SASA NAKUPENDA Sehemu ya 28
Mwandishi; lissa wa huru media
Basi kesho yake jioni sana ndo baraka alianza kujiandaa mana alikuwa anaondoka na basi la usiku. Nilijisikia unyongea sana. Ila alinambia nivumilie mana ni miezi 3 tu na chuo anachagua dar ili niwe nae. Basi nikaona sawaa. Na mzee ndo aliondoka na baraka kumpeleka stand. Jamani nilijikaza ila nilikuwa sipo sawa. Mpaka mama akaniuliza wewe tangia lini umeanza kumsikitikia baraka. Yani kawa mshikaji wako lini. Mpaka leo anaondoka unajisikia vibaya hivyo. Eeeh. Nikasema mama nilishabadilika rohoo na baraka ni mtu ambaye hana shida kabisaa. Mama akaningalia akasema sawa bwana. Ila si atarudi mbona apo jeshi ata hawakaagi sana.nikasema.sawa.
Basi sasa maisha ya kuwa mbali ma baraka yakaanza. Yeye akiwa ndo kaenda uko jeshini kigoma. Ilikata weekk ila baraka alimpigia simu baba mala moja tu kumjulisha baba kuwa kafika salama . Ila hakumpigia mama kama alivyonambia kuwa atakuwa anampigia simu mama ili tuwasiliane ila no hakumpigia simu mama kabisaaa. Basi bwana majibu ya form four yakatoka. Shoga yenu nilipata division 4 ya mwisho kabisa. Baba alichoka yani ata chuo sipangiwi. Mzeee akanmbia ndo ulichokivuna hiki si ulishaanza mapenzi ukiwa shule aya mambo ndo aya . Chamuhimu ata least nilipata cheti. Mzee akasema nikae nyumbani .nikishapata cheti atanipeleka nikasomee urembo tu.nikasema sawa. Basi maisha yakawa yanaenda tu. Japo nilikuwa nammis sana baraka yani.sana..kuna mdaaa mpaka nakaa nmuwaza nalia.naenda kuchukua shati lake nalala nalo ndani yani nilimmis sana kiukweli
Siku iyo.sasa bi mkubwa akanituma sokoni. Nikaenda kuemea sasa wakati naludi.nikaona kuna a gari kama inanifata hivi.mana nilikuwa natembea pembezoni mwa bala bala. Ikawa inanipiga honi .ila nikadhalau nikajifanya kama.sisikii hee si nikasikia sauti ya adrian ananiita shakira .hey shakira .nikasimama kwanza kumsikiliza. Nikasema unasemaje wewe. Kwli bwaana alikuwa ni adrian kazid kupendeza na kwaka sana .bonge la handsome jamani. Nikasema nakusikiliza. Akasema naomba upande katika gari shakira tuongee. Nikasema kwaiyo ayo maongezi kakam sijaongiia kwenye gari hayaongeleki ama. Akasema plsss naomba unisikilize ili tuongeee. Nikasema asa ww una nini cha kunambia mshamba mkubwa ww. Akasema najua una hasira sana shakira ila nilifanya vile kwa sababu shakira. Na nilisafiri nilienda home bukoba. Nimeludi dar kama nna week.plssss shakira tuna mengi ya kuongea naomba tuongeee.nikamuangalia kisha nikakumbuka ile siku kanikana mbele ya wazazi. Nilimsonya bonge la sonyo kisha uyo nimasepa zangu home. Yani nna vyompenda baraka ndo ntaakaa kumsimiliza yeye.
๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ๐ผ
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni