MIRANDA (Binti Yangu) 12 to 13
SEHEMU YA 12
SONGA NAYO.......
Basi safari ilikuwa ndefu kidogo, kwa mara ya kwanza toka nifike Oman hii siku ndio niliigia supermarket bwana, hiviii kumbe waarabu wana pesa hivi na hata kuniambia tu hapana jamani
Maana huko tulipoenda sijui nipaite supermarket au kasri ?? Yani shoga enu nilikuwa nashangaa huku nikiwa na binti yangu nimebeba kwa mbele na ile mibebeo rasmi ya watoto achana na hivi vikoi sijui vitenge huku hawatumii hivi vitu na hawajui kwanza wanabebewaje 😆
Yani nchi yangu raha sana maana mtoto anaweza kubebewa hata mtandio na asianguke but huku uarabuni aisee mambo ni uzungu uzungu sana.
Nikiwa na kabinti kangu huku Anfrey akiongoza njia, tulianza kuchagua sasa niseme tu ukweli kwenye kuchagua kitu me huwa siogopi kabisa
Nilichagua kila kitu ambacho nilikipenda, unakuta kitu kingine nimekipenda na nikakichukua ila sijui matumizi yake 😆 basi mahemezi yalikuwa mengi sana tulinunua vitu kama hatutakuja kununua tena
Tulipomaliza kuchagua kila mtu alikuwa hoi kasoro binti yangu ambaye hakujua kitu chochote kilichokuwa kinaendelea..
"Dah nimechoka sana..."
Andrey alizungumza
( 🙄sasa kama umechoka kwahiyo unataka nikubebe au ??)
Nilijiwazia kisha nikamwambia
"Pole hata kwa upande wangu ni vilevile nasikia pumzi inakata.."
"Hebu tuondoke nahitaji kupumzika kabisa.."
Alizungumza huku akinisaidia kubeba pochi yangu, basi mimi nae sikuwa mbishi nikamfuata nyuma nyuma mpaka kwenye gari, kama kawaida wote tunakaa mbele
So baada ya kupanda gari nilikaa mbele huku binti yangu nimempakata kwa mbele, basi akawasha gari na safari ya kurudi home ikaanza
Tuliwa njiani tukaanza kupiga story za hapa na pale na kujikuta nikimzoea sana
"Hivi Mira, wewe ni kabila gani...??"
Anfrey aliniuliza kwa wakati huo me nilikuwa nikiangalia vitu ambavyo tumenunua 😁
"Ah me msukuma bana, sijui ushawahi kusikia hili kabila??"
"Yaaah nasikiaga tu kuwa wasukuma wanapatikana sana mwanza.."
"Kabisa yani hujakosea.."
"Ndio maana unajua kupigana 😁"
"Kwamba uliniona napigana na nani..??"
"Usijifanye hujui, jana ulimpiga nani na kama sio Ellice??"
"Sema nini huyo nduguyo anazarau sana na ndio maana nikamzoa, ila kusema ukweli wasukuma ni watu wapole mno we jaribu kwenda Tanzania siku moja uone ambavyo utapokelewa yani watahakikisha unakula mpaka na ambavyo hutumiii..."
Basi safari ikawa tamu kidogo kuliko wakati tunakuja, kwa uwezo wa mungu tulifika salama kabisa, nikaashuka kwenye gari na moja kwa moja nikaelekea ndani kwenda kumlaza Nasrat maana alikuwa amelala
Nilipofika chumbani nikamlaza vizuri na kumfunika shuka kisha nikatoka moja kwa moja mpaka nje kwa lengo la kwenda kushusha mizigo.
Tulisomba mizigo mpaka ikaisha, kwa upande wangu nilikuwa Hoi bin Trabant ikanibidi kwanza nipike chakula cha mtoto kisha nikapumzike kidogo
Basi Mira mie nikaingia jikoni, chakula cha Nasrat sijawahi ruhusu kipikwe na mtu yoyote yule zaidi yangu. Basi nikawaanza kupika pale
Nilipika chakula kikapikika, kwa mbali kabisa nikasikia sauti ya mtoto akilia, kitendo cha kusikia ile sauti nikashtuka kisha nikazima jiko kwanza na kuanza kutembea ili kuelekea chumbani
Mara Ellice huyu hapa.
"Unaenda wapi..??"
Aliniuliza sikumjibu nikaendlea na safari yangu,maana sauti ya Nasrat ilinifanya nihisi kuna kitu kibaya kimempata, nikiwa mwenye wasiwasi sana niliekea mpaka chumbani
Lakini niliweza kusikia kilio ambacho kilikuwa cha maumivu kadri ambavyo nilikaribia kuufikia mlango, mapigo yangu ya moyo yaliianza kwenda kasi, niliogopa pale nilipokumbuka maneno ya madam
Nikavaa roho ya ujasiri na kuusogelea mlango kisha nikafungua, sikuona chochote ila mtoto alikuwa analia sana nikasogea kitandani na kumbeba lakini alindelea kulia
Nikajua lbda amekojoa na pampas ndio inamuwasha so ikabidi nimvulishe, 😳 my God hivi mnajua niliona nini ???........
ITAENDELEA........
SEHEMU YA 13
SONGA NAYO......
Katika hii dunia sijawahi kushihudia ukatili na roho ngumu lakini Leo ndio niliweza kuamini na kushuhudia kabisa, binti yangu akilikuwa amechomwa na pini kwenye kitovu 🥹 harafu sasa hiyo pini inaunganishwa na pampazi 😭
Lilikuwa ni tukio lenye kuumiza moyo kwa upande wangu, nililia mno yani nilitamani hata hayo maumivu ambayo anapitia mtoto basi ndio ningekuwa napitia mimi lakini sio huyu Malaika
Hivi kuna watu ambao wanaweza kufanya hivi kweli, ?? 🥹🥹 mtoto mdogo tena Malaika anafanyiwa kitendo cha kikatili hivi aisee nililia huku nikijaribu kuitoa ile pini lakini wapi
Kamasi zilikuwa zikinichuruzika tu machozi nayo ndio kabisa yani nasumbuka mtoto nae ndio anazidi kuongeza kilio, nilikuwa nalia kama mtoto sauti yangu ndio iliwashtua wanafamilia
So baada ya dakika chache wakawa wamefika, baada ya kufka pale na kukuta hali ya mtoto wakamchukua mara moja na kumpeleka hospital
Na vyote ambavyo alifanya hivi alikuwa Anfrey pamoja na swatii hao wengine hawakujousisha kabisa, kwenye gari tulikuwa watatu, nikiwemo mimi, swatii lakini pia na Anfrey ambaye ndie alikuwa anaongoza usukani
Njia nzima nilikuwa nalia nyiee, yani ungeniona ungejua kabisa Nasrat ni mtoto wangu wa kumzaa. Hatimae tulifika hospital na bila kuchelewa mtoto akaanza kufanyiwa matibabu mara moja
Maana hatukupewa usumbufu kwa sababu ilikuwa hospital ya private na gharama zote alilipia Anfrey, mungu azidi kumbariki huyu kaka..
Muda wote nilikuwa nikizunguka nje ya chumba ambacho Nasrat ndimo alimokuwa, nilikuwa nalia kama sina akili nzuri yani kifupi nilichanganyikiwa, hivi angekuwa mtoto wangu wa kumzaa ningekuwa kwenye hali gani eti jamani ???
Si ningekuwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kabisa , niliendelea na mizunguko yangu ambayo kama ungekuwa unahesabu basi hata mia moja ilikuwa inafika
"Mira kila kitu kitakuwa sawa, twende ukapumzike.."
( 😏nikapumzike harafu binti yangu nimuache kwenye hali gani..??)
"Siwezi nasema siwezi.."
Niliendelea kulalamika huku michozi ikinitoka bomba la majii, basi ikabidi waniache tu mpakka nitakapochoka mwenyewe kusimama
Basi muda ulienda na masaa yalisogea, nilijikuta nikiishiwa nguvu kabisa na kundodondoka chini, aliyeniona alikuwa ni swatii maana ndie niliyekuwa nae hapo maana anfrey alitoka nje mara moja
Basi nikabebwa juu juu kuingizwa wodini ambako nikaanza kutibiwa chapu chapu, madaktar walijitahidi kwa uwezo wao kushusha presha ambayo ilikuwa juu sana 😢
Naweza nikasema kwamba nimshukuru sana mungu maana madaktari jasho lilikuwa likiwatoka balaa kwa sababu yangu na wengi wa madaktari walijua kuwa Nasrat ni mtoto wangu so pande zote mbili wakawa wanajitahidi sana kuokoa maisha yetu
Namshukuru mungu nilirudi kwenye hali yangu ya kawaida lakini nilisisitiza sana kutaka kumuona mtoto, bila hinaya wakanipeleka kwenye wodi ambayo ndimo alimokuwa amelazwa Nasrat
Baada ya kufika mle wodini nilimkuta binti yangu akiwa hajitambui kabisa huku puani wamemuwekea mpira wa oksijeni 🥹 hii ilikuwa inaumwa sana
Niliumia sana kuona mtoto anateseka namna vile kwa sababu ya makosa ya mama yake kumkataa hiii iliniuma ndugu yenu na kusababisha tena nirudishwa ICU 🥹
Hii wanelewa wale ambao wanapitia hali kama yangu, hii kitu inauma usikie kwa mwenzio ila omba yasikukute ndugu yangu
Basi bwana, nikowa nimelala sijitambui kabisa nilijiona niko kwenye dunia ambayo haikuwa dunia ambayo tunaishi wanadamu
Dunia ile ilikuwa ni sawa na paradiso 😁 eeeh mimi sio mtenda dhambi lazima nifike huko so hata upende wa hospital niseme tu nilikuwa nimekufa
Maana nafsi iliachana na mwili so nilikuwa dunia nyingine kabisa.Nilikuwa nikitembea huku na huko kama vile nilikuwa nikotafuta kitu..
Kwa mbali nilisikia vilio vya ndugu zangu akiwemo mama yangu mzazi lakini pia na baba huku walkiliita jina langu.
Nikashtuka ndio nikajikuta kuwa nimerudi duniani, yani nilikuwa nakufa kabisa na kumuacha binti yangu, nilinyanyuka pembeni yangu alikuwepo nesi ambaye alikuwa akiandika andika kitu kwenye daftar
Kitendo cha kuzinduka kilimfanya atabasamu kidogo kisha akazungumza
"Unajisikiaje...??"
"Salama.."
😁 yani nilikuwa siko sawa badala ya kumjibu najisikia haueni namjibu salama, basi nesi akaniangalia kwenye macho kama vile kuna kitu anatafuta, nikawa naona ananipotezea muda wangu bure maana nilikuwa na hamu ya kumuona Nasrat.
Wakati yule nesi akiniangalia kama niko sawa mlango ulifunguliwa akaingia mama yangu, nyiee nilijikuta nikinyanyuka bila hata kuambiwa
Sikuweza kuamini eti Leo mama yangu anaweza kuja Oman, nikiwa bado natafakari mama amefikaje fikaje Oman mara baba naye huyu hapa .
"Baba mama, inamaana mmeweza kuja mpaka huku..??"
Niliwauliza, wakatazamana kisha baba akazungumza
"Nafikiri upumzike kwanza, hayo mengine utayajua tu muda bado.."
"Kwanini muda bado eheee, kwanza Nasrat yupo wap..??"
Niliwauliza nikiamini huenda nipo Oman kumbe haikuwa hivyo nilikuwa tanzania.
"Nasrat ndio nani..??"
Mama na baba wakaniuliza kwa pamoja
"Acheni basi masihara kwani hamjamuona mtoto mdogo ana miezi kama saba hivi mzuri mzuri yuko wapi kwani na anendeleaje..??"
Niliwauliza lakini ni kama hawakuwa wakielewa kabisa nilichokuwa nazungumza, wakabaki wasinielewe tu basi wakiwa kwenye sintofahamu mlango ulifunguliwa akaingia Anfrey......
ITAENDELEA........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni