, nilipokutana macho kwa macho na mjomba niliganda nikiwa nimetoa macho, kisha nilisimama juu na kumuita:
"Mjomba!
General nae alishtuka na kugeuka haraka kumuona mjomba wangu, mjomba alisogea adi tulipokuwa na kunishika mkono akanipeleka nje kwenye gari yake, bila kusema kitu chochote kisha akafungua mlango wa gari na kuingia na kisha akawasha gari tukaanza safari, kiukweli alikuwa na hasira sana njia nzima alikuwa kimya hakuongea kitu, nilihisi kuchanganyikiwa sana kwani sijawahi kumuuzi namna hii mjomba wangu, amekuwa akiniamini sikuzote niliwaza sana, na General tumeachana hata namba ya simu hajanipa hapajui kwetu wala sijajua kambi ipi anaenda kufikia, nilijikuta natokwa na machozi kwa mengi kisha nilimuambia mjomba:
"Mjomba nisamehe"
Lakini hakujibu kitu mjomba aliendelea kuendesha gari akiwa kimya, nilihisi leo sijui itakuwaje tulipita chalinze na kusonga mbele kuelekea dar, kumbe tulipo ondoka huku nyuma General aliingia nae kwenye gari, na kutufuata nyuma hadi tunaingia dar alikuwa nyuma yetu, tulienda hadi nyumbani kunduchi bichi General alikuwa nyuma nyuma akatushudia tunaingia kwenye geti la nyumbani hivyo alipaki hapo na kusubili kwa muda kisha alishuka na kuja mpaka getini akagonga mlinzi alifungua na kumuuliza:
"Nikusaidie nini?
"Samahani nilikuwa namuulizia hapa ninyumbani kwa kina Laura?
"Ndio wewe nani mkuu?
"Mimi ni soja mwenzie tumemaliza leo mafunzo, je amefika nyumbani tayari?
"Kaingia sio muda mkuu karibu ndani, au nikuitie?
"Ooh! Asante kama kaingia sio muda atakuwa na mjomba pamoja shangazi yake wanafurahia, sitaki kuwaharibia furaha yao, ngoja nikupe hii kadi yangu utampatia sawa, akikuuliza muambie Ethane"
"Ok sawa mkuu"
Kwakuwa alikuwa anamavazi ya kijeshi hivyo hata mlinzi alimuongopa na kumuita mkuu, alimuachia kadi na kisha akaondoka na kurudi kambini, sasa tulipoingia ndani mimi na mjomba tuliposhuka nikiwa na mavazi yangu yakijeshi shangazi mke wa mjomba wangu alikuwa akinisubili kwa hamu sana tulipofika alinipokea kwa furaha mno na kuniita:
"Karibu nyumbani soja wangu nilikuwa nimekumiss sana mwanangu"
"Mimi pia mama"
Napenda kumuita mama kwani amenilea tangu nikiwa mdogo, nikamkumbatia akanishika mkono na tukaingia ndani, nilikuta kaniandali vitu vingi hatari, ila mjomba alienda zake moja kwa moja chumbani, hata shangazi alielewa tuu kuwa hayupo sawa, shangazi akaniuliza:
"Kwani kulikoni mbona mjomba yupo hivyo kipenzi changu ameudhiwa na nani tena?
"Mama nimemuudhi mimi"
"Ehee! Nini tena, ndio mmekutana tuu leo muda mrefu mliokukuwa mbali kulikoni?
"Nisaidie mamab kumbembeleza, kanikuta nalishwa chakula na General ndio kakasirika hataki kuongea namimi kabisa"
"Mmh! Haya niambie General kwanini akulishe chakula wewe kunanini hapo?
"Mama nakuambia ukweli, kiukweli nimpenzi wa maisha yangu, ninampenda sana General Ethane"
"Mmh! Haya hayo mambo umeanza lini kipenzi jamani?
"Mama jamani nenda kwanza kambembeleze, kisha nitakuelezea kilakitu ngoja nikabadili haya mavazi kwanza"
"Sawa lakini umependeza sana kipenzi changu, umekuwa sasa yaani upo vizuri hatari"
"Asante mama"
Kisha shangazi aliondoka na kwenda chumbani kwao, kumkuta mjomba, namimi nilianza kuonja onja mapishi niliyoandaliwa na shangazi, kisha nikataka kuoondoka kuelekea chumbani kwangu, lakini ile naanza kuondoka tu mlinzi akaniita:
"Samahani mkuu Laura"
Nikageuka na kutabasam kwani leo hii mlinzi ananiita mkuu, kutokana na haya mavazi ya jeshi m, nika muitikia:
"Unasemaje uncle moris?
"Kwanza kabisa hongera kwa kuhitimu mafunzo mkuu, kingine ninahii kadi hapa kuna mkuu moja alikuja hapo getini na kunigongea, nae kavaa mavazi ya jeshi kasema mmetoka kuhitimu wote, hivyo hakutaka kuvuruga furaha yenu na wazazi wako, kaniachia hiyo kadi tuu nikupatie"
Nikaiponea hiyo kadi kusoma jina nilishtuka sana, nikakimbia hadi getini nikafungua mlango, nikatoka nje na kutizama kote lakini sikuona kitu chochote, nikarudi ndani lakini nilikuwa natabasam tuu, kiukweli nilifurahi sana kugundua kumbe General Ethane alikuwa anatufatilia hadi nyumbani kwetu, nilifurahi sana nikawa naingia ndani mlinzi tena akaniita:
"Mkuu Laura huyo jamaa kasema anaitwa Ethane"
Nilitabasam tuu na kuelekea ndani bila kumjibu chochote, nilienda hadi chumbani kwangu nilikuwa nafuraha sana kiukweli, nilivua nguo na kuingia bafuni kuoga, kisha nilipotoka nilivaa pensi yangu fupi na tisheti, kisha nilitoka kuelekea dining nilipoandaliwa misosi mitam tam na shangazi, shangazi alimuambia mjomba:
"Mumewangu binti tayari nimkubwa sasa, chamsingi tushukuru hata hajatuaibisha, amefanikiwa kuhitim vizuri mafunzo yake, apo anasubili apangiwe jeshi la yeye kujiunga tu, jivunie yeye wengine wanawaibisha wazazi mapema sana, kwakubeba mimba au kutoroka na wanaume eeh!, Shukuru mtoto ametuheshimu kuwa namoyo mzuri kwake mumewangu, haya inuka twende tukafurahi nae asijisikie vibaya"
Mjomba alielewa na kuinuka kutoka na kuja dining nilipokuwa mimi, alikuwa na furaha tuu tukala chakula pamoja, tukafungua mvinyo na kuanza kunywa, shangazi akaenda ndani na kuniletea box la simu, na kuniambia:
"Zawadi yangu hii kipenzi kwako"
Nikamkumbatia kwani alijuaje nahitaji simu kwa wakati huu, nilifurahi sana na laini akanipa nikaiweka kwenye simu, na kisha nikaweka vocha pia wakwanza kumpigia alikuwa General, simu iliita sana kisha ilikuja kupokelewa na mdada yaani sauti ya kike
Je nini kitatokea Laura baada ya kusikia sauti ya kike unatamani kujua endelea kuifuatilia............
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni