Simulizi za Maisha,Mafunzo,Mapenzi ,Chombezo Habari za Michezo na Burudani vyote kwa Kiswahili ndani ya – Gonga94 Semajambo
Gonga94 · Stories
12 Mar 2026
79 views
VYOTE NDANI GONGA94
mke wangu kaniambia mtoto sio wangu nifanyaje ndugu zangu
Usimulizi huu ni wa watu wazima. Chukua muda wako, tulia, kisha usome kwa utulivu kama machapisho yetu yanayoendelea moja kwa moja.
Mimi naitwa Baba Derick, Leo asubuhi mapema sana, kama kawaida yangu niliamka kwenda kutafuta riziki. Kabla sijaondoka nyumbani, niliweka shilingi elfu mbili mezani. Nilimwambia mke wangu wazi kabisa kwamba pesa ile ni kwa ajili ya chakula na matumizi madogo ya siku hiyo.
Baada ya hapo nikaondoka zangu kwenda kazini kupambana na maisha.
Ilipofika jioni, nilirudi nyumbani nikiwa nimechoka sana. Lakini nilipofika ndani, nilishangaa kitu ambacho sikutarajia kabisa. Nilikuta mezani kuna kuku wa pilau na vyakula vingi sana, kama vile kuna sherehe fulani imefanyika.
Nikamuuliza mke wangu kwa mshangao:
“Mbona hivi vyakula ni vingi hivi? Mimi si nimeacha elfu mbili tu asubuhi?”
Mke wangu akanijibu tu kwa kifupi:
“Bana mwenyewe nimetafuta na kupambana.”
Lakini moyoni nilihisi kuna kitu hakiko sawa. Nikamwambia tena:
“Hapana, hii siyo kawaida. Hivi vitu haviwezi kununuliwa kwa pesa ile niliyoacha.”
Maneno yakaanza kuongezeka, ugomvi ukaanza pale pale ndani. Tukaanza kutukanana, sauti zikapanda hadi tukaanza hata kusukumana kwa hasira.
“Ngoja nikuambie ukweli wewe mwanaume… huyu mtoto Derick sio wako. Hivo kuanzia leo jua kabisa, baba yake yupo. Na kama hujui, baba yake ndiye aliyetoa hivi vitu na ndiye anayemlea.”
Kiukweli ndugu zangu, maneno yale yamenichoma moyo sana. Nilihisi dunia imenisimama. Mtoto Derick ambaye nimemlea, nimempenda na kumjali kama damu yangu… ghafla naambiwa sio wangu.
Kwa hasira na maumivu, nimeenda nikamchukua Derick, nikapiga naye picha. Nikaamua kuweka mtandaoni ili niwaombe ushauri. Naombeni Ushauri kabla sijaenda kupima DNA.
Maoni
You're not logged in
X
Login
X
signup
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa
+ Endelea kugundua zaidi
Taarifa hii haijathibitishwa lakini watu wanaulizana itakuaje kama kweli ubalozi wa huyu bwana utakuwa umeguswa? SIO KULIPULIWA UGUSWE TU!
Wataalamu wanahofia kuwa Kim Jong Un anaweza kutumia tukio hilo kama kisingizio cha kupanua uungaji mkono wake kwa Tehr...
mke wangu kaniambia mtoto sio wangu nifanyaje ndugu zangu
Mimi naitwa Baba Derick, Leo asubuhi mapema sana, kama kawaida yangu niliamka kwenda kutafuta riziki. Kabla sijaondoka nyumbani, niliweka shilingi elfu mbili mezani. Nilimwambia mke wangu wazi kabisa kwamba pesa ile ni kwa ajili ya chakula na matumizi madogo ya siku hiyo.
Baada ya hapo nikaondoka zangu kwenda kazini kupambana na maisha.
Ilipofika jioni, nilirudi nyumbani nikiwa nimechoka sana. Lakini nilipofika ndani, nilishangaa kitu ambacho sikutarajia kabisa. Nilikuta mezani kuna kuku wa pilau na vyakula vingi sana, kama vile kuna sherehe fulani imefanyika.
Nikamuuliza mke wangu kwa mshangao:
“Mbona hivi vyakula ni vingi hivi? Mimi si nimeacha elfu mbili tu asubuhi?”
Mke wangu akanijibu tu...
👉 Soma zaidi hapa: https://www.gonga94.com/semajambo/mke-wangu-kaniambia-mtoto-sio-wangu-nifanyaje-ndugu-zangu
Maoni