(BARSISA....!) Inasimuliwa kuwa Barsisa alikuwa mtawa miongoni mwa Wana wa Israeli.
Alijijengea kibanda cha ibada mlimani, mbali na watu,
akaamua kutoa maisha yake yote kwa ibada ya Mwenyezi Mungu peke yake...!
Alijinyima starehe zote za dunia,
akaishi maisha ya kujitenga na watu, maisha ya ibada tu.
Chakula chake kilikuwa cha kawaida sana,
hakuoa wala hakuwahi kumgusa mwanamke yeyote katika maisha yake.
Barsisa akawa maarufu sana miongoni mwa Wana wa Israeli
kwa uchamungu wake, ucha-Mungu na kujiepusha na dunia,
jambo hilo liliwafanya watu wamuamini sana.
Miongoni mwao walikuwa vijana watatu
waliolazimika kusafiri kwa ajili ya biashara,
wakaamua kumuacha dada yao chini ya uangalizi wake....
Hawakupata na wala hawakuona mtu muaminifu na salama zaidi kuliko Barsisa,
hivyo wakamuacha dada yao, nao wakaondoka safarini.
Mwanzoni, Barsisa alikuwa mwaminifu kwa dhati.
Msichana aliishi katika chumba chake,
naye Barsisa akaishi katika chumba chake bila kumuona.
Lakini mambo yalianza kubadilika
Barsisa kadri muda ulivyokuwa unaenda alijikuta anaingia kwenye matamanio.
mwanzo Barsisa alikuwa hata msichana akigonga mlango kwajili ya kumletea chakula Barsisa alikuwa hamtazami msichana huyo...!
Ila Hatua kwa hatua,
Shetani akaanza kumpamba msichana machoni mwake.
Tena kwa Yule mtu ambaye alikuwa akiabudu kwa miongo mingi,
bila hata kumgusa mwanamke.
Hatimaye Barsisa siku moja matamanio yalimzidi akajikuta anafanya mapenzi na yule msichana, wakaingia katika uzinzi,
Barsisa katika kuburudika na msichana huyo, msichana akapata ujauzito.
Hapo hofu ikamjaa Barsisa....
hofu ya ndugu zake msichana
na hofu ya watu wa kijiji iwapo wangejua yaliyotokea.
Hapo ndipo Shetani akarudi kwa mara ya pili
kukamilisha hila yake.
Akamshawishi Barsisa
kwamba hakuna njia ya kuokoka aibu na balaa aliloangukia ni mtihani mzito kwake,
Jambo la kufanya ili kuficha aibu ni kumuua msichana.
Barsisa bila kufikiria kwa kina akamuua msichana
na akamzika jangwani.
Ndugu zake bint waliporudi kutoka safarini
wakaulizia kuhusu dada yao,
Barsisa akawaambia kuwa amefariki
na tayari amemzika.
Kwa sababu ya heshima na uaminifu aliokuwa nao Barsisa,
ndugu wakaamini maneno yake
wakaondoka.
Lakini Shetani hakuridhika na hilo.
Akataka kumfikisha Barsisa katika dhambi kubwa zaidi.
Akawatokea ndugu watatu katika ndoto,
akiwaambia kuwa dada yao aliuawa
na amezikwa jangwani,
wakaonyeshwa hata mahali alipozikwa.
Wale ndugu watatu walipoamka mapema sana asubuhi wakajadiliana kuhusu hiyo ndoto, mmoja wao akasema hiyo ndoto ni ya kweli Barsisa itakuwa alimzini mdogo wetu na kahofia aibu, wakasema “tulifatilie hili kuanzia sasa”
Wakaenda pale kaburini walipooteshwa,
wakalifukuwa kaburi,
wakatoa mwili wa dada yao ingawa mwili ulikuwa umeharibika ila kwa mtazamo wao waliamini dada yao ameuliwa.
Hapo wakatambua
kuwa Barsisa ndiye aliyefanya hayo kweli.
Hasira kali ikawajaa,
wakaelekea haraka kwenye kibanda cha Barsisa,
wakiwa wameazimia kumuua kulipiza kisasi.
Ndani ya kibanda barsisa,
akiwa amezidiwa na hofu alijikuta yupo katika wakati mgumu sana kiasi ambacho alianza kuongea maneno ya kufru kwa sauti.
Tazama jinsi Shetani alivyomvuta hatua kwa hatua:
▪️ Alimpamba uzinzi, akazini
▪️ Kisha akampamba mauaji, akaua
▪️ Kisha akamtaka akufuru, naye akakufuru
Hata hivyo,
Shetani hakutimiza ahadi yake.
Alijitenga naye,
akamwacha afe akiwa kafiri kwa Mwenyezi Mungu.
Hivyo ndivyo ulivyokuwa mpango wa Shetani kwa mtawa
aliyejiweka mikononi mwake,
akamfuata hadi kufikia ukafiri.
Naam inaisha namna hiyo hiki ni moja ya kisa maarufu sana na ukweli ni kuwa wapo viongozi wa dini wengi au watu wachamungu wengi hukufa wakiwa waovu, wengine wakiwa wanazini au maovu makubwa yeyote na wote huwa tunaskia mara sheikh kafa akiwa gest na mwanamke wakizini Nk....... ! Anyway JAMBO KUBWA ZAIDI NI KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU MWISHO MWEMA unaweza ukawa mchamungu sasa na ukafa katika hali ya uovu na yule unayemuona muovu sasa akafa haliyakuwa ni mwema.
🤝Follow me Maher bey
✍️Maher bey
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni