Aaaaaah Boss Enzo Chapter 10
Asubuhi na mapema, nilidamka na kuingia mtaani ili niweze kupata chochote kitu Maana nilikuwa Nina njaa sana kwa wakati huo.
Najua wengi mtaniuliza nilipeleka wapi Pesa ambazo nililipwa kwa kina enzo miezi ile miwili Sijui mitatu ambayo nilifanya kazi kwao, iko hivi ni kweli Pesa nilikuwa nayo lakini ilibaki kwenye lile BEGI ambalo alibaki nalo enzo.
Sijawai kuomba omba mtaani lakini kwa siku hiyo niliomba, sijawai kumnyenyekea mtu lakini siku hiyo nilinyenyekea.
Lakini subili kwanza Sijui kwakuwa ni siku ya kwanz jamani maana siku ilikuwa ngumu sana, Muonekano wangu mzuri pia uliwafanya watu kushindwa kunielewa na kuniamini Kuwa Mimi ni homeless lakini pia ni mtu Mwenye uhitaji wa hali ya juu.
hatimaye Giza totoro likashika nafasi nikiwa sijapata Pesa Wala chochote kile cha kutia kinywani mwangu, kwa mwendo wa polepole na kujivuta sana nikarudi kwenye jumba ambalo nilijjifadhi usiku uliopita na nikalala Tena kwa Mara pili.
Baada ya week MBILI kupita, nilijikuta nikiwa ni Mtoto wa mtaani kabisa, kutembea pekua pasi na kuvaa viatu ikawa ni kawaida kabisa, nilichoka na kuchakaa uku nilishindwa ata kubadilisha mavazi yangu mwilini.
Ndani ya week MBILI HIZO, nilijikuta nikipata marafiki wa mtaani na walinisaidia sana kwa namna moja ama nyingine, sikuwa nikilala na njaa Tena Kama hapo hawali na maisha ya mtaani niliyazoea kwa kiasi chake ingawa ni maisha ambayo hayazoeleki.
Siku ziliendelea kwenye uku na uku na hatimaye miezi miwili ikapita uku nikiwa ni mtu wa mtaani tu, nilikonda sana, nilipauka zaidi na zaidi, Kiukweli nilikata tamaa ya maisha, moyo wangu na akili yangu ya kufikilia vilfika mwisho na kuna muda nilitamani ata kujiua nikiamini Kuwa nitaenda kupumzika mbinguni.
Maisha ya mtaani Sawa ni magumu lakini hakuna kipindi kigumu zaidi Kama Kipindi ambacho nakuwa kwenye siku zangu za hedhi (period), iki kipindi kwangu kilikuwa ni kigumu. sana, sikuweza kupata taulo za kike kwaajili ya kujistili, lakini pia maji ya kuoga kwa wakati na hali hii ilipelekea Mimi kunuka sana na ata wenzangu kunitenga
Ikiwa ni Majila ya MCHANA, nimejilaza kwenye moja ya kivuli cha pembezoni Mwa Barabara, akaja mmoja wa marafiki zangu ambaye pia ni Mdada Kama Mimi, akaniamsha na kuniambia.
"Wewe mama Amina kashusha mikungu ya ndizi leo, Twende tukamenye ndizi tupate Ukoko wa usiku"
Nikakurupuka chapu chapu na safari ya kwenda kwa mama amina ikaanza.
Kiukweli naweza nikasema Kuwa huyo mama amina ni msaada mkubwa sana kwetu sisi watu wa mitaani, ooooh sorry kumbe sijamtambulisha mama amina, mama amina bwna ni mama Ntilie mkubwa sana hapa manzese na ni mwanamke Mwema sana Walahi namshukuru sana mama amina.
Ikiwa ni siku ya jumapili, Kama kawaida Ishani Mimi nikaingia mtaani kwajili ya kujitafutia Riziki ili mkono upate kwenda kinywani.
Siku hiyo Bwana matafutizi yangu, Yaani kutafuta kwangu ilikuwa ni dalaja la kijazi la ubungo, siku hiyo nilikuwa na dumu langu la maji, lakini pia na squeeze kwajili ya kusafisha vioo vya magari ya watu, Yaani magari yakisimama tu kwenye Mataa nawai chapu na kwenda kusafisha ili niweze kupata japo miambili Mia Tatu.
Ikiwa ni kwenye mataa, nilisogelea gari moja nzuri sana Tena ya kishu, nikasafisha kioo na nilipomaliza tu nikasogelea upande wa dereva kwajili ya kuchukua Pesa yangu, lahaulaaaaaah nikajikuta nikakutana uso kwa uso na Enzo.
ITAENDELEA.
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni