kwanini usimpe nafasi Veda jamani"
"Sa kwani alisema ananipenda lini Tinner, Alinibaka tu hatukua na maongezi yeyote kabla"
"Mmh mie naamini ana hisia na wewe yule kaka"
"Tinner sikufichi rafiki yangu, Nampenda Mnoo Veda nampenda mno kiasi kwamba hata natamani asinitongoze ataniumiza sanaa kampani yake ndo huyo D, Kwenda makasino usiku unafikiri kuna mwanaume hapo tena Veda alivyo mzuri vile kuna mwanamke anachomoa hapo mmmh hapana nitalia kila siku mie sitaki bwana" ilibidi tu niutoe ukweli mchungu moyoni, na niliongea kwa kumaanisha kabisa
"Mmh ila mie sidhani kama Veda anaweza kuwa kama D bwana sijuii ila Wanaume wengi wavuta bange na wanawake ni maji na mafuta ila kwa nyeto haooo eeeeh yaani Jamaa ule mwichi unaisha siku mojaaa hahahah "
yaani Tinner alifanya nicheke hadi nikasahau matatizo yangu haki tenaa hahaha mwehu huyuu
"We mwehuu kwelii"
"Ohoo ndo nakwambia Embu fanya hivi mpe nafasi mjaribu ukiona ana ujinga mwingi unaachana nae bwana "
"We Tinner unasema tu, Hivi unafikiri mapenzi yanajaribiwa hivyo we mwehu wewe, hujui tu yaani nikimuona Veda nahisi kabisa moyo unataka kutoka kwa kulipuka Yaani basi tu daah "
"Fanya maamuzi kati ya huyo D au Veda kazi kwako"
Wakati tunaongea kengele ya Getini ilitoa mlio yaani kunamtu nje, Tinner akainuka kwenda mie nikabaki natafakari maneno ya Tinner, Sasa nimpe nafasi Veda kwani yeye alishasema ananipenda??
Kabla sijapata jibu nini nifanye akaja Tinner "shoga kuna mtoto yupo hapo anasema anashida na wewe"
"Mtotoo???" Nilishtuka kidogo mie huku nani ananijua jamani
"Mtoto gani??" Nilikuwa nauliza huku nimekunja sura
"Najulia wapi mie?? Nimemwambia pita ndani anasema hapana wewe nenda "
"Mmh"
"Kwahiyo??"
"Hata sijui"
"Kamsikilize ni mitoto tu hata sikujui mie cha kike labda kuna mtu kakuelewa hapa ndo kumtuma shoga una bahati hahaha waleleee"
"We chizi embu niache miee" nikainuka kutoka Sebleni alikuwa amekaa D katunaa kama kwake nikampita akaniuliz bado tuuu?? Nikasema nachukua viatu vyangu hapo tunaenda .. akasema sawa mie nikatoka Kweli nikamkuta mtoto getini hata simjui nikasogea akaniamkia Shikamoo Aunt nikaitikia huku namsogelea zaidi najaribu kuvuta kumbu kumbu niliwahi labda kumuona sehemu lakini hapana ....
Itaendelea....
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni