CEO USINIVUE MI MCHUMBA WA MTU* * Chapter 18
Tulifanya kama tulivyoagizwa na mpenzi wangu, ila sasa kuna kitu kilibadilika jaman, yaaani haikuwa tena wiki moja alikaaa kule zaidi ya miezi miwilii tena bila mawasiliano hili lilitupa mawazo sana kwakweli, lilinifanya nikaamini yale maneno ya dada kwamba alitumia pesa zake ili tu kunipata uzuri tulikuwaga hatujawaeleza wazazi wetu chochote kuhusi hili ila ilikuwa inaniuma sana hil nikifikiriaaa nilikuwa nishaanza kumpenda na kumuwaza nikimuona yeye ni wa maana, ila niliendelea kwenda kazini na pale tulipohamia sikuwahi kuwaza kuhama kwasababu kam alitumia pesaa zake ili anitumie basi yale ni malipo yangu, na kuhusu gari sasa hivi nilikuwa nishaweza kuendesha tayari, sikuwa tena na haja ya dereva hizo gharama za kumlipa dereva bora nikale kuku wa KFC
Upande wa kina Zakia, James alijua kwamba Zakia alikuwa akimsaliti na akaaamua kumbwaga na kumuacha kivyake atajua mwenyew, na yeye pia alikuwa msaada mkubwa sana kwake yule mwanamke mpuuzi, na Zakia alikuwa akinifuatilia sana na ile kuona mafanikio yangu akataka kujilinganisha na mimi, kwahyo akawa anamfosi Hussein mpaka Hussein akawa anaiba pesa kwenye kampuni yao kwa ajili ya kumridhisha zakia hadi Hussein akajulikana kweneye kampuni yao wakamfukuza kazi ikabidi wategeemee duka, nalo liliwashinda wakaamua kuliuza tu ili wa afford mambo mengine yani mambo yakawa tafrani kwao maisha yaliwawia magumu sana, kila walichojaribu kilishindikana hadi Zakia ikabidi awe anatumia mwili wake. kutafuta pesa hii ilimuumiza sana Hussein kwasababu hakutaka mwanamke wake changing na mwanaume mwingine, ila ilikuwa haina jinsi, yaani kwa sababu ya ile tabia ya zakia walijikuta wote wamepata maradhi ya ukimwi walidhoofika ila Hussein alikuwa ananitafuta sana maana alijuta hata kuniacha mimi nilikuwa hata sijui akaja akaniomba msaada ila niseme tu ukweli msaada nao sikuwa nao kwasababu wenyewe waliyonifanyia. inatosha na hayo ni malipo yaao, wajijulee wenyewe mimi mwenyew nina shida zangu kibaoo zimejaa wasinisumbuee miee
Ila upande wa dada angu aliendelea na saloon na tayari alikuwa ashapata umaarufu mkubwa. na saloon yake ilikuwa na wafanyakazi kwa sasa, na kingine alipata mchumba wa kumuoaaa ,aliolewa na ndoa yake ilikuwa pambe na sasa hivi yupo kwake ila hii ilinifanya ninyong'onyee nilijihisi sina bahati maan hata niliemuamini tena kanipotezeaa yaani kanibwaga, dada alikuwa ananipamoyo tu na upande wa kazini James aliendelea kunipa moyo alikuwa ananiambia Ellias ananipends labda tu yatakuwa yametokea matatizo ndio maana hivii vimetokeaa nilijaribu kuwaelewaa sana
Hii siku nimekaaa zangu officine napigiwa simu kwamba kuna ugeni wako nyumbani, nikauliza ni nani wazazi wangu wakaniambia amekuja na familia yake na amejitambulisha anaitwa Salim nilishangaa sana Salim mbona mimi simjui, nilisema nikimaliza kazi ntakuja
Nikamaliza kazi jioni nikarudi zangu nyumbani na gari langu, nafika ndani naambiwa wameleta barua na mahari kabisa, nilishangaa yaani mtu simjuii alete barua na posa pamoja hapana nilisema warudishe tu hivyo vitu mimi sipo tayari, mama alisema sasa binti utakaaa hivi mwenyewe mpak lini sasa mwanangu lazima utafute mwenza dada nae alikuwa amekuja alinishawishi sana na mtu pekee niliekuwa namsikiliza kwa sasa kuliko wote ni dada na niliona sasa kam mtu kaja katoa vyote kwa pamoja maan yake ananifahamu na ananipenda sna nilikubali, na ndoaa ilipangwa baada ya wiki moja
Nilikaaa wiki nzima sijamuona bwana harusi wala yeye hakuwa hajaniona yani tukaonana nilikuwa natawa japo hyo hyo wiki moja nilikuwa tayar tu kuolewa ili niamini kwamba na mimi nina nyota kwenye mahusiano, tena niolewe hata na nisie mjua yaani nilikuwa nimefika mbali kimawazo
Wiki moja, ikapita na siku ya harusi sasa ndio hadi nishamaliza kusema nimekubali mara tatu ndio nakuja kumuoan bwana harusi ule muda wa kuja kunifata chumbani namuona ni Ellias, haya hata nikikataa ndio nishakubali kuolewa tayari yeye alikuwa na tabasamu ila mimi sikuonesh tabasamu usoni ila moyoni nilifurahia hili kwakweli maaana niliolewa na ninaempenda ila nilikuwa nina hasira naee jamni sio poa....
Itaendeleaaa.....
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni