Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

11 - 20🚩🚩🚩🚩🚩🚩 𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞

2nd Aug, 2025 Views 48

:11

kwa kukwama kwama “Nde, Nde”
Kwa upole nikamalizia “Ndeana Boss.”
Akacheka akisema “Una jina la kipekee sana unajua, sijawahi kusikia.”

Sasa mimi namtazama anavyocheka, huyu mwanaume analo tabasamu. Meno yake yamepangika vizuri na anajua tumia tabasamu lake.

Haitoshi kuna kitu sijasema, unazijuia vizuri zile sauti za watangazaji wa vipindi vya mahaba, ndiyo sauto zao nzito fulani hivi ila laini ndiyo hivyo hivyo sauti ya huyu mwanaume ilivyo.

Ana sauti nzuri sana ni kama vile akiongea usimwambie aache kuzungumza. Muda wote awe anazungumza tu, asiache kabisa.

Wakati mimi nashangaa aliniuliza “umekuja na chochote?”
Haraka nikatoa bahasha yangu na kumpatia. Akawa anatazama akisema “Ndeana, Yes nimepatia jina lako sasa.”
Nikatabasamu na akaniambia tena “Ndeana una uzoefu sana. Umefanya kazi hotel
nyingi sana unajua. Na umesoma chuo kizuri tu. Ila kwa hadhi ya hii Hotel yetu, elimu yako ilikuwa bado bado, sasa Ndeana nitafanya nini kwenye hili.”
Moyo wangu ukalia Paaah!!!, akanitazama vile namna naanza tena kutaka kulia.

Wakati ananitazama machozi yakanitoka nikajikuta nasema huku nikiomba sana tena mikono yangu nimeikusanya kwa kuonesha unyenyekevu mkubwa sana “naomba nisaidie kama mdogo wako kaka. Nakuomba sasa usiniache kisa elimu. Mimi naweza kazi, najua kila kitu kuhusu hii kazi. Nisaidie mimi kwaajili ya familia yangu. Ninakuomba sana, nakuomba sana Bosss, naomba kazi hii.”

Huyu mwanaume Stewart, alinitazama kisha akatazama pembeni na baada ya hapo aliinuka kunifuata upande niliokuwa nimekaa na akakaa mbele yangu na aliniambia huku akiinua uso wangu “Ndeana, mwanamke akilia kikawaida moyo wa mwanaume lazima uumie na kama sivyo basi huyo mwanaume ni katili. Ndeana sipendi kuona mtu analia hii huwa inanisumbua. Na mrembo kama wewe unalia sasa nawezaje kuvumilia. Futa machozi nikuambie kitu Ndeana.”

Haraka nikaanza kufuta machozi, na kisha nikawa namtazama . Aliniambia kwa kunitazama usoni “kusema ukweli kutoka moyoni sina mashaka na utendaji wako kazi. Na urembo wako siwezi kupinga.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:12
Kumbuka kila mahali na utaratibu wake si unajua eenh, basi na sisi hapa tunazo taratibu zetu namna ya kuajiri watu na vigezo vyako. Wewe mwenyewe si unaona, kwa heshima ya dada yako Mar, ndiyo maana upo hapa.

Kwa maana sasa tunapitia wakati mgumu kiuchumi juu ya corona ingawa kwasasa ni nafuu ila kuna ncho bado wamefunga mipaka. Lakini mimi bado nilitaka ufike hapa.

Sasa Ndeana nisikilize, ondoa shaka na hofu. Bila shaka umeacha taarifa zako muhimu zote. Utapigiwa simu na utaitwa. kwanza wewe kukaa hivi na mimi ni ushindi tayari niamini.”

Kiukweli wa moyoni nilijikuta ninanyong’onyea. Sikuwa najua kuwa elimu yangu nayo ni tatizo pale. Nilijikuta hata tabasamu siwezi tabasamu tena.

Huyu Boss Stewart akaniuliza “Mrembo, ina maana huniamini tena?”
Nikashindwa kumjibu. Na yeye akaendelea “ndiyo kwanza tumekutana, ila mini nakuamini hata nataka kukupa kazi lakini wewe huniamini mimi, kwanini?”
Kwa upole nikamtazama na kumuuliza “Boss, kweli utanipa kazi mimi?”

Akanitazama na kutabasamu na akaniambia “kwasasa tulia, mimi nitakupa kazi. Tulia niweke mambo sawa kisha utakuja kuanza kazi ila ni lazima ukubali kuwa hutoniangusha.”
Nilijikuta natabasamu tu na kusema “sitakuangusha.”

Akatabasamu na wakati huo simu yake ikaita. Akanitazama na kuniambia “Ndeana, tumemaliza. Subiri simu toka kwetu.”

Nikatabasamu, sasa mimi siwezi kurudi nilipotoka maana hotel ni kubwa aiseee sijui nilipoingilia wala nilipotokea. Akanitazama nahisi alitambua hilo.

Akatabasamu na kisha akanishika mkono wangu. Pamoja tulitoka mpaka kwenye lift akanielekeza cha kufanya na aliniaga. Nilijisikia aibu sana, ila yeye alikuwa anatabasamu tu muda wote.

Mimi nilifuata maelekezo nikarudi mpaka chini kabisa na kutoka pale. Nilikuwa na nusu furaha nikiwaza elimu furaha inaingia nyongo nabaki na huzuni. Kupata usafiri Posta haikuwa kazi kwangu na safari hii niliona tu bora nipande zangu daladala kuliko kupoteza pesa tena na kazi yenyewe sina hakika.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:13

Basi safari ya kurudi nyumbani ilianza na hata nikafika nyumbani. Nilipofika nilikutana na baba na dada yangu wamekaa sebuleni ni wazi walikuwa wananisubiri. Baba aliponiona alitabasamu na kusema “mwanangu Ndeana umependeza sana. Imeendaje huko?, dada yako amenielezea kila kitu nina hamu ya kusikia.”

Niliwatazama kwa upole na kusema “eti nitapigiwa. Naogopa itakuwa wamenipotezea kwa maana anasema elimu yangu ndogo ila anasema nimuamini nitapigiwa.”

Baba alitabasamu na kuniuliza “na ndiyo maana ukalia?. Kaa hapa binti yangu nikuambie.”
Nilisogea na kuketi karibu na baba yangu na kisha alisema “amekuambia ukweli kutokana na hadhi ya sehemu yao ya kazj na hata wewe unajua hiyo Hotel ni kubwa sana mwanangu. Ukweli unauma ila unakomboa.

Badala ya kulia sasa unapaswa kuomba Mungu upate nafasi ili ukusanye pesa uje ujiendeleze tena kidogo ili hadhi yako iongezeke. Na unajua binti yangu, kampuni na taasisi nyingi kwasasa haziajiri watu.

Lakini wewe umeitwa na ahadi umepewa, wewe ni wa pekee. Hii ni nafasi yako, ukisikia Mungu hufanya mambo magumu kuwa rahisi ndiyo namna hii. Mungu hawezi jambo moja tu, nalo ni kushindwa. Mungu hawezi kushindwa, maadamu kwa kinywa chake amekuahidi basi tusubiri simu tu. Ushapata kazi.”

Nikacheka kidogo na kusema “unajua baba wewe ndiyo ulivyo hivyo. Kurahisisha mambo. Unapenda sana kurahisisha mambo baba yangu. Mimi naenda kupumzika nimechoka sana.”

Dada akanitazama na kusema “nakuja huko, bado sijasikia kitu.”
Nikacheka nikisema “dada Vee niache nimechoka sana.”
Nilielekea chumbani nafika tu na kisha dada naye akaingia chumbani. Akanitazama na kuniambia “haupo sawa mdogo wangu kwani kuna nini?”

Basi nikamsumulia maelezo ya Stewart alivyokuwa ananielekeza na kisha dada akatabasamu na kusema “sijui kwanini sizingatii ila naona kabisa ipo namna mdogo wangu. wewe kazi umepata.”

Mara simu yake ikaita. Alikuwa ni dada Martha. Nikamwambia “pokea, pokea eenh tumsikie.”
Dada yangu akaweka loudspeaker na Mar alianza kwa kucheka hata dada aliuliza “sio kwa cheko hilo, kuna nini ndugu yangu?”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:14

Dada Mar akasema “Vanessa mdogo wako kiboko, nimenyoosha maelezo. Tangu nimjue Boss wake sijawahi pata usumbufu kama huu. Kidogo tu anasema Martha ndugu yangu mtoto mzuri, kidogo anatuma ujumbe ana rangi nzuri, mara sijui nimeumia kuona analia hata ananiuliza maisha yake. Nakuambiaje kwa mwendo huu dogo kazi kapata.”

Dada Vanessa anauliza kwa furaha “wewe usinambie, ina maana huyo Boss ndiyo anafanya hivyo?”
Dada Mar akasema “sasa kumbe?”
Dada yangu akanitazama na kisha akasema “asije kuwa kamtamani mdogo wangu na kazi asimpe.”

Mar akaongea sauti ya upole akisema “Vanessa ndugu yangu, mdogo wako ni mdogo wangu. Siwezi mpeleka kwa mtu mbaya. Tangu nimefahamiana na huyu kaka ni mtu wa heshima sana.

Hana hayo mambo na kama ni upendo atakuwa kampenda kweli. Ila kiukweli mimi hajaniambia kuhusu mapenzi. Anamuhurumia tu na kuona ni binti mzuri. Lazima atamsaidia tu. Niamini.”

Dada yangu akasema “najua kipenzi changu, nimesema tu si unajua tena.”
Mar ni kama hakupenda, ile furaha ikawa imekata kabisa na akaaga akisema “haya basi kwaheri.”
Dada yangu akauliza “Rafiki, mbona kama nimekutoa kwa mood.”
Mar akasema “hakuna shida, kukiwa na lolote basi tutawasiliana.”
Akakata simu.

Dada yangu akasema “ni kama nimemuudhi eeh?”
Nikamtazama na kuvuta pumzi nikisema “tutafanyaje sasa dada?”
Dada akasema “nitaomba radhi mdogo wangu.”

Nilimtazama na kumwambia “najua hofu yako dada. Tazama mimi ni msichana mdogo. Nipo hapa mjini siku zote. Nimekutana na mambo mengi sana. Najua mazuri na mabaya naomba sana dada usiwe na wasiwasi. Nakuomba sana, mimi nitajilinda.”
Dada alitabasamu na kusema “Asante mdogo wangu.”

Nikatabasamu na alipiga simu palepale tena. Mar alipokea na dada alisema “rafiki yangu, ni kama nimekukwaza. Nilikuwa natania ndugu yangu naomba nisamehe sana.”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:15
Dada Mar alivuta pumzi na kusema “nimejitoa kusaidia kwa maana mdogo wako ni wangu pia sasa kwanini nimuuze. Mimi sinaga hayo mambo.”
Kweli alikasirika. Dada aliuliza “umenisamehe?”

Mar akcheka akisema “najua unamlinda mdogo wetu, ila bila shaka na yeye anajua mazuri na mabaya. Hawezi kupotea na pia anajua mwanaume mbaya na mzuri kwahiyo sisi kazi yetu kumuelekeza tu.”

Wakacheka mimi nasikiliza tu na kisha dada yangu akasema “sasa itakuaje maana nasikia elimu kigezo.”
Mar akasema “kwasasa siwezi kusema kitu, ila nimepanga kukutana naye kesho. Subirini simu yangu.”

Dada yangu akasema “asante sana ndugu yangu, sina hata neno.”
Dada Mar akacheka kidogo akisema “sisi ni familia, basi ndugu yangu msalimie sana mrembo wetu. Byee.”

Akakata simu, dada akanitazama na kusema “usijali mdogo wangu, utapata tu kazi. Siwezi ongea sana wewe ni mzoefu na hii kazi. Kwahiyo nakuombea upate tu.”

Nikasema “Amen dada, nipumzike sasa.”
Dada alisema “unataka ulale na njaa hii?, twende ukale kisha utarudi kulala.”
Nikamtazama na kusema “sawa dada.”

Nilifanya kama dada alivyotaka na baba yetu alituaga anaingia chumbani kwake kulala. Basi kila kitu kikawa sawa kabisa. Nilikula na nilipomaliza niliona ni heri nioge kwanza ndiyo nipande kitandani. Nilifanya hivyo na nilipomaliza nikapanda kitandani. Wakati nimeshajilaza chali, mikono yangu nimekusanya tumboni nawaza ni nini kinafuata. Ujumbe uliiingia kwa simu yangu, na ilikuwa namba ngeni, alikuwa tu ameandika “Ndeana, Ndeana.”

Kikawaida ukishakuwa mfanya biashara au muomba kazi. Namba yako unayotoa kwenye biashara au Cv unatakiwa kuwa makini sana. Ninakumbuka ninaye dada yangu wa chuoni kipindi anatafuta kazi. Siku moja alipigiwa simu kwa namba mpya. Anaonekana alikuwa na hasira sana ile siku.

Namna alijibishana na ile namba mpya na kukata simu ndiyo iliamua maisha yake. Kwa maana alikuja kugundua kuwa ilikuwa ni siku moja muhimu kutoka Hotel ya ndoto zake na alikuwa anaitwa kwaajili ya kazi baada ya kufanya interview. Hivyo alikosa kazi kizembe kabisa. Tangu hapo nilijifunza ustaarabu kwa namba mpya haswa katika hii namba yangu

16 - 20 🚩🚩🚩🚩🚩🚩
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:16

Hivyo nikajibu “abee, nani mwenzangu?”
Pale pale alinijibu “umefika salama mrembo?”
Nikajikuta natabasamu na kuandika “Boss!!!”

Akanijibu tena “hapana, ni Stewart, sio boss.”
Nikatabasamu na kusema “nimefika salama, asante sana.”
Akanitumia ujumbe “bado unalia totoo?”

Nikacheka ile totoo yake, na kujibu “hapana, hapana kabisa.”
Akaniambia “Nakutakia Usiku mwema Ndeana.”

Nikajibu “Na kwako pia Boss.”
Yeye akanijibu “Stewart.”
Nami nikarudia tena kujibu “na kwako pia Stewart.”

Nikawa natabasamu tu, yaani hataki story nyingi wakati ni kama bado natamani kuendelea kuchart naye. Nilikumbuka lakini, boss hazoeleki hivyo nilishukuru Mungu walau ninaye boss anajali kuhusu mimi.

Ninakumbuka ambavyo siku hii nililala nikikumbuka lile jengo, nikikumbuka aibu baada ya kusindikizwa na boss wangu mpaka kwa lift na kunielekeza namna ya kufanya ili niweze kutoka. Basi nikawa najicheka pale kitandani hata nikapitiwa na usingizi.

Zilipita siku mbili hivi kulikuwa kimya, hakuna simu kutoka kwa Boss wala simu kutoka kwa dada Mar ambaye ni rafiki wa dada yangu. Wamejuana wapi dada alisema ni kazi yake wakafahamiana. Basi ninakumbuka sana nilivyokuwa nikilalamika kwa dada kwamba tayari nimekosa kazi na mambo mengi kama haya.

Siku hii nilikuwa na dada chumbani, dada yangu aliniambia “mdogo wangu usijali, unajua mtu kusimamia hotel kubwa kama ile ni kazi ngumu sana.

Sijui kwanini ila mimi ninayo imani. Ninamuamini kama alivyokuahidi. Hata hivyo mdogo wangu tangu umerudi hujaniambia, huyo tajiri ni mzee, mubaba au yupoje .”

Nikajikuta nacheka nikisema “mimi nina mawazo halafu unaleta masihara dada. Kwanini lakini?”
Dada akacheka na kusema “niambie basi mdogo wangu.”
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:17

Nikamtazama na kusema “ni handsome, ananukia dada, ana sauti nzuri sana, ni sio mzee, sio mubaba sijui hata tuseme nini ila ni mwanaume wa makamo. Wewe kwako mkubwa kiasi.Mcheshi na utani mwingi sana. Jina lake ni Stewart.”

Dada akanitazama na kusema “Unavyo muelezea sasa. Haya mdogo wangu mimi sitasema sana. Ila si unajua hawa matajiri sio watu wakuwa nao karibu. Wana tabia ya kutumikisha watu kingono na kisha wanakuacha wanaajiri mwingine.”

Nikasema “ni la kusema hilo dada, bila hata kuniambia watu wanasema kila siku na mimi ni shahidi, hawa watu mambo yao sio mazuri ingawa ninaye rafiki aliolewa na boss wake ila mmh, siwamini mambo yao.”

Tukacheka na kisha nikasema “hata hivyo dada sina hisia naye mimi wala yeye haoneshi hilo. Ni mcheshi tu.”

Dada yangu akatabasamu na kusema “leo nitampigia simu Mar, tujue tutafute kwingine au tusubiri.”

Kabla sijajibu uliingia ujumbe kwa simu yangu. Na niliposoma alikuwa ni dada Mar. Kitu alichoniandikia kilinishtua kidogo. Aliniandikia “mrembo wangu, tunaweza kukutana leo?, ila please hii ni kati yangu mimi na wewe hakuna mtu anatakiwa kujua kuhusu hili. Ni muhimu mdogo wangu.”

Namna nilikuwa nasoma hata uso ulikuwa unaonesha kuwa nasoma kitu cha ajabu. Basi dada aliniuliza “kuna nini tena mdogo wangu.”

Nikamtazama na nafsi yangu ilikuwa inagoma kumficha dada yangu. Vipi nikienda na nikapata tatizo. Ni bora nimwambie tu. Hivyo nikamuonesha ujumbe. Dada akanitazama na kusema “usikute anataka udadali, kusema kweli mdogo wangu pesa sina kwasasa. Wewe nenda ukirudi utaniambia anasemaje.”

Nikamtazama dada na kusema kwa upole “sawa dada, kwahiyo sasa kama anataka udalali tutakuwa tushakosa kazi.”
Dada alisema akinigusagusa begani “jiandae uende mdogo wangu.”
Nikamwambia dada “niombee dada yangu.”
Dada alitabasamu na kusema “nakusubiri kwa hamu.”
Nikacheka na kusema “nitaanza kukupa habari nikiwa huko huko mbona si unajua sinaga subira kwako mimi.”
Tukacheka tu.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:18

Nilijiandaa na nikawasiliana na Mar. Tulikubaliana mahali nimfuate. Nakumbuka nilikutana naye na nakumbuka tulikaa ndani ya gari alinisalimia huku akiuliza “nyumbani wazima?”

Nikatabasamu nikisema “wazima sana dada.”
Akawa anacheka akisema “Vanessa anaendeleaje?”
Nikamwambia “pia mzima.”
Akanitazama na kuniuliza “hivi mdogo wangu unaye mpenzi?”
Nikashtuka.

Akanitazama akicheka na kusema “sikuulizi kwa maana mbaya Ndeana. Ila una uzuri wa ajabu sana unajua. Kuna mvuto unao aiseee sijui kama huyo mpenzi wako anajua kama anao mgodi kwenye maisha yake. Wewe ni kazuri eti.”

Nikacheka na kusema “dada Mar upoje lakini, mimi sio mzuri hivyo ni vile tu labda mvuto, ila nipo kawaida. Hata hivyo dada wewe pia mzuri sana, jitazame ulivyo.”

Akatabasamu na kuvuta pumzi na kusema “tuachane na hilo mdogo wangu. Ndeana nimekuita hapa nina jambo la muhimu sana. Nataka maisha yako yabadilike. Nataka uwe mwanamke mwenye mafanikio. Si unaona mimi dada yako nilivyo naendesha gari, napendeza na napata kila ninachotaka. Na ndiyo nataka kwako. Tumia vizuri huo uzuri wako.”

Mimi nikawa nashangaa tu, kisha nikamuuliza swali “kubadilisha maisha yangu kivipi dada?”

Dada Mar akanoa koromeo lake, kisha akanitazama akaniambia “wewe sio mtoto. Kinachoongelewa hapa ni baina yetu. Sikia, kuna kitu kimetokea. Stewart kakupenda sana. Anaogopa kukuambia ndiyo kitu nimekiona. Anatamani apate muda wa peke yenu, yaani ninyi wawili tu. Kisha akupe kazi.”

Nikashtuka na kumuuliza “ina maana anataka kulala na mimi kwanza?, dada sitaki kuamini kama ndiyo natakiwa kufanya hivyo.”

Dada Mar akaniambia “mimi nakuibia siri mdogo wangu. Yeye hajasema kila kitu ila kila muda anakuzungumzia. Mdogo wangu Ndeana wangapi wanatamani kufanya kazi Hotel kama ile.

Wewe jitoe kwaajili ya maisha yako. Unafikiri watu waliofanikiwa wamefanikiwa kirahisi. Jitoe mdogo wangu, akupe kazi. Watu kibao wanatamani nafasi kama hii hawapati tena ni wazuri kukushinda wewe.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:19

Wewe kutana naye hata mara moja uone kama hujapewa hiyo kazi. Mimi naona kabisa anakupenda sana, naona hilo namjua yule. Kwani Ndeana nikuulize kitu, wewe ni Bikra kwamba humjui mwanaume maisha yako yote?”

Nilimshangaa na kumuuliza “dada Mar, bikra na kazi wapi na wapi, mimi nataka kazi sitaki mahusiano.”
Dada akanitazama na kusema akitabasamu “mimi sikubembelezi mdogo wangu. Nilikuwa natamani upate maisha mazuri. Stewart ana uwezo wa kupata mwanamke yeyote yule anayemtaka. Unamuonaje kwani?, si wewe mwenye unaona ni mwanaume haswa. Sikia kipenzi. Ndoto ni gharama, watu wanafanikiwa wamepitia mengi sana. Sasa mimi sijui wewe ukimpa raha utapungukiwa nini. Kama hutaki naye mahusiano mpe penzi kisha pata kazi endelea na maish yako. Kama hutaki basi tena wenzako wanatafuta kazi.”

Nikamuuliza machozi yakitoka “ina maana hii ndiyo tabia yake dada?”
Dada akaniambia kwa upole na tabasamu “Stewart amekupenda sana. Kila muda anataja jina lako tu, kila muda ni wewe. Mdogo wangu Ndeana mpe nafasi. Mimi na wewe letu moja ninakusaidia ufanikiwe.

Anakupenda niamini mimi. Sikia najua ni ngumu, hata mimi sikutegemea hili. Kama humpendi sikulazimishi ila ninakupa muda leo ni ijumaa. Uhakika nilio nao ni kuwa muda utakaompa penzi ndiyo muda utaamua lini uanze kazi.

Kazi ushapata yaani ila anatamani muda na wewe wa faragha. Sasa kazi kwako. Hotel ndiyo ile hadhi kubwa mjini na wewe hutaki kisa penzi tu. Penzi kitu gani Ndeana, mpe tu si kitu cha mara moja. Kisha utajua anakupenda au hakupendi.”

Nilimtazama dada Mar na kusema “dada sikudhania kama unaweza kunifanyia hivi. Kusema ukweli umenikosea sana. Mimi Ndeana sijalelewa na kukuzwa hivyo. Abadani asilani siwezi kuvua utu wangu kwasababu ya kupata kitu fulani. Dada asante kwa msaada wako ila sipo tayari.”

Bila hofu wala wasiwasi dada Mar alinitazama na kusema “hata mimi sijazaliwa familia tajiri na bado napambania kufika mbali zaidi ya hapa. Nilipita sehemu kama hizo ninazokuambia na sasa nipo hapa.
𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞:20

Uzuri ni kuwa wewe unapendwa, mimi sikupendwa hata kidogo na mtu aliyenifikisha hapa alinitamani tu. Ndeana bahati haiji mara mbili, na kama ikija mara mbili basi wewe ni wa pekee. Ushauri wangu, usitumie moyo, tumia akili.

Unaweza kuondoka kwasasa, sitaki unitafute mimi ukiwa tayari. Naamini unataka kufanya kazi sehemu nzuri, kulipwa vizuri, na kufurahia maisha. Changamka, mjini kuchangamka.

Usione watu wanahangaika na maisha ukajua wapo wao tu. Kuna maboss na matajiri kama Stewart wapo nyuma yao. Unapendwa mama, nafasi ni yako. Byee, unaweza kwenda sasa.”

Wakati namtazama kwa hasira nisijue hata nimjibu nini. Simu yangu iliita na alikuwa ni boss. Nilimsave hivyohivyo tu Boss. Na Nilipoona simu yake kabla sijashuka hasira zilinibana.

Nikajikuta nalia nikisema “Boss ina maana huwezi kunipa kazi bila masharti si ndiyo. Kwanini unanifanyia hivi mimi. Ina maana hii ndiyo tabia yako?. Vipi kama dada yako, mdogo wako wa kike akafanyiwa unachotaka unifanyie?. Nashukuru sana mimi sipo tayari.”

Nilipotaka kukata tu simu nikasikia ile sauti ya kwenye redio tena vipindi vya mahaba, aliniambia “totoo, tuliza hasira. Sitaki ujisikie vibaya na wala sina maana mbaya kwako. The case is NAKUPENDA. Tangu siku nimekuona kwa picha tu nikakupenda.

Unaweza kuwa mpenzi wangu hata kabla hujaingia kazini. Ndeana wewe ni mwanamke ambaye mimi ninamtaka kufanya naye maisha.

Sina sababu ya kujielezea sana. Nimekupigia kwasababu nilikuwa nimekumiss sana ila uhalisia ni kuwa nina kazi sana leo. Fanya maamuzi sahihi, nakuomba sana, kesho tukutane tuzungumze na sitakulazimisha, nakuomba sana mtoto mzuri.”

Nikajikuta siwezi kumjibu navuta tu pumzi. Na kisha simu ilikata. Dada Mar alinitazama na kutabasamu akaniambia “ni yeye sio?”

Nikavuta pumzi yangu na kumtazama. Dada Mar akasema “Ndeana wewe ni nani boss kama yule anampigia mtu kama wewe. Haya mimi yangu macho. Naomba nikuache tutawasiliana kama nikisikia lolote. Kumbuka ni kati yetu.”

Nikashuka kwa gari nikiwa nimechoka sana. Nikiwa sijui cha kufanya. Boss wangu alitumia ujumbe “Usikasirike Ndeana, uwe na siku njema, I miss you totoo.”
🙌🙌eenh totoo ikawaje💃🏻
Muendelezo sh 1000
Njoo WhatsApp 0781858056.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

11 - 20🚩🚩🚩🚩🚩🚩 𝐉𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐁𝐎𝐒𝐒 𝐌𝐈 𝐍𝐀𝐎𝐍𝐀 𝐀𝐈𝐁𝐔 🍒🙈💞  >>> https://gonga94.com/semajambo/11-20-jamani-boss-mi-naona-aibu
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest