AFANDE MILLANπ 41 to 42
Sehemu ya 41
Basi bwana , zena alivyoniona mnazani alisimama,hapana bali ndo kwanza akaongeza speed ya kuelekea kwake ,na mm nikawa namfata kwa haraka ili asije akajifungia, basi zena akaingia ndani kwake akataka kufunga malango ,ila nilishafika nikazua nami nikaingia ndani ,zena akanmbia unataka nn nakuuliza unataka nn, usinijazie mbuu ondoka ndani kwangu, nyieeeee mi sikutaka maneno mengi ,mwanaume mimi na ujanja wangu wote, nikapiga magoti mbele ya zena , nikamwambia sikia zena nimekosea ile siku, mi binadamu kuna mda natereza mama ,nisamehe , nimekosea kweli kweli, na nimeteleza mnoo ,nakuhaidi zena sitarudia tena kufanya kosa kama lile ,nisamehe sana mama yangi, mi naumia nikikuona wewe na hali yako hii unapambana na biashara za moto na mimi nipo, nisamehe zena ,nisamehe mama yangu, nipe chance sasa niwajibike kama baba, oyaaaa nilinywea hii siku mana nilishaelewa apa nikipanda na nikajifanya na mm kuwa juu, mimi na zena hatutafika kokote, mana na yeye kashakuwa na hasira nikaona apa mm nipoe tu, mana ndo nimezingua
Zena akanmbia nyanyuka uendee, sitaki drama kabisaa, mwanaume gani wewe. ,najuta ata kukujua mjinga wewe, naomba ondoka apaa ,ondoka bwana millan usinitibue mm, unaniletea misamaha yako ya kinafiki mimi, ni lini umewahi kujali millan, ni lini umeewahi kuwa na hiyo hururma, ni mala ngapi nimelia mbele yako na haujajali lolote ,leo unakuja unaanza fyoko fyoko, naona unataka kuniludisha kwenye mifumo yako ya maisha si ndio? Unataka kunirudisha kwenye mambo yako ya kipumbavu ili unitese si ndio, ili unisumbue mm si ndio, millan mi sishindwi kupambana na maisha yangu, mimi na wewe kipindi tunakutana uliknikuta nna maisha yangu na nna kwangu ambapo mm nililizika napo tu, ukanidanganya mengi mpaka nikaingia kwenye mkenge wako wa majuto, leo unajileta tena unakuja kujiongelesha apa, millan sikuhitaji kwa chochote na sitaki niwe na mahusiona na wewe kwa chochote kile naomba uende, kama nilivyokwambia mimba mm naimudi nisikuone apa mshenzi mmoja wewe
Daaaah nikaona apaa ni shidaa, apo zena anaonge akwa hasira mpaka machozi yanmtoka, nikainuka nikamshika mkono, akanipanch mkono wangu, akanmbia usinishike mwanaharamu wwe, na marufuku kuja apa kujibebisha kwa mtoto wangu, mana nakujua we ni mnafiki tu, na wala.hujawahi kumpenda ummy, ila ulikuwa unajifanya kumpenda ikiwa ni moja ya mbinu yako ya kunipata mimi, na unichezeee mjinga wewe, tabia zako zipo wazi millan, mimi nishakubali kuwa nimebug na nimeingia kwenye mkengeee, ila sikubali kulea na wewe, so ondoka apa huna mtoto na mimi, mjinga wewe, daaah nikaona apa nikiendelea kukaa hatutapata muafaka , zena ana hasira sana anaongea mpaka anatetemeka, ikanibidi mm niondoke, nikatoka nje nikaingia kwa gari yangu, aseeee nilijua nimezingua mi ni polisi, naelewa mtu akiwa anaongea kwa kumaanisha kwemye macho yako tu, aseee nilijikuta kama machozi na mimi yananilenga, sikuwa sawa, zena alinambia maneno ya kunikata sana
Nikafika zangu job , sina mood kabisaaa yani, nimepoa kisengee ata hamu ya kuongea na mtu sikuwa nayo, nimeingia ofsinis nikiwa busy na kazi, ila kila nikikumbuka maneno ya zena naumiaa, mi sikutaka kumuelezea ili jambo ibraa wala nn, nilihisi nalimudi na nitaongea nae mwenyewe tu zena tutamaliza, alafu nilikuwa naona aibu mbele ya ibraa mana ile siku nilijitamba sana kuwa naachana nae zena na sina mda nae, lakini leo nilikuwa nahitaji kuwa baba kwake, na familia yake , ila demu ndo kanigomea sasa, basi bwanaa kuanzia apo mi nilikuwa napita sana kwa zena, navizia mida ambayo yupo nyumbani ndo naenda nyieeee,ila sasa zena akawa hana habari na mm kabisaa, na kila nikienda hasira zake ndo zinazidi kupanda ,hataki kunifikilia ata kidogoo , tena apo ananipa na maneno makari mapya kila siku, na nikimkuta yupo na ummy, hataki ata kidogo, nimshike mwanae ,ananmbia mi simpendi yule mtoto ila nilimtumia tu kumpata yey, aseeee mi sikuchoka sielewi ni kwa nn, ila bado nilitaka suruhu na zena, nilifosi kwenda mwezi mzima, apo zena akafikisha mimba ya miez 8, ila bado hatulupata suruhu
Aseeee nakumbuka iyo siku, nimetoka job, nikapita k kooo , nikamnunulia nguo zena , madera madera ya kulelea nafanya ile kumuandalia uzazi, nikamchukulia na ummy nguo, theni nikapita duka kubw la madawa, pale sasa nikamchukulia vifaaaa vyote vya kujifungulia mana nilishajua mimb ina miezi 8, mwezi wa tisa lazima akajifungue ,japo sikuwa tarehe zake za makadilio na hajanieleza kabisaa hii yote sababu tupo katika maugomvi,
so ata muda wa kunielezea aya mambo inakuwa ngumu, basi baada ya maemezi ayo mi nikaenda kwa zena sasa , aseeeee acheni ,yale madera yalichanwa chanawa mbele yangu,,, ummy nimempa zile nguo anashangilia, akapigwa makofi ,na zile nguo zena akazivuta akazichana na kisu mbele ya macho yangu, nikaona isiwe kesi mi nikabeba vifaaa tu, niaondok navyo mana niliona na vyenyewe vitachanwa chanwa na kuvunjwa hivi hivi, ila nilijisikia vibaya sana , nilijisikia vibayaaa mnoooo , asa kwa ummy, yani anafanya mtoto sasa, aniogope mana anajua akinishobokea tu anapigwaa, nilijiuliza uyu mwanamke kwanza kabira gani mana mda wote nadate nae nilikuwa silijuh kabila lake ,na mbona ana hasira hivii, aseeee ulikata mwez na nusu nafatilia msaamaha na hakuna daaah ,nikakakausha wananangu
Niliona nimpe.space kwanza mana daaah, alikuwa akiniona anacharuka kweli kweli, anawaka mda mwengine, ananifungia mlango njeee , nabaki nimesimama tu, wapangaji wengine wananaingalia nakuwa napata aibu, yani hakuwa anataka ata kunisikia kabisaa, nikaona nipoe kwanza, kweli mi nikaacha kwenda kwa zena kwanza ,na pia nilipata kazi ya kusafiri kwa week 2 nikaenda mwanza , uko nikawa busy sna na kazi, sijuh kwa nn but kwa hiki kipindi ata mood ya madame wengi nilikuwa sina yani ilikuwa inanaikata kinoma noma , basi bwana nilikaaa mwanza kwa week 2 kisha ndo nikarudi dar kuendelea na maisha , apa dar nilikaa kama week tu, nikaona ebh nikamuone zena hii siku mana sikuwa nimeenda kwke sasa kama week 3, mi sikuwa nakoma wala nn japo mchumba alikuwa ananikazia kisenge
Tena iyo siku ilikuwa ni usiku , kama.saa 3 ndo nikaenda mana najua naenda kudhalilika, ila usiku ata wapangaji wenzake wanakua ndani kwao so nadhalilika mwenyewe, ila mchana doooh nikaona jau, basi bwana mi nimefika kwa zena nikagonga mlango, na akaja kunifungilia mlango ummy, nikaingia mpaka sebleni, ummy akaniamkia ila ananiogopa mtoto ata kuniwoow kama ile zamani hakuna, sieleiw zena akikuwa anamwambia nn uy mtoto, nikamuuliza mama yuko wapi, akanmbia chumbani anaumwa mama leo, mh nikasema sawa mi sikugonga wala nini ,nikaingia mpaka chunbani, kweli namkuta zena ,amekaa kitandani ila anaangaika anagaika, mh nikamuuliza zena shida nini, akanmbia naumwa naumwa sana nampigia shey hapatikani, mh nikamuuliza unamwa nini, akanmbia kiunoa ,na tumbo uku chini linanaivuta, mh mi nakujua uyu uchungu, mi si naelea anishazalisha sana, nikaona uchungu nyoko leo mtoto kanijibu hakuna ujeuri wala kunufukuza manina zakeπ€£π€£π€£π€£π€£π€£ππππππ
π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦π¦
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi

Maoni