PILOT SITAKI INANIOGOPESHA SEHEMU YA 14
Tukaondoka Mimi na dada ingawa nilijiskia vibaya kwasababu mie ndo nilichangia Hali Ile ya Freeman, tukaenda nyumbani Yan sijiskii hata poa na dada nae akawa ananisema Yan ndo kabisa, nikaona ilinijiskia vizuri nipige simu nyumbani niongee na mama, nikapiga home nikaongea na mama vizur tukawa tunataniana pale akawa ananipa na umbea ya Mtaani kwetu pale tulipokuwa tunakaa mambo yanayojiri hapo kidogo mood yangu ikachange Kwa kiasi nikaacha kuwaza waza.
Kesho yake asubuhi na mapema tukapokea ugeni nyumbni walikuwa ni wazazi wake na Freeman n Kendrick, Tulishangaa mie Kwa haraka haraka nikajua tuu mie basi ndo nshakuja kubebwa nipelekwe polisi, kumbe Wala wao walikuwa wamekuja wanataka kuzungumza na Mimi nilishangaa ila nikakubali niwasikilize wanataka Nini na ni wakalimu kwel ao wazazi wao. Akaanza na yule mbaba akaniasalimia Tena vzuri akaanza kuniambia Binti utakuwa unanijua vizur tuu na kama hunijua unajua taarifa kunihusu, nikamjibu ndio naachaje kukujua wakati we ndo boss wangu mkuu hapo nilikuwa hata siwajui ni kaunafki tu iliwajihisi nawajuaπ.
Yule mbaba akajitambulisha Tena Mimi ndo mmiliki wa zile kampuni mbili ambazo moja anafanyia kazi dadaako na nyingine unapofanyia kazi wewe, nikamjibu sawa akasema sasa Binti nimekuja hapa Nina ombi moja kwako nikawa namsikilizia Kwa umakini mkubwa sana, yule mbaba akaniambia najua utaona kama nakukosea mwanangu ila ninashida kubwa sana Yan nikubwa sana na ninaona utanisaidia na nakuona una roho nzuri sana ya kunisaidia, wakati uo tunaongea dada yeye alikuwa jikoni hivo alikuwa hajui ni Nini kinaongeleka maaana aliombwa atupishe na wale wazee. Nikajibu sawa mnaweza kuongea yule mmama akasema Kwa ukarimu akaniambia tutakupa Nyumba mbili zilizopo njee ya nchi hii na pia Mimi binafsi nitakununulia zawadi ya magari mawili moja wapo ikiwa ni G wagon, na pia mme wangu atakufungulia kampuni ambayo itakuwa inaendeshwa na wewe na bidhaa zitatoka Kwa Jina lako ila tutakupa vyote hivo ili tu uolewe na kijana wetu Freeman.
π³π³Kwanza nilishangaa kuhusu izo Mali wanazotaka kunipa pili nikashangaa kuhusu ilo ombi lao kwaajili ya kijana wao, Ikanibidi niwaulize Kwa ustaarabu Sanaa kwanini wamenichagua Mimi na kwanini watoe ofa zote izo, yule mmama Akanijibu mie naelewa vizuri sana kuhusu kuolewa na mtu usiemtaka inavyokuwa kwenye moyo wa mwanamke na ndo maana nimekutolea izo ofa zote izo na pia kuhusu kukuomba wewe ni kwasababu maisha ya kijana wangu wakati huu yapo kwenye mikono yako Binti yangu kijana wangu sasahivi hapa anaumwa vibaya mno na hatakiwi kuwa nastress zitakazo zidisha ugonjwa alioupata kwasababu ya ajali, Leo ameonesha kukupenda Sanaa maana alivoamka tuu jina la kwanza kulitaja ni lakwako na katuambia akikukosa wewe maishani mwake Hana haja Tena ya kuishi kwasababu atakuwa Hana sababu ya kukaa hapa duani, kwaiyo mwanangu naomba utusaidie. Yule mama akawa Hadi analia sasa Mimi nashindwa kuelewa hapa nafanya Nini kwasababu nampenda Kendrick na uyu Freeman anataka kufariki.
Nikawaambia wale wazee sawa ntafikiria Kisha ntawaambia maana niliwaona kabisa watu wazima wanalia mbele yangu na hio sio sawa kabisa, yule mmama akanikumbatia kabisa na kunishukuru juu Kam vile nimeshamkubali kijana wao Kisha wakaondoka, sasa nikabaki Mimi na dadaangu kwanza nikamkumbatia dada huku nalia maana sielewi nifanyaje na nimchague Nan na kwanini Yani kichwa kilivurugika kabisa Yani, Dada akawa ananibembeleza na pia ananiomba msamaha maana yeye pia kachangia Kwa kumuaminisha Freeman Mimi nampenda nikawa sielewi hapo hapo kama dakika kumi zikapita mlango ukagongwa Tena dada alivoenda kuufungua alikuwa ni Kendrick kaja na maua, dada akamruhusu kupita ndani, Kendrick akanikuta nalia akaanza kunibembeleza nikajua labda kashaambiwa na wazazi wake, kumbe Wala hajui chochote kile yeye kaja na yake. Baadae nilivyonyamaza ndo akaanza kuniuliza kwani shida nini nikamwambia hamna kitu ila tu sijiskii vizuri.
Itaendelea....
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi