MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 10
SONGA NAYO.....
Muda ulienda majira ya saa nane nilitoka nje kwa lengo la kuanua nguo za mtoto, lakini nilipofika nilikuta nguo zote ambazo nilifua na kuanika zikiwa chini
Tena zilionekana kabisa kuna mtu ameziangusha makusudi na kuzikanyaga kanyaga zikiwa bado mbichi, nyie katika siku ambayo nilichukia basi ni hii siku walah
Maana mimi sipendi kuzarauliwa na pia mimi sio mnyonge, na kitu ambacho hamkijui ni kwamba mimi bwana sipendi ile kazi ya kufanya harafu narudishwa nyuma yani sipendi kabisa hii tabia.
Sasa kitendo cha kukuta nguo ambazo nilikuwa nimezifua zikiwa chini tena zikiwa zimechafuka kilinikera sana, nikawa naomba mungu huyo mtu ambaye amefanya hivi ajulikane mapema
Kweli bana huyo mtu akawa amekuja hapo na sio mwingine bali ni yule mdada niliemuona pale seblen, yule dada alisogea mpaka nilipokuwa huku akicheka sana
" inauma eee..??"
Aliniuliza huku akinisogelea lilikuwa kosa kubwa sana kwake kunisogelea maana nilimchota mtama wa maana ๐ msinishangae mimi hayo mambo nayaweza maana nimekulia kwenye familia ambayo ina madume watupu ๐๐๐พ
Yani kule nyumbani kwetu Tanzania ni mimi pekee ndio mtoto wa kike lakini hao saba wote madume, na kibaya zaidi hao madume ni wakatili sana
Kabla sijaja Omani nilikuwa naonewa hatari ๐๐๐พ japo nilikuwa mkubwa wao ila sikuwa naweza kupigana na mwanaume mimi, so kila nilipokuwa nawakosea basi nilichotwa mtama ๐
Ikafika wakati na mimi nikaanza kuwachota mtama wale ambao wananizarau lakini pia kunionea, sasa huyu ndugu yenu ni kama ameviamsha vitu ambavyo vilikuwa vimelaka kwa muda mrefu sana๐ ๐ ๐๐พ
Acha akome, yani sura nzuri ila roho sasa ๐ binti ana roho mbaya huyu sijawahi ona aisee..
Yule mdada baada ya kumchota mtama nikakimbia na kwenda kupotelea kwenye nyasi, ๐ sio kama nilikuwa naogopa hapana nilikuwa nampa funzo kuwa hata mimi hayo nayaweza vizuri tu mbona
"Mama weee, nakufa huku.."
Ni sauti za yule mdada ndio zilikuwa zinasikika baada ya kuangukia makalio na kibaya zaidi aliumbwa na sura nzuri ila kalio hola ๐ ๐ nacheka kama mazuri vile
Maana binti alikuwa hana kalio hata lile la bahati mbaya, sasa kitendo cha kuangukia makalio nahisi aliumia maana kulikuwa na mifupa tu ๐๐
Mungu nifundishe kunyamaza mimi, ๐คซ nisije kuonekana muongo bure na huku naongea vitu vya ukweli kabisa, basi bwana kelele za yule binti ziliwatoa watu ndani
Wakatoka mpaka nje na kumkuta mdada anagalagala hapo chini yani kama ameumia sana na hawezi kusimama ๐ฅบ, upande wangu nikabaki natazama mashetani ya Oman namna ambavyo yanakuwaga kumbe ndo yanakuwaga hivi ๐
"Umekuwaje...??"
Madam alimuuliza huku akimsaidia kunyanyuka pale chini
"Mfanyakazi wako, oooh my God nitatoa wapi tena kalio zangu mie ..."
๐๐๐ yule mdada alikuwa analalamika kama vile aliumbwa na makalio makubwa, haki ya mama nilicheka sio poa, kitendo kilichowafanya watu wageuke sehem nilipokuwa nimejificha
"Mira huko kwenye nyasi unatafuta nini..??"
Madam aliniuliza huku akisogea mpaka nilipokuwa na kunishika mkono huku akinivuta kunitoa kwenye nyasi mie nacheka tu, tumbo linauma kwa kicheko
"Da Mira tuambie basi na sisi kinachokufanya ucheke hivyo.."
Swatii aliniambia, basi ndio akazidi kunifanya nicheke, wakazidi kuangalia mimi,..
"Yani nimepigwa hata kunisaidia hamna kweli.."
Alizungumza yule dada
"Kwani umefanyaje mbona hatuelewi ??, harafu unagalagala kama mtoto bwana.."
Anfrey aliongea
"Si huyu mfanyakazi wenu amenipiga.."
"Mmh we Ellice acha uongo bana, toka lini Milra akaanza kupiga watu..??"
Alizungumza madam akinitetea ndio nikajua yule mdada anaitwa Ellice, basi yule dada akaendelea kusisitiza kuwa nimempiga lakini hakuna aliyemuamini hata kidogo
"Mhhh Mira hizi nguo mbona zimekuwa hivi..??"
Swatii aliniuliza baada ya kuona nguo za mtoto zikiwa chini, nikageuka na kumtazama yule mdada nikamuona akiwa na hofu sana lakini pia alinisisitiza nisiseme
Yani kwenye vitu ambavyo sipendi kwenye maisha yangu, basi ni kuongea uongo, sinaga tabia ya kudanganya watu wakubwa hata kama huyo mtu awe amenikosea kiasi gani siwezi kumdanganya
Sasa huyu binti wa Oman ni kama anataka kuniona mimi matako yake kabisa na hajui nimetokea mkoa gani yeye ananiforce tu
"Kusema ukweli hizi nguo nilikiwa nimezifua il...."
Ellice akadakia
"Muongo muongo me siwezi nikafanya hivyo..??"
Yani ndugu yenu alijichanganya huku, sikuwa na nia ya kuwaambia maana nilimuonea huruma, sasa kitendo cha kudakia maongezi akawa ameharibu kila kitu..
"Ellice ni wewe ndie umefanya hivi..??"
Madame alimuuliza Ellice na siku hiii bwana madame aliweka uso wa serious sana mpaka nikabaki namshangaa huyu mama amekunywa konyangi au vipi??
"Aaah shangazi sijamaanisha hivyo.."
Ndio nikajua kumbe hawa watu wana undugu baada ya Ellice kumuita madam shangazi yake..
"Ila ulimaanisha nini, unajua Ellice acha kuniona mimi kama kijana mwenzio sawa, kwanza hiki kitendo ulichokifanya nilikishuhudia kwa macho yangu kabisa
Ukitoa nguo kwenye kamba na kuzitupa chini kisha ukazikanyaga kanyaga, haya niambie ulikuwa na maana gani kufanya hivi...??"
"Hapana shangazi, me sijafanya.."
Alijitetea
"Hujafanya sio??, tangulia chumbani nakuja.."
"Lakin....."
"Nimesema tangulia chumbani..."
Wakati yote yanaendelea Mira mimi nilikuwa naangalia tu na nisielewe eti, yani kwanini madam alipomwambia Ellice atangulie chumbani Ellice aliogopa sana
Nilikuwa najiuliza tu na nisielewe kinachoendelea kwa muda huo
"Mira.."
Madam alinifata na kunishika mikono yangu, huyu mama ananipenda sana mimi ๐ฅฐ yani ananipenda sijui hata nielezeeje jamani maana dah ๐๐พ huyu mama ni mfano wa kuigwa
Eeeh mfano wa kuigwa kwa kujali watu, na sio kuigwa kwa kutelekeza watoto ogapa hii kitu.....
ITAENDELEA......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni