AFANDE MILLAN😎 Sehemu ya 40
Basi mimi nikaludi nyumbani nipo stressed kinoma , yani mawazo yamenijaa mnoo, nawaza inakuwaje sasa demu ndo kashanikazia ,ila naumia mnoo kwa ile hali yake na bado anaendelea kufanya biashara za moto vile daah ,yule demu anaumia bwana, nilimuwazia zana na alivyo na hasira na mimi sijuh itakuwaje sasa , nikaona ile mimba ina miezi 7, mi nikimkaushia ntanyimwa mtoto kweli, nikaona hapna lazima nipate suluhu na zena, tuongee na tuyamalize ili mimi nipate ata channce ya kuhudumia ile mimba, manaa daah niliona demu anaumia vile, akija kuzaa si atamjaza maneno kibao mtoto , nikaona hapana bwana hasira apa niweke pembeni, nitafute mdaa mimi na zena tuongeee, basi bwan kuna namba yangu uwa ninayo zena haijuh, nikachukua iyo siku nikampigia, na kweli akapokea
Aseee nilivyosema tu halllow, simu ikakatwa napiga tena nayo kashanilamba block, nikajua kasikia sauti kanijua ,dooh nikaona kweli safari hii mchumba kaamua yani, basi mm sasa nikampigia shey uo usiku kama saa 5, kweli shey akapokea, nikamwambia shey sikia, mi ni mtu mzima ila safari hii nimezingua na naelewa kama nimezingua, but now nataka amani, kwa sasa nataka kuwa baba kwa mwnangu, ebu plsss ongea na zena , tumalize hizo shida, shey kanmbia millan, mi kwa sasa sitaki kujiingiza katika shida zenu kabisaa kati yako na zena, hivi unajua zena hataki ata kukusikia nazani umejionea vizur tu leo, aya mm naanzaje kwenda kumwambia ayoo hapana mm siwez , alafu millan we ni mzinguaji alafu ukashindwa kumuelewa zena,
Zena sio mwanamke wa pilika pilika kabisaa kama sie , zena ni mwanamke mtulivu asiye na shida ata akodogo, millan zena alikuwa anakupenda kweli wewe, na hakutarajia yale, lakini ukamfanyia ya kumfanyia na haukujali kabisaaa, tena ukaonesha umwamba wako kama wewe mwanaume ,leo unanambia mie nikaongeee na zena arudi mwako,habadani mimi siwezi, yani siwez kabisa, mana mambo yako afande millan unayajua, dakika mbili ni wewe na dakika 2 sio wewe, kiukweli mm siwez hapana kabisaa, nikasema shey we ndo rafiki wa pekeee wa zena, asa usiponisaidia wewe atanisaidia nani, mi now serious nataka kulea mimba , mbona inakuwa hivi , shey akanmbia issue moja wewe huna wema millan, na unapenda sana kucheza na hisia za watu, kiukweli hapana sitaki, we panga mda nenda kaongee mwenyewe na mwanamke wako, apo sasa shey akanikataima na simu . Nikaona powa hakuna noma
Basi mi nikaandaaa msosi ,nikala kidogo kweli, yani nilijishngaaa mood ya kula kama nnavyokulaga ata sina, baada ya chakura sasa , nikaenda zangu kulala.ata kuoga niliona shida, daaaha asubuh na mapema mi kablaa sijaenda kazini ,hamuwezi amini mi nikapita kwa zena, yani kwa mda uo nilijikuta tu nataka kuwa responsible kama baba, sikutaka zena awe anaangaika vule wakti mi naweza kumsaidia, yani saa 12 nipo kwake, nimefika nikatulia njeee mana kulikuwa kimyaaa, si mnajua asubuh watu hawajaamka na hadi nyumba ilikuwa imefungwa, aseee kama bahati, namuona zena anatoka kavaa dera anampeleka mtoto shule yani ummy , mi sikushuka nikatulia nimngoje aende mpaka arudi na naona gari yangu hakuiona ,mana kwa apa Alipohamia now gari napaki mbali kidogo, basi kweli akaendaaa na mwanae, nilipoona anarudi na mimi haraka nikamuwahi sasa ili nizungumze nae nione kama tunaweza kuelewaana
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni