MIRANDA (Binti Yangu) SEHEMU YA 6
SONGA NAYO.....
nilipokaribia kumfikia nilimsikia akizungumaza
"Sawa baba basi wacha sie tufanye maandalizi kidogo..."
Niliweza kumsikia madam akiongea hivyo, kwakuwa mimi huyu mama namuona boya sikutaka kumjali nilimpita nikaelekea chumbani lakini nikiwa katika kutembea nilisikia madam akiniita.
Nilirudi ili kumsikiliza alichokuwa ananiitia, huyu mama ananipenda sio poa baada ya mimi kufika pale alinikumbatia na alionekana kuwa na furaha sana.
Alinikumbatia kwa wakati kisha akajitoa kwenye kumbato na kunishika viganja vya mikono yangu huku akitabasamu na kunifanya niogope.
"Vip...??"
Niliuliza baada ya kuona natazamwa kama sanamu, hakunijibu zaidi akaibusu mikono yangu, mimi nilikuwa nashangaa na nisielewe chochote.
Ikabidi nijitoe mikono yangu maana hata sikuwa naelewa chochote, akanishika tena mikono kisha akazungumza.
"Mira leo nina furaha sana, kijana wangu yupo uwanja wa ndege anakuja huku..."
Aisee hivi mnajua nilijisikiaje, yaani pamoja na kunisumbua kote kule sijui kufanya hivi na hivi kumbe kijana wake anakuja me nikajua labda amemkubali Nasra kumbe anaongelea habari ya kijana wake aisee nilichukia.
Nikaivuta mikono kwa nguvu, sikumjibu neno lolote zaidi nikaondoka, akaanza kunikimbilia huku ananiita
"Mira mama, hebu simama tuzungumze basi..."
Sikutaka kusikia chochote kutoka kwake maana anaongea vitu vya kipuuzi yani anawaza ujinga ujinga badala ya kujali mtoto aisee ananikera mimi.
Aliendelea kuniita ila mimi sikusimama lakini nilipofika mbele kidogo nilisimama hii ni baada ya kumuona Swatii anatokea chumbani kwake ikabidi nisimame na madam nae akawa amefika pale nilipokuwa Swatii baada ya kutuona aliamua kutufuata..
"Morning mom...!!"
Swatii alimsalimu mama yake, mama mtu macho yote yalikuwa kwangu mwanamke alikuwa ananitazama huku anataka kulia kabisa huyu mama ananipenda hata upendo unaonekana kwenye macho yake.
"Morning..."
Alijibu kifupi tu, basi Swatii anaona Kawaida, madam akanishika mkono wangu huku anaongea.
"Mira, nakuomba uende airport ukampokee Anfrey..."
Madam aliniambia, Swatii kusikia Anfrey anakuja alifurahi sana akaanza kurukaruka huku akinisihi twende.
"Madam siwezi kwenda maana Nasra bado anaumwa.."
"Aah Mira, mtoto utamuachia Shida..."
Nilimuangalia huyu mwanamke yani sikuwa namuelwa kabisa kwenye akili yake kuna akili au matope, hivi naweza kwenda airport kwenda kupokea jitu zima lina akili zake timamu arafu nimuache mtoto anaumwa tena nimuache kwa mdada mpya wa kazi ambae amekuja jana tuu
Sikuwa na neno la kuongea zaidi nikabaki kimya, Swatii nae akaunga hoja ya mama yake basi mtu mbili zikabaki zikinisihi niende airport.
"Nimesema nina mgonjwa hivi hamuelewi nini sasa.."
"Kumbe unamgonjwa..??"
Swatii aliniuliza, alionekana hajui lolote kuhusu afya ya mtoto
"Ndio anaumwa sana, inabidi uende hata wewe na Naina.."
"Usijali kipenzi wewe baki umuangalie mwanao mimi nitaenda kumpokea kaka.."
Swatii alizungumza, madam hakuwa na neno la kuongea zaidi alikubali kishingo upande na sikutaka hata kubakia hapo niliondoka nikimuacha akiniangalia sikugeuka hata kumtazama.
Basi kama kawaida yangu nilikuwa namcare sana Nasra yani binti yangu alikuwa mzuri mpaka nikawa naona wivu sasa maana sio kwa uzuri huo arafu jitu lenye akili zake timamu linakataa mtoto kwa sababu za kijinga
Kama alikuwa na nia ya kujiunga freemason si angejitoa mwenyewe na sio mtoto ambae hana aita, kuna upande nilikuwa nikishindwa kabisa kuamini eti hii familia wamejiunga freemason na huku nawaona wanahudhuria sana ibada
Lakini inawezekana ikawa kweli maana siku hizi watu wanaishi kwa kuigiza ni watu wema machoni kwa watu lakini huku ndani ya nyumba balaa tupu kama lililo ndani ya nyumba hii
Nilitamani kujua kuwa yale maneno aliyoniambia madam ni ya kweli, niliamua kufanya uchunguzi ili kuhakikisha zaidi. Nafanya hivi ili kulinda maisha ya mtoto Nasra
Basi bwana siku hiyo hapo nyumbani yani kuanzia kwenye ile mida ya saa tatu asubuhi kulikuwa na heka heka nyingi, kwa siku moja wwaliweza kualika watu kibao huku wakipanga party iwe usiku.
Upande wangu sikujishughulisha na chochote zaidi ya kumuangalia mwanangu ambaye muda wote alikuwa hajui lolote likiendelea..........
ITAENDELEA......
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni