MY CRAZY BOSS 09
SONGA NAYO
Niliingia ndani , sikuwa na usingizi kabisa , ni ajabu sana kwani nilijikuta nikiwaza sana kuhusu Boss Erick muda wote. Kwenye maisha yangu yote nimewahi kukosewa na wanaume lakini hakuna hata mmoja aliyewahi kuinesha juhudi ya kuimba msamaha kama Boss Erick.
Nilijikuta nikikumbuka jinsi alivyonihandle na kunikumbatia ule usiku kwa mahaba, ๐ฅฐ๐ฅฐnikawa najikuta nacheka cheka mwenyewe hata sijui cheko linatokea wapi jamani๐คฃ๐คฃmuda wote khaa๐๐
Siku iliisha nikiwa mwingi wa furaha na hatimae asubuhi iliwadia , siku hio niliamka mwepesi nikaanza kujiandaa huku nikihakikisha sirudii kachumbari yangu kabisa. Nilivaa zangu kagauni keupe na raba nyeusi na kamkoba kangu.
Ikiwa ni majira ya saa kumi na moja na nusu asubuhi niliwasili nyumbani kwa boss Mikocheni B. Sikuwa mgeni hivyo nilizama moja kwa moja hadi ndani, nilisubiri kwa nusu saa na sikuona dalili ya utokaji wake hivyo niliamua kumguata.
"Hodi boss, hodi boss". Niligonga lakini hakukuwa na majibu hivyo nilikata shauri na kuingia ndani.
Gafla nikamuona Erick akitoka bafuni akiwa amevalia taulo kiunoni kwa chini huku akiwa na majimaji kifuani๐ฅฐ๐ฅฐ,moyo ulidunda puuh puuuh puuuuh !!!!!!!, miguu ilitaka niondoke japo macho yalitaka nibaki niendelee kumtazama .
Nilikata shauri la kutoka nnje hivyo nikaanza kurudi nyuma taratibu kwa uoga huku macho yote yakiwa kwa boss๐ฅฐsio siri ana body hatari๐.
Nikiwa narudi nyuma nikajikuta nimeteleza bahati haikuwa upande wangu kabisa,nilianguka kama mzigo puuuh!!!!!!!!!,muda huo boss alikuwa akijifuta maji ,alishtushwa na mlio wa kuanguka kwangu.Moja kwa moja alinifuata hadi nilipokuwa na kuninyanyua.kwa namna moyo ulivyokuwa ukipiga kwa kasi kama unataka kuchomoza kwenyw kifua,huku boss akiwa ananiangalia machoni wakati ananinyanyua najikuta naishiwa pawa๐,haikuwa kawaida nilianza kuhisi vitu vinashuka miguuni mwangu vengine vinasambaa mwilini mwangu.
"Upo sawa,Joy?.Boss aliuliza.
Nipo sawa boss.Nilijibu kisha nikatoka nnje huku nikiwaza kilichojiri.Baada ya dakika kadhaa boss Erick alitoka nnje akiwa amejiandaa safi kabisa na kwa pamoja tuliongozana hadi kazini.
Tuliingia hadi ofisini kwake kisha nikamuandalia kahawa pamoja na ratiba yake ya siku nzima
"Hodi boss".
"Karibu".
Boss nimekuja kukuuliza utatumia chakula gani kwa lunch?
Ntakula wewe.Alijibu.
What boss?
Sitakula mchana kuwa free,halafu jitahidi kubadili nguo ili uendane na hadhi yangu.
Kwanini unanambia hivyo boss?niliuliza.
Kuna blauzi nyeupe huwa unavaa kila alhamisi na jumatatu nyingine ya bluu huwa unavaa kila jumanne na alhamisi na kila ijumaa huvaa gauni,hivyo jitahidi .Boss aliweka nukta
Mie nilitoka nnje kwa aibu jamani๐ni kweli sina nguo kabisa ila sio kwa kunidhalilisha hivi jamani.
"Mbona mnyonge kimeumana nini?".Si mwengine bali leila mwanadada alieonesha kunichukia toka siku ya kwanza kabisa nilipoanza kazi.
"Unawashwa wewe?,kazi yako huitaki sio?".Nilimuuliza kwa kifupi.
Mmmh basi unajifanya una jeuri ama kweli masikini akipata........kabla hajamaliza boss akatokea...alimuangalia sana leila.mdada mwenye weusi wa Kenya,shape ya kihindi pamoja na miguu ya kiethiopia.
"Twende lunch joy,boss alizungumza".Nilibaki nikiduwaa kwani haikuwa kwenye mpango kabisa,ila ilinilazimu kumfuata.
"Hivi Joyce kwanini unawaachia watu wakunyanyapae kama nzi kwenye biriani?".Boss aliniuliza.
"Sikila mtu wa kumjibu ,wengine ni busara kuwanyamazia na kuendelea na mambo yako".
"Sahihi najivunia secretary kama wewe,boss alijibu".
Safari yetu ilitia nanga nnje ya restaurant kubwa iitwayo VYNN Cafe iliyopo Kisiwa Kawe.
"Shuka tuingie humo,usishangazwe na menu za chakula wala usitetemeke ni vyakula vya kawaida japo bei ni ghali hilo ni moja,mbili usitumie mkono kula tumia uma na kijiko na ukitumia mkono basi punguza ukubwa wa matonge yako".
Ila boss ๐๐๐๐,niliitikia kiunyonge tu,sawa boss nimekuelewa kisha tukashuka hao hadi kwenye hio Cafe,si haba ni nzuri na vyakula ni vizuri pia
Mie niliagiza chipsi na kuku ,boss yeye akaagiza sijui salad sijui manini hata sikumuelewa,Tulikaa tukinywa juisi huku tukiangalia angalia mazingira maana hakukuwa na story kabisa .
Baada ya muda mfupi vyakula vililetwa,jamani jamani๐๐๐,hio kula yangu sasa sijui ndo ushamba wa matumizi ya umma na kisu ama vipi nilijikuta siinjoy chakula nakula kama konokono,nikimuangalia boss yeye anakalibia kumaliza weeeh๐๐๐๐๐๐nikajikaza kula hivyohivyoo akili ilinijia nilipoona amenyanyuka na kwenda kulipa.bill
Buana we kwani ananiona ,nikafakamia ile chipsi yai kama sina akili nzuri,kuku sasa nilitafuna hadi mifupa mbwa mimi๐๐๐๐acheni tu ushambaa huu,kuku inameremeta hatari inaonesha imepikiwa mafuta safi ukiachana na zile nyeusi za uswazi(kuku petrol).
"Tuondoke nadhani umefakamia vya kutosha niliponyanyuka,siku nyingine tutaoda sio kuja hapa huwezi kunidhalilisha".Boss alizungumza
Tuliongozana na kupanda kwenye gari ,baada ya muda tulifika mchikichini ambapo boss alinishusha kisha akaondoka.
Mie sasa๐๐naingia ndani huku najinusa nusa mikono nyie naona raha kula msosi adimu๐๐๐๐hatarii na nusu.
Buana mie ndo nshakula hapo ratiba sikuwa nayo tena,nikajilaza zangu pwaa
Titlitili tilitili๐๐๐nikiwa nimelala nilishtushwa na mlio wa simu ,"Hee boss anashisa gani saa tano hii?" Nilijiuliza kabla sijapokea.
"Haloo nipo nnje naomba uje mara moja".
"Sawa nakuja,niliitikia."
Nilijikongoja hadi sehemu aliposimama boss,haikuwa mbali sana na chumba changu,nilimkuta akiwa amesimama kichwani mwake kukiwa na kofia nyeupe kwa kifupi rangi nyeupe ilitawala mwilini mwake.
"Nakuskiliza boss kuna shida yeyote?".Niliuliza.
Hapana.Nimekuletea nguo baadhi natumaini sitakufaa,boss aliongea hayo kisha akanikabidhi nguo zile .
"Shukran boss,japo hakukuwa na haja kabisa ya kuninulia ningenunua mwenyewr kwa mshahara wangu".Nilijibu.
"Ukifanikiwa kutoka huku chooni na kuhamia panapoeleweka ntaamini kweli mshahara unasaidia๐๐".Boss alijibu hivyo.
"Chooni ??ina maana kwangu ni chooni?Hata hivyo watoto wa kishua ndo mlivyo".Boss hakujibu kitu aliniangalia kisha akapanda gari na kuondoka.
Itaendelea
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni