MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 7
SONGA NAYO.....
Hatimae ule mda wa kuwasili huyo mkaka wa kuitwa Anfrey ulifika walimpokea kwa furaha sana wazazi kama wazazi walimzawadia kijana wao gari ya milioni 80
Mimi nilikuwa kwa mbali natazama tu namna walivyokuwa wanampenda huyu kijana, kuna muda nilikuwa nawaza hivi vitu wangekuwa wanamfanyia na rast born wao pia
Lakini kwenye akili zao wamemfanya Swatii kuwa rast born, eeh mungu nifundishe kunyamaza.
"Hatimae umepakumbuka nyumbani maana ulikuwa umetukimbia..."
Madam aliongea.
"Hahaha hata amna mama, ni vile tuu nilipenda kuwa mbali ili mnimiss sana..."
"Na kweli umetuweza maana tulikumiss sio poa, eeh karibu tena nyumbani kaka.."
Naina alizungumza, basi walisogea mpaka nilipokuwa nimekaa maana wakati wao wanajishughulisha na kumpokea mimi nilikuwa nimewaachia wana familia wampokee kipenzi chao.
"Mira.."
Madam aliniita, sikuitika zaidi nikanyanyua uso na kumtazama.
"She is my son, it's everything in my life.."
Madam aliongea aisee huyu mama sijui amepanga kumuumiza nani maana kama anafanya vyote hivi kwa Nasra hawezi kumuelewa kama anafanya kwa ajiri ya mimi kuumia basi nampa pole
Maana mimi nina moyo wa jiwe ๐ kuumia nitaumia kidogo kisha nasahau na maisha yanaendelea ndivyo nilivyo mimi sasa kama ananifanyia hivi mimi ni sawa na kuumiza figo zake.
"Saw.."
Nilijibu kwa kifupi, sikutaka mambo yawe mengi, akamgeukia tena kijana wake..
"Anfrey huyu ni mtoto wangu yani namaanisha Mira nimemfanya kama binti yangu nampenda kama ninavyowapenda nyie.."
Alizungumza madam lile likaka likanitazama sasa, niwaambie tuu hili likaka lizuri yani limekuwa lizuri kuliko hata nilivyoliona jana kwenye laptop.
"Hi Mira...."
Alinisalimia.
"Hi too.."
Nilijibu kwa haiba ya kike si mnajua tena mtu ambaye hujamzoea lazima umuonee viaibu aibu lakini pia lazima umuogope ๐๐๐
"Wooow nakuona upo na Queen hapo, ila mtoto wako mzuri mashallah..."
Alisema Anfrey na kunifanya kwanza nitabasamu, kama mlezi hili la kusifiwa kuwa mtoto wangu mzuri na huku sijamzaa mimi lilinifurahisaha sana basi nikacheka pale muda wote madam alikuwa kanuna kama amekula hamira ๐๐
"Hakika ni mzuri sana, naweza kusema pia amefanana sana na mama..."
Swatii aliongea, mama yake aalimkata jicho binti akabaki anacheka cheka tuu bila mpangilio mimi nilikuwa nawachora tuu
"Really, hebu naomba nikusaidie kidogo maana toka nafika hapa nakuona hujapumzika..."
Alisema Anfrey huku akisogea nilipo ili kumchukua mtoto, Nilimuangalia madam nilimuona kabisa akiwa hajapendezwa na tukio lile basi ikabidi nikatae kwa kusema.
"Kaka unajua ndio umefika hivi, so ni bora upumzike kwanza mtoto utambeba tuu mbona bado yupo sana hapa.."
"Ni kweli.."
Madam akadakia, kweli bwana Anfrey hakuwa mbishi alielekea chumbani kwake chumba ambacho kiliandaliwa kwa ajiri yake, huku sebleni tulibaki mimi na madam maana hawa wengine walitoka wakisema wanaenda salon
"Sitaki Anfrey ajue kuwa nina mtoto mwingine, naomba hii ibaki kuwa siri yako hata hawa vijakazi wapya sitaki wajue hii siri ni ya watu watatu tuu ambao ni mimi na baba yako lakini pia na Naina.."
"Nafikiri ungeenda kuendelea na kazi zako maana hakuna chochote cha maana unachoongea.."
Nilimwambia.
"Sawa, lakini nimefikiria nikaona itapendeza zaidi kama utakubali kuwa mchumba wa Anfrey.."
"Leo naona umekunywa pombe sio bure.."
Nilimjibu, kimya kilipita kwa muda akamuua kuvunja ukimya
"Hii issue iko serious sana, napenda wewe uwe mkwe wangu kwa kijana wangu, nitaongea nae nazani atakubali.."
"Huo mda ulitakiwa kuwa na binti yako, na sio kuongea vitu vya kipuuzi ambavyo havina kichwa wala miguu.."
Ila mimi yani boss wangu namjibu hivi, ngoja nitimuliwe kazi ndio nitakoma, hata kama nimejua napendwa bwana lakini sio hivyo.........
ITAENDELEA........
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni