MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 9
SONGA NAYO....
Kisha kwa ujasiri mkubwa nikazungumza.
"Madam kwanza nasema asante kwa kuniamini lakini pia kwa kunijali nikuambie kitu siwezi kuolewa na kijana wako ile hali mimi ni mfanyakazi wako, sina thamani ya kuolewa na huyu pia sina hadhi ya kuwa naye ukiangalia mimi ni masikini na nipo hapa kwa ajiri ya kazi.
So ndugu zangu hiyo habari ya kuolewa na mtoto wenu mfute kabisa kwenye akili zenu maana mimi ni binti wa kimaskini.."
Nilimaliza kuongea hapo kisha nikaondoka sikutaka kusubiri neno lolote kutoka kwao nkaelekea moja kwa moja mpaka chumbani kwangu ambapo nilimkuta binti yangu akiwa bado kalala
Kwa kuwa usiku ulikuwa mkubwa nami nikapanda kitandani nikalala lakini ndio hivyo sikulala usingizi maana kwanza nilianza kuperuzi mtandaoni si mnajua tena simu mpya.
Hakuna siku nililala kwa kuchelewa kama hii siku maana nililala saa kumi na moja kamili ndio nikalala ๐๐๐๐พ, kichwa kinaniuma yani macho ndio kabisa basi nikalala zangu.
Nimelala kidogo tu pakapambazuka kutokana na usingizi wa jana yake hivyo niliamka saa tano, hapo sijampa chakula mtoto na ukiangalia mtoto anatumia chakula maalumu so nikaamka kwa kukurupuka kama nimemwagiwa maji.
Nilisahau hata kupiga mswaki maana namjali sana mtoto hivyo nikatoka chumbani mpaka jikoni, seblen nilipishana na watu mbalimbali kutokana na kuharakisha sikuweza kuwazingatia.
Basi niliweza kuandaa uji kwanza ili Nasrat apate kupooza njaa kwanza ndio nifuate chakula cha kuongeza nguvu, baada ya kumaliza kuandaa uji wa mtoto nikashika njia mpaka chumbani
Lakini nilishangaa baada ya kufika chumbani kwangu na kutokumkuta mtoto, hivi mnajua kuweuka ndio kulinikuta mimi sasa maana nilichanganyikiwa balaa moja kwa moja nikashika njia mpaka alipokuwa madam.
"Mtoto yuko wapi..??"
Baada ya kufika kwa madam sikumsalimia zaidi ya kuanza kumuuliza habari za mtoto.
"Mira upo sawa kweli..?"
Madam aliniuliza.
"Bwanae mambo ya kuwa sawa hayakuhusu, nauliza mtoto yuko wapi..??"
Niliuliza nikiwa nimepaniki..
"We binti unaongea kuhusu nini, harafu kumbuka huyu ni boss wako hutakiwi kumpandishia sauti.."
Kuna mdada mmoja aliniambia.
"We binti kaa kimya sawa, mambo ya familia hayakuhusu.."
"Msicheeew, kwahiyo na wewe unajiona ni mwanafamilia.?"
Nikaona wananiletea mambo meusi, nikaanza kuzunguka karibia nyumba nzima huku namuita lakini sikumuona nilichanganyikiwa taratibu machozi yalianza kunitoka nilijua tayari wameshamtoa kafara mtoto..
"Aaaaaaaaaah.."
Nilipiga sauti moja ya ukunga kisha nikapoteza fahamu, nilikuja kuzinduka nikiwa chumbani kwangu lakini pia pembeni yangu alikuwepo nasrat, nilifikiri nipo ndotoni
Nilinyanyuka na kukaa huku nikimuchukua mtoto na kumkumbatia na muda huo mlango wa chumbani ukafunguliwa akaingia Anfrey.
"Umeamka..??"
Aliniuliza, sikumjibu mimi akili yangu ilikuwa inamuwaza Nasrat tu.
"Samahani kwa kilichotokea, maana mimi ndie nilikuja kumchukua bila ridhaa yako.."
Anfrey aliniambia.
"Hakuna shida.."
Nilimwambia, basi akatoka nikabaki mimi na kipenzi changu, nilimuogesha na kumpa uji, na muda wote huo sikuweza kutoka sebleni.
Majira ya saa sita nilitoka sebleni huku nikiwa nimebeba beseni lenye nguo za mtoto kwa lengo la kwenda nje kufua, nilipofika seblen ndio nikaanglia vizru bwana bwana ๐
Kulikuwa na mdada mzuri yani mzuri huyo mashallah ๐ฅฐ nyie nilibaki namtazama huyu dada bila kummaliza bwana maana alikuwa ๐ฅ
"Unaniangalia nini, si uende huko ukafue.."
Eeeh sasa me kosa langu ni kumtazama tu au kuna lingine?? Ikabidi niondoke na kuendelea na kazi zangu, nilifua haraka haraka ili kumuwahi binti yangu huko nilikokuwa nimemuacha
Baada ya kumaliza kufua nikaanika nguo vizuri kisha nikaingia ndani, ambapo nilipitiliza mpaka chumbani kwangu na kumkuta Nasrat amelala.
Kwanza najivunia kwa kuwa na binti mpole lakini pia mzuri ๐ฅฐ eeeh binti yangu mpole na mtulivu, sio mtoto wa kulia lakini ni mstaarabu sana
Naweza kumuacha na mtu yoyote na kumkuta akiwa sawa tu labda awe anaumwa au hajala ndio huwa analia lia sana, basi nilisogea na kuanza kucheza nako pale
Nasra alikuwa ameshaanza kutambaa so me nikawa namfunza kwenye kutambaa vile vile huyu dogo anakuwa haraka haraka sijui anataka kuniletea wajukuu me sijui ๐๐๐๐พ.....
ITAENDELEA......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni