Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya β Gonga94 Semajambo
Gonga94 Β· Stories
13 Mar 2026
6 views
VYOTE NDANI GONGA94
BARUA ZA KAKA YANGU; Nikikupenda Mimi Inatosha!
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Nikikupenda mimi inatosha, acha kuwa na presha, acha kuhangaika na ndugu zangu, kama wakikupenda ni ziada tu lakini haibadilishi chochote! Nani alikudanganya kuwa wanapaswa kukupenda! Mimi mwenyewe sina uhakika kama wananipenda zaidi ya kupenda pesa zangu sembuse wewe ambaye ni mgeni hapa!
Shida nikuwa, nakupenda mimi ila hukai ukatulia, hunipi amani kwakua tu Mama yangu hakupendi! Kwakua tu Dada zangu hawakupendi! Hivi unategemea nini! Dada yangu wa kwanza ndoa hana, kila siku anaumizwa kwenye mahusiano, mtoto wa pili huyu kazalishwa na mwanaume hahudumii chochote mimi ndiyo namsaidia kila kitu!
Haya huyu Dada yangu kaolewa juzi tu lakini ashadundwa mara ngapi na mume wake anakuja sisi ndiyo tunaamua! Mimi si ndiyo namtumiaga mpaka pesa ya matumizi ananililia, sasa unataka akupende badala ya kukuonea wivu, unafikiri yeye hatamani hizi raha ninazo kupa apate mtu wa kumpa!
Halafu eti utegemee akupende kwa raha zote hizi unazonipa! Lakini sasa mke wangu, kwa hali unayoendelea nayo hata mimi nitakuchoka, nimekuchagua wewe, nishakuambia ndugu zangu hawakupendi, wana mambo yao, sijui makabila, sijui dini na vitu vingine!
Kuna mwanamke wao wanamtaka mimi nimuoe, hata simjui na wala simjali. Ni kweli huyo mwanamke alishanipigia simu, sijui Mama yangu kamchukua anaishi naye, sijui Dada yangu anampost sasa mimi yananihusu nini, wewe yanakuhusu nini? Mimi si niko na wewe, badala ya kunipa raha, nilogeke kabisa nisahau kama nina ndugu kila siku ni Kelele Mama yako hanipendi!
Mara wifi kapost tena yule mwanamke! Kwani mimi nawanunuolia Bado mpaka niwapangie cha kupost! Mimi lini uliniona nimempost huyo mwanamke, lini ulinifumania naye, muache abwabwaje wewe kula raha kwangu. Ila mambo ya kuninyima amani kisa hupendwi na ndugu zangu yashanichosha utanifanya nitafuta mwanamke mwingine wa kula raha, sikukuoa kwaajili ya ndugu zangu nimekuoa kwaajili yangu, mimi, wangu peke yangu!
Maoni
You're not logged in
X
Login
X
signup
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 19 - 20
SONGA NAYO......... miezi kama miwili ilipita huku nikiishi Tanzania pamoja na wifi yangu kipenzi BLESS π₯° yes amekuwa w...
Nikikupenda mimi inatosha, acha kuwa na presha, acha kuhangaika na ndugu zangu, kama wakikupenda ni ziada tu lakini haibadilishi chochote! Nani alikudanganya kuwa wanapaswa kukupenda! Mimi mwenyewe sina uhakika kama wananipenda zaidi ya kupenda pesa zangu sembuse wewe ambaye ni mgeni hapa!
Shida nikuwa, nakupenda mimi ila hukai ukatulia, hunipi amani kwakua tu Mama yangu hakupendi! Kwakua tu Dada zangu hawakupendi! Hivi unategemea nini! Dada yangu wa kwanza ndoa hana, kila siku anaumizwa kwenye mahusiano, mtoto wa pili huyu kazalishwa na mwanaume hahudumii chochote mimi ndiyo namsaidia kila kitu!
Haya huyu Dada yangu kaolewa juzi tu lakini ashadundwa mara ngapi na mume...
π Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/barua-za-kaka-yangu-nikikupenda-mimi-inatosha
Maoni