Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
05 Mar 2026
38 views
VYOTE NDANI GONGA94
Jinsi ya kutuma pesa kutoka Safaricom Kenya kwenda Vodacom Tanzania
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Kutokana na ongezeko la watumiaji wa Safaricom M-Pesa wanaohitaji kutuma pesa kwenda Vodacom M-Pesa Tanzania, nimeamua kuandika makala hii ili kuwasaidia wale ambao hawafahamu jinsi ya kufanya muamala huo.
Tuma pesa kutoka Kenya kwenda Tanzania
Fuata mtiririko ufuatao kufahamu jinsi ya kutuma pesa kutoka M-Pesa Kenya kwenda M-Pesa Tanzania
Kwenye simu yako, fungua application ya ku manage SIM CARD (Sim Toolkit)
Chagua Safaricom kisha fungua M-Pesa
Chagua “LIPA NA MPESA”
Chagua Pay Bill kisha weka namba ya biashara yaani Business Number ambayo ni 255255
Sehemu ya kuweka “Account Number” weka namba ya simu ya Tanzania kwa kuanza na code ya Tanzania pekee bila + yaani 2557XXXXXXXX
Andika kiwango unachotaka kutuma katika Kenyan Shillings KES.
Ingiza namba yako ya siri ya M-Pesa halafu kubali muamala.
Baada ya kukamilisha mtiririko huo, utaulizwa kama unataka kuzuia muamala, uandike herufi yoyote ndani ya sekunde 25, usiandike chochote, acha kama palivyo au waweza bofya CANCEL, baada ya hapo utaambiwa “Thanks for using M-Pesa” na kiwango ulichotuma kitatumwa moja kwa moja kwenye namba uliyotuma Tanzania.
NJIA MBADALA
Iwapo upo Tanzania, na ungependa kutoa pesa moja kwa moja kutoka kwenye laini yako ya Safaricom bila kuituma Vodacom kwanza, unachopaswa kufanya ni ku bofya namba ya M-Pesa ya Safaricom ambayo ni *840#.
Kama ndio mara yako ya kwanza kubofya namba hiyo, utaambiwa uandike eneo ulilopo, utaandika eneo lolote ulilopo kwa Mfano, Dodoma, au Arusha.
Baada ya kufanikiwa kuhifadhi eneo ulikopo, utabofya tena *840# na utachagua ROAMING PICK UP, hapo sasa utaweka nambaya wakala wa M-Pesa unapotaka kuchukua pesa yako na utaendelea kufuata maelekezo kama kawaida, kwenye njia hii ya pili, badala ya kuweka kiwango kwenye Shilingi za Kenya, unaweka katika Shilingi za Tanzania.
Endelea kuwa pamoja nasi kufurahia elimu tunayoitoa kupitia blog hii
Maoni
You're not logged in
X
Login
X
signup
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
NILILETEWA MFANYAKAZI KUTOKA KIJIJINI 1--2
SEHEMU YA 1 ANZA NAYO SASA....... Ndugu zangu, dada zangu mama zangu na watu wangu kwa ujumla kwanza kabisa nianze na f...
Je wajua Joseph Ogolan Olita muigizaji kutoka Kenya ndiye aliyecheza Uhusika wa Idd Amin dada katika filamu ya The Rise and Fall of Idd Amin ya mwaka 1981 na Mississippi Masala ya mwaka 1991
ambayo aliigiza sambamba na staa mkubwa Denzel Washington Joseph alikuwa anamjua Idd Amin kwa kiasi alichofanya ni kuji...
Jinsi ya kutuma pesa kutoka Safaricom Kenya kwenda Vodacom Tanzania
Kutokana na ongezeko la watumiaji wa Safaricom M-Pesa wanaohitaji kutuma pesa kwenda Vodacom M-Pesa Tanzania, nimeamua kuandika makala hii ili kuwasaidia wale ambao hawafahamu jinsi ya kufanya muamala huo.
Tuma pesa kutoka Kenya kwenda Tanzania
Fuata mtiririko ufuatao kufahamu jinsi ya kutuma pesa kutoka M-Pesa Kenya kwenda M-Pesa Tanzania
Kwenye simu yako, fungua application ya ku manage SIM CARD (Sim Toolkit)
Chagua Safaricom kisha fungua M-Pesa
Chagua “LIPA NA MPESA”
Chagua Pay Bill kisha weka namba ya biashara yaani Business Number ambayo ni 255255
Sehemu ya kuweka “Account Number” weka namba ya simu ya Tanzania kwa kuanza na code ya Tanzania pekee bila + yaani 2557XXXXXXXX
Andika...
👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/jinsi-ya-kutuma-pesa-kutoka-safaricom-kenya-kwenda-vodacom-tanzania
Maoni